Quantcast
Channel: Gospel Kitaa™
Viewing all 1245 articles
Browse latest View live

BASATA YAWATAKA WAIMBAJI NYIMBO ZA INJILI KUJISAJILI

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
Ephraim Sekeleti kwenye tamasha la pasaka Jijini Mwanza (bofya kuona picha)
BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata) limezidi kutoa wito kwa Waimbaji wa muziki wa Injili kujisajili katika baraza hilo ili stahiki zao zitambulike inavyotakiwa.

Mkurugenzi wa ukuzaji Sanaa na Mtukio wa Basata, Maregesi Kwirujira Ng’oko alisema waimbaji wengi wa muziki wa Injili wa Tanzania kuzingatia hilo.

Ng’oko alisema kujisajili Basata kuna faida na fursa nyingi ambazo ni msaada ambao utasaidia kupata haki zao kupitia kazi zao.

Ng’oko alisema kwa kuwa wao ndio wasimamizi wa kazi za sanaa ni jukumu lao kuwakumbusha mara kwa mara wasanii kujisajili.

Aidha Ng’oko alisema wanatoa salamu hizo kwa wasanii pindi inapotokea mikinzano katika ufanikishaji wa kazi zao.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Abihudi Mang’era alisema wanafikiria kuongeza msukumo kwa waimbaji wa muziki wa Injili kuhusu kujisajili Basata katika baadhi ya matukio.

Mang’era alisema wanafikiria kutoa elimu ya kujisajili BASATA katika matamasha yao ama kusaka namna ya kufanikisha utambuzi wa waimbaji katika baraza hilo.
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ni Shirika la umma lililoundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 23 ya Mwaka 1984.Historia inaonyesha kuwa, Sheria ya kuunda upya Baraza hili ilifanywa kwa kuunganishwa Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa ya Mwaka 1974 na Baraza la Muziki la Taifa (BAMUTA) ya Mwaka 1974. Baraza liliundwa ili lisimamie maendeleo ya sanaa nchini

Dira Kuwa chombo chenye uwezo wa hali ya juu wa kutoa huduma bora kitaifa katika maendeleo ya sanaa

Lengo kuu Kufufua, kukuza na kuongeza maendeleo ya utengenezaji wa kazi bora za sanaa.

Maadili Maadili ya msingi ya Baraza la Sanaa la Taifa ni kuhimiza na kukukuza utamaduni halisi wa sanaa ya Kitanzania, kudumisha ubobezi na ubora wa hali ya juu na kuchochea ubunifu na uvumbuzi katika sanaa
  • Limepania kuhimiza na kukuza utamaduni halisi wa sanaa ya Kitanzania
  • Limepania kudumisha ubobezi na ubora wa hali ya juu
  • Limepania kuhimiza ubunifu na uvumbuzi katika sanaa


DINA MGOMERA ASHUKURU WADAU WALIOJITOKEZA UZINDUZI WAKE

$
0
0

Dina Mgomera.

Mara baada ya kumaliza tukio la uzinduzi wa albumya DVD yake ya 'Nina Haja Nawe', Dina Mgomera ameamua kuwashukuru wadau wa muziki wa Injili waliojitokeza kwa wingi tofauti na ilivyotarajiwa siku ya tukio hilo la tarehe 17 Januari 2016 ndani ya kanisa la T.A.G Ilala.

Dina ambaye aliamua kufaya live, ameelezea tofauti kubwa ambapo kati ya uimbaji wa kutumia vyombo na ule wa kuimba kwa kutumia CD, ambapouimbaji wa live unatoa fursa ya kuwa huru zaidi kuliko kubanwa na "mshindo nyuma".

Aidha, pamoja na changamoto kadha wa kadha kuwepo kwenye siku hiyo, bado imekuwa ni sehemu ya kujifunza na kuboresha zaidi pale palipopungua. Udhamini huo umesimamiwa na Great Quality na kudhaminiwa na Gospel Kitaa.

"Shetani kwa kila namna alipanga huu uzinduzi usifanyike... lakini kwa rehema ya Mungu ulifanyika - na kwa mafanikio" Anaeleza Dina katika mahojiano na mwandishi wa habari hii.

Tazama picha kamili za tukio hilo kwenye album yetu kwa kubofya hapa;

Uzinduzi - Nina Haja Nawe (Dina Mgomera))

HOJA: TOFAUTI KATI YA AJIRA NA KAZI

$
0
0
Na Askofu Sylvester Gamanywa,
WAPO Mission International.
Toleo la wiki hii nimekusudia kufafanua misamiati ya maneno kati ya “ajira’ na “kazi” ili kuweza kuweka bayana njia bora ya kuinua uchumi binafsi na taifa kwa jumla. Nina hakika ukisoma ukiwa na mtazamo chanya utapata picha nzima ya ni wapi uelekeze dua na nguzu zako kwa habari ya kupanua uchumi wako:

Tafsiri ya maneno
 ya ajira na kazi

Tafsiri ya neno ajira maana yake ni: “Kazi zitolewazo au zifanywazo kwa malipo katika serikali, kampuni au kwa mtu binafsi.” Ajiri “kumpa mtu kazi kwa ujira au mshahara” Tafsiri ya neno kazi maana yake ni: “shughuli anayofanya mtu km kulima, kuandika au kufundisha.”

Kwa tafsiri fupi tumepata picha kwamba “Ajira”na “kazi” ni vitu viwili tofauti. “Ajira” ni “kufanya kazi ya mwingine kwa malipo”! Ni kufanya kazi ya mwingine kwa mkataba unaoweka bayana majukumu ya kufanya na malipo stahiki kwa majukumu hayo.  Lakini “kazi” ni “kufanya shughuli yako binafsi inayotegemea kipaji au ujuzi wako kwa kuzalisha au kutoa huduma kwa wateja ili kupata faida kama mapato yako.”

Tofauti kubwa kati ya ajira na kazi

AJIRA
KAZI
Kazi ya mwajiri
Shughuli ya mtu binafsi
Mkataba unaoanisha majukumu na viashiria vya ufanisi wa kazi kulingana na muda wa kazi
Mipango kazi kwa ajili ya uzalishaji au utoaji huduma ili kutosheleza mahitaji ya wateja
Kulipwa mshahara/mafao ya uzeeni
Kupata faida/ akiba


Malalamiko kuhusu
 ukosefu wa ajira

Sababu kubwa iliyonisukuma kuandika habari ya tofauti ya ajira na kazi ni mkazo mkubwa unaowekwa katika kutafuta ajira kana kwamba hii ndiyo njia pekee ya kuinuka kiuchumi. Na changamoto kubwa iko kwa jamii ya wahitimu wa vyuo vikuu ambapo Ongezeko lao la kila mwaka haliendi sambamba na ongezeko la uzalishaji unaotoa fursa za ajira.

Katika kuweka mkazo kwenye ajira nimegundua kwamba, ufumbuzi wa changamoto ya ukosefu wa ajira ina mbadala ulio bora zaidi isipokuwa wahusika hawana uelewa na kupitia makala hii napenda kuwafunbua macho. Kabla ya kwenda mbali zaidi napenda ziweka bayana sababu tatu ajira si njia pekee ya kuinuka kiuchumi:

Kwanza; katika Kama nilivyotangulia kusema kwamba kutokana na ongozeko kubwa la wahitimu wa vyuo wanaotafuta ajira ni kubwa kuliko fursa zilizopo kwenye soko la ajira. Kwa hiyo sio kila mtu atajaliwa kupata fursa au nafasi ya ajira. Aidha tujikumbushe kwamba “ajira” ni kazi ya mtu mwingine ambaye ndiye anayewajibika kukulipa mshahara kwa kazi utakayomfanyia. Kila mwajiri anayetoa nafasi za ajira ni kulingana na ukubwa wa mradi, biashara au huduma anazozitoa kwa wateja wake.

Hakuna mwajiri anayeanzisha mradi, biashara au huduma kwa msukumo wa kuajiri watu ili wapate kujiendeleza kimaisha. Kipaumbele cha mwajiri ni kuzalisha/kutoa huduma ili apate faida kama sehemu ya mapato ya kazi yake.
Mwajiriwa yupo kama sehemu ya gharama za uzalishaji ili ajipatie faida na sio amnufaishe sana mwajiriwa wake. Ndiyo maana malipo ya mwajiriwa ni kidogo kuliko faida inayokwenda kwa mwajiri.


Pili, pamoja na kwamba watu wengi wanatamani kupata ajira. Lakini sio lazima kwamba kila mtu lazima aajiriwe. Kwanini? Kuna baadhi ya watu wenye uwezo  mkubwa wa ubunifu na uzalishaji kiasi kwamba wao ndio walistahili kutengeneza ajira kwa ajili ya wengine.

Ni ajabu sana ambapo kumkuta mtu ana elimu, ujuzi na uwezo wa kuanzisha kampuni na kupata vibali vya kuendesha miradi au biashara au huduma na kupata faida kubwa; lakini mtu huyo anang’ang’ana na ajira na kutumia vipaji na uwezo wake mkubwa kumpatia faida mwajiri wake! Kumbuka kwamba mtu kama huyu akiondoa woga na kuamua kuanzisha kazi anayoisimamia mwenyewe atasaidia wengi ambao watanufaika na vipaji vyake badala yay eye kumnufaisha mwajiri mmoja.

Tatu, pamoja na kwamba ni watu wengi ambao wanatamani ajira lakini sio wote wenye sifa za kuajiriwa na kuajirika. Ajira ina sifa zake na vigezo vinavyotumika kumthibitisha mtu kuwa ana sifa za kuajiriwa. Ingawa kila mtu “ana haki ya kuajiriwa” lakini sio kila mtu ana sifa za kuajiriwa mahali popote anapotaka yeye.


Hata kama ajira ni chache bado
kila mtu anatakiwa kufanya kazi

Kama wewe sio mlemavu wa viungo, sio mtoto wa umri mdogo, si mzee uliyepita umri wa kufanya kazi; basi ni bora ujue kwamba ni wajibu wako binafsi kujitegemea katika kupata mahitaji yako ya lazima km chakula, mavazi na malazi.

Kuanzia binadamu wa kwanza, tunasoma kwamba mara tu baada ya kuumbwa alikabidhiwa bustani ya Edeni ili ailime na kuitunza. Ile haikuwa ajira bali ilikuwa ni kazi. Wala si Adamu aliyeitafuta bustani ya Edeni bali alikabidhiwa na Muumbaji wake. Huu ni ushahidi kwamba kwa asili binadamu aliumbiwa uwezo, ubunifu, na nguvu za kufanya kazi. Uwezo wa kufanya kazi ni wa kimaumbile na hautegemei elimu, ujuzi wa kitaaluma unaopatikana kwenye taasisi za elimu.

Japokuwa watu wengine wanatafuta ajira na kuzikosa, lakini kila mtu anayo fursa ya kufanya kazi. Maana yake kukosa ajira sio kukosa kazi ya kufanya. Mpaka sasa kuna mamilioni ya watu hawana ajira kabisaaa lakini wanaishi kwa jasho lao bila kuiba au kuwa tegemezi kwa wengine. Maana yake wanazo kazi wanafanya na kumudu maisha yao kwa jasho lao wenyewe.


MWENYEKITI WA KWAYA AJERUHIWA KWA MAPANGA NA MAJAMBAZI AKIELEKEA HUDUMANI

$
0
0

Siku ya jana tukiwa tunajiandaa na huduma ya mbez beach mishale ya alfajiri mwenyekiti wetu Bestus kalokola(kakobe ) wakati akitoka nyumban kwake Sinza Mori kuja church ili tuelekee mbez beach MAJAMBAZ HATARI walimvamia kwa MAPANGA na kumkata kata mwilini na kumuibia simu na some other Stuffs of him...

TUNAMSHUKURU MUNGU kwani lengo lao la kummaliza halikufanikiwa tulimuaisha hospital na anaendelea VIZUR KIASI...
Tuwe makin ndugu Wakristo hali ya usalama sio nzur kwa sasa tumuombe Mungu atuepushie na uovu wa adui Shetani...vibaka na majambazi ni wengi sana..TUWE MAKINI..Huduma still going on Tunaomba maombi yenu kwetu..
Simu yake pia walimuibia hvo hapatikani..ili kuweza kumjulia pole 
wasiliana na #zifuatazo.....0657 344 425/0718 75 00 

Taarifa na picha ni kwa mujibu wa kwaya husika.






MWALIMU MWAKASEGE NDANI YA JIJI LA ARUSHA

$
0
0
Kama unafikiria namna ambavyo umeanza mwaka kitofauti na kwa mawazo, basi waweza kubadilisha hiyo hali uliyonayo kwa kuhudhuria mafundisho ya Neno la Mungu yanayoletwa kwako na Mwalimu Christopher Mwakasege kuanzia kuanzia tarehe 24 hadi tarehe 31 kwenye uwanja wa Reli Jijini Arusha.

Semina hiyo ambayo huanza saa nane na nusu mchana hadi saa kumi na mbili kamili jioni, inaletwa kwako kupitia huduma ya Mana. Tukutane Uwanja wa Reli leo na kuendelea ili kupata ufunuo mpya.  

SOMO: PASIPO MUNGU HUWEZI KUBARIKIWA - MTUMISHI SAM

$
0
0

Na Mtumishi Sam


PASIPO MUNGU HAUTAWEZA KUBARIKIWA

Mwanzo  25:23
BWANA akamwambia, Mataifa mawili yako tumboni mwako, Na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako. Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili, Na mkubwa atamtumikia mdogo.

MUNGU ALIKUJUWA TOKA TUMBONI KWA HIYO WEWE ILI UJE UWE KAMA ALIVYOKUFANYA UWE KABLA HAUJAZALIWA NI LAZIMA UMTAFUTE UMTUMAINIE YEYE PEKE YAKE,MUNGU ALIMJUWA YAKOBO NA ESAU KABLA HAWAJAZALIWA NA YAKOBO TOKA TUMBONI ALITAKA ATOKE WA KWANZA NDIYO MAANA WALIKUWA WANAPIGANA NANI AWE MKUBWA NANI AWE TAIFA HODARI,MUNGU ALISEMA JUU YA YAKOBO KWAMBA MKUBWA ATAMTUMIKIA MDOGO KWA HIYO WEWE USIANGALIE YAKOBO KAMA MDANGANYIFU HAPANA ILIKUWA IWE HIVYO,

Yeremia 1:5
Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

WATU UWA WANATEGEMEA AKILI ZAO BADALA YA KUMTEGEMEA MUNGU WANATUMIA JUHUDI NA MAARIFA PASIPO KUMPA MUNGU NAFASI NA NDIYO MAANA HAWAJAFANIKIWA HAWAJUI MUNGU NDIYE ANAYEJUWA WATAKUWA AKINA NANI HAPA DUNIANI LAKINI KWA SABABU WAMEZITUMAINIA AKILI ZAO MUNGU AMEWAACHA,YAKOBO ALIMTUMAINIA MUNGU ALIKUWA ANAPENDA KUWA BARIBU NA MUNGU KIHISTORIA NA BIBLIA INASEMA ALIPENDA KUKAA HEMANI LAKINI ESAU YEYE ALIKUWA ANAJUHUDI KUTAKA KUFANIKIWA NA NDIYO MAANA HAKUWA KAMA YAKOBO KWA SABABU JUHUDI ZAKO SIYO NDIZO ZINAKUFANYA UBARIKIWE BALI NI MUNGU NDIYE MWENYE NJIA ZAKO,USIPO MTAFUTA UTABAKI HAPO TU,

Mwanzo  25:27
Watoto wakakua, Esau alikuwa mtu ajuaye kuwinda wanyama, mtu wa nyikani, na Yakobo alikuwa mtu mtulivu, mwenye kukaa hemani.

MUNGU ANAZIDI KUKUONYESHA ANASEMA HAYA MANENO ILI UJUWE WEWE SIYE NDIYE UTAKAYEFANYA KITU UFANIKIWE BALI NI MUNGU ATAKAYE KUFANYA ILI UFANIKIWE,

Methali 19:21
Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri la BWANA ndilo litakalosimama.

KAMA HAUTAKUWA NA MUDA NA MUNGU KILA SIKU UJEWE KABISA KIZAZI CHAKO UNAKIJENGEA MSINGI WA MATESO MSINGI WA KUTAABIKA KWA SABABU HUKUWEZA KUUJENGA WEWE LAZIMA NA WAO WATATESEKA HAIJALISHI HAKO KABIASHARA UNAKOFANYA PASIPO KUWA NA MUDA NA MUNGU JUWA TU UWEZI FIKA MBALI UTABAKIA TU HAPO UNABIASHARA LAKINI UWEZI KUSAIDIA WATU AU WEWE MWENYEWE UWEZI KUFURAHIA HIYO MAANA UNAONA UKITUMIA HIZO PESA UTAFILISIKA,JUWA TU BADO WEWE NI MASIKINI UTAJIRI UNAPATIKANA KWA MUNGU NA MPAKA UMEMPATA MUNGU VINGINEVYO SHIDA HAZITAISHA KWAKO ITAKUWA LEO UGONJWA HUU KWESHO HASARA YA KUPOTEZA AU KUIBIWA NK

Kumbukumbu la torati 8:18
Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.

DAUDI MWENYEWE NI MFALME ANASEMA ANATAMANI KUFANYIKA BAWABU YA MLANGO NYUMBANI MWA MUNGU YAANI HASIWE HANAONDOKA HUKO,JE WEWE MASIKINI USIYETAKA KUMTAFUTA MUNGU UNAKIPATO TU CHA KUNUNUA CHAKULA LAKINI KIBURI KIMEJAA GEUKA LEO UMTAFUTE MUNGU USIPOGEUKA JUWA MAISHA ULIYONAYO NDIYO HAYO UTAISHI NA TENA HUKU TUNAKOKWENDANAKO UCHIMI WA DUNIA UTAKUWA MBAYA NI KWA WALE TU WENYE UCHUMI WA MUNGU HAWATALIA,UNAKUMBUKA KILICHOTOKEA KWA WANA WA ISRAEL WALIPOKUWA MISRI

Kutoka 9:26
Katika nchi ya Gosheni peke yake, walikokaa wana wa Israeli, haikuwako mvua ya mawe.
Kutoka 9:4
Kisha BWANA atawatenga wanyama wa Israeli na wanyama wa Misri; wala hakitakufa kitu cho chote cha wana wa Israeli.
5 Naye BWANA akaweka muda, akasema, Kesho BWANA atalifanya jambo hili katika nchi.
6 BWANA akalifanya jambo hilo siku ya pili, na wanyama wote wa kufugwa wa Misri wakafa; lakini katika wanyama wa wana wa Israeli hakufa hata mmoja.

WATU WATAKAO BARIKIWA NA MUNGU KWA KUMTAFUTA NDIYO AMBAO KATIKA DUNIA HII HAWATALIA KWA KITU CHOCHOTE KIBAYA KITAKACHO UPATA ULIMWENGUU.......
MTAFUTE MUNGU NAYE ANAPATIKA,UBARIKIWE NA YESU NDUGU.


    Jikumbushe ujumbe huu kutoka kwa marehemu mtumishi Angela Chibalonza Muliri

SOMO: VITU VITAKAVYOKUWEZESHA UITUMIE IPASAVYO MAMLAKA ULIYOPEWA NA MUNGU - MWAL MWAKASEGE

$
0
0


SEMINA YA NENO LA MUNGU
VITU VITAKAVYOKUWEZESHA UITUMIE IPASAVYO MAMLAKA ULIYOPEWA NA MUNGU.
NA MWL MWAKASEGE
ARUSHA MJINI UWANJA WA RELI
TAR 24-JANUARY-2016
DAY 1


Marko 11: 27-28 ‘’ 27Wakafika tena Yerusalemu, wakati Yesu akitembea hekaluni, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria pamoja na wazee wakamjia.
28Wakamwuliza, “UNAFANYA MAMBO HAYA KWA MAMLAKA GANI? Naye ni nani aliyekupa MAMLAKA YA KUFANYA HAYO?
Matendo ya Mitume 4:5-7 ‘’ 5Siku ya pili yake viongozi wa Kiyahudi, wazee na waandishi wa sheria wakakusanyika Yerusalemu, 6walikuwepo Kuhani Mkuu Anasi, Kayafa, Yohana, Iskanda na wengi wa jamaa ya Kuhani Mkuu. 7Wakiisha kuwasimamisha Petro na Yohana katikati yao, wakawauliza, “Ni kwa UWEZO GANI AU KWA JINA LA NANI mmefanya jambo hili?”’’
Yesu aliulizwa swali hili kuwa ni kwa mamlaka ya nani unafanya jambo hili. Hata wanafuzni wa Yesu pia waliulizwa swali hili. Maana kwa akati ule viongozi wa dini hawakujua kuwa walifanya kwa mamlaka ya nani na ni nani aliwepa mamlaka kwa sababu hawakuwahi ona. Maana wangejua wasingeuliza. Pointi ni kuwa si vile vinavyofanyika unapokuwa na mamlaka bali ni VITU GANI vitakuwezesha kutumia mamlaka uliyopewa na Mungu.
MAANA YA MAMLAKA-- ni haki ya kisheria inayompa mtu uwezo wa kuamua na kusimamia utii juu ya kile alichokiamua.
Kwa hiyo kwa kujua maana hii utajua ni kwanini wale viongozi wa dini waliomuuliza Yesu lile swali na walilowauliza akina Petro na wanafunzi ili wajue kuwa ni mamlaka ipi ndiyo waliyokuwa nayo na ni nani aliyesimamia utii wa kile walichofanya maana wakuu wa dini walijua vizuri sana sharia.
LEO TUTAPITIA MAMLAKA AINA 11 AMBAZO YESU AMETUPA.

1. MAMLAKA JUU YA UUMBAJI NA MUNGU.
Mwanzo 1: 24-27 , Mungu katupa mamlaka ya kutawala kila kitu alichokiumba Yeye. Na ona sasa ugomvi wa Musa na Farao na wale waganga na wachawi ulikuwa kwenye viumbe. Ndio maana utaona Musa aligeuza fimbo yake ikawa nyoka na ikameza zingine za wale wachawi. Ivi unajua wachawi wanapigana vita kwa kutumia viumbe mfano Paka, Panya,Nyoka,Mbwa, bundi n.k
Musa alisema kama mimi ni mtumishi wa Mungu na tuone kinachowatokea na ghafla ardi ikafumbua kinywa chake na ikawameza. Yoshua alipojua kuwa maadui zake walikuwa wanapigana nae kutoka kwenye nguvu zilizokuwa kwenye jua na yeye akaamua kulisimamisha jua. Nae Shetani aliamua kutumia mawambi na upepo ili kupigana na Yesu na wanafunzi wa Yesu hawakujua cha kufanya lakini Yesu alijua cha kufanya.

2. MAMLAKA JUU YA PEPO NA MARADHI.
Luka 9:1 ‘’ Yesu akiisha kuwaita wale kumi na wawili pamoja, aliwapa mamalaka na uwezo wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya magonjwa yote,’’
Kuwa na mamlaka haimaanishi kuwa unaweza kuitumia sawasawa kama Mungu anavyotaka bali kwa hiyo unahitaji sana kuomba sana ili Mungu akupe maarifa vizuri namna ya kutumia mamlaka hii uliyopewa na Mungu.

3. MAMLAKA JUU YA MFUMO WA UTAWALA WA GIZA/ SHETANI.
Waefeso 6:12 ‘’ wamba mweze kuzipinga hila za Shetani. 12Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho’’
Mamlaka ya hapa ni tofauti na ile mamlaka ya kwenye Luka 9:1 , kwa mfano mamlaka juu ya Tanzania na mamlaka ya juu ya watanzania ni tofauti kwa sababu Mamlaka juu ya Tanzania ni juu ya mfumo bali mamalaka juu ya watanzania ni juu ya watu. Kwa hiyo mfano Tanzania kiongozi akifa, watu watahuzunika afu baadae watateua mwingine maana nafasi ile ipo kisheria. Kwa maana hiyo huwezi tumia mamlaka juu ya pepo ili kuja kushughulikia falme. Hizi ni mamlaka unahitaji kujua.

4. MAMLAKA JUU YA UFALME WA MBINGUNI.
Mathayo 16:19 ‘’ 19Nitakupa funguo za Ufalme wa Mbinguni na lo lote utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa Mbinguni, lo lote utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.’’
Kwa hiyo jua kuwa mamlaka zina mipaka, kwa hiyo ili jambo lifunguliwa Duniani ndipo linafunguliwa na mbinguni. Lakini order intoka Duniani.
Pia Mungu ametupa kufungua vitu vingine. Kwa hiyo ujio wa Dhambi Duniani iliondoa ufalme wa Mungu. Hata wale waliofungwa na kuzimu unaweza wafungua. Kwa hali hii ni hatari sana kwa Mtu aliyeokoka kutokaa kwenye mamlaka ya ufalme wa Mungu. Hivyo Mungu anaweka watu kwenye mamlaka ili waweze kuzisimamia. Mtu yeyote anapookoka anahamishwa kutoka ufalme wa giza na kuletwa kwenye ufalme wa Mungu.

5. MAMLAKA JUU YA DHAMBI.
Warumi 6:12-14 ‘’ 12Kwa hiyo, msiruhusu dhambi itawale ndani ya miili yenu, ipatikanayo na kufa, ili kuwafanya mzitii tamaa mbaya. 13Wala msivitoe viungo vya miili yenu vitumike kama vyombo vya uovu vya kutenda dhambi, bali jitoeni kwa Mungu, kama watu waliotolewa kutoka mautini kuingia uzimani. Nanyi vitoeni viungo vya miili yenu Kwake kama vyombo vya haki. 14Kwa maana dhambi haitakuwa na mamlaka juu yenu, kwa sababu hampo chini ya sheria, bali chini ya neema.
Warumi 7:15-24 ‘’14Kwa maana tunajua kwamba sheria ni ya kiroho, lakini mimi ni wa kimwili nikiwa nimeuzwa kwenye utumwa wa dhambi. 15Sielewi nitendalo, kwa maana lile ninalotaka kulitenda, silitendi, lakini ninatenda lile ninalolichukia. 16Basi kama ninatenda lile nisilotaka kutenda, ni kwamba ninakubali kuwa sheria ni njema. 17Lakini, kwa kweli si mimi tena nitendaye lile nisilotaka bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. 18Kwa maana ninafahamu kwamba hakuna jema lo lote likaalo ndani yangu, yaani, katika asili yangu ya dhambi. Kwa kuwa nina shauku ya kutenda lililo jema, lakini siwezi kulitenda. 19Sitendi lile jema nitakalo kutenda bali lile baya nisilolitaka, ndilo nitendalo. 20Basi kama ninatenda lile nisilotaka kutenda, si mimi tena nifanyaye hivyo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
21Hivyo naiona sheria ikitenda kazi. Ninapotaka kutenda jema, jambo baya liko papo hapo. 22Kwa maana katika utu wangu wa ndani naifurahia sheria ya Mungu. 23Lakini ninaona kuna sheria nyingine inayotenda kazi katika viungo vya mwili wangu inayopigana vita dhidi ya ile sheria ya akili yangu.Sheria hii inanifanya mateka wa ile sheria ya dhambi inayofanya kazi katika viungo vya mwili wangu. 24Ole wangu, mimi maskini! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?.’’
Kwa hiyo tulitegemea hapa Paulo aliposema kuwa Dhambi isitawale maishani mwenu na tulitegema Yeye asiwe na dhambi lakini tunachokiona hapa ni kuwa Pualo anakiri kuwa anadhambi, Kwa hiyo haikukugurantee wewe kuwa na upako kama Paulo na usiwe na dhambi. Na Tafsri ya dhambi ni Uasi lakini hii nayo uhalali wa dhambi kututawala bali sisi tushinde dhambi.

Utajiuliza ni Kitu gani kilikuwa kinamkwamisha Paulo jibu lake ni hili ni MWILI, hata siku moja jaribu kumuuliza Yesu kuwa ni kitu gani kilikuwa kinakukwamisha kwenda msalabani na ulilia sana pale Getsamen atakuambia ni Mwili ndio maana alisema roho I radhi ila mwili ni dhaifu.
Nia na Mwili ni Mauti , maana mwwili hauendi mbinguni na mwili hautiii cha Mungu.
Kwa hiyo ile wewe kuwa na mamlaka juu ya pepo wabaya au maradhi haikupi kibali cha kwenda mbinguni maana Yesu alisema watasema mbona tulitoa unabii, pepo kwa jin lako lakini yeye atawaambia kuwa sikuwajua ninyi. Na ndio maana aliwaambia wanafunzi wake msifurahi kwa kuwa pepo wanawatii bali furahini kwa kuwa majina Yenu yameandikwa mbinguni.
Kwa hiyo mamlaka hizi zinatupa namna ya kutembea hapa Duniani na sio kwenda mbinguni. Suala la kwenda mbinguni ni suala jingine kabisa. Ukiwa na mamlaka iiswe sababu ya wewe kuoandisha mabega na kumsahau Mungu wako.

Lengo la kukuonesha utofauti wa mamlaka hizi ni kujua namna ya kwenda nazo maana kila mlango unafunguo zake maana huwezi tumia funguo za Bedroom ili kufungulia stoo uwe na uhakika hazitafungua.
Yakobo 5:15 Biblia inasema kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana akiomba kwa bidii maana maombi kama hayo yanaweza mfungua mgonjwa na kumponya magonjwa yake na kusamehewa dhambi zake. Kwa hiyo unaweza kumuombea Mtu hata kama hana mpango wa kutubu ila kwa sababu wewe umeomb Mungu anamsamehe kabisa.
Ndio maana Mungu anatumia kuhani na kuwaombea watu au kufanya upatanisho na namna ya kufanya toba ili Mungu aje na atengeze hapo mahali ambapo pana dhambi.Unahitaji kujua sana siri hii ya kufanya maombi ambayo yatashughulika na chanzo cha maradhi au magonjwa mabacho ni dhambi.

6: MAMLAKA JUU YA MALANGO YA ADUI.
Mwanzo 22:17 Uzao wako utamiliki malango ya adui. Galatia 3:13,14,29 Biblia inasema amelaaniwa yuke angakue juu ya mti, na Yesu alifanyika laana ili kwa ajili yake ili sisi tupate neema ya kufikiwa na Braka za Ibrahimu ambazo Mungu alituahidi kwa watu wa Duniani kote.

7: MAMLAKA JUU YA MIJI.
Luka 19:16-19 Habari za Yule kabaila au kwa lugha ya sasa tungemwita Mwekezaji na wale watu walipewa yale mafungu ya fedha.
Mafungu 10 alileta faida mara 10 na akapewa mamlaka juu ya miji kumi.
Mafungu 5 alileta faida mara 5 na akapewa mamlaka juu ya miji mitano.
fungu 1 alileta Hakuleta faida yoyote bali alirudisha fedha tu na haikuwa na faida na akinyimwa mamlaka juu ya miji.
Uaminifu juu ya fedha hauleti mamlaka bali uaminifu juu ya matumizi ya fedha ndio unaleta mamlaka juu ya miji.Mwekezaji anaanza kuheshimika kwenye jamii au mji aliopo kwa sababu ya kuwa na fedha. Kwa hiyo hata dini yake nayo inapata sauti kila mtu ataanza kuiheshumu. Usijulize hili ni swala la ulimwengu wa Roho.

8: MAMLAKA JUU YA MIFUMO YA KIUTAWALA YA WANADAMU.
Waefeso 2:6. 6Mungu alitufufua pamoja na Kristo na kutuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu
Waefeso 1:20-23 20ambayo aliitumia alipomfufua Kristo kutoka kwa wafu, akamketisha mkono Wake wa kuume katika mbingu, 21juu sana kuliko falme zote na mamlaka, enzi na milki na juu ya kila jina litajwalo, si katika ulimwengu huu tu, bali na katika ule ujao pia. 22Naye Mungu ameweka vitu vyote viwe chini ya miguu Yake na amemfanya Yeye awe kichwa cha vitu vyote kwa ajili ya Kanisa, 23ambalo ndilo mwili Wake, ukamilifu Wake Yeye aliye yote katika yote.
Ufalme wa wadamu umetambulishwa kama NGUVU AU USULTANI lakini vyote ni ufalme wa wanadamu.
Soma Ufunuo 17:1-2

9: MAMLAKA JUU YA MAENEO MUHIMU YENYE MAKUSNYIKO YA WATU.
Ufunuo 5: 9-12 Wanamiliki juu ya
i) Kabila
ii) Lugha
iii) Jamaa/ukoo
iv) Taifa.
Ufunuo 17:15-
Ndio maanampinga kristo anafuatilia juu ya soko yaani kuuza na kununua kila sehemu yeye anafuatilia hasi kwenye mitandao. Soma Ufunuo 13.

10: MAMLAKA JUU YA KILA FIKRA.
2Wakorintho 10:3-5 3Ingawa tunaishi duniani lakini hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo. 4Silaha za vita vyetu si za mwili, Bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome. 5Tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo
Jiulize swali hili je kuna fikra ngapi ambazo hazimtii kristo na je sisi tumechukua hatia gani ili kuzifanya zimtii kristo. Chukua hatua kushughulika na kila fikra isyomtii kristo na iweze kumtii kristo.

11: MAMLAKA JUU YA ULIMI NA KINYWA CHAKO.
Yakobo 3:1-12 Mtu Yupo kama meli, mtu atakula matunda ya kinywa chake. Kwa hiyo hata ndoa nyingi huvunjika kwa sababu ya maneno na hadi hufika hatua ya kusambaratika kabisa.
Ulimi ni Karamu na Roho Mtakatifu ni wino. Kwa hiyo kuwa makini sana na matumizi ya ulimi wako.

Itaendelea Kesho.....

SOMO: KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU (5) - MCHUNGAJI MADUMLA

$
0
0
Mchungaji Gasper Madumla
Kusoma sehemu iliyopita Bonyeza Hapa.

Endelea.....

Karama hii imepangwa kwenye kundi la karama za uwezo,kwa sababu inahusisha nguvu katika utendaji wake wa kazi. Hivyo inajulikana pia ni “ Karama ya nguvu” au “ karama maalum” majina haya tofauti tofauti juu ya karama hii hutambulisha uwezo wa kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo tena ni bayana ya mambo yanayoonekana ( katika matendo).

Karama ya imani ni tofauti kabisa na imani ya kumuamini Mungu. Kwa sababu kila mtu anapookoka anapaswa amuamini Mungu yaani awe na imani kwa Mungu wake.

Hivyo basi kitendo cha kuamini uwepo wa Mungu na nguvu zake katika Kristo Yesu ni kitendo ambacho kila mwamini anapaswa awe nacho,na imani hiyo ni imani ya kawaida kabisa wala sio karama. Lakini papo hapo kuna kiwango cha juu cha imani ambacho Roho mtakatifu anakiachilia kwa baadhi ya wapendwa kama apendavyo yeye,kiwango hiki ndicho karama ya imani.

Hivyo basi kumuamini Mungu ni pale tunapohubiriwa neno la Mungu,kisha tunalipokea neno hilo na kuanza kuliishi. Imani hii chanzo chake ni kusikia neno la Kristo,Warumi 10:17. Soma pia Waefeso 2:8,Waebrania 10:38. Bali karama ya imani ni pale baada ya kuamini kisha kutumia uweza wa Roho mtakatifu kutika matendo.

Mfano wa karama hii;

~ Haikuwa imani ya kawaida kwa Nuhu kutengeneza safina kwa miaka 100,Nuhu alihitaji apate uwezo au nguvu ya kuhamisha kile alichokiamini na kukitenda.Katika eneo hili ilihitajika karama ya imani kuwezesha kutengeneza safina kama alivyoambiwa na Mungu. Hatumuoni Nuhu akihoji hoji namna itakavyokuwa bali alifanya kama vile BWANA alivyomuamuru ( Mwanzo 7:5).

Hivyo,karama ya imani haina maswali maswali kwa kile unachokiamini,bali ni kutenda katika uweza wa Roho mtakatifu maana atendaye si wewe bali ni Roho mwenyewe.

~ Petro pia,alikuwa ni mmoja wa mitume mwenye karama ya imani. Jambo hili tunaliona pale alipoamua kumfuata Yesu juu ya maji (Mathayo 14;25-29). Hapo,sio suala la kuamini tu,!! Bali kutenda kwa uweza wa Roho mtakatifu.

Tazama suala la Petro,si rahisi kuamini kwamba ukitembea kwenye maji hautazama hali ukijua kabisa endapo utakanyaka maji basi ni dhahili utazama,uwezo huu ndio karama ya imani~ yaani unaamini zaidi ya mipaka ya kawaida kisha unatenda.

Kanisa la leo limepungukiwa kwa wingi karama hii ya imani maana wengi leo wanaamini kawaida tu,mtu mwenye karama hii ni mtendaji,mahali pale kanisa limeshindwa yeye anaweza kwa msaada wa Roho mtakatifu. Kuamini pekee hakutoshi,bali kile kinachotosha ni kuleta imani ile ya kawaida katika utendaji kazi kwa uweza wa Roho mtakatifu.

Utendaji kazi wa karama hii;

Hutenda katika nguvu,(na uweza wa Roho mtakatifu).

~ Nguvu hii inahusisha pia na nguvu ya mwilini kwamba lazima uchukue hatua ya kutenda maana kuamini pekee haitoshi. Matendo 3:4-7, Ukisoma hapo; utaona Petro akijawa na karama ya imani juu ya uponyaji kwa jina la Yesu Kristo,lakini kule kujawa na imani.

hakukujitosheleza kumponya yule kiwete,bali alihitaji amshike mkono na kumuinua kwa jina la Yesu. Kumbuka,Petro alimuinua yule kiwete akiwa katika hali yake ile ile ya ukiwete akiamini kwamba anakwenda kutembea sasa,hilo sio jambo dogo!

(ii) Karama ya uponyaji.( 1 Wakorintho 12:9)

Ikumbukwe kwamba Yeye aponyaye ni Mungu kwa njia ya Roho mtakatifu. Hivyo,hii ni karama yenye uweza wa Roho mtakatifu katika uponyaji. Ikumbukwe pia uponyaji ni mali yetu sote tuliookoka,kila aliyeokoka anapaswa awe na nguvu ya kutamka neno la uponyaji kwa wengine kisha kupokea uponyaji huo.

Uwezo huu ni ule uwezo wa kawaida kwa kila aaminie “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.” Marko 16:17-18

Huo ni uwezo wa kawaida ambao sio karama ya uponyaji. Karama yenyewe ni pale Roho mtakatifu anaweka uweza wake wa uponyaji kwa watu aliopenda kuwapa,sio watu wote. Watu wa namna hii ni zaidi ya madaktari wa kawaida,maana maneno yao yanaganga mioyo,nasfi na miili yetu pia sababu si wao waponyao bali ni Roho mwenyewe akiwa kazini.

(a) Kusudi la karama ya uponyaji.

Kulithibitisha neno la Mungu katika uweza wake.

~ Neno la Mungu limejawa na uponyaji tosha,karama hii ulithibitisha neno la Mungu kwamba linaponya kwa sababu karama hii hutenda kazi chini ya msingi wa neno la Mungu. Kwa lugha nyepesi ni hivi;kama hakuna neno la Mungu,basi hakuna karama ya upinyaji. Tukimwangalia Yesu, Yeye Neno alijawa na uponyaji “ Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.” Mathayo 8:8

Kuwavuta watu kwa Yesu,

~ roho za watu wengi leo zimeokoka kwa sababu waliponywa magonjwa yao. Hata wale wasioamini,waliamini baada ya uponyaji kufanyika katika maisha yao. Karama hii imevuna roho za watu wengi sana,na bado itaendelea kuvuna na kuvuna pasipo idadi kabisa. “ Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa hawawezi, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.Na makutano mengi wakamfuata, kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu, na Uyahudi, na ng’ambo ya Yordani” Mathayo 4:24-25

Kuwafungua waliofungwa kwa magonjwa na mateso mengi.

~ Kusudi hili ni la muhimu sana katika maisha yetu. Sababu ibilisi amejaribu kupanda pando la magonjwa kwenye miili ya watu wengi hivi leo,lakini kwa sababu ya karama hii~ watu hao wanafunguliwa mbali na magonjwa na huru na afya zao Matendo 10:38.

Kumtwalia BWANA Mungu utukufu.

~ Mungu wetu ni Mungu aponyaye ~ Kutoka 15:26. Karama hii ya uponyaji inamtambulisha Mungu tuliyenaye kwamba yupo tofauti kabisa na miungu,kwa sababu miungu haina uweza wa kuponya bali mwenye uweza wa kuponya ni mmoja tu,naye ndiye BWANA MUNGU wetu,JEHOVA. Karama hii inampa MUNGU utukufu mno.

(b) Utendaji kazi wa karama ya uponyaji;

Uponyaji ufanyika katika jina la Yesu Kristo pekee.

~ Karama hii hutenda kazi ndani ya jina la Yesu pekee. Hakuna jina jingine litupasalo sisi kuokolewa kwalo isipokuwa jina la Yesu tu~Matendo 4:12.,Yoh. 14:14 Ukiona uponyaji unaofanywa nje ya jina hili,basi ujue uponyaji huo sio wa Mungu bali ni mazingaombwe ya shetani tu~na ukimbie,utoke eneo hilo.

Kuponya roho,nafsi na mwili.

Roho mtakatifu huponya roho zetu,tazama pale tulipokuwa nje ya Kristo tulikuwa wafu. Roho mtakatifu akatuhuisha roho zetu. Pia,nafsi zetu hazikuwa hai,lakini ziligangwa pamoja na miili yetu ilikuwa ikiugua ugua,ikaponywa nayo. Karama ya uponyaji ushughulikia vyote hivyo na kuponya.

Kuponya ardhi,mazao,mifugo (kufanya ukombozi)N.K

~ Rafiki yangu mmoja alikuwa akifuga paka nyumbani kwake. Siku moja paka wake alikunywa sumu huko nje katika mizunguko yake,kisha gafla sumu ikamlevya na kale kapaka kakazidiwa kalikuwa hakapumui kabisaa! Basi wakachimba shimo wakafukie. Sasa huyu rafiki yangu alipoingia nyumbani mwake akaona ndio wanamfukia paka wake,akasikia sauti;

“ muombee” kisha akawakataza wasimfukie. Akaanza kumuombea paka,gafla kakaanza kupumua kwa mbaliii,baadae akapata nguvu,kakatembea~ kaleee,mara kakachangamka! Umeona!!! Karama ikafanya kazi hata kwa mifugo.

~Ardhi pia inaweza ikawa imekufa, kisha ikakombolewa. Hata mazao pia yanaweza yakawa ni dhaifu,karama ya uponyaji ikayainua tena na kuwa hai.

Hutegemea watu ili ifanye kazi.

~ Ikiwa hakuna watu,uponyaji hautaonekana kabisaa. Bali tunauona uponyaji kwa sababu wahusika wenye kuhitajika kuponywa wapo. Karama hii inafanya kazi ndani ya watu.

(iii) Karama ya miujiza. 1 Wakorintho 12:10

~ Karama zote zimejawa na miujiza,mfano karama ya uponyaji,karama ya imani N.K Lakini karama hii,ni zaidi ya muujiza ya kawaida bali ni matendo makuu ya MUNGU mwenyewe. Matendo haya ni karama apewayo mtu kama Roho apendavyo Yeye. Karama hii inathibitisha uhai wa BWANA YESU yakwamba yupo hai hata sasa…

“Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.” Matendo 4:13

(a) Utendaji kazi wa karama hii;

Kutumia jina la BWANA Yesu.

Karama zote ni lazima zitumie jina la Yesu Bwana wetu. Miujiza pia,ni lazima ifungamanishwe na Yesu mwenyewe maana Yeye ndie aifanyae yote hayo,U hai. Tazama miujiza fake,haitumii jina la Bwana Yesu,au hata kama wakidanya hadhara kwa kulitaja jina la Bwana basi ni dhahili kabisa watakuwa wakilitaja tu,na wala si kulitumia. Kutaja jina ni tofauti na kulitumia. Hivyo karama hii inahusisha sana matumizi ya jina la Yesu.

Kumfunua Mungu kwa watu wote.

Mungu hutambulikana pia katika miujiza. Wapo watu waliokuwa hawafahamu uwepo wa Mungu chini ya jua,lakini kwa njia ya karama hii wamemtambua Mungu. Tazama mfano,wako ambao hawakuamini kabisa uwepo wa MUNGU na wengine wamediriki kusema “hakuna Mungu” lakini walipoziona ishara na miujiza wakaamini.

Hutegemea imani.

Inafahamika wazi kwamba imani ni daraja lako la kupokea muujiza. Kumbe kama imani itakosekana hapa,basi inawezekana usipokee muujiza wako. Karama hii ya miujiza hutegemea kiwango chako cha imani,pia yule mwenye karama hii ni lazima ajawe na imani katika jina la Yesu Kristo.

(b) Matokeo ya karama ya miujiza.

~ Yapo matokeo mengi kuhusu utendaji kazi wa karama hii ya miujiza. Matokeo haya yote ni mazuri,ila ubaya ni pale namna watu wanavyoyapokea wao wenyewe.

Karama hii,imesababisha kuenea kwa injili kote ulimwenguni.

~ Tunaweza tukaanza kuangali hata katika kipindi cha Yesu. Kabla Yesu hajaanza kutenda miujiza hakuna mtu aliyemfuata popote. Bila shaka alikuwa amehubiri mara nyingi katika masinagogi,kwani LUKA 4:16,Anasema kwamba ilikuwa ni desturi yake.

Lakini miujiza katika Luka 4:33-35, ilipotendeka tu,tunaona sasa Habari za Yesu zikienea katika nchi ile. Imeandikwa; “ Habari zake zikaenea kila mahali katika nchi ile.” Luka 4:37

Hivyo basi,matendo haya makuu ni ya Bwana mwenyewe akiyaweka ndani ya wale aliowapenda Yeye,ili kusudi wakayadhihilishe nje. Na pindi yanapodhihilishwa nje huwa ni karama ya miujiza sasa…

ITAENDELEA…

~ Kwa huduma ya maombezi,usisite kunipigia kwa simu yangu hii;+255 655 11 11 49.

Mchungaji Gasper Madumla.

Beroya bible fellowship church(Kimara,Dar,TZ)

UBARIKIWE.

KWA TAARIFA YAKO : JOYOUS WANAPOMUWEKA MTU BENCHI KUTAFUTA UBORA

$
0
0
Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu

Qhubekani Mthethwa


KWA TAARIFA YAKO kama hujui ni kwamba GK ilikuripotia taarifa ya kuondoka ama kumaliza mkataba kwa kijana mwenye uwezo mkubwa wa kupiga gitaa la bass ndani ya Joyous aitwaye Bheka Mthethwa mapema mwaka jana, pia tukakuweka wazi kwamba nafasi yake ilizibwa na mdogo wake wa damu aitwaye Qhubekani Mthethwa ambaye pia inatajwa kuwa anauwezo wa kumiliki gitaa hilo vyema. Hata hivyo pasipo sababu ambazo GK haijazipata au kufahamu ni kwamba kijana huyo hakuweza kuandika historia kwa kuipigia Joyous wakati wa recording yake ya 20 iliyofanyika kwenye uwanja wa Moses Mabhida December mwaka jana.

KWA TAARIFA YAKO bado hajaifahamika kama ni kiwango ndio kilichosababisha kijana huyo kutojumuishwa kwenye kikosi cha wapigaji ama alipatwa na tukio jingine lililomlazimu kukaa pembeni toka wakati wa maandalizi hadi recording yenyewe. Badala yake gitaa la bass limepigwa na kijana mwingine anayesifika vyema miongoni mwa makundi ya injili na waimbaji binafsi nchini humo aitwaye Sipho Mabena, kijana huyu aliweza kushiriki mazoezi toka awali na kufanikiwa kupanda na Joyous jukwaani kurekodi album hiyo ya kihistoria kwa kundi hilo.

Sipho Mabena


KWA TAARIFA YAKO kwa mujibu wa baadhi ya waimbaji wa injili nchini humo ambao walifanikiwa kumuona Mabena jukwaani na Joyous hawakuacha kumpigia chapuo kwamba juhudi zake zilishaonekana mapema ilikuwa wakati tu ufike ili nyota yake ing'are vyema na kwa pamoja wakaonekana kumpongeza kwakutokata tamaa na kufanikiwa kuonwa na Joyous. KWA TAARIFA YAKO kumbuka sio Qhubekani pekee aliyefikwa na tukio la kutoweza kupanda jukwaani kurekodi na kundi hilo, pia kijana Irebolaji aliyemrithi Sabu kwenye ngoma pia hajafanikiwa kukubalika hadi kuachiwa kupiga wakati wa recording ya kundi hilo badala yake alichukuliwa Bafana Sukwene.

KWA TAARIFA YAKO Kama haitoshi kwasasa Joyous wanampiga drum kijana Thato Rapapane
waliyempachika jina la utani last born akikung'uta ngoma (drums) hata kufanikiwa kupanda jukwaani kurekodi nao. Pia hapana shaka unamkumbuka kijana Uyanda aliyekuwa mdogo wa miaka 11 wakati alipotambulishwa katika ukumbi wa ICC Durban na kupiga kidogo wimbo wa Uvalo Lwami wa kwake pastor Jabu, ni kwamba kundi hilo bado lipo na huyo kijana likiendelea kumkuza ili baadae aje awe mpigaji wao kamili. Hata hivyo bado haijawa wazi kama Sipho ataendelea kuwa mpigaji wa Joyous au alialikwa maalumu kwaajili ya kurekodi nao, vilevile kama kijana Qhubekani Mthetwa bado yupo na Joyous au walishaachana naye.

                        Jikumbushe upigaji bass wa Bheka Mthethwa katika Joyous 19




Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO kwa leo, vinginevyo tukutane wiki ijayo...

SOMO: VITU VITAKAVYOKUWEZESHA UITUMIE IPASAVYO MAMLAKA ULIYOPEWA NA MUNGU - MWAL MWAKASEGE

$
0
0


SEMINA YA NENO LA MUNGU 
VITU VITAKAVYOKUWEZESHA UITUMIE IPASAVYO MAMLAKA ULIYOPEWA NA MUNGU.
NA MWL MWAKASEGE
ARUSHA MJINI UWANJA WA RELI
DAY 2⃣
TAR 25-JANUARY-2016

Kusoma sehemu iliyopita BONYEZA HAPA

📖Marko 11: 27-28 ‘’ 27Wakafika tena Yerusalemu, wakati Yesu akitembea hekaluni, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria pamoja na wazee wakamjia. 28Wakamwuliza, “UNAFANYA MAMBO HAYA KWA MAMLAKA GANI? Naye ni nani aliyekupa MAMLAKA YA KUFANYA HAYO?

📖Matendo ya Mitume 4:5-7 ‘’ 5Siku ya pili yake viongozi wa Kiyahudi, wazee na waandishi wa sheria wakakusanyika Yerusalemu, 6walikuwepo Kuhani Mkuu Anasi, Kayafa, Yohana, Iskanda na wengi wa jamaa ya Kuhani Mkuu. 7Wakiisha kuwasimamisha Petro na Yohana katikati yao, wakawauliza, “Ni kwa UWEZO GANI AU KWA JINA LA NANI mmefanya jambo hili?”’’
Ile kuwa tu na mamlaka haitoshi bali leo nataka tuangalie Zaidi kuwa hizo mamlaka nilizokufundisha jana utazitumiaje.
👇👇
Leo tunaangalie     VITU VITAKAVYOKUWEZESHA UITUMIE IPASAVYO MAMLAKA ULIYOPEWA NA MUNGU

Mwanzo 1:28 ‘’ 28Mungu AKAWABARIKI na akawaambia, “Zaeni na mkaongezeke, mkaijaze tena dunia b na kuitiisha. Mkatawale samaki wa baharini, ndege wa angani na kila kiumbe hai kiendacho juu ya ardhi.’
Neno AKAWABARIKIA maana yake ni kuwa akawapa vitu ambavyo vitawawezesha  kufanya yale ambayo Mungu aliwaagiza kufanya. Na ukiangalia vizuri utaona kuwa Mungu aliwabariki kabla ya kuwaingiza kazini au kuwapaagizo la kuwa zaeni mkaongezeke na kuijaza nchi na kuitisha.

KAZI YA BARAKA.
Kazi ya Baraka ni kukuwezesha kuwa kama Mungu anavyotaka uwe au anavyotaka ufanye kama vile yeye anavyotaka.

MAANA YA KUITISHA, ni kumiliki kwa amri au mamalaka hata kama nchi haitaki.
Kwa hiyo msisitizo wa Somo kuwa tu na mamlaka bali ni kujua namna ya kuitumia.

☀POINTI YA 1 . MUNGU AKUPE KUJUA YA KUWA MAMLAKA ALIYOKUPA KATIKA KRISTO NI MAMLAKA AMBAYO CHIMBUKO LAKE NI ULIMWENGU WA ROHO.

Leo natakata twende kwa mifano ili tuweze kuelewana katika somo hili.

Tuangalie mamlaka amabayo Mungu amaetupa katika uumbaji wake

 Mwanzo 1 :24-28  Katika kitabu cha mwanzo utaona uumbaji wa Mungu na Mungu kuwabarikia watu wake. Kumbuka kuwa Mtu ni Roho anayo nafsi anaishi katika mwili.

Na ukisoma katika Mwanzo sura ya 1 na 2, tunaona Sura ya 1 roho ya mwanadamu ikiumbwa na baadae kaika sura ya pili ndio tunoana mwili kuumbwa na kuweka pumzi na kuwa nafsi hai.Hivyo Mwanaume na Mwanamke waliumbwa wote kwenye sura ya kwanza ila miili yao ndio imekuja kuumbwa kwenye sura ya pili.

Suala la Mwanamke ni kuzaa au kutozaa ni sauala la ulimwengu wa roho kabla halijawa suala la kimwili.

☀MFANO: Kuna mwanamke mmoja katika mkoa mmoja nilikukokwa nafanya semina na alikuwa na tatizo la kupata mimba maana kila akipata mimba zinakaa miezi miwili tu na huwa zinatoka. Na yapata mimba kama 6 ivi zilikuwa tayari zimeshatoka. Na akaja na tukaomba Mungu lile tatizo liondoke na kweli baada ya Muda akaja akapata mimba  na hiyo mimba nayo ikatoka. Na alipokuja tena kwangu nikamuuliza kwanini umetoa mimba.

 Akaanza kujitetea kuwa Mwakasege mimi sijatoa mimba imetoka yenyewe, bali mimi nikamuuliza jibu swali kwa nini umetoa mimba. Ilikuwa ni ngumu sana kwa yule mama kunielewa ila nikamuuliza kuwa ivi je maiti huwa inapata mimba. Akasema hapa ni kasema kwa hiyo kipi kinapata mimba ni roho au mwili wako? Na akasema ni roho kwa hiyo nikamuambia ukipata mimba nyingine tena isemeshe kuwa usitoke hadi miezi tisa itakapotimia. Tukaomba nikamuacha.

Baada ya Muda akaja akapata mimba tena na baada ya miezi miwili dalili za kutoka mimba zikaanza tena na akaanza kutatufuta kila mahali na Mungu alituficha kila akija mahali tulipo anatukosa mara utasikia tumeondoka na kwenda mahali pengine. Baada ya kutukosa akarudi kwake na kuanza kusoma yale tuliyomfundisha. Na alipoanza kikiri ile mistari mara ile hali ikakoma na akapata mtoto wa kwanza na wa pili na wa tatu …. Ooh haleluya haleluya.

 Hapa nataka uone jinsi Mungu alivyomfundisha Imani na hakika Mungu alimsaidia. Jifunze sana juu ya kutumia mamlaka ambazo Mungu ametupa.

📖Kutoka 10:21-23 21Kisha BWANA akamwambia Musa, “Nyosha mkono wako kuelekea angani ili giza litande katika nchi ya Misri, giza ambalo watu wanaweza kulipapasa na kulihisi.’’ 22Kwa hiyo Musa akaunyosha mkono wake kuelekea angani, na giza nene likafunika pote katika nchi ya Misri kwa muda wa siku tatu. 23Hakuna mtu ye yote aliyeweza kumwona mwenzake, wala kuondoka mahali alipokuwa kwa muda wa siku tatu. Lakini Wasraeli wote walikuwa na mwanga katika maeneo yao waliyokuwa wanaishi
Hapa tunaona wana wa Israel wakiwa na Nuru na Wamisri wakiwa na giza na ili uelewe vizuri mamlaka hii aliyoitumia Musa kuingilia mfumo wa Nuru inabidi uone kilichoandikwa kwenye kitabu cha

📖 Mwanzo 1:14-15 ‘’ Mungu akasema, “Iwepo mianga kwenye nafasi ya anga ili itenganishe mchana na usiku, nayo iwe alama ya kutambulisha majira mbali mbali, siku na miaka, 15nayo iwe ndiyo mianga kwenye nafasi ya anga itoe nuru juu ya dunia.’’

👉🏼Ikawa hivyo
Kazi ya Jua ni kutawala mchana na mwezi utawale usiku. Lakini Musa alipewa mamlaka ya kuweza kuingilia mfumo wa jua na kukata  mwanga wa wamisri  na kuweka mwanga kwa wana wa Israel.

 Yaani ina maana wamisri walikuwa hata wakiwa na taa zilikuwa hazitoi mwanga. Suala la giza na nuru kabla halijawa suala la kimwili limekuwa suala la kwanza kabisa katika ulimwengu wa roho.

👉🏼Chanzo cha kusoma haya ni kutokana na hali iliyokuwa ikinusumbua sana ya mvua kunyesha kila mahali ukiweka hema hii ya kwetu mvua ilikuwa inaanza kunyesha  au hata me mwenyewe nikenda mahali utakuta mvua tu inaaanza hata kama sio majira yake. Ndio nikaanza kutafuta majibu kwenye biblia.  Na ndipo Mungu aliponifundisha namna ya kuingilia majira na  namna ya kuidhibiti mvua.

☀MFANO WA MOROGORO.

Nakumbuka mwaka mmoja tulikuwa tunaandaa semina ya Morogoro na nikawauliza wenyeji wakasema mvua kwa sasa imeisha na tukapeleka hema na sku ile tunafunga hema mvua kubwa ikawa inanyesha na wenzutu walijenga hema katikati ya mvua na semina nayo ilianza kwenye mvua kama siku tatu ivi mvua ilikuwa inanyesha na watu walikuwa wanakuja wengi na miamvuli. Hapo nikaona sasa hii mvua itatuharibia utaratibu  na utulivu nikaomba Mungu mvua ile iache kunyesha hadi tutakopamaliza semina. Na nilikuwa nakaa kwenye hoteli karibu na milima ya uluguru. Na mvua ikaanza kunyesha milimani nilikuwa nainyoshea kidole kuwa ewe mvua usije huku mjini hadi nimalize semina. Na baada ya hapo unaona wingu linaondoka na mvua inakoma kabisa.


Basi siku ile ya mwisho tunamaliza semina nikawaambia wakazi wa Morogoro kuwa samahani jamani nilimaisha mvua ili tuwe na semina ila kuanzia kesho saa kumi mvua itarudi (baada ya kuwaambia wenzangu kuwa hema litaanuliwa kabla ya saa kumi na kuweka kwenye gari tayari kwa safari). Basi mtu mmoja alisema haya anayoyasema yakitokea me ntaokoka.

Baada ya saa kumaliza semina ile kesho yake tulimtembelea mtu mmoja Morogoro tukawa tunamsalimia na ilipofika saa kumi baada ya kuwasiliana na wenzangu kuwa hema na ila kitu tayari wamepakia kwenye lori la kwetu  na manyunyu ya mvua yakaanza taratibu, na mkwe wangu akanikumbusha kuwa tuliiambia mvua inyeshe kuanzia saa kumi na kuendelea sisi kukaa pale ile tulikuwa tunaizuia ile mvua.

 Basi tukaaga na tulipoanza kuondoka maana tulikuwa tunaenda Dar es Salaam kwa gari. Mvua kubwa ilinyesha Morogoro usiku kucha  na kesh yake ikaendelea kusnyesha na kunyesha. Watu wakampigia simu mwenyekiti wa kamati ya kwetu Morogoro ya kuwa tunaomba Mwambie mwakasege aisimamishe mvua sasa maana inatosha sasa.  Oooh haleluya haleluya…..


Hii ni mamlaka ambayo Mungu anakupa  lazima unajua kuwa ni mamlaka ya ulimwengu wa roho na inahitaji hekima sana kuitumia na usiitumie wewe utakavyo maana utaanza kuleta usumbufu kwa watu wengine.

🎆MAMLAKA JUU YA MFUMO WA SHETANI.
Waefeso 6:12 ‘’ 12Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Waefeso 3:8-11 ’’ 8Ingawa mimi ni mdogo kuliko aliye mdogo kabisa miongoni mwa watakatifu wote, nilipewa neema hii ili niwahubirie watu Mataifa kuhusu utajiri usiopimika ulio ndani ya Kristo na 9kuweka wazi kwa kila mtu jinsi ile siri iliyokuwa imefichwa kwa nyakati zote katika Mungu aliyeumba vitu vyote. 10Ili kwa njia ya Kanisa, hekima yote ya Mungu ipate kujulikana kwa watawala na WENYE MAMLAKA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO, 11SAWASAWA NA KUSUDI LAKE LA MILELE KATIKA KRISTO YESU BWANA WETU. 12YEYE AMBAYE NDANI YAKE NA KWA NJIA YA IMANI KATIKA YEYE TUWEZE KUMKARIBIA MUNGU KWA UJASIRI NA KWA UHURU. 13Kwa hiyo, nawaomba msikate tamaa kwa sababu ya mateso yangu kwa ajili yenu, hayo ni utukufu wenu.
Kwa hiyo ile kuwa na mamlaka juu ya mfumo wa shetani haitoshi bali inahitajika pia kujua mamlaka juu ya mfuno wa utawala wa wanadamu.

 Angalia Waefeso 1:20 utaona neno katika Ulimwengu wa roho juu sana kuliko falme na mamlaka na kila jina litajwalo. Mungu katuweka juu sana juu ya mamlaka juu ya ufalme wa Shetani na ufalme wa Wanadamu. Hivyo ni muhimu sana kuwa na maarifa ya kushughulika na watu na mifumo yao ya kiutalawa.

🙇🏼MAMLAKA JUU YA KILA FIKRA.
   2Wakorintho 10:3-5  ‘’ 3Ingawa tunaishi duniani lakini hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo. 4Silaha za vita vyetu si za mwili, Bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome. 5Tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo.
Hapa tunaona kuwa hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili bali tunafanya kwa jinsi ya rohoni na tukiangusha mawazo na kila fikra isiyo mtii kristo na ipate kumtii kristo. Na kila kijiinuacho juu ya Elimu ya Mungu nacho kipate kumtii Mungu.
👇👇

Twende kwa Yesu tukawaangalie wanafunzi wawili yaani Yuda na Petro. Yuda alikuwa  ni mpole sana na Petro kwa lugha ya sasa tungesema alikwa na kiherehere sana au msemaji sana. Petro aliposikia habari za Yesu kwenda msalabani alimwita na akaanza kumkemea na kumwambia rudi nyuma ewe shetani kwa sababu huwazi ya Mungu. Yesu alikuwa anamwambia petro umeside/ umeingiliwa na shetani saa ngapi. Bila Yesu kumkemea shetani lile pepo lingeendelea kumsumbua sana Petro. Hii ilitokana na Shetani kuomba kibali kuwa anataka awapepete kama ngano na Yesu akamwambia Petro shetani ameomba kibali ili awapepete kama ngano lakini mimi Yesu nimekuombea ili utakapoongoka uwaimarishe na dnugu zako.

Yesu alipokuwa anazungumza na wanafuzni wake kuwa watamkibia na kumkataa ila Petro alisema mimi sitaweza, Yesu alimwambia kuwa Petro utanikana Mara tatu na Petro alimkana Yesu mara tatu na mara ya  tatu alinaani kabisa. Ina maana alikuwa maejitoa kwenye uanafunzi wa Yesu.

Ndio maana Yesu alipofufuka aliwaambia waambieni wanafunzi wangu na Petro ile neno Na Petro ina maana petro hakuwa mwanafunzi tena. Na ndio maana Yesu alipokuwa nazngumza nao alimwambia Petro mata tatu kuwa je wanipenda, hii ilikuwa ni kumsaidia Petro maan aalimkana Yesu mara tatu.

MFANO. Wangapi hapa wanajua kuendesha baiskeli, 🚲na je unaweza kuacha kuandesha baiskeli, jibu ni hapana. Maana yake ni kuwa kitu kimeingia kwenye mfumo wako wa fahamu na halitoki. Hata kama haumkumbuki aliyekufundisha kuendesha baiskeli ila hautakauja ushahau kuendesha baiskeli.
Kwa hiyo kumkemea pepo tu haitoshi maana huwezi jua kuwa ni kitu gani kaweka kwenye fikra za mu huyo. Hivyo pia kuomba matengenezo kutoka kwa Mungu juu ya mtu ambaye umekea lile pepo limtoke ili mfumo wake wa fikra urudi kama Mungu alivyoagiza.

📖Luka 22:1-6  Hapa tunaona Shetani akimwingia Yuda na kumfanya amsaliti Yesu, na Yuda aliwaambia wakuu wa makuhani kuwa yeye ndiye aliyekuwa karibu sana na Yesu  na akawapa na mbinu za namna ya kumkamata na jinsi atavyofanikisha ndipo akapewa rushwa ya vipande thelathini vya fedha.
Shetani nae alikamata fikra za Yuda hadi hukumu ilipoingia ndani ya Yuda na aksahau hadi kumwamini MUngu ili kuwa anawezakumsamehe maana Mungu anasema dhambi yako ijapokuwa nyekundu kama damu itakuwa nyeupe kama theluji, ila Yuda alisahauna hadi akajinyonga. Hata kama umemkosea Mungu namna gani rudi kwa Mungu na Mungu atakusamehe, usiogope rudi kwa Bwana maana huko  kwingine hakuna msaada na usije fanya maamuzi kama Yuda, Njoo kwa Yesu ndio maana alikufia msalabali rudi rudi kwa Bwana.

👉🏼Elimu ni suala la kiroho kabla halijawa la kimwili na ona maarifa ambayo watu wanapewa baada ya Muda utakuja kuona watu wanaanza kujitenga na Yesu na kuanza kukaa mbali na uso wa Mungu. Kwa hiyo ni muhimu sana kuombea elimu ambazo watu wanapewa ili ziwe za Elimu ya Mungu na sio zingine maana shetani nae ana elimu yake inayomnfanya amkatae Mungu.
Ili kujinaua hapo mahali Fanya maombi ya aina tatu.
👇👇
1: OMBA KWA MUNGU MACHO YAKO YATIWE NURU.
Waefeso1:17-23  ndio maana Paulo aliwaombea watu wa efeso japo walikuwa wameokoka lakini aliwaombea maombi haya. Na mimi ni sala yangu  ya kila siku huwa najiombe maombi haya mara kwa mara.na wewe chukua sala hii ni ya kwako jiombee kila siku  kila siku na iwe ni utaratibu wa maisha yako ya kila siku
👇👇
2: OMBA MUNGU AKUPE KUTAFSIRI KWA JINSI YA ROHONI KWA MANENO YA ROHONI.
1Wakorintho 10:10-14  na Waebrania 11:3 Kwa Imani twafahamu  kuwa ulimwengu uliumbwa kwa vitu visivyooneka, na katika warumi 10:17 imani huja kwa kusikia na katika ulimwengu war oho inatupa kufahamu.
👇👇
3: OMBA MUNGU AKUSAIDIE KUKUA KIROHO.
Wagalatia 4:1-2 Lakini nalisema nanyi kama watoto. Mrithi ajapokuwa mtoto huwa kama mtu hadi pale wakati ule ulioamriwa na Bwana wake. Kwa hiyo lazima ukue kiroho ili ukue kiroho na ndipo vitu vingine utaweza kuvitumia.
Mfano: Ukiwa na mtoto wako mwenye miaka 10 ukamnunulia gari na ukampa kuwa uwe ni urithi wake, hata kama anajua kuendesha sharia ya nchi haimruhusu kuanza kuendesha gari kwa sababu hajatimiza miaka 18. Kwa hiyo ukubwa (ukomavu) ni muhimu sana katika ulimwengu wa roho.

☀Jiombee sana sana maombi haya, na usiseme ntasubiri sema hii iishe ndio nianze kuifanyia kazi. Bali nakushauri anza sasa kuitendea kazi usiache semina hili lipite bure.

Itaendelea kesho..

NAKUPENDA NDIO CHAGUO LA GK KUTOKA KWA THE WORSHIPPERZ ARUSHA

$
0
0


Katika chaguo la GK hii leo tupo jijini Arusha ambako tunakutana na moja ya kundi linalozidi kushika kasi katika medani ya kumwinua Mwokozi wa ulimwengu. Kundi hili si lingine bali ni The Worshipperz wakiongozwa na mwimbaji nguli wa injili nchini Peter Abednego ambaye amejulikana zaidi kwa huduma yake akiwa na kundi zima la New Life Band nayo ya jijini humo.

Kutoka kwao tumekuchagulia wimbo "Nakupenda" natumaini wimbo huu utafanyika baraka katika maisha yako. Uwe na jumapili njema


SOMO: JANGWA HALITANIZUIA - MCHUNGAJI KILIMA

$
0
0


SOMO: JANGWA HALITANIZUIA
Mchungaji John Kilima

Kutoka 14:3…Nae Farao akasema katika habari za wana wa Israeli wametatanishwa katikati ile jangwa imewazuia wasitoke…….
- Kuna jambo laweza kumpata mtu.lakini hata kama likimpata, jibu lipo mahali hapa penye madhabahu halisi ya Mungu YEHOVA.
- Luka 9:11…
- Mungu anakutana na watu wenye haja ya kuponywa/wanaohitaji kuhudumiwa,Mungu ni Mungu wa ahadi hivyo anavyoahidi jambo ni lazima alitimize.
-Mungu anaweza kukuvusha mapema ila amekuacha ili ajitwalie utukufu,Mungu huwa anajifanya kama siye ili ajitwalie utukufu.
-Jangwa na kukataliwa,kukosa fedha kusemwa vibaya na kuteswa Mungu hurusu si kwa lengo la kukuangamiza bali likufikishe katika hatima yako ,Mungu huwa anaruhu Mashetani kutengeneza Jangwa katika Maisha yako ili ukitoka uwe kama dhahabu safi.Mungu huwa anaonekana katika Jangwa,magonjwa n.k, Mungu alimtokea Musa akiwa Jangwani haikuwa nyumbani kwa Yethro wala kwa Mfalme,Ukitaka Mungu akutumikie huna budi kupita jangwani bila kukwepa.
- Kama hukupita Jangwani ukikutana na mlima hutovuka,lile Jangwa lililotengenezwa ukivuka ndilo litakalokufikisha kwenye hatma yako.
- Kusudi la Mungu kukupitisha /kukuweka Jangwani ni ili uwe vizuri maana hata kama ulikuwa huombi ila ukiwa Jangwani lazima utaomba tu,Pia utajua thamani ya wokovu ulio nao ,hivyo huwezi kuchezea wokovu.
- Kwa nini tunavaa siraha –Ili kuweza kushindana wakati wa uwovu Ukiwa na ndoto Mungu anakuwa na mpango na wewe mfano Yusuph.
Mwanzo 28:15..Na tazama mimi nipo pamoja nawe nitakurinda kila uendako name ntakuleta tenna mpaka nchi hii kwa maana sitakuachaa hata nitakapo kufanyia hayo niliyokuambia.
- Wakati Mwingine si kama tunaelewa tunakoenda bali tunamuamini Mungu,kama Musa alivyokuwa akifuatwa na Faroa na Majeshi yake, mbele Bahari, na Pembeni mlima akawaambia wana wa Israel wasiogope,Bwana atawapigania nao watanyamaza kimya japo Moyoni aliwaza mbona Bwana amemruhusu Farao awafuate?,Mungu akamwambia Musa awaambie wana wa Israel waendelee mbele.

-Kila mtu ana Farao wa Maisha yake ila cha msingi hatupaswi kuogopa maana hawawezi kutudhuru,kwa sababu uhai wetu umefichwa ndani ya Kristo.
-Ili ushinde kesho lazima ushindane ufanye vita leo
Yohana 1:19-25….Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, wayahudi walipotumwa kwakemakuhani walawi kutoka yerusalemu illi wamuulize wewe u nani?....23..Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani inyoosheni njia ya Bwana kama vile alivyonena nabii Isaya.
- Mtu aliyepita katika Jangwa akitamka kitu kinakua,Yohana alisema Yeye ni sauti ya mtu aliaye nyikani,inamaana amepita jangwani hivyo yeye ni mzoefu wa jangwa,
-Lengo la Jangwa ni kukutengeneza na sio kukuangamiza mtu aweza kugeuka na kuwa jangwa(mtesi)
Jangwa haliwezi kumzuia mtu aliyetumwa na Bwana.
Torati 8:1..Amri hii ninayokuamuru leo hii mtaishika kuitenda mpate kuishi na kuongezeka na kuingia katika nchi ile amabayo Bwana aliwaapia Baba zenu nanyi mtaimiliki..2..Nawe utaikumbuka njia ile yote Bwana Mungu wako aliokuongoza miaka hii arobaini katika Jangwa ili akutweze kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake au sivyo.
- Mungu huwa anaruhusu jangwa lije kwako ili aone je! utaendelea kumpenda kuzishika amri na sheria za Mungu?
Hata kama tatizo ulilonao ni kubwa namna gani cha kukumbuka ni kwamba Mungu ndie mkubwa kuliko tatizo Lako.
Maombolezo 3:33…Maana Moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu wala kuwahuzunisha.
- Alivyokupeleka Jangwani si kwa lengo la kukutesa laa ni kwa lengo la kukujenga,kiimani juu ya kumuamini yeye.
- Waamuzi 4:1
- Kutoka 15:1-20…
- Unapopita katika jangwa si wakati wa kulalamika bali ni wakati wa kuomba na kusonga mbele kwa Jina la YESU.
UKIRI
- Kila jangwa lililoachiliwa juu ya maisha yangu haliwezi kunizuia,Jangwa la mikosi,kuachwa,umaskini nakutangazia hutanizuia kwa jina la Yesu

- Kuna magonjwa mengine hutokea wala si kwa sababu Mungu ameiruhusu,ila ni kwa sababu umefungua Mlango,Imeandikwa wala usimpe Ibilisi nafasi,Majangwa haya huwa yanang’ang’ania sana,Maadamu umekuja nyumbani mwa Bwana Kila jangwa lazima ling’oke sababu tumepewa mamlaka/uwezo wa kung’oa kila kisichopandwa na Mungu.

INFORMATION AND MEDIA MINISTRY
UFUFUO NA UZIMA TANGA

SOMO: VITU VITAKAVYOKUWEZESHA UITUMIE IPASAVYO MAMLAKA ULIYOPEWA NA MUNGU - MWAL MWAKASEGE

$
0
0


SEMINA YA NENO LA MUNGU..
VITU VITAKAVYOKUWEZESHA UITUMIE IPASAVYO MAMLAKA ULIYOPEWA NA MUNGU.
NA MWL MWAKASEGE
ARUSHA MJINI UWANJA WA RELI

Kusoma sehemu iliyopita BONYEZA HAPA
                                                   


Marko 11: 27-28 ‘’ 27Wakafika tena Yerusalemu, wakati Yesu akitembea hekaluni, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria pamoja na wazee wakamjia.

28Wakamwuliza, “UNAFANYA MAMBO HAYA KWA MAMLAKA GANI? Naye ni nani aliyekupa MAMLAKA YA KUFANYA HAYO?

Kuna kiwango cha maisha ambacho huwezi kufikia kama hujajua kutembea ndani ya mamlaka uliyopewa na Yesu.Jana tuliangalia mamlaka ambazo Mungu kazitoa kwa ajili yetu.Mwanza 1:28 neno akawabarikia maana yake ni akawapa vitu ndani mwao ili wawe na uwezo wa kufikia kiwango ambacho Mungu anataka wafikie.

Ndio maana aliwapa Baraka ya kuwa zaeni. Lakini kuna baadhi ya nchi wameweka sheria kuwa wasizae mtoto zaidi ya mmoja ina maana Mungu ameondoa Baraka zake katika uzazi.Baraka maana yake ni kukuwezesha kufikia viwango ambavyo Mungu anataka uwe navyo.

2 POINTI YA 2: KUJUA KUWA MAMLAKA NA MATUMIZI YAKE NI JAMBO LA KISHERIA 2..

Na sheria yenyewe ipo kwenye ulimwengu wa roho. Na hapa tunaona mamlaka ya kutawala wamepewa Adamu katika sura ya kwanza ya kitabu cha mwanzo muda huo ambapo walikuwa ni roho tu. Kwa hiyo hili jambo la sheria ni jambo la kiroho kwanza kabla halijawa la kimwili.

*SHERIA NA MAMLAKA VINAFANYA KAZI KWA KUSHIRIKIANA

Mimi nimesoma sheria ya biblia japo sheria ya kawaida sijasoma ila ya kwenye biblia ndio nimeisoma vizuri sana. Sheria imetoka kwenye biblia japo kuna mambo ambayo yanaingilia na hii sheria ya kawaida. Na jua hili suala la kuwa hakuna mamlaka bila sheria na hakuna sheria bila mamlaka. Na sheria bila mamlaka haina nguvu na mamlaka bila sheria haina nguvu. Ukitaka kubadilisha sheria lazima kwanza ubadillishe mamlaka na ukitaka kubadilisha mamlaka badilisha sheria.

📖

Daniel 7:25 ‘’25Atanena maneno kinyume cha Aliye Juu Sana na kuwaonea watakatifu wake Yeye Aliye Juu Sana, huku akijaribu kubadili majira pamoja na sheria. Watakatifu watatiwa chini ya mamlaka yake kwa wakati, nyakati mbili na nusu wakati’’.

Kwa hiyo ukiangalia mistari hiyo utaona kuwa ili kuweza kuwabana watakatifu iliwapasa kubadili majira na sheria kwa lengo la kudhoofisha na kuua nguvu za watakatifu.

Hili neno kwa Nyakati mbili na nusu ina maana kuwa ni kipindi Fulani ambacho kuna kitu wanataka kupitisha kwa ajili kuwafunga watakatifu. Na kuwafanya wawe dhaifu kwenye majira na sheria. Ukitaka kuwadhoofisha watu badilisha majira na sheria.

Ukiamua kusimamia sheria ya Bwana shetani atawinda ili aweze kukudhoofisha ili ushindwe kushughulika na sheria ambazo Mungu amekupa.

SHERIA. Ni utaratibu unaotengeneza mfumo wa mwelekeo wa maisha chini ya mamlaka husika iwe ni nchi au taifa. Lakini kwa wakati wa sasa kuna sheria za kimataifa na pia kuna mahakama ya kimataifa ili iweze kusimamia sheria.

Kumbuka hili siku zote kuwa sheria bila mamlaka inakuwa haina nguvu na ili mamlaka iwe na nguvu lazima iwepo sheria ya kusimamia na ili sheria iwe na nguvu lazima iwepo mamlaka ya kusimamia sheria. Kwa mfano chombo cha kusimamia sheria ni mahakama. Kwa hiyo mahakama bila sheria haina mamlaka na mahakama haina nguvu pasipo sheria. Tuko pamoja mpaka hapo?

Nakumbuka kuna mtu mmoja alisema biblia ni kitabu cha sheria, au unaweza sema biblia ni kitabu cha kuongoza utaratibu wa maisha ya mwanadamu kama Mungu anavyotaka.

☀MFUMO UNAONGOZA SHERIA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO NI MAMLAKA YA KIUTAWALA NI YA KIFALME.

Kwa hiyo ukitaka kuimarisha mamlaka lazima utafute sheria zinazosimamia hiyo mamlaka.

Daniel 2:27-45. Hapa tunaona habari za Nebukadreza na ndoto yake. Na kuanzia mstari wa 27-30 tunaona Daniel akitoa maana ya ndoto ya mfalme Nebukadreza na ilikuwa ni hakika Mungu ataithibitisha ile ndoto.

Katika hali ya kawaida ambayo Mungua aliumba ulimwengu uliumbwa ili uendeshwe kwa mfumo wa Kifalme na sio Kidemokrasia. Japo kuna sheria za mifumo yote hii miwili ila Mungu aliumba ulimwengu kwa mfumo wa kifalme.

Waefeso 6:12 Kwa maana kushindana kwetu si juu ya damu na nyama bali ni juu ya falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho. Kwa hiyo tunaona katika ulimwengu war oho tunapambana na falme maana hakuna demokrasia kule.

Daniel 7:21-22, 25-27.’’

21Nilipoendelea kutazama, pembe hii ilikuwa inapigana vita dhidi ya watakatifu na kuwashinda, 22mpaka huyo MZEE WA SIKU (YESU) alipokuja na kutamka hukumu kwa kuwapa ushindi watakatifu wa Yeye Aliye Juu Sana, na wakati ukawadia walipomiliki ufalme.

’25Atanena maneno kinyume cha Aliye Juu Sana na kuwaonea watakatifu wake Yeye Aliye Juu Sana, huku akijaribu kubadili majira pamoja na sheria. Watakatifu watatiwa chini ya mamlaka yake kwa wakati, nyakati mbili na nusu wakati’’. 26‘ “Lakini ndipo mahakama itakapokaa kuhukumu, nayo mamlaka yake yataondolewa na kuangamizwa kabisa milele. 27Ndipo ufalme, mamlaka na ukuu wa falme chini ya mbingu yote utakabidhiwa kwa watakatifu, watu wa Yeye Aliye Juu Sana. Ufalme wake utakuwa ufalme wa milele, nao watawala wote watamwabudu na kumtii Yeye.’

Umeona hapo , Shetani akivuruga majira anavuruga na sheria na mwisho anavuruga na hukumu.Lakini hukumu itawekwa nao watamwondolea shetani mamlaka katika ulimwengu wa roho.

Kwa jinsi Mungu alivyomuweka alikuwa Bwana Jela kwa wana wa Israel ndio maana kiti chake kilikuwa na pingu na alitakiwa kuwafunga wana wa Israel hadi Muda utakapowadia. Ndio maana Nebukadreza alipokiuka maadili ya kazi yake ambayo Mungu alimpa ilibidi aondolewe kwenye nafasi yake Mungu alimwambia hukumu hii imekuja kwa kwa amri ya walinzi ambao ndio walikuwa waombaji. Na alisema atarudishwa mpaka atakapokumbuka kuwa mbingu ndio zinazotawala. Lakini mtoa amri ni mlinzi yaani mwamboji ndio maana Yesu alisema nimeweka walinzi juu ya kuta zako ee Yerusalemu ambao hawatanyamaza mchana wala usiku.

☀SHERIA NA MAJIRA VINA UWEZO WA KUIMARISHA NA KUDHOOFISHA MAMLAKA.

Mungu aliweka nyakati na ndipo akamuweka mwanadamu ili aweze kuishi kwa kadri nyakati zile zilivyowekwa.

👉🏼Ndio maana mtu aakikuibia muda anakuwa kakuibia muda maisha, na mtu akikupotezea muda ina maana anakupotezea muda.

Majira na nyakati zinaenda pamoja na ndio maana utasikia huku mjini watu wakisema sheria imepitwa na wakati kwa hiyo inapaswa kuwa kila majira yakibadilika nayo sheria inapaswa ibadilike ili kuweza kuendana na wakati uliopo. Biblia peke yake ndio sheria zake hazibadiliki kabisa.

👉🏼POINT 3: UIMARA WA MAMLAKA YAKO HAOA DUNIANI INATEGEMEA UNAAMINI NA UNAJUA KWA KIWANGO GANI KUWA MBINGU NDIZO ZINAZOTAWALA.

Daniel 7:26-27 na Daniel 4:26 ‘’ naye humtawaza ye yote amtakaye. 26Amri ya kuacha kisiki pamoja na mizizi yake inamaanisha kwamba ufalme wako utarejezwa kwako utakapokubali kwamba👉🏼 MBINGU NDIZO ZITAWALAZO.’’ Na Kumbuka kuwa MBINGU NI KITI CHA ENZI CHA MUNGU.

Ayubu 38:33 ‘’ 33Je, unajua sheria zinazotawala mbingu? Waweza kuweka utawala wa Mungu duniani?.

Kwa hiyo ili umjue Mungu vizuri zijue sheria zake.

Ukitaka kuijua biashara vizuri zijue sheria za biashara vizuri.

Ukitaka kilimo vizuri jua sheria za kilimo. Kwa mfano kuna baadhi ya mazao yamewekewa sheria hata kama kama ni ya kwako hairuhusiwi kung’oa. Mfano chai uking’oa chai hata kama ni ya kwako hairuhusiwi. Na uking’oa unashtakiwa kwa mujibu wa sheria.


👉🏼POINT 4: UWEZO WA MUNGU NA MAMLAKA YA MUNGU INATAKIWA IFANYE KAZI KWA SHERIA YA NENO LA MUNGU.

Luka 9:1-2 ‘’Yesu akiisha kuwaita wale kumi na wawili pamoja, aliwapa MAMALAKA NA UWEZO wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya magonjwa yote, 2kisha akawatuma waende wakahubiri UFALME WA MUNGU na kuponya wagonjwa’’

Kwa hiyo ina maana ukipewa uwezo na mamlaka na ufalme wa Mungu unakuwa tayari upo. Kwa sababu hakuna mamlaka isiyokuwa chini ya Mungu.




📖Mathayo 12:28-29 ‘’ 28Lakini kama Mimi ninatoa pepo wachafu kwa Roho wa Mungu, basi Ufalme wa Mungu umekuja juu yenu.

29“Au tena, mtu awezaje kuingia katika nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuteka nyara mali zake asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Akiisha mfunga, ndipo hakika anaweza kuteka nyara mali zake.


👇👇

Umeelewa hapo Yesu alipokuwa na mamlaka ya kutoa pepo na alipokuwa anatoa pepo ina maana alikuwa naleta na ufalame wa Mungu. Na ndio maana alisema ‘’ mtu awezaje kuingia katika nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuteka nyara mali zake asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Akiisha mfunga, ndipo hakika anaweza kuteka nyara mali zake’. Kwa hiyo ujio wa Yesu ulikuwa chini ya sheria ambayo ilisimamiwa na mamlaka ya mbinguni.

👇

Kumbuka kuwa mamlaka ni uwezo wa kisheria wa kuta amri na kusimamia kile ilicho amuru. Kwa mfano niliulize swali je mkuu wa wilaya anaweza mfukuza kazi mkuu wa mkoa?

👉🏼 ’ukweli ni kuwa anaweza fanya hivyo ila hana uwezo huo na mamlaka ya kusimamia utekelezaji wake mpaka mamlaka nyingine ambayo ndiyo inaweza kuwa na nguvu za kumfukuza kazi.

Pia angalia mfano wa wana wa skewa katika




📖 Matendo Ya Mitume 19:11-17.

Wana wa skewa walikuwa wapunga pepo na walijua kuwa Paulo alikuwa nauwezo juu yao nao wakasema isiwe tabu nao wafanye kama Paulo. Na wakamwambia yule mtu mwenye pepo kwa jina la Yesu anayehubiriwa na Paulo mtoke huyu. Yule pepo alisema kuwa Paulo namfahamu na Yesu namfahamu nyie ni nani? Hili lilikuwa ni swali lakisheria.

👇👇

Fahamu sana hii siri itakusaidia. Kwa mfano Raisi popote alipo analindwa sana , usisikie tu Obama yuko mtaani au dukani kununua vitu kama wegine hapo ujue hayuko peke yake alia na walinzi wengi hata kama huwaoni. Pia ulinzi wa Mtu unategema sana nafasi aliyonayo huyo mtu.

👇👇

Soma Isaya 49:24,’’ 24Je, nyara zaweza kuchukuliwa kutoka kwa mashujaa wa vita, au mateka kuokolewa kutoka kwa watu wakali?.. Je aliye hodari aweza kuokolewa na mateka yake.

📖

Matendo 10 :38 ‘’ 38Jinsi Mungu alivyomtia Yesu wa Nazareti mafuta katika Roho Mtakatifu na jinsi Shetani, kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye.

Kwa hiyo lazima ucheki katika kuwa ni sheria ipi ambayo inaweza kuwafungua wafungwa halali? Ndio maana kasema mateka yake maana si wote waliofungwa kuwa wameonewa na shetani.


☀KUWAFUNGUA WATU WALIOMILIKIWA NA FALME MBILI KWA WAKATI MMOJA.

Wakorintho 5: 4-5 4Mnapokutana katika Jina la Bwana wetu Yesu nami nikiwepo pamoja nanyi katika roho na uweza wa Bwana Yesu ukiwepo, 5mkabidhini mtu huyu kwa Shetani, ili asili ya dhambi iangamizwe lakini roho yake iokolewe katika siku ya Bwana,’’

👇👇

Mtu huyu alikabidhiwa kwa Shetani mwili wake na roho yake ikakbidhiwa na Yesu na Yesu alikuwepo je mtu huyu unamfunguaje sasa.

Kwa hiyo ili kumsaidia mtu huyu inakupasa ujue mamlaka na sheria ili ujue cha kufanya.


🙇🏼KAZI YA SHERIA.

Sheria zote zilshatungwa na Mungu. Na katika ulimwengu wa Roho kuna sheria kuu mbili tu.

👇👇

1: SHERIA YA UZIMA.

2: SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI.

Shetani hawajawahi kutunga sheria yoyote na wala hata ufalme wake ni wa kucopy.na anachofanya shetani anajua kuitumia sheria ya dhambi na mauti.

👇

Na sasa ili kumshinda inahitaji maarifa maana biblia inasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa na sio kwamba shetani yupo. Ndio maana Yesu leo kakuletea maarifa haya ili ujue namna na kumshida shetani.

📖

Wagalatia 3:24.24Hivyo, sheria ilikuwa kiongozi kutufikisha kwa Kristo, ili tupate tuhesabiwa haki kwa Imani.

Kazi kuu ya sheria ni kutuleta kwa KristoChunguza sheria zilizoko huko uliko au ni kazini au kanisani au mahali popote. Je inakuleta kwa kristo au inakupeka mbali na Mungu. Ndio maana biblia inasema pasipo maono watu huacha kuziuia ila anaheri mtu yule anayetii sheria.

Ukitaka kuona nchi inataka ikupeleke wapi cheki sheria/katiba ya nchi hiyo.




Itaendelea kesho

MWANACHUO MTANZANIA ASULUBIWA NA KUCHOMEWA GARI NCHINI INDIA

$
0
0
Mabaki ya gari alilokuwa akiendesha Mtanzania ©DailyO
Mtanzania mmoja aishie India, amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kushambuliwa na kuchomewa gari yake, kisha kutembezwa uchi, kama adhabu ya kosa lililofanywa na muafrika mwenzake kutoka Sudan.

Tukio hilo ambalo limeripotiwa kutokea Jumapili tarehe 31 January, linaelezwa kushuhudiwa na polisi huku wakishindwa kuchukua hatua yoyote kwa mujibu wa mashuhuda. Hali hii inazidi kuipa India picha mbaya, taifa ambalo pia lina ripoti mbalimbali za unyanyasaji kwa wanawake.

Mlolongo wa matukio

Mitaa ya Bangalore, ajali ya gari inatokea, ambapo gari moja ilitokuwa ikiendeshwa na mwanaume kutoka Sudan, inamgonga mtu mmoja anayetajwa kuwa na umri wa miaka 35 na kufariki papo hapo. Dakika 30 baadae, mwanadada mtanzania mwenye umri wa miaka 21 akiwa na wenzake wanne wanapita eneo la tukio ambapo wanasimamishwa na kisha kuteremshwa kwenye gari yao.

Kinachofuata ni kushambuliwa miili yao, na kisha Mtanzania huyo kuvuliwa nguo zake na kisha kutembezwa hadharani akiwa mtupu. Gari yake nayo inachomwa moto. Mtu mmoja aliyejitokeza na kumpa tshirt apate kujihifadhi, naye anashambuliwa. Ni tukio la namna yake.

Kwa mujibu wa India Today, Polisi walikuwa wameshafika eneo la tukio tayari, lakini katu hawakuthubutu kuingilia kati tukio hilo la kunyanyaswa kwa watu hao, na kwamba hata walipoenda hospitali, walikataliwa huduma. Tayari ubalozi wa Tanzania nchini humo umeripotiwa kuagiza uchunguzi kufanyika kutokana na jambo hilo.

Kwa mujibu wa DailyO ya India,  tukio hilo linachochewa na ubaguzi wa rangi nchini humo, pamoja na sababu kadha wa kadha za kisiasa.

India ni taifa lenye wanafunzi wengi kutoka Afrika, Tanzania ikiwemo, ambapo mdada aliyeshambuliwa ametajwa kuwa kimasomo nchini humo, akichukua Shahada ya Usimamizi wa Biashara, BBA.

WAZIRI MKUU KUSHUHUDIA USIMIKWAJI ASKOFU MKUU WA EAGT

$
0
0

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye tukio la kumsimika  rasmi Askofu Mkuu wa Pili wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania, Dkt. Bruno A Mwakipesile.

Tukio hilo la kihistoria ambalo linafanyika kwenye kanisa la Mlimwa West Jijini Dodoma, ambapo maadalizi ya shughuli yanaendelea huku wageni mbalimbali wakiwasili kutoka ndani na nje ya Taifa la Tanzania.

Kanisa la Evangelistic Assemblies of God linapata Askofu Mkuu wa Pili mara baada ya mwanzilishi, Askofu Mkuu Dkt. Moses Kulola kufariki dunia Agosti 2013 (bonyeza kuona picha za mazishi) Kusimikwa kwa Askofu Mkuu kutaambatana na wasaidizi wake ambao ni Makamu wake, Askofu John Mahene kutokea Bugando, Mwanza; na Katibu, Askofu Dkt. Leonard Mwizarubi kutokea Arusha.

Gospel Kitaa imeweka kambi kwenye Jiji hili ili kukupatia kila kinachojiri mwanzo hadi mwisho. Zifuatazo ni picha za maandalizi ya tukio hilo.















SOMO: KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU (6 & 7) - MCHUNGAJI MADUMLA

$
0
0
Mchungaji Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe…

Kusoma sehemu iliyopita Bonyeza hapa

Karibu tuendelee kujifunza;

04.SIFA KUU ZA KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU.

Kila karama ya Roho mtakatifu ina sifa yake ya kipekee kabisa.Upekee huu unaitambulisha karama husika. Mfano sifa za karama za kusema,ni tofauti na sifa za karama za ufunuo,tena sifa hizo zinatofautiana na karama za uwezo(nguvu). Lakini katika hayo yote,zipo sifa zinazofanana ambapo kila karama ni lazima iwe na sifa hizo. Sifa hizo ni kama ifuatavyo;

Karama zote hutolewa na kusimamiwa na Roho mtakatifu.~Yeye Roho ndio atoaye karama na kuzisimamia kama apendavyo Yeye“ lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.” 1 Wakorintho 12:11

Karama zote zimejawa na ishara,ajabu na miujiza. ~Mbali na karama ya matendo ya miujiza,bali ukweli ni kwamba;kila karama imebeba miujiza kwa sababu anayepafomu ni Roho mwenyewe. Mfano ukiziangalia karama zote za Roho mtakatifu utagundua kwamba,kuna nguvu isiyo ya kawaida ya wanadamu,nguvu hii ni ishara,ajabu na miujiza kutendeka kwa nguvu hii.

Karama zote hutumia watu,na kutumika kwa watu.~ ili karama ifanye kazi yake,basi ni lazima iwe ndani ya mtu aliyepewa na Roho mtakatifu lakini pia mtu huyo mwenye karama huitaji watu ili karama yake ifanye kazi. Hakuna karama inayotenda kazi pasipo watu.

Zinafungua wale waliofungwa~Kila karama ni lazima iwaweke huru watu hata kama ni karama za lugha,karama za kufasiri lugha au karama za unabii~zote hizi na nyinginezo zinatufanya kufunguliwa. Mfano,karama za lugha,zinaweza kutufungua kiufahamu kile Mungu asemacho kwetu alikadhalika karama ya unabii. Karama za uponyaji,zinatuponya roho,nafsi na miili na yetu.

Karama zote humuinua Mungu.~Karama za Roho mtakatifu ni zile zenye kumuinua BWANA MUNGU. Sifa zote na utukufu wote huishia kwa Mungu. Ukiona mtu anajipa sifa na utukufu katika karama aliyonayo,basi ujue mtu huyo atakuwa amepungukiwa na kitu fulani kwenye karama yake. Mfano;mwenye karama ya uponyaji,aponyaye ni Mungu ndani yake,wala si yeye,hivyo haipaswi kujiinua na kujisifu. Leo shida hii imelikumba kanisa,maana wapo watu wenye kujisifu kana kwamba wanaponya wao,utakuta mtumishi amejiita majina mengi ya sifa,na hata kudiriki kusema yeye ndio Mungu aponyaye,haya ni machukizo mbele za BWANA.

Zinatenda kazi kwa wanyenyekevu na wapole wa moyo. ~Waweza kujifunza maisha ya Bwana Yesu jinsi yalivyo. Yeye ni mnyenyekevu na mpole wa moyo (Mathayo 11:29). Unyenyekevu na upole wa moyo ndio sura yenyewe ya mkristo. Mtu mwenye karama ya aina yoyote ile anapaswa kuwa mnyenyekevu yaani awe ni mtu wa kujishusha wakati wote na kukubali aibu kwa ajili ya jina la Bwana Yesu. Lakini tazama hali ilivyo leo,utakuta mtumishi hawezi kutembea na miguu ( yaani hata kwa dala dala )aendapo katika huduma,ni lazima akodiwe gari tena gari ya thamani,la kama hakuna gari basi haendi!!!

Mfano ulio hai ni huu hapa; “…mwaka fulani,nilikuwa nimeenda katika huduma huko Tukuyu (Mbeya),nilikuwa nimeambatana na baadhi ya wachungaji na waimbaji niliotoka nao huku Dar,tulipofika Tukuyu majira ya usiku kama saa mbili hivi,kisha tukapelekwa hotelini kwa mapumziko ili kesho yake tuanze huduma ya mkutano wa nje. Tukiwa hotelini,muimbaji mmoja tuliyetoka naye Dar,alikataa kulala katika hoteli ile akisema eti ile ni hoteli ya kiwango cha chini hali yeye ni muimbaji supa staa(muimbaji wa viwango vya juu). Basi,akatuacha, akaenda kulala anakukojua yeye. Akawa analalamika hata allowance ( posho ) aliyolipwa kwamba hamstahili ni ndogo mno.Hivyo akahudumu ili mradi tu,waswahili wanasema bora liende. Mtu huyu alitaraji kulipwa vizuri,ale vizuri na kulala katika hoteli za kisasa ndipo atoe huduma ya uimbaji,~Aah Anyway! Haya yote huonesha hakuna unyenyekevu kabisa yake...”

Karama hazina gharama za kulipia pesa.~ umepewa bure,toa bure.( Mathayo 10:8)

“Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema,Nipeni na mimi uwezo huu, ili kila mtu nitakayemweka mikono yangu, apokee Roho Mtakatifu. Lakini Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali.Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu.Basi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana, ili kama yamkini, usamehewe fikira hii ya moyo wako.” Matendo 8:18-22

Simoni alidhania kwamba karama inaweza kununuliwa kama bidhaa,kumbe karama ya Mungu haipatikaniki kwa mali. Hali ya namna hii hata leo ipo,tunaona baadhi ya watu wakiomba kupewa karama kwa pesa au mali zao. Utakuta mtu kanisani unapewa wadhifa fulani wa kiroho kwa sababu anapesa na mali nyingi,wengine huitwa wazee wa kanisa,wengine hata huitwa manabii,lakini ukichunguza watu hao utagundua utumishi wao ni kwa sababu ya pesa wanazotoaga. Lakini utambue kwamba sifa ya karama haipatikani kwa pesa. Wengine,watumishi wa Mungu hawafanyi maombi mpaka ulete pesa kwanza tena sio kajipesa,bali pesa ya kueleweka. Hii ni hatari sana,mtu wa namna hii kwa kweli hakutumwa na MUNGU bali amejituma yeye mwenyewe na hukumu ipo juu yake.

Karama hutegemeana~Sifa hii ni ya muhimu sana,maana haiwezekani mtu mmoja akapewa karama zote tisa. Bali kila mmoja hupewa kwa sehemu ili kufaidiana sote. “ Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.” 1 Wakorintho 12:7. Ni ajabu kumkuta mtu mmoja yeye hunena,hutafsiri lugha,hutoa unabii,kisha akawa na neno la hekima,kisha neno la maarifa,kisha akapambanua roho,tena mtu huyo huyo akawa na karama ya imani,akawa na uponyaji kisha akawa na karama za miujiza. Ukimuona mtu wa namna hiyo lazima ujiulize je inawezekana?!! Bali tumepewa karama kwa sehemu tu ili tufaidiane.

Karama yoyote ile haipatikani kwa kusomea shule~ Huwezi kusomea karama,bali karama zinatolewa na Mungu. Mfano mtu hawezi kwenda kusomea karama ya kunena kwa lugha. Au mtu hawezi kusomea karama za miujiza. Shida hii imeikumba kanisa la leo,maana wapo watu wameenda kusomea karama alafu baadae wakajiita majina mbali mbali ya karama hizo. Mfano naliona mahali fulani wanafundisha kozi ya kuwa nabii. Huwezi kusomea karama ya unabii,kisha ukawa nabii wala karama ya aina yoyote ile haisomewi. Bali mtu anaweza kuwa na karama fulani kisha akaenda shule kupanua mipaka zaidi ya karama yake katika utendaji kazi kimaarifa. Shule ni muhimu sana kwa kutoa maarifa katika ufanisi wa utendaji kazi…

06. UTAWEZAJE KUITAMBUA KARAMA YAKO?

~Ukweli ni kwamba watu wengi leo hawazitambui karama zao hali wao ni wakristo. Hali hii inawapelekea kushindwa kulijua kusudi la Mungu ndani ya maisha yao. Ikumbukwe ya kwamba,kila mmoja anakusudi maalum;hakuna aliyezaliwa bahati mbaya!Awali ya yote tujikumbushe tena; kila mkristo ana karama yake kwa kumfaidia mwingine maana sote tu viungo vya Kristo ~1 Wakorintho 12:12. Mkristo mwenye karama ni yule aliyeokoka yaani ni yule aliyempa maisha yake BWANA YESU,naye huongozwa na MUNGU.

Ikumbukwe tena; Siku ile ya wito wako pale unaokoka,Roho mtakatifu anaweka kipawa chake ndani yako,kipawa(karama) cha kutumika katika ufalme wa Mungu. Kutoka siku hiyo karama imezaliwa ndani yako,tayari kwa ajili ya kutumika. Hivyo Karama inaachiliwa na Roho mtakatifu ndani ya mtu,mara nyingine Roho anamtumia mtumishi wake. Tunaona hili kwa Paulo huko Rumi;“ Kwa maana ninatamani sana kuwaona, nipate kuwapa karama ya rohoni, ili mfanywe imara.” Warumi 1:11

“ Ila nipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo; walakini kila mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi.” 1 Wakorintho 7:7 Kile asemacho Paulo hapa,ni kwamba anatamani kila mtu akautumie uweza wa ki-Mungu uliopo ndani yake yeye mwenyewe. Huwezo huu ni kipawa cha Mungu mwenyewe kilichopo ndani yako wewe. Njia zifuatazo zinaweza kukufanya utambue karama yako;

(i) Kudumu katika mfumo wa maisha ya mafundisho na maombi~njia hii ni ya kwanza kabisa yenye kumtengeneza mtu aliyeokoka kukuulia wokovu wake. Kipindi hiki,cha mafundisho ya neno la MUNGU na maombi kinakufanya ukue kiroho maana karama inategemea ukuaji wako wa kiroho. Kukosa mafundisho ya neno la Mungu ya kina pamoja na maombi endelevu kumewafanya wengi wasiweze kutambua karama zao. Waweza kujipima wewe mwenyewe kiwango chako cha kula neno la Mungu kwa siku pamoja na maombi kikoje?,kisha jiangalie kwa mwezi,sasa;tathimini maisha yako ya wokovu kwa ujumla,kwamba yakoje? Je ni kweli umedumu katika fundisho na maombi? Utagundua kwamba si kweli,hujakaa sawa sawa kimafundisho wala maombi,na hali ikiwa ndio hivyo, basi je utatambuaje karama yako?

Karama nyingi zinavikwa kwenye maombi katika Roho. Kwa njia ya maombi,wengine uanza kunena,kupata maono,kujawa na ujasiri wa kuhubiri,kupokea nguvu ya imani (Matendo 13:2) N.K ~Maombi yanasababisha karama nyingi kujitokeza taratibu. Mfano ni huu; unaweza ukawa una imani fulani hivi,ile imani ya kawaida kabisa. Lakini kupitia maombi endelevu,gafla unajikuta ukivikwa imani isiyo kawaida,kiasi kwamba unaona mambo yatarajiwayo na hakika. Hii,sasa inavumbua karama ya imani. Wakati mwingine Roho mtakatifu anaweza akakuonesha orodha ya watu wa kuwaombea,na ukaanza kuwaombea kwa muda mrefu hivi,na kumbe Roho anamakusudi ya kukuonesha karama yako ya uponyaji iliyojificha.

Neno la MUNGU lina nafasi kubwa sana katika kuitambua karama yako. Maana vile unavyozidi kukaa ndani ya neno ndivyo ukaavyo ndani ya Yesu,naye Yesu hukaa ndani yako,hapo waweza kuomba lolote ikiwa pamoja na kuomba kufunuliwa karama yako na utatendewa~Yoh.15:7

(ii) Hakikisha unajitenga mbali na maisha ya dhambi~ Mimi ninakuambia hivi kwamba; inawezekana kukaa mbali na anasa za dunia ya leo,tena inawezekana kuishi maisha matakatifu.

Dhambi inaficha karama yako,tunaweza kuona mifano ya watu ambao walitakiwa watumike katika kuinjilisha lakini dhambi ilificha uinjilisti wao,tazama yule mwanamke msamalia aliyekutana na Yesu kisimani. Mwanamke huyu alikuwa ni mwinjilisti,lakini dhambi ikaficha karama yake. Baada ya kuonana na Yesu,tunaona akaenda kuinjilisha;

“Basi yule mwanamke akauacha mtungi wake, akaenda zake mjini, akawaambia watu, Njoni, mtazame mtu aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda. Je! Haimkini huyu kuwa ndiye Kristo?Basi wakatoka mjini, wakamwendea.” Yoh.4:28-30.Kitendo cha kuzitangaza habari za Yesu,ni kitendo cha kuinjilisha~Ona sasa,biblia inaeleza kwamba watu wa mjini baada ya kuelezwa habari za BWANA Yesu walitoka mjini na kumuendea.

Mfano mwingine waweza kuona kwa yule mtu aliyekuwa na jeshi la mapepo. Baada ya kutokwa na nguvu hizo za mapepo,alioshwa kwa neno la Bwana Yesu,kisha tunaona akienda kuhubiri habari za Bwana Yesu ndani ya miji kumi~Dekapoli ( Marko 5:1-20)

Leo hii;Wapo watu waliookoka nusu nusu kwamba Mungu kidogo dhambi kidogo tena papo hapo ukiwakuta wanaomba,maombi yao ni ya kulia kwa habari ya kutaka kuzijua karama zao. Watu hawa wamesahau kuwa,maovu yao yanawafarikisha wao na Mungu ( Isaya 59:2 ). Walokole wengi leo wameshindwa kujua karama zao sababu ya kushindwa kuishi maisha matakatifu,hii ni shida kubwa sana. Jitahidi kuepukana na maisha ya kidunia,wewe ni mwana wa Mungu.

(iii) Angalia unapenda kutumika eneo gani,yaani unapenda kufanya nini haswa katika ufalme wa Mungu. ~ Ni lazima ujihoji mwenyewe kile ambacho unapendelea kufanya katika kazi ya BWANA. Je unapenda kuimba,na ukiimba unapata bubujiko la rohoni? Au,Je unapenda kuinjilisha,unajisikia furaha ya moyoni ukilinena neno la Bwana,Au Je unapata ndoto mara kwa mara,kisha ndoto hizo zinajidhihilisha? Au Je unaona mambo ya siri ambayo wenzako hawaoni?.N.K

Vyote hivyo vinaweza vikawa vyanzo ya karama yako. Ukiona unapitia katika hali hiyo,basi ujitahidi kuomba kwanza umwambie Mungu azidi kujidhihilisha na akueleze ni nini haswa cha kufanya. Tena,ni lazima ukimbie kwa mchungaji wako na umueleze unaona nini,unaota nini,unajisikiaje ndani yako,ili mchungaji naye akusaidie katika ushauri na maombi.

(iv) Toa nafasi ya kipekee kuombewa na mtumishi wa Mungu kwa kuwekewa mikono,na umuelezee unajisikia unapenda nini katika kazi ya Bwana.~ Mtumishi wa Mungu anayo nafasi kubwa ya kuifichua karama iliyofichwa katika maombi maalum. Akiomba,Roho hushuka na kugusa moyo wako. Je umeshawahi kumueleza mtumishi wa MUNGU vile ujisikiavyo? Fanya hivyo leo,maana inawezekana wewe mwenyewe huelewi cha kufanya,basi nenda kwa mtu wa Mungu akusaidie…

ITAENDELEA…

~ Kwa huduma ya maombezi,usisite kunipigia kwa simu yangu hii;+255 655 11 11 49.

Mchungaji Gasper Madumla.

Beroya bible fellowship church(Kimara,Dar,TZ)

UBARIKIWE.

CHAGUO LA GK NI KUTOKA KWA WANA WA FURAHA GANI TOKA ST JAMES ARUSHA

$
0
0


Katika chaguo la GK kwa siku ya leo tupo jijini Arusha kwa mara nyingine, safari hii tunakupa wimbo mzuri uitwao "Sisi tumetenda dhambi" kutoka kwaya kongwe ya Upendo kutoka St. James Kaloleni Arusha ambao wanatambulika zaidi kwa jina la Furaha Gani kutokana na kazi nzuri waliyoifanya kwenye video ya kwanza iliyopewa jina hilo. Wimbo huu tuliokuchagulia unapatikana katika video yao ya pili. Hapana shaka utakubaliana nasi kwamba usharika huu wa St James umebarikiwa kuwa na kwaya nzuri ambazo zinafanyika baraka kwa watu wengi. Tunakutakia utazamaji mzuri na jumapili njema

PICHA ZA AWALI: DODOMA KULIVYOFANA TUKIO LA KUSIMIKWA KWA ASKOFU MKUU EAGT

$
0
0



Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) imekuwa na tukio kubwa na la kipekee. Marafiki wa EAGT ndani na nje ya nchi walitiririka kutoka pande zote kuhudhuria tukio la kihistoria la kusimikwa kwa Askofu Mkuu wa pili wa kanisa hilo, Dkt. Bruno A Mwakipesile pamoja na wasaidizi wake; tukio ambalo serikali imewakilishwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa.


Mashuhuda tangu awali walikuwa na shauku ya kuona mwisho wa siku utakavyokuwa, wapate kueleza historia ilivyoandikwa, Gospel Kitaa nayo ikaweka kambi. Mwandishi wetu Desideri Hotay (Dezzy) amekuandalia picha zifuatazo kutoka Dodoma.


Kusimikwa Askofu Mkuu EAGT 2016
Unaweza kutazama picha zaidi kwa kubofya hapa; https://flic.kr/s/aHskue2fGk

Ambatana nasi kwa picha na habari kamili punde.

ROSE MUHANDO RASMI TAMASHA LA PASAKA KANDA YA ZIWA

$
0
0


Mwimbaji nguli wa muziki wa Injili Afrika Mashariki, Rose Muhando amekuwa wa pili kuthibitisha kushiriki katika Tamasha la Pasaka linalotarajia mikoa ya Geita, Mwanza na Wilaya ya Kahama.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo Alex Msama Muhando ameungana na mwenzake Bonny Mwaitege ambaye alikuwa wa kwanza kuthibitisha katika tamasha hilo.

Msama alisema tamasha hilo mwaka huu linatarajia kufanyika Geita (Machi 26), Mwanza (Machi 27) na Kahama (Machi 28) ambako alitoa wito kutoa wito kwa wakazi wa mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi kufanikisha tamasha hilo.

Aidha Msama alisema dhamira ya Tamasha la Pasaka ni wenye uhitaji maalum ambao ni yatima, walemavu na wajane.

Msama alisema sababu ya kupeleka Tamasha la Pasaka mikoa ya Kanda ya ziwa ni kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa wakazi wa mikoa hiyo sambamba na kupiga vita mauaji ya walemavu wa ngozi 'albino'.

"Tunalipeleka Tamasha la Pasaka mikoa ya Kanda ya ziwa kwa sababu ya kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa wakazi wa mikoa hiyo ambayo miaka iliyopita iligubikwa na mauaji ya walemavu wa ngozi 'albino'," alisema Msama.

HOJA: TUACHE HOFU BALI TUWE TAYARI HATA KUFA

$
0
0
Askofu Sylvester Gamanywa,
Mwangalizi Mkuu, WAPO Mission International 
©ebibleteacher
Wiki hii nzima kwenye vipindi vya TUAMKE PAMOJA kupitia WAPO Radio nimewasilisha jumbe mbali mbali zenye kuwaandaa washiriki wangu kujengeka kiimani ili waweze kukabiliana na changamoto za kiimani zinazotukabili kila siku. Sehemu ya jumbe hizo ni pamoja na kujitahidi kupambana na hofu pale tunapokabiliana na vitisho na badala yake tuwe tayari hata kufa kuliko kiikana imani kwa kuogopa kufa:

Kupiga yowe kwa hofu

“Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu. Mara Yesu alinena, akawaambia, jipeni moyo ni mimi; msiogope.”(MT.14:26-27)

Yowe maana yake ni “kilio cha hali ya juu sana, hasa kwa kuomba msaada.”! Hofu inapomwingia mtu haina jambo la matumaini, ila ni vitisho vya maumivu makali na mauti. Na nafsi ya binadamu inatishwa sana na kila tisho la mauti.

Hawa ni wanafunzi wa Yesu waliomwona akija huku anatembea juu ya maji, wakamdhana kuwa ni mzuka/mzimu/ na mara wakaogopa kwamba, unakuja kuwazamisha majini.

Hali hii inaendelea kuwatokea wacha Mungu katika maisha ya kila siku. Mara tunapojikuta ghafla tunakabiliana na hali ya hatari inayotishia maisha, tunaingiwa na hofu na kuanza kupiga mayowe= kuna maombi ya mayowe.

Kuna vilio vya hali ya juu sana vinavyofanyika kwenye nyumba za ibada na huduma za maombezi ili kuomba msaada kwa Mungu lakini si kwa njia sahihi. Huwezi kuomba na kujibiwa huku umejaa hofu. Ndiyo maana kitu cha kwanza kuwatuliza wanafunzi wake ni kuwaambia

“Jipeni moyo” Maana yake “dhibiti wenyewe kwanza hali ya kuogopo” kulikopitiliza.
Ukitafakari msamiati wa “kujipa moyo” utagundua hapo si suala la kupata msaada kutoka mahali! Kumbuka Yesu hakusema “nawapeni moyo ili msiogope” bali alisema “jipeni moyo msiogope”

Ni suala la “kujitawala kibinafsi” yaani “kujizuia kibinafsi usitawaliwe na hofu”! Unajua hofu haimwingii mtu pasipo kuiruhusu. Kila mtu ana uwezo kamili wa kuzuia hofu isimwingie, tatizo hatuna elimu ya kuutumia.

Natambua kwamba si jambo jepesi “kudhibiti hali ya kuingiwa na hofu” kwa sababu vitisho vyake pia si mzaha wala nadharia tu na mazingira halisi na hali halisi. Lakini pamoja na hali halisi, bado kila mmoja wetu ameumbiwa uwezo wa “kudhibiti hali ya kuingiwa na hofu”! Ni wakati wa kuanza mazoezi ya kiroho ya kudhibiti hofu.

Na njia pekee ya kudhibiti hofu ni IMANI kwa Yesu Kristo. Ukifanya zoezi la kuchochea imani ikajaa moyoni, kamwe HOFU haiwezi kupenya na kuingia moyoni mwako hata kama uko kwenye mazingira hatarishi kupindukia. Utashangaa katika mazingira ambayo watu wengine wanaogopa mpaka wanazirai, wewe ndio unafanya kazi ya kuwafariji na kuwahimiza “wajipe moyo wasiogope.”

Unajua wacha Mungu wengi wanaogopa wakidhani hii ni sifa ya kuwasaidia kupata msaada kutoka kwa Mungu. Mungu anavutiwa na IMANI tuliyo nayo kwake na si HOFU tuliyo nayo kwa Shetani. UNAPOJAA HOFU MAANA UNAMFANYA SHETANI KUWA NA NGUVU KULIKO MUNGU na hali hii inamuudhi Mungu. LKINI UKIJAA IMANI kwa Mungu unadhihirisha kwamba MUNGU ni Mkuu kuliko Shteni na vitisho vyake, na MUNGU ni MWAMINIFU kwa ahadi zake, hata kama zinaonekana kuchelewa bado zitatimia.

Yesu anatarajia wanafunzi wake
kuwa waaminifu hata kifo

 “Usiogope mambo yatakayokupata, tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, name nitakupa taji ya uzima.” (Ufu. 2:10)

Usiogope yatakayokupata: Unajua maana yake? Maana yake kuna mambo yatakayokupata; mambo hayo hayatoki kwa Mungu bali yanatoka kwa Ibilisi; na mambo hayo si mazuri bali ni mateso na kashfa na vitisho vya mauti.

Yesu hakusema “Usiogope hayatakupata”; alisema usiogope “mambo yatakayokupata”! Mara nyingi sisi tunaomba sana Yesu atuepushe “mambo magumu na mabaya yasitupate. Lakini tunasahau kwamba yeye mwenye alikwisha kututahadharisha kwamba ulimwenguni tutachukiwa na kuudhiwa kama yeye mwenyewe alivyochukiwa na kuudhiwa. Ndio maana hapa hasemi hayatawapa bali vumilia yatakapowapata.

Natambua sana sisi tungependa kuendelea kuishi maisha yasiyo na misukosuko ya kiimani. Na ni maombi yangu kwa ajili yako kwamba uweze kuishi katika utulivu usiona na maudhi na majaribu. Lakini changamoto haziko kwa Mungu bali zinatoka kwa adui Ibilisi. Na ameruhusiwa kwa muda mfupi atumie fursa ya kutujaribu ili tuthibitike kiimani kwamba tunampenda Mungu kwa utashi wetu au tumeshinikizwa.

Lakini wakati wote ambapo tunapitia katika mitihani ya imani Mungu yuko pamoja nasi kuhakikisha kwamba hatujaribiwi kupita uwezo wa imani yetu kwake. Vigezo vya kujaribiwa kwetu vimezingatiwa kikamilifu.

Hata hivyo sehemu ya ujumbe huu iko kwenye tamko la Yesu kuhusiana na ukomo wa kuvumilia. Yesu anasema hivi “…..uwe mwaminifu hata kufa…….”! Sisi huwa tunajiwekea muda wa kuvumilia mambo magumu tunayopitia kwa kufikiri kwamba ukomo huo ndio kigezo cha Mungu kutuondoa katika mapito magumu. La hasha. Kigezo cha Mungu kwetu ni tunapovumilia mpaka mwisho wa uhai wetu.

Tunamwamini Mungu na kumtumia yeye bila kulegeza msimamo wa imani yetu MPAKA KUFA. Tunavumilia katika mateso dhidi ya IMANI mpaka KUFA. Hata tukifanyiwa maovu kwa makusudi ili kutushawishi tubadili msimamo kwa ajili ya kupunguza ukali wa mateso bado tunasimama imara kuvumilia MPAKA KUFA.





Viewing all 1245 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>