Quantcast
Channel: Gospel Kitaa™
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1245

SOMO: UNDANI WA MAOMBI (4) - MCHUNGAJI MADUMLA

$
0
0

Na Mchungaji Gasper Madumla

Bwana Yesu asifiwe…

Karibu tuendelee kujifunza,leo tunaingia katika kipengele cha tatu,hiki ni kipengele kipya tunachokianza leo;

03.AINA ZA MAOMBI.

Zipo aina nyingi za maombi zinazotumika kila siku. Leo tuziangalie aina chache haswa zile tunazozitumia mara kwa mara; lakini ikumbukwe kwamba maombi yamegawanywa katika sehemu mbili kuu nazo ni maombi ya kufunga na maombi ya kawaida.

Kwa sababu hakuna maombi nje ya sehemu hizo mbili,maana hata kama utafanya maombi ya namna gani basi ujue maombi yako yatakuwa ni ya kufunga au ni maombi ya kawaida. Kupitia maombi ya kufunga na maombi ya kawaida,ndipo zinazaliwa aina mbali mbali tena tofauti tofauti za maombi kama ifuatavyo;

(i)Maombi ya shukrani

(ii)Maombi ya sifa na kuabudu

(iii)Maombi ya Toba na rehema.

(iv)Maombi ya kumsii Mungu na kumuuliza

(v)Maombi ya vita

(vi)Maombi ya Nadhili

(vii) Maombi ya mapatano na maombi binafsi.N.K



(I.) MAOMBI YA SHUKRANI.

Awali ya yote ni lazima tujifunze nini maana ya neno hili “shukrani” neno hili maana yake ni neno lenye kueleza furaha ya moyo wako kwa mema yote uliyonayo. Mara nyingi katika hutumika neno “ninakushukuru BWANA,MUNGU wangu kwa...” au “ BWANA MUNGU asante kwa...” au ` BWANA YESU,pokea shukrani zangu kwa...” N.K yaani kutegemea na nini unachowiwa kushukuru.

Siku zote “neno la kushukuru” halifundishwi kwa maana yapaswa kutoka moyoni mwako. Mfano wa kawaida kabisa; ikiwa mtu amekupa pesa,je utafundishwa kumshukuru mtu huyo? Jibu ; hautafundishwa kwa maana utajikuta ukianza kusema “ asante kwa msaada wako wa pesa” au “kwa kweli,ninakushukuru sana kwa kunisaidia maana nilikuwa sina kitu kabisa,ninakushukuru sana rafiki” N.K tena gafla unaanza na kumwita “rafiki” hata kama hakuwa rafiki yako.

Hivyo kushukuru kwatoka moyoni mwa mtu,huja moja kwa moja ( automatically). Sasa jambo la kushangaza leo,watu wamekosa shukrani mbele za MUNGU wao,mpaka wafundishwe maneno ya kusema,hii haiko sawa,kwa maana maneno hayo ya mdomoni hayatoki moyoni.

( Isipokuwa watu waweza kufundishwa maneno ya kusema kama sehemu tu ya muongozo ili mtu aweze kujua anaombaje,lakini kile akiombacho ni lazima kitoke moyoni ).Asili ya kushukuru ni moyoni,moyo ni lazima umshangilie BWANA,ndio maana tunasoma;

“ BWANA ni nguvu zangu na ngao yangu.Moyo wangu umemtumaini,Nami nimesaidiwa;Basi, moyo wangu unashangilia,Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.“Zab.28:7

Hivyo basi,maombi ya kushukuru ni maombi ya kumshukuru BWANA MUNGU kwa yote uliyonayo. Neno “kwa yote” ina maana kwa mema na yale na hata yale magumu unayoyapitia,yakupasa kushukuru. Neno la Mungu linasema “shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.” 1 Wathesalonike 5:18

Aina hii ya maombi,ni muhimu sana kwa maana huwezi kuanza maombi yoyote bila kuanza na shukrani. Ni ukweli usiopingika kwamba kila mtu ametendewa makuu na BWANA MUNGU Yeye MUNGU amekuwa mwaminifu sana hata pale tulipokuwa dhambini,Yeye hakutuacha bali alisubiri tutubu na tuanze upya na Yeye.

Ukiyatafakari maisha yako,utagundua kwamba ni neema na rehema za MUNGU tu,zinazokufanya wewe uwe hivyo ulivyo sasa. Wewe si bora sana kuliko wote waliokufa,wala si bora sana kuliko wote waliopata ajali bali ni mkono wa BWANA tu.

Ikiwa ni hivyo,basi yakupasa kusema “ asante Mungu” kabla ya kuanza na maombi yoyote yale. Hapa napo pana shida sana kwa wengi maana watu wamekosa kuyatafakari maisha yao kwa kumtazama MUNGU bali watu huangalia shida zaidi kiasi kwamba wanaona kana kwamba MUNGU hakuwatendea chochote.

~ Maombi ya kushukuru yakitoka moyoni yana nguvu ya ajabu. Wote walioshukuru vizuri walitendewa zaidi ya yale waliyoshukuru. Mifano ipo mingi hata katika maisha ya leo, labda litazame jambo hili kwanza katika maisha yako binafsi. Pale ambapo ulipotendewa mema na mtu yeyote yule kisha ukarudi kumshukuru mtu huyo. Je mtu huyo uliyemshukuru hatajisiki vizuri akutendee mema mengine?

Mfano ;

wewe umemshukuru jirani yako kwa msaada wa usafiri/lifti aliyokupa labda ulipokuwa huwezi/unaumwa. Shukrani zako zinamfanya akufikirie tena hata kama ulikuwa hauumwi bali atakupa lifti tena. Tazama jambo hili kibiblia kwa wale wakoma kumi waliotakaswa kisha mmoja wao akarudi kushukuru tena alikuwa ni mgeni tu yaani ni msamalia “ Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa.” Luka 17:19

Yesu anamwambia Msamalia situ kwa habari ya kuponywa bali pia kwa habari ya imani. Msamalia alipokea mara mbili zaidi ya wale tisa walioondoka bila shukrani. Msamalia alipata neema ya kupokea imani kwa Kristo Yesu pale aliporudi kwa shukrani,kwa maneno mengine alipokea na vya rohoni pia…

ITAENDELEA…

Kwa huduma ya maombezi,nipigie sasa +255 655 11 11 49.

Mchungaji Gasper Madumla.

Beroya bible fellowship church(Kimara,Dar,TZ)

UBARIKIWE.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1245

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>