Quantcast
Channel: Gospel Kitaa™
Viewing all 1245 articles
Browse latest View live

UZINDUZI WA CHURCH BOY CHURCH GIRL DAR ES SALAAM IJUMAA HII

$
0
0

Imezoeleka Church Boy Church Girl kufanyika kila mara Jijini Arusha. Sasa ni zamu ya Dar es Salaam katika usiku wa Turn Up For Jesus tarehe 7/8/2015 Word Alive (Sinza Mori), kwenye tamasha litakalofanyika kuanzia muda wa saa tatu kamili usiku hadi saa kumi na moja asubuhi.

Tukio hilo la kipekee litaongozwa na waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili wakiwemo Glorious Worship Team (GWT), Paul Clement, The Doxas, Sam Yona, Calvary Band, Francis Sotely, Shedrack Robert (kutoka Arusha) Sir Mbezi na waimbaji wengine wengi wa muziki wa injili.

Wana Dar es salaam ni zamu yako sasa usipange kukosa, njoo ubarikiwe na huduma hii mpya. Hakuna kiingilio. GK itakuwepo.

Kufahamu zaidi kuhusu Church Boy Church Girl, bofya hapa.

MAMBO MACHACHE YATAKAYOFANYA JINA LAKO LIWE NA SIFA NJEMA

$
0
0
Faraja Naftal Mndeme,
GK Contributor.


I.  UADILIFU.
Muda mwingi tumetamani majina yetu yazungumzwe vizuri kwenye maisha yetu ya kila siku hata baada ya sisi kufa, au kuwepo mbali na mahali husika ambapo jina lako linatajwa. Lakini ni watu wachache sana ambao wamejua mbinu ambazo zitafanya majina yao yawepo kwenye vinywa vya watu bila ukomo. Jina la mtu ni utambulisho wa mtu. Jina la mtu linaweza kuwa nguvu mahali husika hata bila yeye mwenyewe kuwepo katika eneo hilo. Uadilifu kwenye kila jambo na kwenye kila eneo la maisha yako kutafanya jina lako liendelee kudumu na kuwepo. Je Unaposikia jina kama Mwalimu Julius Kambarage Nyerere unakumbuka nini ingawa mwenywewe alishafariki zaidi ya miaka kumi iliyopita? Je Ukisikia Nelson Mandela unapata picha gani kichwani mwako? Jina lako tu linaweza kukupa kibali kwa mtu anayelisikia bila hata wewe mwenyewe kuwepo. Ni muhimu kuhakikisha unakuwa muadilifu kwa asilimia zote kwenye maisha yako.

II. UKWELI
Kuna watu wewe binafsi ukisikia majina bila hata wewe kuwepo kuna aina fulani ya tabia yao unaikumbuka. Jina la mtu ni utambulisho wa mtu. Kuna Mahali unaweza kwenda lakini sifa zako na jina lako zinakuwa zimeshakutangulia kwa namna tabia yao ilivyo. Kuishi maisha ya kweli kuna faida. Ni mara ngapi umesema uongo ukahisi unapata faida yako kwa mtu uliyemdanganya? Hasara ya kuishi maisha yasiyo na ukweli ndani yake ni kubwa zaidi kuliko ilivyo kawaida. Ni muhimu kujenga utaratibu ya kwamba kweli yako iwe kweli na hapana yako iwe hapana ili kujijengea jina ambalo litakumbukwa daima na hata usipokuwepo. Kumbuka jina lako ni urithi wa vizazi vijavyo. Unafikiri vizazi hivyo vitakumbuka jina lako kwa lipi?

III. UAMINIFU.
Je, jina lako linapotajwa linawakumbusha nini watu wanaolisikia? Je linawakumbusha maisha yako na hasara ulizowaletea kwa kukosa kwako uaminifu na maumivu tele mioyoni mwao? Uaminifu ni bidhaa ambayo huleta harufu nzuri ya manukato kwa wale wanaosikia jina kako. Jina lako linaweza likakupa kibali sehemu yoyote kutokana na namna unavyoendesha maisha yako ya kila siku. Unaweza ukahisi unapomtendea mtu mmoja vibaya watu wengine hawaoni, kumbe wanaona lakini hawasemi tu. Hakikisha unajenga haiba ya uaminifu ili kulijengea jina lako sifa njema. Jina lako linaweza likawa mtaji wa kibiashara. Jina lako linaweza kuwa urithi bora kwa vizazi vijavyo. Mfano Mzuri unaposikia Bill Gates au CocaCola na Pepsi unafikiri unaelewa nini? Majina haya yamejengwa katika uaminifu kwa jamii kiasi ukitaka tu kuyatumia lazima ulipe kodi kwa mwenye jina. Hasara ya jina baya si kwamba itakuathiri wewe tu bali itaathiri na watu wengine kwenye kizazi chako. Kuna majina kwenye nchi yetu (unayafahamu) yakitajwa tu kuna namna unajisikia moyoni, kwanini?

IV. HAKI
Haki imekuwa bidhaa adimu sana miongoni mwa wanadamu, lakini wewe hakikisha unamtendea haki kila ajaye kwenye maisha yako; mkubwa kwa mdogo. Haki pamoja na kuzunguzwa kwenye vinywa lakini hakikisha unaitenda. Mara nyingi tumehubiri haki lakini linapofika swala la utendaji imekuwa ni ngumu, sababu ya aina ya maslahi mabaya tunayopata kwa kutokutenda kwetu haki. Haki itakufanya uendelee kuishi hata bila wewe mwenyewe kuendelea kuwepo. Unaposikia  NYERERE unakumbuka nini kwenye hili taifa? Je hakuna viongozi wengine kwenye hili taifa? Jina lako likitajwa je linakumbusha dhuluma, ubabe na mambo mengi maovu uliyotenda? Jina lako litakumbukwa zaidi iwapo utatenda haki kwenye kila jambo. Jina lako linaweza kukupa fedha bila hata wewe kutumia nguvu, tunasikia mifuko mbali mbali ya kijamii ina majina ya baaadhi ya watu ambao wiliishi kwa haki. Jina likitajwa tu basi fedha hulifwata jina hilo. Je Wewe jina lako likitajwa sehemu ni nini kinatokea?

Mwisho
Jina lako linaweza kukupa kibali sehemu au kukunyima kibali kabisa. Kuna watu wamekosa kazi, fedha, kwasababu ya ubovu na ubaya wa majina waliyorithi kwenye maisha yao, hadi kuna wengine wameacha kuyatumia si kwa sababu hayana ladha nzuri yanapotamwaka bali ujumbe uliopo nyuma ya jina unaleta matatizo. Jina lako ni urithi kwa vizazi vijavyo. Ukilitumia vizuri basi kuna wakati vizazi vijavyo wanaweza kutumia jina lako kama mtaji kwenye maisha yao na wanaweza kufaidika. Jina lako linaweza kutumika kama nembo ya kibiashara. Fikiria jina lako limehusishwa kwenye wizi, uongo, dhuluma unafikiri likitumika kama nembo ya bidhaa kuna mtu atasogelea hiyo bidhaa? Jina lako ni mtaji unaodumu kizazi hata kizazi.

Email : naki1419@gmail.com
+255788454585
God Bless You All

KWA TAARIFA YAKO: JE HII NI DALILI YA KUNDI LA UPENDO GROUP KUWA LIMEKUFA RASMI?

$
0
0
Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu

Kutoka kushoto Albert, Lilian, Joshua pamoja na Esther waanzilishi wa Upendo Group


KWA TAARIFA YAKO ni takribani miaka mitatu sasa, kundi maarufu la muziki wa injili liitwalo Upendo Group limekuwa kimya katika tasnia ya muziki huo nchini Tanzania na kwingineko ambako walikuwa wakifahamika kwenda na kutoa huduma. Kundi hilo ambalo lilivuma sana miaka ya mwanzoni mwa elfu mbili lilikuwa likiundwa na takribani waimbaji saba na lilifanikiwa kuteka anga la muziki wa injili kwa kiasi kikubwa huku likiibua vikundi vingine vidogovidogo na hata kuamsha ari ya waimbaji binafsi katika muziki huu wa kumsifu Mungu.

Hata hivyo kimya cha Upendo Group kwa miaka hii minne kimezidi kuwaacha njia panda wapenzi wa kundi hili pamoja na mashabiki wa muziki wa injili ambako wengi wanajiuliza kama kundi hili limefikia tamati. KWA TAARIFA YAKO hali hii ya sintofahamu imeibuka tena hivi karibuni baada ya muimbaji mwingine mashuhuri wa kundi hilo Eliwinjuka Mafwenga akionekana kuhudumu katika kwaya yake ya zamani aliyoiimbia ya Uinjilisti Kijitonyama. Kwaya ya Uinjilisti ilialikwa kuhudumu katika uzinduzi wa album ya Boniface Mwaitege Diamond Jubilee Hall Jumapili ya tarehe 2 Agosti, uzinduzi ambao uliandaliwa na Msama Promotions.

Kitendo cha Eliwinjuka ambaye alikuwa mmoja wa waimbaji tegemeo wa Upendo Group kurejea katika kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama kimezua maswali sana na kuthibitisha kuwa huenda Upendo Group imemaliza muda wake, maana ni vigumu kutumikia vikundi viwili. KWA TAARIFA YAKO Ikumbukwe kuwa kabla ya kuanzishwa Upendo Group waimbaji wake walikuwa ni sehemu ya Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama na kitendo cha wao kuanza kurejea kinaleta tafsiri nyingi kwa washabiki na wadau wa muziki wa injili nchini.

Eliwinjuka alipopanda madhabahuni mwaka juzi kwa mara ya kwanza na kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama wakisherehekea jubilei ya kwaya hiyo. 


KWA TAARIFA YAKO Eliwinjuka ambaye anafahamika sana kwa wimbo wa Bam Bam alioimba na Upendo Group alianza kuwika ndani ya miaka ya tisini akiwa na kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama ambako alikuwa mmoja wa waimbaji viongozi akishirikiana na Lilian Joshua. Ndani ya Uinjilisti Eliwinjuka alivuma na nyimbo kama Nikimbilie Wapi, Nakutafuta Mponyaji na Nafarijika. Uongozi wa Uinjilisti Kijitonyama ulipoulizwa ulithibitisha kumpokea muimbaji huyo mwenye sauti nyororo na kuwa ni kweli ameanza kuhudumu na kwaya hiyo tena.

Hali ya wasiwasi ya kumeguka kwa kundi la Upendo ilianza mnamo mwanzoni mwa mwaka 2011 ambapo muimbaji maaruufu wa kundi hili, Joshua Mlelwa aliamua kuachia ngazi na kwenda kuanza huduma ya peke yake. Duru za ndani ya Upendo Group zinasema Mlelwa aliaga rasmi baada tu ya kutoka safari ya huduma Ulaya. KWA TAARIFA YAKO hata hivyo katika mahojiano mbalimbali na vyombo vya habari Joshua amekuwa akisema kuwa alihama Upendo Group baada ya wingu kuhama hivyo alienda kutafuta wingu mahali pengine. Hata hivyo habari zisizo rasmi zinasema kulitokea mtafaruku baina ya Joshua na uongozi wa Upendo Group hasa pale ambapo uongozi haukuridhia Joshua kubaki Uingereza ambapo alikuwa ameomba abaki kwa muda kufanya shughuli binafsi.

“Kitendo cha kubaki Uingereza hakikuwafurahisha viongozi maana walijua Joshua ni nguzo muhimu hivyo kukosekana kwake kungezuia mambo Fulani Fulani“, kilisema chanzo kimoja cha karibu na kundi hilo ambacho kisingependa kutajwa jina kwa sababu kadha wa kadha.

KWA TAARIFA YAKO mtu wa pili kumeguka alikuwa ni mke wa Joshua anayejulikana kwa jina la Lilian ambaye aliachana na Upendo na kuungana na mumewe katika huduma ya pamoja. Wawili hawa wamebaki kuwa maarufu na wameonekana wakihudumu katika mikutano na matamasha mbalimbali ikiwamo semina za mwalimu Christopher Mwakasege. Joshua anatamba na album yake iitwayo Ni Wewe. Habari za kuaminika zilizoifikia Gospel Kitaa zinasema kuwa mkewe Lilian naye yuko studio akimalizia kutengeneza album yake ambayo mpaka sasa haijapewa jina.

Esther Castory

Ikumbukwe kuwa kuhama kwa Joshua na mkewe kulikuwa ni pigo kwani yeye ndiye alikuwa mtunzi, mwalimu na muimbishaji kiongozi lakini pia mkewe alikuwa ni mmoja wa vivutio vya kwaya hiyo sio tu kwa uimbaji na sauti nzuri bali hata uchezaji wake. Hata hivyo kuhama huko hakukuwazuia Upendo Group kuzindua album yao ya mwisho iliyokwenda kwa jina la Mungu wa Ushindi ambapo nyimbo nyingi zilianzishwa na Joshua na mkewe na baada ya hapo miaka mitatu baadae hakuna ambalo limesikika ndani ya kundi hilo, kuachana na huduma za hapa na pale.


“Waimbaji wamekuwa wazito, hawajiamini tena mara nyingi wanakataa kwenda kwenye huduma
maana wanaogopa kama watafanya huduma chini ya kiwango,“ kinasema chanzo kingine kilichoko karibu na kundi hilo. KWA TAARIFA YAKO, Upendo ilipata pigo lingine baada ya muimbaji wake Esther Castory, kuhamia Mbeya kimakazi kama wakili wa mahakama hivyo kufanya pengo lizidi kuwa kubwa ndani ya kundi hilo. Muimbaji pekee aliyebaki na kuonekana labda angeweza kumudu kulishikilia kundi hilo alikuwa ni Eliwinjuka ambaye naye sasa anaonekana kujitoa na kurudi makazi yake ya zamani yaani Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama.



Mashabiki wengi wanakaa mkao wa kusikiliza tena nini kitatokea na kama Eliwinjuka atawika tena ndani ya Uinjilisti Kijitonyama kama ilivyokuwa zamani alipokuwa akihudumu na kundi hilo ambalo nalo limejipatia umaarufu sana sio tu nchini Tanzania bali hata mipaka ya nje ya Tanzania.

MTAZAME ELIWINJUKA AKIIMBA WIMBO MAARUFU NA UPENDO GROUP


Uinjilisti Kijitonyama


Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO vinginevyo tukutane wiki ijayo….

INJILI KUTOKA MTAANI: CHUNGA MANENO YA MDOMO WAKO

$
0
0

Hakika usiseme hakuna mtu anayetaka kuhubiriwa injili siku hizi, watu wana kiu ya injili mahala popote. Na hili limedhihirika kaw GK mara baada ya kukutana na Mtume Melikizedeki kwenye Jiji la Arusha, Kwa Mromboo, akipanda mbegu kwenye udongo wa kila aina.




Katika pitapita yake, GK ilikutana na kikosi hiki chenye lengo la kuharibu kazi zote za yule mwovu shetani. Mixer ndogo tu, jenereta, meghaphone na spika (pamoja na mkokoteni wa kubebea vifaa), ndio zana ambazo zimehitajika katika kueneza habari njema kwa wakazi wa mji uliochangamka wa Kwa Mromboo.

Tumia dakika zako 46 kufuatilia injili hii nawe ufunguliwe, ambapo mtumishi huyu alihubiri kuhusu namna ambavyo watu huwa wanajiuzilia baraka zao kupitia midomo yao wenyewe.

Giza lilipoingia. ndipo siku ikaahirishwa


SOMO: SHERIA YA UFALME - ASKOFU GWAJIMA

$
0
0



Somo: Sheria ya Ufalme

Isaya 9:6
Ufalme wa mbinguni tayari upo duniani na ndani ya ufalme huo kuna nguvu za Mungu na utukufu wa Mungu,ndani ya nguvu hizo za Mungu kuna jeshi la Ufalme ambalo ni malaika watakatifu pamoja na watakatifu na raisi wa Ufalme huo ni Yesu Kristo mwenyewe na katiba yake ni Biblia takatifu. Ndani ya Ufalme wa Mungu kuna funguo za Ufalme za kufungulia biashara, ndoa, mafanikio, elimu, safari, utajiri n.k na kila mtu anayempokea Yesu anakuwa tayari ameingia ndani ya Ufalme na Kuwa na funguo hizo. Ufalme wa Mbinguni ni nchi ya mbinguni iliyopo hapa duniani na ili kuingia ndani yake unatakiwa uzaliwe mara ya pili.


Ufalme wa Mungu hauigwi bali unaigwa mfano wake ni kama “chachu inayochachua donge zima” Ufalme wa Mungu unaimarika sana hapa duniani kiasi kwamba unakuwa unaushawishi mpaka kwenye wizara za serikali, mpaka Ikulu, mpaka Bungeni na nchi nzima inageuka na kuwa Ufalme wa mwanakondoo. Ufalme wa Mungu ukienea na kuimeza nchi inafikia watu wakiwaona raia wa Ufalme wameingia mahali ‘wanasema wale watu walioupindua ulimwengu wamefika na huku’ mpaka kufikia kila sehemu watu waseme majeshi majeshi.

Ndege kubwa kuliko zote aina ya Boeing 737 yenye uzito wa tani 270 ikitaka kupaa inaanza kukimbia mpaka sipi yake ifikie kilomita 160 kwa lisaa limoja ndipo inakuwa na uwezo wa kupaa hewani kasababu inakuwa imeshajitengenezea uwezo wa kupingana na Sheria ya uvutano wa kwenda chini na kutengeneza Sheria ya uvutano wa kwenda juu. Kwa uhakika napoanza kwenda juu ule uvutano wa kwenda chini unapungua kwasababu ya spidi iliyotengeneza Sheria ya kupaa juu na inakuwa haipungui kwasababu ikipungua Sheria ya kwenda chini itapata nguvu zaidi. Kutokana na Sheria hii tunajifunza unatakiwa ukianza kupaa kwenda juu usipunguze spidi yako na kumuomba Mungu akupe nguvu zaidi ya kupaa juu ya matatizo na magumu yote kwa spidi ile ile uliyoanza nayo kwa jina la Yesu.

Sheria ya kutembea Juu ya maji
Kwenye maisha kuna jambo ambalo mtu limemshinda kabisa amekata tamaa au kuna njia imeziba na hakuna matumaini tena, mtu huyo anatakiwa atumie Sheria ya Ufalme ya kutembea juu ya maji.

“Hata ilipofika sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti Herodia alicheza mbele ya watu, akampendeza Herode. Hata akaahidi kwa kiapo ya kwamba atampa lo lote atakaloliomba. Naye, huku akichochewa na mamaye, akasema, Nipe hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji. Naye mfalme akasikitika; lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya wale walioketi chakulani pamoja naye, akaamuru apewe; akatuma mtu, akamkata kichwa Yohana mle gerezani. Kichwa chake kikaletwa katika kombe, akapewa yule kijana; akakichukua kwa mamaye. Wanafunzi wake wakaenda, wakamchukua yule maiti, wakamzika; kisha wakaenda wakampasha Yesu habari. Naye Yesu aliposikia; hayo, aliondoka huko katika chombo, akaenda mahali pasipo watu, faraghani. Na makutano waliposikia, walimfuata kwa miguu kutoka mijini mwao. Yesu akatoka, akaona mkutano mkuu, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao. Hata kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na saa imekwisha pita; uwaage makutano, waende zao vijijini, wakajinunulie vyakula. 
Yesu akawaambia, Hawana haja kwenda zao, wapeni ninyi vyakula. Wakamwambia, Hamna kitu hapa ila mikate mitano na samaki wawili. Akasema, Nileteeni hapa. Akawaagiza makutano waketi katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi, wanafunzi wakawapa makutano. Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, vikapu kumi na viwili, vimejaa. Nao waliokula walikuwa wanaume wapata elfu tano, bila wanawake na watoto. Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ng'ambo, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano. Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake. Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; maana upepo ulikuwa wa mbisho. 
Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari. Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu.Mara Yesu alinena, akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope. Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji. Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu. Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe. Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka? Nao walipopanda chomboni, upepo ulikoma. Nao waliokuwamo ndani ya chombo wakamsujudia, wakisema, Hakika wewe u Mwana wa Mungu.” Mathayo 14: 6 - 33

Yesu aliwalazimisha wanafunzi wake waende peke yao ngambo ili awafundishe Sheria ya kutembea juu ya maji, Sheria hii ndiyo inayokusaidia mahala ambapo unaona utakufa haufi na mahala unapoona utaanguka hauanguki. Ni Sheria ambayo Yesu alikuwa anatufundisha kwamba kipindi ambacho huna msaada wowote unatakiwa uitumie Sheria ya kutembea juu ya maji na utafanikiwa.
Sheria ya Ufalme ni Sheria inayofuta Sheria nyingine.

Yesu kabla hajakwenda kuitumia Sheria ya kutembea juu ya maji alianza kuomba kwanza, maana yake kabla hatujaanza kuitumia Sheria ya kutembea juu ya maji lazima tuombe. Maombi maana yake ni kuyaomba makao makuu ya mbinguni yaingilie kati maisha yetu na kutupatia ufumbuzi. Tunatakiwa tuombe tuombe kula siku ili tuwe na uwezo wa kuitumia Sheria ya kutembea juu ya maji.

“ Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.” Luka 18:1

Mathayo 14:24

Kwenye zamu ya nne Yesu hutembea juu ya maji kukifuata chombo. Kwenye kinywa chako kuna Sheria ya Ufalme wa Mungu inayozifuta Sheria zingine zote na ukisema kitu kinakuwa vilevile kama ulivyosema.

Wanafunzi wa Yesu walipomwona Yesu anakuja juu ya maji walipiga kelele kwa hofu na uoga, lakini Yesu aliwaambia wajipe moyo ni yeye. Inamaanisha ukiwa ndani ya dhoruba kali Yesu huja kwenye zamu ya nne na kuituliza dhoruba hiyo nayo ikamtii.

Ukiri
“ Bwana Yesu ikiwa ni wewe uliyeniponya magonjwa, ikiwa ni wewe uliye ikomboa familia yangu, ikiwa ni wewe uliyefufua wafu, ikiwa ni wewe uliyeniokoa kwenye mitego ya mauti naomba uniamuru nitembee juu ya maji”

“Tumeambiwa tutembee juu ya maji kwasababu tumeamriwa”

Petro alimwambia Yesu ikiwa ni yeye amwamuru amfuate na yesu alimwambia NJOO ndipo Petro alishuka chomboni akatembea juu ya maji huku akimfuata Yesu na alipojaribu kuangalia maji akaanza kuzama. Tunajifunza kwamba unaweza kumwona mtu ameokoka hana fedha, hajaenda shule, hana elimu yeyote lakini anaishi bila wasiwasi maana yake anatembea juu ya maji lakini akianza kuangalia matatizo yake na mambo mengine ya maisha yake yanavyokwenda tofauti na wengine mtu huyo ataanza kuzama kwasababu ya kupoteza imani,

Usiangalie matatizo yako mwangalie Yesu pekee ndiye mwenye kukupa uwezo wa kutembea juu ya maji, usingalie maadui au marafiki wanasema nini bali mwangalie Yesu na utafanikiwa kwa jina la Yesu.

Utakapotuliza chombo utajulikana wewe ni mwana wa Mungu.
Sheria ya Ufalme inaweza kubatilisha mambo ambayo hayawezekani kabisa yakawezekana mambo ya kuhuzunisha, mambo ya kutia balaa, kuangamiza, mambo ya kuogopesha yakaepukika na kutokutokea kwasababu ya Sheria ya Ufalme ya kutembea juu ya maji na Mungu huwa anasubiri zamu ya nne ndio atende kazi yake Mungu huingilia mambo yako pale unapomruhusu.

Ukiri.
Nabatilisha kila mpango wa kuzamisha chombo kwa jina la Yesu, ninatembea juu ya maji kwenye kazi yangu kwa jina la Yesu,natembea juu ya maji kwenye biashara zangu kwa jina la Yesu,natembea juu ya maji kwenye maisha yangu kwa jina la Yesu, mimi sio mtu wa kuliallia ninasimama na kusonga mbele nikiwa juu ya maji kwa jina la Yesu. Mimi ni mwana wa Ufalme wa mbinguni, mimi ni raia wa Ufalme, mimi ni mwana wa Mungu, mimi ni balozi wa Mbinguni hapa duniani naishi ndani ya Ufalme kwa jina la Yesu Kristo. Amen

SHANGWE ZA GK NI FRANK NA ROSE MITIMINGI

$
0
0
Katika shangwe za GK hii leo ni kati ya Bwana Frank na Rose Mitimingi ambao walikula kiapo cha kuishi pamoja kama mke na mume kwa maisha yao yote, katika ibada ya ndoa iliyofanyika Jumamosi iliyopita katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu James Kaloleni jijini Arusha.

Bwana harusi ni mmoja kati ya waimbaji wakongwe wa kwaya ya Tumaini Shangilieni ya kanisani hapo ambao nao kama ilivyokuwa ada, harusi waliisimamia vyema harusi ya mwanafamilia mwenzao. Zifuatazo ni baadhi ya picha za tukio hilo kama zilivyowasilishwa na mdau wa GK Samuel Kusamba.



















CHAGUO LA GK NI KUCHAGUA MOJA NA AIC DAR ES SALAAM CHOIR

$
0
0


Katika chaguo la GK jumapili ya leo tupo na waimbaji wakongwe waliotokea kubariki wengi miaka iliyopita kwa uimbaji wao, upangiliaji wa sare bila kusahau namna ya uchezaji wao. Hawa si wengine bali ni AIC Dar es salaam Choir, kutoka kanisa la AIC Magomeni mapipa jijini Dar es salaam. 

Kupitia album yao ya 'Watu wangu wanaangamizwa' tumekuchagulia wimbo uitwao 'Huwezi' ulioimbishwa na mwanadada mahiri katika ushambuliaji wa jukwaa awapo hudumani Mercy Nyagwaswa Mwakilasa ambaye pia amekuwa mmoja wa walimu wa kwaya hiyo kwa kipindi kirefu bila kusahau akihusika pia katika kufundisha namna ya uchezaji.

Nimatumaini yetu wimbo huu utakupatia ujumbe mahususi endapo umekuwa mtu wa kutangatanga katika njia mbili. Sikiliza na tazama ili upate burudiko ndani ya Roho bila kusahau kupata baraka kupitia waimbaji hawa ambao bado wapo ngangali katika kumtokomeza shetani na mawakala zake kupitia uimbaji wa kumsifu Mungu kwa viwango. Uwe na jumapili njema.



KANISA HILLSONG LAWEKA WAZI MSIMAMO WAKE JUU YA WAPENZI WA JINSIA MOJA

$
0
0
Mchungaji Brian Houston

Mchungaji kiongozi wa kanisa maarufu duniani la Hillsong Brian Houston wa Australia ameweka wazi msimamo wa kanisa hilo dhidi ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kufuatia ripoti iliyokuwa imesambaa katika mitandao kuhusu kati ya waongozaji uimbaji wawili wa kiume wa kanisa hilo jijini New York nchini Marekani  kutangaza hadharani kwamba wanauhusiano wa kimapenzi.

Katika ujumbe wake mchungaji Houston aliamua kuweka wazi kuhusiana na taarifa hiyo kwamba kanisa hilo limeruhusu wanaume hao walioweka wazi uhusiano wao kuimbisha kwaya kanisani hapo. Mchungaji Houston amenukuliwa kupitia blog ya kanisa hilo kwamba msimamo wa kanisa hilo katika suala la mapenzi na ndoa za jinsia moja haujabadirika sawasawa na maandiko yasemavyo. Alisema, kama alivyowahi kuzungumza awali akisema anaamini maandiko ya mtume Paulo yako wazi kuhusu jambo hilo. 

"Miezi michache iliyopita wakati mmoja wa waongozaji wetu wa kwaya alipotoa tangazo kwa jamii ambalo hatukulitegemea kwamba amevalishwa pete ya uchumba na mmoja wa waimbaji ambaye huimba kanisani hapo, lilikuwa jambo la kustua na kushangaza kwetu pia. Katika uelewa wangu ni kwamba hawajawahi kupewa ama kuwemo kwenye uongozi wa kanisa hilo tangu walipotangaza uhusiano wao. Lakini bado tunawapenda na tunajua ni watu kama sisi, tupo kwenye safari moja, na jukumu letu kama kanisa ni kuwasaidia katika safari hii kwa upendo na rehema". alisema mchungaji
Houston.

Katika blog ya kanisa hilo yenye kichwa "Je ninawapenda mashoga? 'Do I love gay people?' mchungaji Houston amesema, Kanisa la Hillsong linawakaribisha watu wa aina zote isipokuwa haikubaliani na aina zote za kimaisha ama kimienendo, ikiwa pamoja na kuwapa nafasi za uongozi wa kanisa watu wenye mapenzi ya jinsia moja iwe kwa kazi ya kulipwa ama ya kujitolea. "Ninajua ujumbe huu utawavunja watu nguvu katika pande zote za jambo hili ambalo pia ni gumzo kwa makanisa yote duniani"aliandika mchungaji Houston.

Hata hivyo pamoja na mchungaji Houston kusema inakaribisha watu wa aina zote lakini sivyo kwa
Mchungaji Carl Lentz
watu wanaopanga kuleta fujo ama migongano, watu wanaopenda ugomvi pamoja na wenye tabia za ubakaji na kulaghai watoto wadogo kwa mambo ya ngono" alimalizia mchungaji Houston. Kanisa la Hillsong New York linasimamiwa na mchungaji Carl Lentz aliyetokea kupendwa sana na waumini wa kanisa hilo duniani ikiwemo London kutokana na namna ya ufundishaji wake huku pia mtoto wa kwanza wa mchungaji huyo ambaye pia ni mtunzi na mwimbaji maarufu wa kanisa hilo Joel Houston anashiriki katika kanisa la Hillsong New York.



SOMO: NITATUMAINI WALA SITAOGOPA - ASKOFU KAKOBE

$
0
0


SOMO: NITATUMAINI WALA SITAOGOPA

NENO LA MSINGI:

ISAYA 12:2

“Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu; NITAMTUMAINI WALA SITAOGOPA; Maana BWANA YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; naye amekuwa wokovu wangu.”

Tangu katika kitabu cha MWANZO mpaka katika kitabu cha mwisho cha Biblia, UFUNUO, mara nyingi mno Mungu amekuwa akiwaambia watu wake wasiogope. Katika MWANZO 15:1, Mungu alimwambia Abramu, “USIOGOPE, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana”. Katika UFUNUO WA YOHANA 1:17, Yesu Kristo alimwambia Yohana, “USIOGOPE, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho”. Nyakati zote, Mungu amerudia mara nyingi akiwaambia watu wake wasiogope. Hata leo, ujumbe wa Mungu ni huohuo kwa kila mtu aliyeokoka. Hupaswi kuogopa katika mazingira yoyote. Roho ya woga, haitokani na Mungu bali ni ya shetani. Biblia inasema katika 2 TIMOTHEO 1:7, “Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi”. Biblia inasema katika UFUNUO 21:8, kwamba waoga watatupwa katika ziwa la moto sawasawa na waabudu sanamu, waongo, wachawi, wauaji na wazinzi. Mtu aliyeokoka hapaswi kamwe kuogopa katika mazingira yoyote yanayomkabili. Unapoogopa na kubabaika, unakuwa umeshiriki kufanya mambo matatu ya hatari yanayosababishwa na woga.

MAMBO MATATU YA HATARI YANAYOSABABISHWA NA WOGA

1. KUOGOPA NI KUMPA NGUVU SHETANI YA KUKURARUA:

Shetani ni kama mbwa koko asiye na nguvu yoyote. Anachokifanya mbwa huyu ni kumtishia mtu na kubweka kwa sauti na kuunguruma. Kama mtu akiogopa na kuamua kurudi nyuma, mbwa yule anatiwa nguvu zaidi na kumfukuza mtu yule na hata kumjeruhi. Kama mtu yule asipoogopa na kuendelea kutulia na kutokubabaika, mbwa yule mara moja huamua kukimbia kwa woga mkubwa. Biblia inaeleza jambo hili kwa tukio lililompata Petro katika MATHAYO 14:30, “Lakini alipouona upepo AKAOGOPA, AKAANZA KUZAMA, AKAPIGA YOWE…….” Shetani aliunguruma kwa kutumia upepo mkali kumtisha Petro na aliogopa na kuacha kumtumaini Yesu alimwambia “Njoo”; mara ileile akampa nguvu shetani na akamzamisha majini. Mara nyingi watu waliookoka wameraruliwa na shetani kwa sababu ya woga wao uliompa shetani nguvu ya kuwazamisha. Shetani nguvu zake ni ndogo mno kwa mtu aliyeokoka. Ni nyoka ambaye amepondwa kichwa na kinachopigapiga huku na huku ni mkia tu. Nyoka huyu, alipondwa kichwa na Yesu Kristo pale msalabani, na sisi wote tuliookoka tumepewa amri au mamlaka ya kumponda kichwa, na kumkanyaga wakati wowote [MWANZO 3:15, LUKA 10:19].

2. KUOGOPA NI KUKOSA KUWA NA IMANI

Imani ndiyo ngao ya mtu aliyeokoka ambayo tunaitumia kuizima MISHALE YOTE YENYE MOTO ya yule mwovu. [SOMA WAEFESO 6:16] Mtu aliyeokoka anapoogopa, ni kwamba woga huo, unanyonya imani yote ya mtu huyo na kumuacha tupu; na ndipo mishale ya moto ya shetani inampiga kwa urahisi maana hana ngao yoyote ya kuizima. Angalia maandiko yafuatayo:

MARKO 4:40:

“(Yesu) Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado?”

MARKO 5:36:

“Lakini Yesu, alipolisikia lile neno likinenwa, akamwambia mkuu wa Sinagogi, Usiogope, amini tu.”

Kamwe, woga na imani, haviwezi kuwa katika furushi moja. Ni lazima woga ufukuzwe, ndipo imani ya kumshinda shetani iendelee kuwapo.

3. KUOGOPA NI KUMDHARAU MUNGU NA NENO LAKE

Unapokabiliwa na magumu yoyote na ukajaa woga na kuanza kubabaika na kukosa matumaini, kwa kufanya hivyo, umemdharau Mungu na Neno lake linalosema katika YEREMIA 32:27, “Tazama, mimi ni BWANA, Mungu wa wote wenye mwili; je! kuna neno gumu LOLOTEnisiloliweza?”

Ukimdharau Mungu na Neno lake, na kuona kwamba Mungu hawezi lolote, hana nguvu, hana uwezo, na kwamba Neno lake siyo kweli; basi ujue uko katika hatari kubwa. Shetani umempa nafsi mwenyewe ya kuendelea kukupiga, ukiwakimbilia waganga wa kienyeji, wachawi, wote hao ni maajenti wake, ndipo utakapopigwa zaidi bila msaada. Umemkataa mwenye nguvu ya kukusaidia kwa kumdharau, na kamwe huwezi kufanikiwa bali unatafuta kuangamizwa.

2 SAMWELI 12:9-10

“Kwa nini umelidharau neno la BWANA……….Basi, sasa upanga hautaondoka nyumbani mwako, KWA SABABU UMENIDHARAU“.

HESABU 15:31:

“Kwa sababu amelidharau neno la BWANA……….mtu huyo atakatiliwa mbali……….”.

HATUPASWI KUOGOPA, MUNGU MWENYE NGUVU YUKO PAMOJA NASI.

Yeye mwenye nguvu na uwezo wote yuko upande wetu watu tuliookoka. Kwa nini uogope? Kwa nini usimtumaini?

MWANZO 26:24, “…………… Usiogope, maana mimi ni pamoja nawe ………”

ISAYA 41:10, “Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu naam nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu”.

TUNAPASWA KUMTUMAINI MUNGU NA KUMWOMBA
Tunapokabiliana na mazingira yoyote ya maisha, iwe ni mateso mwilini, magonjwa kwa watoto na ndugu, hali mbaya ya kibiashara, masimango kazini, kutokufanikiwa kikazi au masomoni, vitisho vya wachawi kwamba watatuua, au mazingira yoyote yale magumu, hatupaswi kuogopa bali kutumaini na kumwomba BWANA. Yeye ana nguvu za kutushindia. [SOMA ZABURI 31:13-15, ZABURI 3:4,6] Tutaendelea kumwomba BWANA kwa kutumaini huku tukiwa na moyo imara, na lazima tutawaona watesi wetu wakishindwa.

ZABURI 112:7,8:

“Hataogopa habari mbaya; moyo wake u imara ukimtumaini BWANA. Moyo wake umethibitika hataogopa, hata awaone watesi wake wameshindwa”.

KUNA BARAKA KUU KATIKA KUMTUMAINI BWANA ALIYETUOKOA

ISAYA 57:13:

“……. Anayenitumaini ataimiliki nchi, na kuurithi mlima wangu mtakatifu”.

MISTARI YA KUIWEKA MOYONI

ZABURI 91:2:

“Nitasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini”.

KUTOKA 14:13-14:

“Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele, Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.”

ZABURI 20:7:

“Hawa wanataja magari na hawa farasi, bali sisi tutalitaja jina la BWANA, Mungu wetu.”Je! kuna jambo lililo gumu linalokukabili katika maisha yako? Je, ni ugonjwa ulioshindikana? Je ni vitisho vya Uchawi au kuachiwa “laana” na wazazi kwa ajili ya kuokoka? Je ni kutishwa kufukuzwa na mumeo au nduguzo sababu ya wokovu? Je ni masomo magumu? Je ni kukosa mtoto? Je ni vitisho vya kufukuzwa kazi? Je ni vitisho kwamba hutafanikiwa katika biashara yako? Ni nini? USIOGOPE, SIMAMA TU UKAUONE WOKOVU WA BWANA. Iambie nafsi yako na jirani yako pia, “NITAMTUMAINI, SITAOGOPA.”

SOMO: FIMBO NI INJILI YA MTOTO (2)

$
0
0
Kelvin Kitaso,
GK Contributor.

picha ya mtandao
Wiki iliyopita tulitazama dhana nzima ya fimbo kwa ufupi, unaweza kubofya hapa kusoma kisha uendelee na sehemu hii ya pili.

Kwa nini adhabu ya viboko ni muhimu kwa mtoto.    
ü  Ni ishara ya upendo wa mzazi kwa mtoto wake kwa kuonyesha hutaki apotee, afanye makosa na kuharibikiwa. “Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi, basi uwe na bidii ukatubu (Yohana 3:19).” Na Mithali 13:24 “Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanae bali yeye ampendae humrudi mapema”

  • Huleta faida kwa mtoto ya kuwa makini sana kwa vile atendavyo na umfanya kufanya vitu makini. Mithali 19:18 “Mrudi mwanao, kwa maana lipo tumaini, wala usikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake.” 

  • Huondoa ujinga ambao umefungwa ndani ya mtoto, Mithali 22:15“Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali”

  • Humpa kuijua njia ya kuiendea ambayo hataiacha hata akiwa mkubwa.

  • Humfanya kukuheshimu na kuheshimu jamii ya watu wakubwa, Mithali 29:15 “Fimbo na maonyo hutia hekima; Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye”.

  • Watoto wengi wamekuwa na nidhamu ya uoga ila si heshima. Wanavyofanya mbele za watu ni kama wana heshima ila wamejaa nidhamu ya uoga.

  • Humfanya kuwa mtoto wa tabia njema ambaye uweza changia kubadilisha watoto wenzake wakawa na tabia njema pia.

  • Humfanya mtoto kuwa na hofu ya kurudia kosa kwa kuwa anajua akirudia ni lazima atapigwa tena. Ni kwa kupitia viboko mtoto aweza jua ipi ni sahihi na ipi si sahihi.

  • Huongeza umakini kwa mtoto hata kwenye hatua ya Kufanya mambo kwa umakini mkubwa (smart).

  • Humfanya mtoto akuletee sifa njema katika jamii inayokuzunguka, Mithali 29:17 “Mrudi mwanao naye atakustarehesha; Naam atakufurahisha nafsi yako.”

  • Humuongezea kibari yeye na wewe mbele za Mungu kwa kule kurekebishika kwa tabia.

Adhabu katika wakati wa kutolewa kwake huwa ni kitu kibaya sana ila uleta matokeo mazuri kwake yeye aipokeaye. Fimbo ni jambo la umuhimu sana katika malezi bora, suala la vyombo vikubwa vya kimataifa kukataza adhabu ya viboko kwa mtoto ni kupingana na Mungu na hii ni mbinu ya shetani ya kuchafua kizazi kilichopo sasa. 
“kumbuka kuwa samaki hukunjwa akiwa mbichi na akikauka hakunjiki tena na hata kama ukimkunja wajisumbua bure tu kwa kuwa ameshakauka na kumsababishia maumivu ambayo hayawezi kumkunja na ukilazimisha waweza mvunja”


Namna ya kutoa adhabu ya viboko kwa mtoto.
Wengi wamekuwa wakikili kuwa adhabu ya viboko haifai kwa vile walivyowahi kuitumia na ikasababisha watu wakawa sugu au kwa vile walivyoona wengine wakiitumia na ikasababisha bado kuharibikiwa kwa watoto kwa kuwa watoto wengine uwa sugu pasipo kujali adhabu hiyo itolewapo kwao.
Si kila kiboko kinaweza kuleta matokeo mema niliyoyataja hapo juu, ila ni kiboko kitolewacho kwa njia sahihi, kwa wakati sahihi na juu ya jambo sahihi. Namna njema ya kutoa adhabu kwa mtoto ni kwa mzazi kurejea kwenye zile nafasi za yeye kama mzazi kwa kuangalia anapaswa kufanya nini kama kiongzi, mwalimu na rafiki, nakadharika.
Kama kiongozi, mzazi hutoa adhabu na huku akimsaidia mtoto kuijua njia na kutembea katika njia, na kama mkufunzi anapaswa kumchapa mtoto huku hakimfanya kujua ni kwa sababu gani anamchapa na kumfundisha ili kwa siku nyingine asijerudia tena, na kama rafiki huweza kuifanya kazi yake kwa kuwa karibu naye ili aweze kufahamu mengi, ila ni vyema kuzingatia kuwa hii nafasi ya urafiki haifanyi kazi sana katika wakati huu wa adhabu.

Ukali, adhabu ya viboko na makelele  havitoshi kumfunza mtoto katika njia impasayo
Ni ukweli kabisa kuwa wapo wazazi wengi sana ambao wametumia muda wao mwingi kupiga makelele kwa watoto wao kuhusu tabia mbaya na wengine wamekuwa wakali sana na huogopwa kila wakati wafikapo mbele za watoto wao, na utumia fimbo kila wakoseapo watoto wao, ila kwa jitihada zote hizo bado juhudi zao zinagonga mwamba kwa kutokuwa na matunda mazuri ya kuwakuza watoto hao, hii ni kwa sababu ukali, fimbo na makelele mengi havitoshi kumfanya mtoto abadilike, ila kutumia fimbo pamoja na kumfunza neno la Mungu na likakaa vizuri ndani umfanya mtoto kuwa na hofu ya Mungu ambayo itamzuia kujishughulisha katika uovu ajishughulishao.
Ni neno la Mungu ndilo lina nguvu ya kumkuza mtoto likiambatanishwa na fimbo pale makosa yanapotokea ila likikaa vizuri ndani litamfanya mtoto kujua ni yapi yaliyo makusudi ya Mungu. 

Katika mfululizo wa somo la namna ya kumlea mtoto katika njia ipasayo (soma hapa) wiki ijayo tutatazamia malezi ya Yesu na malezi ya Samweli.
_____
Mwalimu Kelvin Kitaso anapatikana kupitia 0767190019 / 0713804078 na pia kupitia barua pepe; kitasokelvin@gmail.com


NIDHAMU HUJENGA MAFANIKIO YASIYO NA UKOMO

$
0
0
Faraja Mndeme,
GK Contributor.


Huwezi kutenganisha mafanikio na mtu kwenye jambo lolote lile na nidhamu yake. Nidhamu ni jambo ambalo linajenga mafanikio yasiyo na ukomo na hudumu kwa muda mrefu hata usipokuwepo. Mfumo wa maisha yetu kwenye kila jambo umejengwa kwenye nidhamu. Ili ufanikiwe kwenye jambo fulani ni lazima uwe na aina fulani ya nidhamu.

Maisha ya mwanadamu yamejengwa kwenye mfumo wa nidhamu. Bila nidhamu kwenye mambo mbalimbali basi kusingekuwa na mfumo mzuri na bora kwenye maisha yetu ya kila siku. Ukiona maisha yanaendelea na vitu mbali mbali vinafanikiwa na kutokea, basi tambua kuna aina fulani ya nidhamu ilijengwa vyema juu ya nidhamu katika jambo husika. Mafanikio huendana na nidhamu.

Nidhamu huongeza siku za kuishi. Mara nyingi tumekuwa na maswali mbali mbali. Je ni namna gani wanadamu wa kale waliweza kuishi kwa muda mrefu zaidi kuliko binadamu wa sasa? Jibu naloweza kukupa haraka haraka ni aina ya nidhamu waliyokuwa nayo. Nidhamu hiyo ilikuwa imejengwa katika mfumo wa vyakula. Kuna aina fulani ya vyakula vililiwa na pia nidhamu kwenye namna ya kulinda afya zao. Nidhamu kwenye utumizi na ulinzi wa afya zao. Watu wa kale walijenga mfumo ambao nidhamu ilianzia kwenye familia hadi nje ya familia ndio maana hata mmoja wa wanafamilia alipokiuka taratibu za maisha basi alihukumiwa na kuadhibiwa na familia.

Nidhamu itakufanya usonge mbele haraka zaidi kuliko wengine. Mafanikio ya mtu ni nidhamu ya mtu. Ukimuona mtu amefanikiwa kwenye swala la fedha basi tambua kuwa mtu huyo kwenye swala la pesa amejenga nidhamu ya hali ya juu. Unaweza kumkumta mtu ni tajiri lakini fedha kwake haitoki kirahisi na mpaka uipate umefanya kazi ya ziada. Kiukweli si kwamba hapendi kutoa bali aina ya nidhamu aliyoijenga mpaka kufikia hatua ya kuipata hiyo fedha ndio inayomuongoza namna ya kutoa fedha. Huwezi kutofautisha nidhamu ya mtu kwenye maswala ya fedha na mafanikio yake. Nidhamu ya mtu aliyefanikiwa katika maswala ya fedha imejengwa katika sehemu kuu mbili; mapato na matumizi. Huwezi kumkuta mtu mwenye mafanikio ya fedha anatumia fedha hovyo hovyo bila kuwepo na bajeti ya matumizi.

Nidhamu kwenye Afya. Unapomuona mtu ana afya njema na haugui hugui kila wakati, basi tambua kuna aina fulani ya nidhamu ambayo amejijengea kwenye afya yake. Unaweza kumkuta mtu huyo kila jioni anafanya mazoezi, analala vyema na anakula vyema. Mtu huyu amezingatia kanuni na taratibu zinazofanya afya yake iwe muhimu. Huwezi kumkuta anavuta sigara au anakunywa aina fulani ya vilevi, si kwasababu havipendi, ila ameona afya yake ni bora kuliko vilevi hivyo. Mtu huyu ukimfwatilia utagundua mfumo mzima wa maisha yake umejengwa katika nidhamu iliyo thabiti na isiyotikisika ili kuiweka afya yake kwenye hali njema na salama.

Nimezungumzia maeneo machache kwa sehemu tu kuonyesha namna nidhamu ilivyo na sehemu kubwa na mchango mkubwa kwenye maisha yetu wandamu. Hauwezi kutenganisha maisha ya mwanadamu na mafanikio aliyo nayo na nidhamu yake. Ukiona mtu amefanikiwa katika ndoa, uchumi, kiroho, na hata kijamii utagundua kuna aina fulani ya nidhamu ambayo ameiwekeza kwa kiwango cha juu tofauti na watu wengine ambayo inafanya aende mbele zaidi ya wengine. Maisha ni nidhamu, na nidhamu ni maisha. Bila hivi hatuwezi kufurahia maisha wala hatutafanikiwa kwenye jambo lolote maana tumekiuka sheria za uhai wa mwanadamu na mfumo mzima na taratibu za kuishi.

Email : naki1419@gmail.com
+255788454585
God Bless You All

SOMO: JE WEWE NI KUKU AMA TAI

$
0
0
Elie Chansa,
GK Staff Writer.

©Smarty Brain
Rafiki yangu mmoja alinigusia kuhusu hadithi ya tai na kuku, nikahamasika kuifuatilia zaidi, ikanifunza jambo na kunifunua. Nimebarikiwa kukufikishia ujumbe huu.

Hapo zamani kulikuwa na tai ambaye alilelewa kwenye familia ya kuku, yaani tangu kuzaliwa (kutotoka kwenye yai) hadi akawa mkubwa, hakuwahi kuwa nje ya familia ya kuku.

Mama kuku alikuwa mwenye upendo sana, na alimlelea pasi na tofauti yoyote. kifufupi alikuwa mtoto wake. Alifunzwa kula kama kuku, kujinyoosha kama kuku, kunywa kama kuku na kutembea kama kuku. Zaidi ya rangi na umbile, hakuwa tofauti na kuku wenzake. Amecheza nao, amekua nao, na anaishi nao kama kawaida.

Siku moja yule tai (hebu tumuite kadogoo) katika cheza cheza yao na parua parua ya kusaka chakula kwenye udongo na majalalani, aliona kitu chenye kupendeza sana kikipita angani, akakipenda sana. Akauliza wenzake, ile ni nini? Akaambiwa, wale ni ndege aina ya tai, wao maisha yao ni ya namna hiyo, wana nguvu kubwa mno tofauti na sisi kuku, hatuwawezi katu.

Na hata Kadogoo alipotaka kuonesha shauku ya kuuliza zaidi kwa nini ni kama anafanana nao, alishutumiwa vikali na baadhi ya wenzake, wakimwambia; “mbona wewe huna shukurani, umekosa kitu gani hapa nyumbani hadi utake kujifananisha nao, wewe ni kuku tu, na utabakia hivyo”.

Na kweli yule tai akaridhika, maisha yakaendelea akiwa kuku, na si tai tena. Aliishi maisha yake mazuri tu, na alikuka kufa akiwa kuku.

Kuna jambo ambalo Mungu ameweka ndani yako na anataka ulitimize, lakini kuna kuku wanakuambia kwamba hiyo si saizi yako, ina wenyewe. Kwamba umri wako haukurushu kuwa diwani ama mbunge, kwamba asili yako huwezi kufanya kazi ya aina fulani. Kwamba elimu yako haitakufikisha popote, kwamba ule mradi unaotaka kuanza utakutia hasara kubwa - na kwamba usithubutu katu. Haya yote umeridhika kuyasikia kwasababu unaishi 'good life', bila kufahamu kwamba unastahili "a better life’. Ukisalia kwenye good life, utakufa na good life na kuku ‘wenzako’ bila ya kutambua kwanini Mungu alikupa mabawa makubwa yenye kukufanya uruke juu sana na kuelea angani kinyume na uelekeo wa upepo.

©Google Maps

Hutajua kwanini Mungu alikupa macho makali ya kuona umbali mrefu sana na kuchambua bidhaa iliyo njema dhidi ya bidhaa chakavu. (tai huweza kumuona sungura umbali wa kilomita 3.2, yaani kwa lugha rahisi anaona kutoka Ubungo hadi Mwananchi), ama kama hujui hiyo njia, basi ni kutoka Ubungo - Mlimani City iache uende mbele zaidi karibu na wanapochonga vinyago. Ndipo umbali huo). Ana uwezo wa kujinyonyoa mabawa na kujawa na nguvu mpya licha ya uzee.

Hizi zote ni baadhi tu ya ahadi za Mungu kwetu, maana tunatambua ya kwamba sisi tu washindi zaidi ya washindi (We are MORE THAN CONQUERORS.) Na pasi na shaka tunayaweza yote kupitia yeye (Mungu) atutiaye nguvu. Sasa wewe aliyekuambia better life si kwa ajili yako ni nani hata ukamkubalia na kuridhika? Unaweza kuwa vile utakavyo. Asitokee mtu akakueleza kwamba wewe huwezi kufanya jambo fulani kwa sababu kadha wa kadha - nawe ukamkubalia.

Muigizaji maarufu duniani, Arnold Schwarzenegger amepitia mengi katika safari yake hadi kutoka kwenye tasnia ya filamu huko Hollywood, Marekani. Katika safari yake akiwa bado mbeba vitu vizito, amewahi kuambiwa, "you are nothing but a bunch of muscles", kwamba yeye si kitu bali ni jamaa tu kama boya lililojaa misuli, mara kwamba lafudhi yake ni kituko, hatoweza kuongea mbele ya watu.. na kila aina ya dhihaka.

Lakini alichokifanya Schwarzenegger ni kufanya tofauti na kile ambacho watu wanasema. Aliamua kudhihirisha kwamba maneno yao si mawazo aliyokuwa nayo Mungu kwa ajili yake. Hakufikia kukata tamaa kwenye hararakati zake, na katika kuonesha juhudi anasema, "nilikuwa nafanya mazoezi mara kwa mara, na kitu ambacho watu walisema sitaweza kukinyanyua, basi mi niliamua kutilia mkazo ili niwaache mdomo wazi pale nitakapofanikiwa."  Mwisho wa siku Arnold amepata tuzo kadhaa kwenye uigizaji, ushindi kadhaa kwenye unyanyuaji wa vitu vizito, na hata kufanikiwa kuwa gavana wa jimbo la California kwa vipindi viwili, 2004-2011. Mifano iko mingi ambayo ningeweza kuelezea, lakini nukuu mojawapo ambayo huwa anaifanyia kazi ni, "you can not climb the ladder of success with your hand in the pocket". Yani kwamba huwezi kuikwea ngazi ya mafanikio ukiwa umeweka mikono yako mfukoni.

Chochote kilichopo ndani yako, anza sasa kukifanyia kazi kwa bidii bila kujali kuku wanakusemaje ama wanakutazamaje. Unaweza kufanikiwa, maana Mungu ameweka kitu ndani yako, usife nacho kama tai aliyeaminishwa na maneno ya watu akashindwa kutumia kile alichopewa. Uwe na safari yenye mafanikio.


UKIRI
___
BWANA Yesu ahsante kwa ufunuo huu, niwezeshe kuishi kulingana na mapenzi yako. Badili ninavyofikiri BWANA. Ninaomba uandae watu watakaoambatana nami, ili kusudi lako juu ya maisha yangu lipate kutimia. Ninaomba haya kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu, Amen!

ALIYEJIITA MUNGU AFARIKI NA KUACHA WAKE 35 NA WATOTO 95

$
0
0
Jehovah Wanyonyi ©Nationa Media Group
Wahenga walisema; “duniani kuna mambo.” Jamaa mmoja aliyejiita ‘mungu’ huko nchini Kenya, Jehova Wanyanyi amefariki duniani na kuacha wake 35 na watoto zaidi ya 95.

Wanyonyi alizaliwa mwaka 1924 magharibi mwa Kenya, karibu na Mlima Elgon ambako anatambuliwa kama Mlima Sayuni.

Wanafamilia na waumini wa kiongozi huyo wa dini aliyoianzisha na kuiongoza, wanasisitiza kuwa ‘mungu’ wao bado yupo hai, ingawa uongozi wa Serikali ya kijiji alichokuwa akiishi unasema Wanyanyi alifariki dunia Julai 18 mwaka huu.

Taarifa za kufariki dunia kwa Wanyanyi zilianza kusambaa tangu Julai mwaka huu, lakini ndugu zake walikuwa wakisisitiza kuwa mungu wao hajafa na kwamba hakuna mwenye mamlaka ya kuhoji mahali alipo.

Baadhi ya viongozi katika eneo alilokuwa akiishi Wanyonyi wanasema kuwa ‘mungu’ huyo alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa katika Hospitali ya Kitale baada ya kuzidiwa.

“Wanafamilia walikuja kwangu kuomba kibali cha mazishi, baada ya aliyejiita Jehova Wanyonyi kushikwa na ugonjwa akiwa njiani kwenda Cherangany Nursing Home Kitale mjini,” alisema Chifu Kipsomba Daniel Busienei alipozungumza na gazeti la The Standard la Kenya.

Chifu Busienei alisema wanafamilia walikwendea kumwomba kibali ya mazishi ili waende hospitali wakachukue mwili wa Wanyonyi kwa kuwa wasingekabidhiwa maiti hiyo bila ya kuwa na kibali hicho.

“Nilimwambia msaidizi wangu awape kibali, waende wakampumzishe Wanyonyi,” alisema Chied Busienei.

Msaidizi wa chifu, Paul Bett anathibitisha kuwa alitoa kibali kwa familia hiyo Julai 19, siku moja baada ya uvumi kuenea kuwa Wanyonyi amefariki dunia.

“Alifariki dunia Julai 18, akiwa njiani kuelekea hospitali na kijana wake ndiye aliyekuja kuomba kibali siku iliyofuata,” alisema Bett.

Wiki mbili zilizopita vyombo vya habari vilizuiliwa kuingia katika makazi ya Wanyanyi yaliyopo katika Kijiji cha Chemororoch, Jimbo la Soy kwa maelezo kwamba ‘mungu’ wao alikuwa mzima wa afya.

Waandishi hao walifika katika eneo hilo baada ya kupata taarifa kuwa Wanyonyi amefariki dunia. Baadhi ya wanafamilia wakiwamo watoto na wake zao, walisema kuwa mungu wao mwenye enzi alikuwa salama.

Awali, ilielezwa kuwa Jehova amelazwa katika Hospitali ya Cherangany kabla ya kusafirishwa kwenda katika Hospitali ya Rufaa ya Moi huko Eldoret.

Hata hivyo, utata wa kifo hicho uliongezeka baada ya waandishi wa habari kushindwa kuliona jina la ‘mungu’ huyo katika orodha ya majina ya watu waliokuwa wamehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.

Utata wa kifo cha mungu huyo aliyekuwa kiongozi wa huduma ya Lost Israelites of Kenya, yenye wafuasi wengi katika mpaka wa majimbo ya Uasin Gishu na Kakamega, ulichochewa na maoni tofauti yaliyokuwa yakitolewa na watu mbalimbali.

Msemaji wa familia ya kiongozi huyo, Eliab Masinde aliendelea kukanusha kuwa mauti imemchukua mungu wao, licha ya uongozi kuthibitisha kifo hicho.

Masinde alisema: “Jehova ni mzima, ingawa hali yake si nzuri sana, amelazwa katika moja ya hospitali jijini Nairobi akipatiwa matibabu kwa usimamizi wa watoto wake wawili.”

“Alikuwa na maumivu ya mgongo kwa muda mrefu, lakini alipelekwa hospitali na watoto wake huko Nairobi. Mungu huwa hafi, kama angekuwa amekufa, tungeshapata taarifa,” alisema Masinde.

Msemaji huyo wa familia ambaye pia ni mwangalizi wa madhabahu wa huduma hiyo, alisema majirani wa Wanyonyi waliomwona alipokuwa akipelekwa hospitali ndio walioeneza uvumi wa kifo chake.

Mkazi mmoja wa kijijini hapo, ambaye hakutaka kutaja jina kwa kuihofia familia ya mungu huyo, alisema kiongozi huyo alifariki ingawa wanafamilia wanaficha suala hilo.

“Jehova alikuwa ana maumivu ya mgongo kwa muda mrefu, alikuwa anatembelea kiti cha magurudumu kabla hajatoweka. Alikuwa ni mzee na tunachokijua, familia inatawa kumweka mrithi wake kwa siri,” alisema.

Anaongeza kuwa Jehova ana wafuasi wengine nchini Uganda na kwamba inawezekana mwili wake umepelekwa huko kwa ajili ya mazishi.

Tangu taarifa za kifo hicho kutolewa, waumini wengi wamekuwa wakifika nyumbani kwa kiongozi wanayemtaja kuwa ni ‘mungu aliye hai’ kumwombea ili apate nafuu haraka.

Baadhi ya wananchi wamekuwa na maoni tofauti kuhusu kifo hicho, huku wengine wakisema haiwezekani mungu kufariki dunia.

John Paul alisema kupitia mtandao kuwa: “Inakuwaje mungu akafa au kuugua? Kama kweli alikuwa mungu, hakupaswa hata kuugua, achilia mbali kifo.”


Wanavyoabudu


Waumini wa Wanyanyi, husujudu mbele yake na kuomba wanachotaka. Mwandishi wa BBC, Muliro Terewa aliingia katika kanisa hilo na kumsikia muumini akisali:

“Mungu mkuu, uliyekuwepo, upo na utakuwepo Jehova. Wewe ndiye aliyezungumzwa kwenye Biblia katika Kitabu cha Isaya 11. Tunakuheshimu kwa sababu kama ulivyosema mwisho umekaribia, tunaomba utuongoze kwenda mbinguni.”

Akihojiwa na BBC, Wanyonyi alisema:”Mimi ni masikini nina watoto 95 wa kuwalisha. Waangalie watoto hawa, hawajala kitu chochote asubuhi hii, nahitaji dola 13 (Sh26, 000) niwanunulie mikate.”

‘Mungu’ huyo alisema aliingia kwenye mwili wa mwanadamu miaka mingi iliyopita kama ilivyoandikwa katika vitabu vitakatifu.

Aliongeza: “Jehova nilimtuma mwana wangu kuwaokoa watu wake lakini wanakataa, hivyo nimeamua kuja mwenyewe labda watu wanaweza kuacha uovu wao.” Alihadharisha kuwa kama hawatakubali na kubadilika, ataagiza moto kutoka mbinguni uwachome, lakini wanaoamini kuwa yeye ni mungu hawataungua.

Waumini wa Wanyanyi wanasema wameshuhudia ‘mungu’ wao akifanya miujiza, ukiwamo ule wa mume na mke waliokuwa wakiugua Ukimwi kupona kabisa.

Hata hivyo, wakati waumini wake wakipaza sauti kuwa Wanyonyi ni ‘mungu’, baadhi ya watu walitishia kumuua iwapo wangemtia mikononi mwao.

“Wanyonyi ni nabii wa uongo. Ni miongoni mwa manabii wa uongo waliosemwa kwenye Biblia,” alisema Mchungaji Julius Makona.

Patrick Busolo alisema: “Wanyanyi siyo Mungu, anajikusanyia mali tu kwa kutumia imani aliyowajengea waumini wake. Anawalazimisha watu wamfanyie kazi ili aweze kuishi vizuri.”

Wanyanyi alisema kuwa aliuteremsha Ukimwi duniani kama adhabu kwa wanadamu wanaodharau amri za Mungu.

Wakati ikithibitika kuwa ‘mungu’ Wanyanyi amefariki dunia, kazi iliyobaki ni kwa waumini wake kumteua kiongozi mwingine atakayesimamia mamia ya waumini wa dhehebu hilo.

Pia, itakumbukwa kwamba, ‘mungu’ huyo alikuwa akisisitiza kwamba hakuna Mungu mwingine isipokuwa yeye pekee aliyeumba vitu vyote. Kiongozi ajaye atasema ametoka wapi?

Bila shaka jibu wanalo waumini wa The Lost Israelites, wanaoomboleza kifo cha ‘mungu’ wao.

Gazeti Mwananchi limeandika.

KWA TAARIFA YAKO: MTAYARISHAJI NA MUIMBAJI ANAYEJIANDAA KUMALIZA 2015 KWA KISHINDO

$
0
0
Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu

Watayarishaji wa muziki, Goodluck Gozbert na Gaston.
Jina Goodluck Gozbert linabeba taswirwa nyingi kwenye tasnia ya muziki wa injili. Kwa upande mmoja ni mtayarishaji wa muziki, kwa upande mwingine ni mwandishi na mtunzi wa nyimbo. Achilia mbali uimbaji.

Goodluck Gozbert ameanza huduma ya uimbaji mwaka 2004 akiwa mwanakwaya katika Kanisa la KKKT Usharika wa Imani Mwanza. KWA TAARIFA YAKO mwaka 2008 aliingia studio kwa mara ya kwanza na kufanya album ambayo aliipa jina la, "Nimelipiwa Deni".


Safari haikuishia hapo kwani mwaka 2012 mara baada ya kuwa amemaliza masomo yake ya kidato cha sita aliingia studio na kurekodi album aliyoipa jina la Nimeuona. Na KW TAARIFA YAKO mwaka huu 2015 mnamo mwezi wa kwanza aliachia single inayokwenda kwa jina la Acha Waambiane, kwa mfumo wa sauti na picha za sauti (audio na video), ambapo wimbo huo ulipata kibali na nafasi ya kuchezwa katika vituo vyote vya Redio na Runinga ndani na nje ya nchi.


Kwa sasa Goodluck ameachia wimbo wake mpya unaoitwa Ipo Siku, ambayo imebeba jina la albam yake mpya, anayotarajia kuiachia mwezi huu, Agosti 2015.

Kwa upande wa kuwa mtayarishaji, halikuwa jambo jipya sana kwake, kwani alikuwa akifanya tokea akiwa shuleni, na hivyo alipomaliza kidato cha sita aliingia rasmi. KWA TAARIFA YAKO sababu mojawapo pia ni kutokana na vikwazo ambavyo amekuwa akikutana nazo kila alipokuwa akienda studio. Hatimaye akaamua kuanzisha Mini Sound, jina la studio yake.

©Examiner UK

Kama ambavyo watu kadha wa kadha wamekuwa na majina mbalimbali, Goodluck yeye hujita Lollipop Man, yaani kwa lugha rahisi, ni mtu anayesaidia kuvusha watu barabarani, mathalani wanafunzi na hata wale wasiojiweza (hasa kwa nchi zilizoendelea). hivyo KWA TAARIFA YAKO lengo lake hasa ni kuvusha watu kutoka hatua moja kwenda nyingine, hasa waimbaji.

Katika hatua nyingine, Goodluck, ambaye anaeleza kwamba yeye kurekodi na kuimba si tatizo kwake, na kwamba namna pekee ya kuepukana na changamoto za ujana ni kumuweka Mungu kwanza, maana kupitia yeye tunayaweza yote.

Sikiliza Ipo Siku, huku ukiimba sanjari na mashairi yake.


Mashairi ya Goodluck Gozbert, Ipo Siku

Ubeti wa 1

Ni Mbali Nimetoka tena Ni ajabu kuwa Hai Maana Ningeshakufaga
Ni mengi Nimeona tena Ya Kuvunja Moyo Labda Ningeshamwacha Mungu

Kibwagizo
Kama Ni Misongo ya Mawazo, Magonjwa Mama, Nimepitia, Ninajipa Moyo

Kiitikio
Ipo siku Yangu Tu Ipo Siku Ipo siku Yangu Tu, Nami Nibarikiwe Nami Nibarikiwe (Nibarikiwe) Aah Nibarikiwe (Nibarikiwe) Nami Nibarikiwe (Nibarikiwe) Niba, Niba, Nibarikiwe

Ubeti wa 2
Ingawa kwa sasa Wananisema vibaya Nami sishangai Najua ni ya Wanadamu Hayo Ingawa sipati Na ni Kwa Muda Mrefu Siachi Kuomba, Mungu Si Kiziwi Binadamu Wema, Ukiwa nacho, Kwa Sasa Wani epuka Sina Rafiki wa dhati Bridge

Kiitikio

Ipo siku Yangu Tu Ipo Siku Ipo siku Yangu Tu, Nami Nibarikiwe Nami Nibarikiwe ( Nibarikiwe) Aah Nibarikiwe ( Nibarikiwe) Nami Nibarikiwe ( Nibarikiwe) Niba, Niba, Nibarikiwe

Ubeti wa 3
Miaka Imepita Unaombaga Mtoto Hupati, Vuta Subira Maana Yeye Hachelewi, Ona Biashara Imeandamwa Mikosi Hupati, Usimwache Mungu Waganga Watakuponza,

Mpo Kwa Ndoa Ila nyumbani Amani Hakuna

Msimwache Mungu Michepuko sio Jibu

Umeugua Tumaini La Kupona Hakuna, Usimtazame Mwanadamu Siku Yako Imekaribia,

Kibwagizo cha 2
Najua Ayaya x ( Ipo Oo aaaah) Najua Ayaya x ( Ipoo Oo aaah)

Ubeti wa 4
Misuko Suko Ya Ndoa Mtoto Anakusumbua Giza Likiingia Unawaza Wapi Utalala Masimango Mashemeji Ati Huzai Mtoto Masimango Mama Wa Kambo Umemchosha Nyumbani Usiwaze Usiumie Najua yote Yatapita Nawe Ubarikiwe ( Nibarikiwe) Aah Ubarikiwe ( Nibarikiwe) Nawe Ubarikiwe ( Nibarikiwe) Niba, Niba, Nibarikiweee

Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO kwa wiki hii tukiwa na Goodluck Gozbert, vinginevyo tukutane wiki ijayo...

SOMO: KUJENGA KATIKATI YA UPINZANI - ASKOFU GWAJIMA

$
0
0


ASKOFU MKUU Dr. JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: Kujenga Katikati ya Upinzani


“katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danielii, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini.” Danie 9:2 - 27

Waana wa Israeli walipotoka katika nchi ya Misri Mungu aliwapa Sheria ambazo kwa hizo wakizishika watafaninikiwa na wasipozishika ataruhusu mfalme wa Babeli nebkadneza kuwachukua na kuwapeleka babeli kwa muda wa miaka sabuni wale chakula cha taabu kwa muda wa maka sabini na kulala kwa shida kwa muda wa miaka sabini, Danieli aligundua kwa kusoma vitabu miaka imetimia.

“Basi adui za Yuda na Benyamini, waliposikia ya kuwa wana wa uhamisho wanamjengea Bwana, Mungu wa Israeli, hekalu, wakamkaribia Zerubabeli, na wakuu wa mbari za mababa, wakawaambia, Na tujenge sisi nasi pamoja nanyi; kwa maana tunamtafuta Mungu wenu kama ninyi, nasi twamtolea dhabihu tangu zamani za Esar-hadoni, mfalme wa Ashuru, aliyetupandisha mpaka hapa. Lakini Zerubabeli, na Yoshua, na wakuu wengine wa mbari za mababa katika Israeli, wakawaambia, Ninyi haiwahusu kushirikiana nasi katika kumjengea Mungu wetu nyumba; bali sisi wenyewe peke yetu tutamjengea Bwana, Mungu wa Israeli, nyumba, kama mfalme Koreshi, mfalme wa Uajemi, alivyotuamuru. Ndipo watu wa nchi wakaidhoofisha mikono ya watu wa Yuda, wakawasumbua, walipokuwa wakijenga. Wakawaajiri washauri juu yao, ili kuwapinga kusudi lao, siku zote za Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata wakati wa kutawala kwake Dario, mfalme wa Uajemi. Tena, wakati wa kutawala kwake Ahasuero, mwanzo wa kutawala kwake, watu wakaandika mashitaka juu ya wenyeji wa Yuda na Yerusalemu.” Ezra 4:1-24

Utawala wa uajemi ulikuwa na nguvu mwaka wa mia sita na sita kabla ya kuzaliwa kristo, ulikuwa na nguvu kama Marekani ilivyo leo. Mfalme mpaka koreshi akafariki na akatokea mwingine tena akafa na alipotokea mfalme wa tatu akasema roho yake imeamua iwaache waende nyumbani kwao wakamjengee Bwana wao nyumba, tunajifunza kumbe yule wa kukuumiza muda wake ukifika ule uwezo wake wa kukushikilia unakwisha na kuamua akuruhusu uende zako.

Mfalme koreshi aliamua kuandika barua kwamba wana wa Israeli waende nyumbani kwao, na walipofika maadui wakaamua wajichanganye nao ndani ili wajenge pamoja, adui anatabia ya kujipenyeza ili naye aonekane anajenga pamoja na wewe kumbe anabomoa, Joshua alipoona hayo aliwajibu haiwahusu na wakaamua wajenge wenyewe.

Mfalme Koresh alipowaruhusu wana wa Israeli warudi wakamjengee Mungu wao hawakwenda muda ule ule bali ilipita miaka mpaka mingi mpaka Mfalme aliyewaruhusu akafariki na akaja mwingine, sio kwavile Mungu amekwisha kusema jambo fulani inakuwa muda huo huo bali hupita muda fulani ndipo jambo lile litokee kwa kumtumia mtu, Mungu alipotaka kumwangusha haman alimtumia Esta, Mungu alipotaka kugawa bahari ya shamu alimtumia Musa, Mungu alipotaka kuwakomboa watu alimtumia Yesu, Mungu anatafuta mtu wa kurusha makombora mahali panapotakiwa kurushwa, kwenye kila kizazi Mungu hutumia watu kuwavusha watu waende kwenye ahadi zao. Kwenye kizazi hiki Mungu anakutumia wewe uipeleke nchi ya Tanzania ivuke mpaka mahali inapotakiwai kufika. Ukinyamaza hakuna kitakachofanyika lazima uamke uipeleke nchi mahali inapotakiwa kufika kama balozi wa Ufalme wa mbinguni duniani.

Mungu huinua watu wakuvushe pale shetani anapokuvunja moyo ili usiendelee mbele.

Ukiri:
“Ninaamuru kwenye ulimwengu wa roho tukio litokee la kukutia moyo uende kwenye mafanikio yako kwa jina la Yesu.”

Wana wa Israeli walipovunjwa moyo mikono yao ilidhohofika wakashindwa kuendelea kumjengea Mungu nyumba, njia moja ya adui anaweza kuitumia ni kulegeza mikono yako ili usiendelee mbele.

Silaha tatu zimetumika ili kuzuia kusudi la Mungu lisifanywe na wana wa Israeli, ya kwanza imetumika kuomba kujiunga nao ikashindikana, ya pili ni ile ya kuvunjwa moyo mpaka mikono yao ikalegea, walivunjwa moyo miaka miwili na hawakulifanya kusudi la Mungu lakini baadaye wakatokea watu wawili hagai na zekaria ambao wao walikuwa si wajenzi waliwakuta watu wamekata tamaa wakaanza kuwachochea kwa kuwaambia inukeni mumjengee Bwana anasema adui zenu wamewekwa chini yenu, Bwana amesema adui zenu wamejikwaa na kuanguka ndipo walipoamka na kuendelea kujenga, silaha nyingine ni ile ya kwenda kuwashitakia kwa mfalme ili awaondolee kibali wasinjenge nayo haikufanikiwa bali mfalme aliwalinda mpaka wakamaliza ujenzi. Tunatakiwa tuamke tuijenge Tanzania liwe taifa jipya la kustawi, wabunge wake waamke waijenge nchi tena bado tunaweza kulijenga Taifa letu tena likastawi bila kujali maadui wanatumia mbinu gani kutuvunja mioyo kwa jina la Yesu. na ilo roho yako iamke sababu inawezekana unaweza kusimaa tena na kujenga.

“Basi manabii, Hagai nabii, na Zekaria mwana wa Ido, wakawafanyia unabii Wayahudi waliokuwako Yerusalemu na Yuda; waliwafanyia unabii kwa jina la Mungu wa Israeli. Ndipo akaondoka Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yosadaki, wakaanza kuijenga nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu; na pamoja nao walikuwa manabii wa Mungu, wakiwasaidia.” Ezra 5:1-

Unabii maana yake ni Mungu anazungumza kutumia kinywa cha mwanadamu, unabii ni Mungu anatoa maelekezo kupitia kinywa cha wanadamu. Maadui wa Israeli walipoona Israeli wameanza kujenga wakawa wanawashambulia na wana wa Israeli kwa kuwapiga ili wasijenge lakini waisraeli waliamua kujenga kwa mkono mmoja na mkono mwingine wakitumia silaha kupigana na adui, kumbe hata katikati ya matatizo unaweza kuendelea kujenga yako huku ukipigana ya adui. Kama mtu akiwa hana kazi akija kukusemesha na wewe ukaacha kazi ukamsikiliza ujue wewe ndiye unayepoteza maana yeye hana kazi hana cha kupoteza, Unatakiwa ubaki kwenye kazi yako huku mkono mmoja ukibeba silaha na mwingine endelea kufanya kazi kama askari wa Bwana Yesu kristo.

Kwenye mojawapo ya kanuni ya kivita inasema “Wakikushinda wanunue, na wakikushinda ungana nao”

Tunaona maadui hawa wa Israeli walipoona njia zote zimeshindikana wakaamua kumwita Joshua afanye maongezi juu ya ujenzi wao lakini Joshua alikataa kuacha ujenzi na kuwafuata na kuwasikiliza, walipoona amekataa waliamua kumwandikia mfalme barua kwamba kuna watu wameanza kujenga nyumba kwa bidii sana ambayo ilibomolewa miaka mingi iliyopita. Tunajifunza adui ukisha mshinda sikuzote hujaribu kukushawishi ili uache kazi yako na kumsikiliza anachokitaka lakini unatakiwa ubaki ndani ya kazi yako na akisogea fyeka na endelea na kazi yako kwa jina na Yesu.

Maadui walitumia kila njia kukwamisha ujenzi huu lakini walishindwa kwasababu Mungu akiamua kufanya jambo lazima litafanyika na kutimia.

Mtu ambaye anaongea sana na kutisha sana kwamba ataweza ataweza ujue mtu huyo hawezi anaogopa bali mtu akiwa amekaa kimya huyu ni wa kumwogopa sana, Imani ya kikristo imeanzia msalabani na leo imejaa duniani kote Ukristo duniani hautavunjwa na mtu yeyote tena kwa jina la Yesu na tunayaweza mambo yote katika yeye apaye nguvu. Mambo ya Mungu huwa yana upinzani sana lakini mwisho wake huwa yanaushindi wa kishindo kikuu, ni ushahidi tosha mtu kama yupo safi kila idara hana changamoto zozote zile yeye kile itu kwake kimefanikiwa basi yupo upande wa shetani. Kila tatizo unalolipata ni nafasi ya Mungu ili umtukuze baadaye.

Ukiri
“Dhiki yangu ni nyepesi na ya muda mfupi lakini inanitengenezea utukufu baadaye”

“Ndipo mfalme Dario akatoa amri, na watu wakatafuta katika nyumba ya vyuo vya tarehe, hapo akiba zilipowekwa katika Babeli. Na chuo kimoja kilipatikana huko Akmetha, katika nyumba ya mfalme iliyo katika wilaya ya Umedi, na ndani yake maneno haya yameandikwa ili yakumbukwe. Katika mwaka wa kwanza wa mfalme Koreshi, mfalme Koreshi alitoa amri, Kwa habari ya nyumba ya Mungu huko Yerusalemu, nyumba hiyo na ijengwe, mahali watoapo dhabihu, na misingi yake ipigwe na kufanywa imara sana; kuinuka kwake kuwe mikono sitini, na upana wake mikono sitini; ziwepo safu tatu za mawe makubwa, na safu moja ya miti mipya; gharama zake zitolewe katika nyumba ya mfalme. Na vyombo vya dhahabu na fedha, vya nyumba ya Mungu, ambavyo mfalme Nebukadreza alivitoa katika nyumba ya Mungu, iliyoko Yerusalemu, akavileta mpaka Babeli, na virudishwe, vikaingizwe tena katika hekalu lililoko Yerusalemu, kila kimoja mahali pake, na wewe uvitie katika nyumba ya Mungu. Basi sasa ninyi, Tatenai, liwali wa ng'ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na hao wenzi wenu wa Kiajemi, mlio ng'ambo ya Mto, jitengeni na mahali pale; iacheni kazi hii ya nyumba ya Mungu, msiizuie; waacheni liwali wa Wayahudi, na wazee wa Wayahudi, waijenge nyumba hii ya Mungu mahali pake. Tena, natoa amri kuwaagiza ninyi mtakayowatendea wazee hao wa Wayahudi, kwa kazi hii ya kuijenga nyumba ya Mungu; katika mali ya mfalme, yaani, katika kodi za nchi iliyo ng'ambo ya Mto, watu hao wapewe gharama zote kwa bidii, ili wasizuiliwe. Na kila kitu wanachokihitaji, katika ng'ombe wachanga, na kondoo waume, na wana-kondoo, kwa sadaka za kuteketezwa watakazomtolea Mungu wa mbinguni, na ngano, na chumvi, na divai, na mafuta, kama makuhani walioko Yerusalemu watakavyosema, na wapewe vitu hivyo vyote siku kwa siku, msikose kuwapa; wapate kumtolea Mungu wa mbinguni sadaka zenye harufu nzuri, na kumwombea mfalme, na wanawe, wapate uzima. Pia nimetoa amri kwamba, mtu awaye yote atakayelibadili neno hili, boriti na itolewe katika nyumba yake, akainuliwe na kutungikwa juu yake; tena nyumba yake ikafanywe jaa kwa ajili ya neno hili. Na Mungu huyu, aliyelifanya jina lake likae pale, na aangamize wafalme wote, na watu wote, watakaonyosha mikono yao kulibadili neno hili, na kuiharibu nyumba hii ya Mungu, iliyoko Yerusalemu. Mimi, Dario, nimetoa amri; na ifanyike kwa bidii nyingi. Ndipo Tatenai, liwali wa ng'ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na wenzi wao, wakafanya hayo kwa bidii, kwa sababu mfalme Dario alikuwa ametuma watu kwao. Nao wazee wa Wayahudi wakajenga, wakafanikiwa, kwa msaada wa kuhubiri kwao Hagai nabii, na Zekaria mwana wa Ido. Wakajenga, wakaimaliza kazi yao, kwa maagizo ya Mungu wa Israeli, na kwa amri ya Koreshi, na Dario, na Artashasta mfalme wa Uajemi. Nyumba hiyo ikamalizika siku ya tatu ya mwezi Adari, katika mwaka wa sita wa kutawala kwake mfalme Dario. Na wana wa Israeli, na makuhani na Walawi, na watu wengine katika hao waliohamishwa, wakaiweka wakfu nyumba ya Mungu kwa furaha.” Ezra 6: 1 - 16

Amri ikitolewa na Mungu hata kama shetani atoke shimoni kuipinga lazima jambo lililokusudiwa litimie. Majira hayawafuati watu bali watu wanayafuata majira, usishindane na majira ukishindana nayo majira yatakuuwa. Kwenye ulimwengu wa rohoni kuna sauti inasema hii ni saa ya Ufufuo na Uzima Duniani hii ni saa ya Bwana.

Ufunuo12:7
Shetani jina lingine anaitwa nyoka wa zamani,
Yohana 11,
Shetani ni Mungu wa ulimwengu huu na hana uwezo wa kukunyanganya kile ulicho nacho bali anauwezo wa kukucheleweshea muda tu kisitimie amka upigane ulitimize kusudi lilowekwa ndani yako kwa jina la Yesu.

Mahubiri yeyote kama hayajagusa kwenye maisha ya mtu basi hayana maana lakiniYesu alipokuja duniani hakuja kuleta dini ndiomaana alikuwa anaongea na watu, anaponnya watu na kuongea lugha za watu, kila tatizo linachanzo chake na ukitaka kuleta ufumbuzi unateketeza chanzo cha tatizo hilo kwanza ndipo tatizo linaondoka. Lazima ujue chanzo ili uondoe matatizo uliyoyano kwa jina la Yesu.

Amen

HAPPY BIRTHDAY FARAJA NAFTAL MNDEME

$
0
0

Wiki hii amezaliwa mmoja kati ya watu wanaosukuma mbele gurudumu la GK kwa kuandika makala mbalimbali zenye mafunzo kwako msomaji wetu. Mtu huyu si mwingine bali ni kijana anayejitambua katika nafasi yake Faraja Naftal Mndeme.

Team GK inajivunia na kumshukuru Mungu kwa ajili ya kipawa alichokupa cha kubadilisha wengine kupitia makala zako. Tunakuombea baraka na heri katika maisha yako kwamba kila utakachogusa kikapate baraka na Mungu akakujaze baraka maishani mwako sawasawa na mahitaji ya moyo wako. HAPPY BIRTHDAY FARAJA.

WASTAHILI NDIO CHAGUO LA GK ALBUM MPYA YA WANA WA NG'ANG'ANIA SHINYANGA

$
0
0


Hakuna ubishi kwamba linapokuja suala la uimbaji mzuri uliopangiliwa vyema basi kwaya ya AIC Shinyanga ni moja ya kwaya nchini inayoendelea kutumika kwa viwango vya juu na kuendelea kushikilia usukani wa kufanya vyema kwenye tasnia ya muziki wa injili nchini. Kupitia chaguo la GK jumapili ya leo tumeamua kukuwekea moja ya nyimbo zinazopatikana katika album yao mpya kabisa iliyotoka karibuni iitwayo 'Pigo la Fainali' wimbo tuliokuchagulia unaitwa 'Wastahili' ni wimbo wa kumrudishia Mungu sifa na utukufu kwa matendo makuu anayotutendea kila iitwapo leo.

Licha ya kwamba wimbo huu una maneno mazuri lakini pia mpangilio wa sauti ukiongozwa na solo aliyeanzisha basi utakubaliana na GK kwamba wana wa Ng'ang'ania wamefanya kazi nzuri inayostahili pongezi. Basi tukutakie utazamaji na usikilizaji mwema wa wimbo huu. Jumapili njema



SOMO: NITAWEZAJE KUISHINDA ZINAA - MCHUNGAJI MADUMLA

$
0
0

Na Mchungaji Gasper Madumla.

Bwana Yesu asifiwe…

Kati ya dhambi yenye kusumbua watu wengi leo katika jamii ya watu mbali mbali tena hata kwa wapendwa makanisani ni dhambi ya zinaa,ambayo ni dhambi yenye matokeo mabaya kuliko dhambi ziwayo zote ingawa dhambi zote zi sawa. Hukumu ya dhambi zote ni katika ziwa la moto,hivyo dhambi zote zinafanana katika hukumu,lakini dhambi hutofautiana kwa matokeo yake kwa kila dhambi.

Mfano matokeo ya mtu adanganyaye ni tofauti na matokeo ya mtu afanyaye zinaa sababu dhambi nyingine hazihusishwi na agano isipokuwa zinaa. Matokeo ya dhambi yenye kufungamanishwa na agano ni mabaya sana,sababu agano linadai uhalali wa ile dhambi. Mfano mtu yeyote alalaye na mwanamke asiye mke wake,watu hawa huungamanishwa kwa lile tendo la zinaa,nao huwa mwili mmoja. Ndivyo ilivyoandikwa;

” Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. ” 1 Wakorintho 6:16

Kinachomfanya mtu kuungwa na mwingine ni agano lililopo kati ya wawili kuwa mmoja,agano lina nguvu ya kuyaleta mawili na kuyaunganisha kuwa ni mamoja.Kumbuka pia agano linaweka mshabiano wa tabia za wawili kufanana.

Ndio maana hata kwa wanandoa kwa kipindi fulani hufanana tabia hata sura zao pia.(Tazama mke na mume si wawili tena bali ni mwili mmoja,Mwanzo 2:24 ).Agano hili linakamilishwa na la tendo la kujamiiana. Mtu akijiungamanisha na kahaba,ujue naye atakuwa ni kahaba tu,sababu ya agano.

Tazama mfano mwingine wa matokeo ya dhambi hii yenye agano la wawili kuwa mmoja. Biblia inasema;

” Yesu akamwambia, Nenda kamwite mumeo, uje naye hapa. Yule mwanamke akajibu, akasema, Sina mume. Yesu akamwambia, Umesema vema, Sina mume; kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako; hapo umesema kweli. ” Yoh.4:16-18

Huyu mwanamke si kana kwamba aliolewa na wanaume wote sita kama vile wanawake wanavyoolewa leo kanisani kisha sherehe,hapana. Bali alishiriki zinaa na wanaume hao sita. Kwa kitendo cha kujamiiana na wanaume hao sita,tayari kimewaunganisha kuwa mwili mmoja ingawa hakuolewa nao.

Kwa sababu ya agano liliopo kati yao,wanaume hawa wana haki ya kudai uhalali wa dhambi ya zinaa kwa mwanamke huyo,hata kama yeye hataki. Hapo ndipo mwanamke wa namna hii hujikuta akiendelea kushiriki nao zinaa ingawa hapendi kabisa,kwa sababu ya ile nguvu ya agano la zinaa.

Hali ya namna hii imewakamata watu wengi mno si wanawake,wala wanaume,wote wote. Na ndio maana unakuta mtu hufanya zinaa,mpaka inafika wakati kila mmoja anamshangaa tena mtu mwengine hataki kabisa zinaa lakini hujikuta akiendelea kufanya hali akiugua moyo wake sana.

Huko makanisani ndio hali inatisha hivi sasa,maana wengine hawapendi kufanya zinaa ila wanajikuta wakishiriki alafu baadae wanajutia kwa toba fulani hivi,alafu tena kesho yake hufanya. Kwa hiyo imekuwa kama kamchezo fulani hivi ka kuigiza.

Ndiposa mtu mmoja alipoona yamemshinda,maana kila alipojaribu kuacha zinaa hakufanikiwa akauliza nitawezaje kuacha zinaa?

Swali la namna hili limekuja kwa sababu ya mtu ambaye amejaribu kuacha dhambi ya zinaa lakini ameshindwa,kila akijaribu anajikuta akinguka katika dhambi hiyo hiyo ya zinaa,mtu huyo anaweza akawa ni wewe. Maana zinaa si lazima kufanya manualy bali hata kwa kuwaza tu katika hali ya kumtamani mwanamke/mwanaume.

Kwanza,waweza kujiuliza mbona natumia neno zinaa na nisitumie neno uzinzi,au uasherati katika maelezo yangu yote ya hapo juu.

Jibu linapatikana endapo tutajua ni nini maana ya zinaa,uzinzi na uasherati. Na tufanyeje basi kuyaacha haya yote maana ni dhambi za machukizo kwa Bwana.

ZINAA.

Neno zinaa linawakirisha uzinzi na uesharati. Hivyo mtu asemapo zinaa ni sawa na kusema ” uzinzi na uesharati.” Katika maelezo yangu mahali pote nimezungumzia zinaa nikiwa na maana ya uzinzi na uesharati.Sasa Uzinzi ni nini? Na uesharati ni nini?

UZINZI.

~Uzinzi ni tendo la kujamiana kwa mwanandoa na yule asiyekuwa na ndoa. Mfano mwanamke mwenye ndoa akichepuka kwa kujamiana na mwanaume asiyeoa basi mwanamke huyu amezini. Alikadhalika kwa mwanaume ni vile vile kwamba mwanaume mwenye ndoa akichepuka akazini na mwanamke asiye na ndoa basi… …mwanaume huyo amezini.

Sasa hiyo ni maana ya kwanza ya uzinzi. Maana ya pili ni mwanaume au mwanamke mwenye ndoa akajamiana na mwanaume au mwanamke mwenye ndoa nyingine Mfano. Mwanaume katika ndoa akatoka akalala na mke wa mtu,basi mwanaume huyu huitwa mzinzi. Mwanamke naye ni vivyo hivyo.

” Basi wakati awapo hai mumewe, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. ” Warumi 7:3a

Hivyo uzinzi ni lazima uhusishe ndoa~kwamba mmoja katoka katika ndoa yake,naye mtu huyo huitwa mzinzi. Uzinzi katika biblia una maana mbili, maana ya kwanza ndio hiyo iliyopo katika zinaa.

Maana ya pili ya uzinzi ni ile hali ya kumuacha Bwana ambaye Yeye Bwana amekuwa kama mume kwetu sababu tuna agano naye katika Kristo Yesu. Ikiwa kama tutaiacha imani yetu kwake Mungu,basi tumekuwa wazinzi ( Warumi 7:3-4) pia tunasoma ;

” Ingawa wewe, Israeli, unafanya uzinzi, lakini asiasi Yuda; nanyi msiende Gilgali wala msipande mpaka Beth-Aveni, wala msiape mkisema, Aishivyo Bwana. ” Hosea 4:15

UASHERATI.

Ni hali ya kujamiana kwa yule asiyekuwa na ndoa kwa asiyekuwa na ndoa mwenzake au hata yule asiyekuwa na ndoa kujamiiana kwa mwenye ndoa.

Mfano. Binti au kijana wa kiume akijamiiana na mtu mwenye ndoa au siyekuwa nayo,basi binti huyu au kijana huyu huitwa mwesharati.

Zinaa inayo dawa,ambayo kwa dawa hiyo utaweza kuishinda kabisa. Hizi nikupazo hapa chini ni dawa zitakazoweza kukufanya uwe mbali na uzinzi na uasherati ukiwa umeokoka kwanza.

Na ikiwa bado hujaokoka basi anza kuokoka kwa kumpokea Bwana Yesu Kristo,awe Bwana na mwokozi wa maisha yako kwa kutubia dhambi zako zote sawa sawa na atakavyoongozwa na mchungaji wako na kuombewa,kisha ndipo utumie dawa hizi hapa chini;

Kuikimbia zinaa. 1 Wakorintho 6:18.

~ Kuikimbia zinaa ni kujitenga mbali na mtu anayekufanya udondoke katika zinaa pia ni kujitenga na kila aina ya mazingira hatarishi,na tabia zote hatarishi.

Mfano; Wewe ni kweli umeokoka na unampenda Mungu,lakini bado una namba za simu za aliyekuwa boy friend au girl friend wako wa zamani ambaye wala sio mchumba kusema mtaoana kwa sasa.

Sasa kipindi hicho mlipokuwa duniani mlikuwa mkifanya dhambi ya uasherati,lakini sasa umeokoka na bado una mawasiliano yake ya karibu~ anakupigia,nawe wampigia~ tena umejidanganya kwamba utamuombea ili abadilike lakini ukaribu wenu unaamsha hisia za kipindi kile cha uasherati,gafla unajikuta badala ya wewe kumbadilisha,wewe ndio unabadilishwa imani yako kwa uasherati.

Au mke umeolewa na mume mwingine lakini bado una mawasiliano ya karibu na aliyekuwa akikutaka kukuoa na huko nyuma alikuchezea,bahati nzuri ukaolewa na mwingine aliyeletwa na Bwana. Kumbe! Mawasiliano yenu ya ukaribu yanawasogeza karibu,hatimaye unaanguka katika dhambi ya uzinzi.

Na mwanamume naye ni vivyo hivyo,kwa yule mwenye mawasiliano ya karibu naye anaweza kudondoka katika uzinzi.

Ujitenge mbali na mazingira chochezi pamoja na tabia. Mfano leo kumeibuka makanisani tabia ya kutaniana taniana kitamaa kati ya binti na mwanaume.

Wengine hudiliki hata kushikana shikana wakati wakitembea au hata kama wamekaa. Mambo haya ni machukizo ambayo hupelekea kufikiria zinaa kwamba ” ….aahaa tuzini kidogo alafu tutatubu bhana…” Hatua hii ya kwanza ni ya kuishinda zinaa ni kukimbia kama ukoma…

Bwana Yesu asifiwe…

Njia ya pili ambayo itakuwezesha kuishinda zinaa ni;

Kujitengamanisha na roho ya zinaa.

~Wapo watu ambao wamefungamanishwa na roho za zinaa pasipo kujijua,wanajikuta wakiwaka tamaa katika miili yao. Mfano shetani anaweza akawa amekutafuta katika kila kona ya maisha yako akuangushe,akiona amekushindwa anajaribu akuletee zinaa,hapo sasa anakuja binti/kijana mwenye vishawishi vya hali ya juu akikuanzia mbaliiii kiasi kwamba huwezi kumshtukia kwa haraka na anajua ya kwamba ukidondoka katika dhambi hii si rahisi kuinuka mara moja ikiwa hujadhamilia kikamilifu kwa sababu ya uwepo wa agano la zinaa.

Watu wengi wanazini na kufanya uasherati si kana kwamba wana penda,wengine ni miroho michafu ya zinaa inawasukuma kufanya. Mfano unaweza kukuta binti alinayedondoka dhambini mara kadha wa kadha na ukimuuliza anakujibu ya kwamba hata yeye mwenyewe hajui kwa nini amezini na mtu huyo.

Hili ni tatizo kwa watu wengi,kukumbwa na roho za zinaa. Kanisa la leo nalo limevamiwa na roho ya zinaa,baadhi ya watumishi wamedondokea huko. Dawa ni kujitengamanisha mbali na roho za zinaa,kwanza kwa kuchukia dhambi hii. Kisha kumsihi Roho mtakatifu achukue nafasi ya kuziondoa roho hizi,katika maombi rasmi kabisa ya kuvunja nira ya roho ya zinaa.

Kukaa uweponi mwa Bwana.

~ kukaa uweponi ni hali endelevu ya kudumu katika fundisho muda wote hata kama ukiwa unafanya kazi zako binafsi lakini muda wako mwingi una mawasiliano na Mungu. Ni hali ya kushughurika na mambo ya Mungu katik kiwango cha juu. Mtu yeyote mwenye ushirika na Bwana Mungu ni mtu aliyekaa uweponi.

Mfano mdogo ni huu; kama vile bawabu ilivyoungamanishwa na mlango wa chumba. Kiasi kwamba ukiingia chumbani yenyewe unaikuta pale pale,na hata kama ukitoka bado unaikuta pale pale imengangana katika mlango wa chumba,ndio maana Daudi akasema;

” Hakika siku moja katika nyua zako Ni bora kuliko siku elfu. Ningependa kuwa bawabu nyumbani mwa Mungu wangu, Kuliko kukaa katika hema za uovu. ” Zab.84:10

Sasa,ukiweza kujibidiisha kukaa uweponi mwa Mungu kama bawabu ilivyoshikamanishwa na mlango,ndivyo mawazo ya zinaa hukosa nafasi na ndivyo hata roho za zinaa hukosa mlango w kukuvamia. Siku zote roho chafu hukaa mahali pachafu,ikiwa hema ya moyo wako ni safi basi ni dhahili kabisa hakutakuwa na zinaa yoyote ile itakayotajwa kwako.

Shida kubwa ni kwamba watu wengi wapo uvugu uvugu katika imani zao,kwa hali ya kuwa uvugu uvugu kwamba unaamini lakini huku bado unaonja onja dhambi hapo ndipo zinaa nayo inakungangania. Bali dawa ya yote hayo ni kukaa uweponi full time.

Ikiwa roho ya zinaa imekukamata kiasi kwamba umejaribu kukimbia lakini hukufanikiwa,tafadhali nipigie basi ili tuombe pamoja ili Bwana akuhudumie.
Kwa huduma ya maombi nipigie sasa kwa namba 0655111149.
Mchungaji Gasper Madumla.
Beroya bible fellowship church.(Kimara,Dar-TZ)
UBARIKIWE.

AKUTWA NA UMAUTI NYIKANI AKIJARIBU KUFUNGA KAMA YESU KWASIKU 40 BILA KULA CHOCHOTE

$
0
0


Mwanaume mwenye miaka 73 aliyefahamika kwa jina la Reinfirst Manyuka kutoka Zimuto huko nchini Zimbabwe amefariki dunia baada ya kujaribu kufunga siku 40 bila kula chochote wala maji usiku na mchana nyikani kama alivyofanya Bwana Yesu wakati akijaribiwa na shetani.

Kwa mujibu wa mtandao wa NewZimbabwe.com pamoja na Christian Post umeandika kwamba marehemu aliondoka nyumbani kwake june 15 mwaka huu nakuelekea jangwani ama mwituni ikiwa safari yake ya kiroho katika kujaribu kufunga kama alivyofanya Bwana Yesu. Kwa mujibu wa familia yake marehemu wamesema licha ya tukio hilo kumpata, marehemu alikuwa mtu mwenye imani na mamlaka safi katika Bwana na kwamba alikumbwa na umati sizaidi ya siku 30 bila ya chakula wala maji alipokuwa milimani.

Taarifa zinasema Manyuka aliamua kuondoka nyumbani kwake ili apate wakati mzuri wa maombi ili kugeuza akili yake kumwangalia Mungu na kuondokana na tamaa za kidunia. Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Polisi wa eneo la Masvingo inspekta Nkuleko Nduna ameuambia mtandao huo kwamba mwili wa Manyuka ulipatiakana vichakani mnamo July 15 ikiwa ni mwezi mmoja kamili toka alipoondoka nyumbani kwake. Aidha katika taarifa nyingine kutoka kwa familia ya marehemu inasema licha ya umri aliokuwa nao Manyuka bado alikuwa mtu mwenye afya njema na kwamba hakuwa na dalili ya kwamba angefariki ama yupo katika hatari ya kifo wakati anaondoka nyumbani.

Hata hivyo licha ya taarifa kudai kwamba marehemu aliweza kufunga siku 30 bado uhakika wa kifo chake haujulikani kama alikufa kitambo nyikani kabla ya mwili wake kugundulika na mtu aliyetoa taarifa polisi au la. Ingawa inaonekana ni jambo la ajabu kwa mtu mzee kuondoka nyumbani kwake na kuelekea nyikani kufunga kwa zaidi ya mwezi, lakini kitengo chake kimekuwa kikikumbana na vifo mbalimbali vinavyotokana na watu kufunga bila kula chochote, lakini hatuwezi kuwazuia raia kufunga kwasababu ni jambo la kiimani alisema Inspekta Nduna.

Aidha katika hatua nyingine kuonyesha kwamba waumini wengi hudhani kama wanaweza kuhimili kufunga kwa siku 40 bila chakula wala maji ni kwasababu ya mitume wengine ndani ya Biblia ukiachana na Yesu, kwenye kitabu cha Kutoka imeeleza kwamba Musa alifunga siku 40 bila chakula katika mlima wa Sinai kisha kupatiwa amri 10 za Mungu. Kama haitoshi baada ya kumshinda mtume wa Baali kama ilivyoandikwa kwenye kitabu cha Wafalme mtume Eliya alifunga siku 40 bila chochote mpaka alipofikia mlima Sinai.

Picha ya Mlima Sinai unayoonekana kwasasa huko nchini Misri©YouTube


HOJA: INJILI YA UFALME WA MUNGU ILIYOPOTEA

$
0
0
Askofu Sylvester Gamanywa
WAPO Mission International.

Kila msomi wa maandiko matakatifu ya agano jipya, kama anataka kuwa mkweli katika nafsi yake, atakubaliana nami kwamba, injili ile iliyohubiriwa na Yesu Kristo mwenyewe na kisha kupokelewa na wanafunzi wake, sio injili ile ile inayohubiriwa katika ulimwengu wa leo. Na kama “injili ya leo sio ile ile “injili ya kwanza” sio ajabu kuona hatuoni ishara zile zile “injili ya kwanza”! Katika hoja ya leo, nachukua fursa hii kuirejea “Injili ya kwanza” ili yamkini wahubiri wa “Injili ya leo” tutubu na kurejea katika “Injili ya kwanza”

Injili ya ufalme wa Mungu
ndiyo injili ya kwanza na asilia

Injili ya ufalme wa Mungu ndiyo Injili ndiyo iliyohubiriwa na Yesu Kristo na akawaamuru wanafunzi wake waihubiri kila mahali baada ya kuondoka kwake. Injili ya ufalme wa Mungu ndiyo ilikuwa na “ujumbe muafaka” uliobeba taarifa muhimu kwa kila binadamu duniani. Kabla sijaingia kwa kina hebu tupate tafsiri fupi za misamiati ya maneno magumu yakiwemo  neno “injili” na pili neno “ufalme wa Mungu”!

1.    Msamiati wa neno “Injili”

Neno Injili tafsiri yake ni “habari njema”! Enzi za karne za Biblia, jamii ilizoea maisha ya vita vya kikabila. Wakati wa vita jamii ilikuwa katika hali ya maficho au wasiwasi wakati jeshi lake liko mstari wa mbele. Lakini jeshi moja liliposhinda maadui zake, mjumbe maalum alipelekwa kupeleka taarifa maalum kwenye miji ile ambayo jeshi lake limeshinda vita. Neno hili, “habari njema” (Injili) ndilo lilipigiwa mbiu kwa wenyeji walioshinda na furaha ikawashukia wakaanza kupiga vilegele na shangwe za amani.

Yesu Kristo alipoanza huduma rasmi, ujumbe wake wa kwanza, ulikuwa ni “Tubuni, ufalme wa Mungu umekaribia.” (Mathayo. 3:2). Kuanzia wakati huo, mahubiri na mafundisho yake yalihusu habari za “ufalme wa Mungu”! Hata baada ya kufa na kufufuka kwake, siku 40 za mwisho kabla ya kupaa, tunasoma alizitumia kuwakumbusha habari za ufalme wa Mungu.

2.    Msamiati wa neno “Ufalme wa Mungu”

Kwanza neno “Ufalme” maana yake ni eneo ambalo mfalme anamiliki na kutawala. Pili, “ufalme” ni mfumo wa utawala ambao mtawala ndiye mmiliki wa vitu vyote. Tunapokuja kwenye msamiati kuhusu “Ufalme wa Mungu” tunapata maana ya “mfumo wa utawala ambao Mungu ndiye mwumbaji na mmiliki wa vitu vyote” na ndiye “mwenye mamlaka ya juu na ya mwisho juu ya wote na vyote”

Enzi za karne ya kwanza, mfumo wa kifalme ndio mfumo uliokuwa unatawala ulimwengu wa nyakati hizo. Hata hivi sasa, bado yako mataifa na makabila ambayo tawala zake zimeendeleza mfumo wa kifalme, japokuwa sio kwa mikazo ile ile ya karne ya kwanza.

Kabla sijaingia kwa kina kuhusu mada kuu ya “injili ya ufalme wa Mungu” hapa duniani, ambayo nadiriki kusema kwamba imepotea kabisa; hebu kwanza niweke tofauti zilizopo kati ya “mfumo wa utawala wa duniani hii” na “mfumo wa utawala wa Mungu” unaotakiwa kuonekana hapa duniani:

Tofauti zilizopo kati ya “utawala wa
duniani hii” na “ufalme wa Mungu”

Zipo tofauti kubwa kati ya mifumo hii hususan kwa utawala wa Tanzania na “mfumo wa kifalme”! Kwa hapa Tanzania tunatumia “mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa”. Huu ni mfumo ambao “utawala wake hupatikana kwa njia ya uchaguzi wa walio wengi; na pia  “utawala wa uwakilishi” wa walio wengi.

Tukirejea kwenye mfumo wa Ufalme wa Mungu kama tulivyokwisha kuchambua kwamba huoni “mfumo wa utawala ambao Mungu ambaye ndiye muumbaji wa binadamu wote na viumbe vyote,, ndiye mwenye mamlaka ya juu na ya mwisho juu yake.” Kimsingi, asili ya mfumo huu wa “ufalme wa Mungu” sio wa hapa duniani. Hii iliwekwa bayana na Yesu mwenyewe pale alipokuwa akijibu swali la Pilato akasema:

“Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa.” (Yh.18:36)

Kwa hapa napenda kutoa angalizo kwa jamii ya baadhi ya Wakristo ambao, kwa kutokujua tofauti zilizipo kati ya mifumo ya tawala hizi; wao wamekuwa wakichanganya itikadi zake na kulazimisha “mfumo wa kidemokrasia unaotawala Tanzania” ubadilike na kutumia itikadi za “mfumo wa kifalme” jambo ambalo haliwezekani. Na sio kwamba haliwezekani tu bali linachangia kupotosha maana sahihi ya “Ufalme wa Mungu” unaotakiwa kuonekana hapa duniani.

Ninatambua uwepo wa tafsiri mbali mbali zinazoshinikiza na kulazimisha kuwapata viongozi wa kisiasa, wenye sifa za kimungu kwa madai kwamba, tunahitaji kuongozwa kisiasa na wacha Mungu ambao watatawala kwa haki na kuzingatia miiko ya utakatifu. Hii ni shauku nzuri na yenye kusisimua. Lakini lazima tutambue kwamba, “kuwa na watawala wacha Mungu” ni tofauti kabisa na kuwa na “utawala wa Mungu” ndani ya “mfumo wa utawala wa duniani hii”!

Ni kweli mtawala anaweza kuwa mcha Mungu kama mtu binafsi, na akasaidia kutawala kwa hofu ya Mungu, lakini hii haimaanishi kwamba ataweza “kubadilisha mfumo wa utawala wa duniani hii” uanze kutumia misingi ya “ufalme wa Mungu” kama ndio sheria za kuongoza nchi.

Bila shaka unaweza kujiuliza kama “mfumo wa utawala wa Mungu” hauna nafasi ndani ya “mfumo wa utawala wa duniani hii”; Yesu alikuwa na maana gani aliposema tuombe kwamba “Ufalme wako uje…”? Jibu la swali hili la sehemu kuu mbili.

Kwanza, upo wakati maalum wa kinabii uliotabiri kuhusu “mfumo wa ufalme wa Mungu” utakapotawala duniani hii kwa 100%! Hiki kinajulikana kama kipindi cha miaka elfu moja maarufu kwa jina la “utawala wa milenia” ambapo Mtawala mwenyewe atakuwa ni Yesu Kristo mwenyewe. Sasa wakati huo haujafika bado mpaka hapo Yesu Kristo atakaporudi mara ya pili duniani.

Lakini kwa sasa, “mfumo wa utawala wa Mungu” unaotakiwa kudhihirika hapa duniani ni uwepo wa jamii ya wana wa ufalme kama watu binafsi waliovikwa mamlaka ya kifalme na wanaishi kwa kanuni za ufalme wa Mungu katikati ya jamii ya wana wa ulimwengu huu.

Itaendelea juma lijalo

Viewing all 1245 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>