![]() |
Lungelo akiwa anapapasa kinanda chake kabla ya kuibiwa wiki jana |
Kupitia ukurasa wake wa Facebook mpigaji huyo alitoa tangazo hilo la wizi ambao umetokea kuwasikitisha wengi hasa kutokana na namna kijana huyo anavyojulikana kwa kupenda kazi yake na muziki kwa ujumla. Ambapo hii yawezekana ikawa moja ya historia kuandikwa, marafiki na ndugu na jamaa wa kijana huyo wanayemfuata kwenye ukurasa wake wa Facebook wameamua kutangaziana kukisaka kinanda hicho mpaka kipatikane ikiwa pamoja na kutwajwa sehemu zote zinazohusika na kununua vitu vya wizi na watu ambao wanahusika katika kuviuza vitu hivyo. Ushirkiano ambao marafiki hao wameuonyesha mpaka sasa unaonekana utazaa matunda hasa baada ya taarifa kuanza kupatikana kuhusiana na kuonekana mtu akikiuza kinanda hicho.
Lungelo alianza kuonekana katika jukwaa la Joyous kuanzia album ya 17 na amemaliza mkataba wake mwaka huu mara baada ya kurekodi nao album ya 20 mapema mwezi Decemba mwaka jana. Kwasasa anajihusisha na muziki katika makanisa na sehemu mbalimbali ambakoan anaalikwa katika kuongoza muziki. Kijana huyu pia mapema mwaka jana alishinda kinyang'anyiro cha mpigaji bora wa piano nchini Afrika ya kusini.
Joyous 20 Eric Moyo kutoka Zimbabwe anakwambia Praise The Lord