Uhali gani mdau wa GK, wiki hii Chaguo la GK linatoka kwa Angel Benard (muite Mrs Sakafu). Wimbo wake wa Have Your Way kutoka album ya Need You to Reign. Wimbo huu ni wa kipekee, pale unapomsihi Mungu akufinyange, akufanye vile apendavyo, akuhuishe, akutumie, akufanye wa maana katika ufalme wake uliotukuka, basi ndio Angel ameuweka kwa lugha rahisi; Have Your Way.
Kama ambavyo Mungu alitujua tangia hatujatungwa tumboni mwa mama zetu, ndivyo ambayo tunamuomba aendelee kufanya jambo juu ya maisha yako tangu sasa na hata milele.
Uwe na Jumapili yenye baraka tele, na Mungu aseme nawe kwa upya.