Quantcast
Channel: Gospel Kitaa™
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1245

SOMO: UNDANI WA MAOMBI (3) - MCHUNGAJI MADUMLA

$
0
0

Na Mchungaji Gasper Madumla

Kusoma sehemu iliyopita BONYEZA HAPA

Bwana Yesu asifiwe…

Karibu tena,Kumbuka; tunaendelea kujibu lile swali,kwa nini tunaomba?

03.Tunaomba kwa sababu ya kuimarisha imani zetu.

Neno la Mungu ni kama mbegu,bali maombi ni kama maji.Kama vile mbegu isivyoweza kukua bila maji ndivyo ilivyo imani yako haiwezi kukua bila maombi. Kwa kuwa tunahitaji kukua kiimani basi hatuna budi kuomba mara kwa mara;maombi hupandisha imani kwa kiwango kikubwa,tazama mfano huu;

Inawezekana unamuamini Yesu katika uponyaji,lakini kule kuamini tu hakutoshi ni lazima uchukue hatua ya kumuomba,angalia jambo hili kwa wanafunzi wake Yesu jinsi ilivyokuwa; `` [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]” Mathayo 17:21 & Marko 9:29

Tazama hapo (Mathayo 17:14-21),wanafunzi wa Yesu walimuamini Yesu,lakini kilichokuwa kimepungua ni nguvu ya maombi ya mara kwa mara na mifungo. Na kwa sababu maombi huimarisha imani,hivyo kama yatakosekana kwako basi ni dhahiri kabisa kwamba hautakuwa na imani iokoayo,utakuwa na imani haba kama vile hao wanafunzi walikuwa na imani haba.

Ukiwa ni muombaji mzuri,basi kiwango chako cha imani hupanda kiasi kwamba yale yote magumu unaanza kuyaona mepesi. Mahali ambapo wenzako hawaoni njia bali wewe waiona kwa imani kwa sababu wewe ni muombaji.

Mimi nakumbuka,wakati fulani nalikuwa ninaaomba na wenzangu katika maandalizi ya mkutano wa nje. Kisha maombi yangu yakanipandisha imani kiasi kwamba nikasema hata kama kuna mchawi yoyote yule nataka aje kwangu nionane nae kwa macho ya damu na nyama,tuone atanifanya nini mimi mwenye nguvu za Mungu.

Wenzangu nao ndio kabisaa maana wao walisema akija tutampiga na mateke mpaka akome kuloga. Lakini imani yote ya ushindi ilijengwa katika maaombi. Hivyo basi maombi yana sehemu kubwa ya kukuza imani yako.

04.Tunaomba kwa sababu ya kupata udhihilisho wa nguvu za MUNGU.

Huduma zetu haziwezi kusonga mbele kama zitakosa nguvu za MUNGU. ikumbukwe kwamba; moja wapo ya njia ambayo Mungu huitumia kutuvika nguvu za rohoni ni njia ya maombi. Tazama, maombi yanavyotia nguvu karama zetu,kwa njia ya maombi watu huanza kunena,kutabili,kupata masomo ya kufundisha,kwenye maombi ndipo mahali watu hupata maono N.K

Tuangalie mfano huu;Luka 22:40-43. Yesu akiomba na tunaambiwa hivi;“ Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.” Luka 22:43 Kumbe,kuna kipindi kigumu ambacho ni lazima kiachiliwe kwako,mara nyingi watu hawaombi wapitiapo katika kipiindi hicho. Lakini Mungu hamwachi mtu,bali Yupo kwa ajili yako,ukiomba hakika atakutia nguvu ya kusonga mbele.

05. Tunaomba Kwa sababu ya kuzipinga hila za yule muovu.(shetani).

Mshtaki wetu yupo,naye ni adui yetu sikuzote. shetani hawezi kutuachia kimya kimya pasipo kumpinga katika maombi. Kama hatutaomba kwa jina la Yesu,basi tutapigwa mpaka tuchanganyikiwe,ni lazima tuombe tumpige na sisi. Biblia inatuambia,tukimpinga yeye atatukimbia;

“ Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.” Yakobo 4:7

Mtu asiyeomba ni chakula cha wachawi,wanga,washirikina N.K Bali aombaye ni moto uteketezao kila nguvu ya giza. shetani ni roho,roho husikia~tukimpiga katika maombi ni lazima apigike,tukiikeemea roho hiyo,itasikia na kukimbia kutoka kwetu.

06.Tunaomba kwa sababu sisi tu miungu,tunaendelea kuumba.

Ni ukweli usiopingika kwamba maombi ni njia ya kuumba vitu visivyoonekana na hata vile vionekanavyo. Mfano tazama pale unapopitia katika udhaifu wa mwili kwa sababu ya magonjwa,hapo ukiomba unaiumba afya iliyotoweka sasa unairejesha kwa upya,kuifanya iwe nzuri tofauti kabisa na vile ulivyo.

Yapo mambo mengi yaliyokufa katika maisha yetu,lakini kwa njia hii ya maombi tunayafufua na kuyaumba tena. Mfano; inawezekana ukaitengeneza nyumba yako vile utakavyo wewe katika maombi,hali wewe huna hata kiwanja.

Lakini ukamuomba MUNGU huku ukiiona nyumba yako katika ulimwengu wa roho jinsi itakavyokuwa hapo baadaye. Yaani twaweza kuumba vitu vingi ambavyo kwa sasa havipo kabisa. BWANA MUNGU ametuheshimisha mno,hata kutupa uwezo huu,wa kushiriki uumbaji kwa maana tu miungu.

Je nini asili ya maombi?

Tunaweza tukajiuliza swali hilo,kwamba maombi yalitoka wapi? Au ni nani kaleta maombi?

Maelezo juu ya asili ya maombi.

Hapo mwanzo Mungu alipoumba ndege,wanyama mbali mbali,samaki wa baharini,na kila kiendacho chenye uhai aliona kuwa ni vyema. Lakini BWANA MUNGU hakushuka ili azungumze nao. Bali alipomuumba mwanadamu,Mungu alishuka azungumze naye. Mazungumzo haya yalikuwa ni kati ya Mungu na mwanadamu aliyemuumba; Kwa sababu Adamu alikuwa yupo rohoni kabla ya anguko,aliweza kuwasiliana na Mungu moja kwa moja.

Hivyo,BWANA MUNGU aliweka utaratibu wa kuzungumza na watu wake aliyewaumba (Adam na Hawa). Ndani ya mazungumzo haya,palikuwa na utofauti wa nani mkubwa kati yao, Mungu alikuwa mkubwa sana wakuogopwa,na mwanadamu alikuwa mdogo, mwanadamu hakukamilika maana alihitaji msaada kutoka kwa Mungu kwa njia ya mazungumzo. Asili ya maombi ni mazungumzo aliyeyaweka Mungu mwenyewe akizungumza na watu wake.

Baada ya dhambi kutokea,mwanadamu akatengwa mbali na Mungu. Dhambi ikaweka kiambaza kilichowatenganisha maana Yeye ni MUNGU mtakatifu,hivyo mwanadamu akatolewa kutoka katika uwepo wa BWANA hata ufu wa kiroho na kimwili pia.

Watu wakaongezeka ulimwenguni kabla ya gharika. Kwa maana vizazi vikazaliwa. Maombi yakakauka kwa muda fulani. Lakini kipindi ambapo Adamu alipomjua mke wake tena alimzaa mwana mwanamume akamwita Sethi. Sethi naye akazaa mwana akamwita Enoshi. Hapo ndipo watu walipoanza kuendeleza maombi. Mwanzo 4:26

Biblia imetaja kwamba eneo hilo ndilo eneo la kwanza kabisa ambapo watu wameanza kuomba baada ya yote kutokea katika anguko la dhambi ya akina Adamu. Hivyo tokea hapo tunaona maombi yakianza tena,na kuendelea mpaka katika ujio wa Yesu,mpaka leo hii. Hii ndio asili ya maombi.

ITAENDELEA…

Kwa huduma ya maombi na ushauri wa bure,nipigie sasa +255 655 11 11 49.

Mch.Gasper Madumla.

Beroya bible fellowship church(Kimara,Dar,TZ)

S.l.p 55051,Dar.

UBARIKIWE.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1245

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>