Siku ya jumapili iliyoisha katika uwanja wa mpira wa Uhuru zamani kama uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kulifanyika tamasha kubwa la uimbaji lenye lengo la kuzungumza kupitia uimbaji na atakayekuwa Rais mtarajiwa wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tamasha hilo liliandaliwa na kwaya ya Efatha kutoka Uhuru Moravian Kariakoo na kuhudhuriwa na watu mbalimbali pia kwaya hiyo ilitumia wasaa wa tamasha hilo kufanya live Recording yao
Baadhi ya kwaya zilizohudhuria tamasha hilo ni pamoja na Neema Gospel ya AIC Chang'ombe, Uinjilisti Kijitonyama, Eden Tabata Moravian, Uinjilisti Sayuni Kinondoni, Tumaini Shangilieni St James Arusha. Ambapo licha ya mahudhurio kutokuwa makubwa sana kama ilivyokuwa ikitazamiwa lakini watu waliofika waliweza kuburudika na lengo la tamasha hilo kufikiwa na vyombo vilivyotumika kutoleta shida kama matamasha mengi yanayofanyika uwanja wa taifa yanavyokuwa
![]() |
Uinjilisti Sayuni Kinondoni |
![]() |
Tumaini Shangilieni St James Arusha |
![]() |
Efatha Uhuru Moravian Kwaya |
![]() |
Baadhi ya watumishi wa Mungu waliohudhuria |
![]() |
Neema Gospel Choir Chang'ombe |
Efatha Choir na live Recording