Quantcast
Channel: Gospel Kitaa™
Viewing all 1245 articles
Browse latest View live

CHAGUO LA GK: NATAKA MAPATANO - MCH FAUSTIN MUNISHI

$
0
0


Twatumai umzima mdau wa Gospel Kitaa popote pale ulipo ulimwenguni. Chaguo letu kwa wiki hii linatoka kwa Mchungaji mwenye maskani yake nchini Kenya, Faustin Munishi.

Hivi karibuni Mchungaji Munishi alikuwepo kuhudumu kwenye tamasha la kimataifa la pasaka ambalo huandaliwa na kampuni ya Msama Promotions, ambapo aliimba wimbo; Nataka Mapatano. Wimbo ambao ulitungwa kwenda kinyume na wimbo wa marehemu Remmy Ongala, kifo hakina huruma.

Tunakutakia Jumapili yenye baraka huku tukikukumbsha kwamba ukipatana na BWANA Yesu, hutokuwa na haja ya kukiogopa kifo wala vichochezi vyake.

NENO LA LEO - ALHAMISI

$
0
0




NENO LA LEO
"Itakuwa kabla hawajaomba nitajibu, wakiwa katika kusema nitasikia" (Isaya 65:24).

Mambo ya kujifunza:

1. Mungu hajawahi kuchoshwa na maombi ya watu.

Mungu anataka kujibu maombi yako kuliko wewe unavyopenda kumwomba.
(Mathayo 7:7-10).

Mungu anataka kutatua shida, changamoto, majaribu na magumu unayopitia kuliko hata wewe unavyotamani kuvushwa.
(Zaburi 91:14-16).

Mungu hafurahii hali nzito na ngumu unazopitia na anataka ashiriki kuzitatua na kukupa furaha iliyopotea.
(Yoh 16:23-24).

Mungu ameweka maombi kama njia pekee ya kuuleta Ufalme wa mbinguni kwenye changamoto, magumu na hali tunazopitia.
(Mathayo 6:9-12).

Kadri unavyokuwa na kiwango cha kukutosha cha Neno la Mungu (Mapenzi yake kuhusu jambo unaloliombea), ndivyo unavyokuwa na uhakika wa kupata kile alichosema na kuahidi kwako.
(Yohana 15:7, 1Yoh 5:13-14).

Mungu anataka kugeuza maisha yako kuliko wewe unavyotamani ageuze maisha yako.
(Isaya 43:18-19, Ayubu 14:7-9).

2. Majibu ya maombi yako huwa yanatolewa tangu muda ule unapoamua kwa dhati kumtafuta Mungu japo inaweza kuchukua muda kiasi kuonekana mwilini.
"Kabla hawajaomba nitajibu"

Danieli alijibiwa tangu siku ya kwanza japo majibu yalifika siku ya Ishirini na moja (Danieli 10).

Yabezi alijibiwa na Mungu siku ileile aliyomwendea Mungu ili abadilishe maisha yake, japo mabadiliko yalikuja kuonekana baada ya muda kiasi (1Nyakati 4:9-10).

Mungu aliyajibu maombi ya Hana tangu alipotamkiwa Neno na kuhani Eli lakini ilichukua karibu mwaka mzima kumpata Samweli (1Samweli 1).

Linapokuja swala la maombi, usitie shaka.
Mungu wa Bwana wetu Yesu bado anajibu maombi.
"Mkumbushe, mhojiane, mueleze mambo yako akupe haki zako" (Isaya 43:26).
"Umuombe naye atakupa" (Zaburi 2:8).

NB: Hakikisha umesoma maandiko haya yote na kuyatafakari ili kuzalisha imani ndani yako.

Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila


HOJA: MAMBO MAKUU MATATU YA KUPEWA KIPAUMBELE KATIKA MAOMBI (Sehemu ya mwisho)

$
0
0
Jumapili iliyopita (soma hapa) tuliendelea na mada yetu ambapo tulianza uchambuzi wa kipengele cha 3 za ujumbe kinachosema kuhusu “kuuona utukufu wa Mungu”. Humo nilifafanua maana ya kipengele na kisha nikaanza kusimulia sehemu ya ushuhuda wangu binafsi, sehemu ambayo 
inaendelea katika toleo hili pia”

Askofu Sylvester Gamanywa

Mwendeleo wa sehemu
ya ushuhuda wangu binafsi

Baada ya kuisikia sauti hii, nilisisimka pale mahali nilipokuwa nimketi na kuamka kisha nikaondoka huku nikiwa natafakari ujumbe ule niliopokea. Kwa mara yangu ya kwanza, niliweza kutambua bila shaka kwamba hiyo ilikuwa ni sauti ya Roho Mtakatifu akiwasilisha ujumbe wa Yesu Kristo kwangu. Isingeliwezekana kuwa ni mawazo yangu kwa sababu naifahamu sauti ya mawazo yangu. Pia naliikumbuka siku ile niliyoweka nadhiri yangu mbele za Mungu kule porini.
 
Ni kweli, Mungu alisikia dua yangu na alinitoa kule porini kwa miujiza yake. Ni kweli baada ya kutoka huko nilijifanya kutoa sadaka kwa maskini na kutoa shukrani kwenye ibada ya dini. Lakini baada ya hapo sikukumbuka suala la “kiapo changu cha kumtumikia Mungu”. Niliendelea na maisha yangu ya dhambi kama kawaida na kusahau yote yalikuwa yamekumba wakati uliopita.
Hata haikuchukua miezi zaidi ya mitatu, nilikutana na Injili ya wokovu na kuamua kutubu na kumpokea Kristo kuwa Mwokozi wangu binafsi. Suala la wokovu wangu na lenyewe lilikuwa na kishindo chake katika mji ndogo niliokuwa ninaishi. Hilo sina muda wa kulishuhudia mahali hapa sasa hivi.

Lakini baada ya kuokoka hakikuchukua muda mrefu nilifundishwa habari za kumpokea Roho Mtakatifu na nikashuhudia tukio jingine la kishindo cha kiroho katika maisha yangu. Hilo ni tukio la kumpokea Roho Mtakatifu. Nalo hilo lina masimulizi yake pia. Hoja yangu ya sasa ni kukupa picha ufupi yaliyojiri tangu siku nilipoweka nadhiri yangu mbele za Mungu na jinsi Mungu alivyoniokoa kwenye mazingira magumu, lakini anaenda mbele zaidi akaniokoa katika kongwa la dhambi.
Na sasa baada ya kuokolewa na kujazwa Roho, ndipo Mungu anazungumuza rasmi kwa mara ya kwanza akinikumbusha mahali aliponitoa na kiapo nilichoweka na kwamba yeye amefanya sehemu yake na kwamba sasa ilikuwa ni wajibu wangu “kutimiza nadhiri yangu kwake”.
Haya ushuhuda huu una uhusiano gani na mada hii katika kipengele cha “kuuona utukufu wa Mungu”? Uhusiano upo tena mkubwa sana. Siwezi kukufundisha habari za “kuuona utukufu wa Mungu” kama mimi binafsi ningekuwa sijawa kuuona katika dhahiri katika maisha yangu.
Pili, “kuuona utukufu wa Mungu” hauishii kwa mtu binafsi anayehusika, bali na hata wengine wanaomzunguka na wanaomfahamu. Nilisema kwamba, “kuuona utukufu wa Mungu” ni “kuyaona kwa dhahiri matendo ya Mungu” ambayo hushuhudiwa kwa na wengine katika mahali husika.
Mathalan, Tukio la kuokoka kwangu licha ya kwamba “niliuona utukufu wa Mungu” kibinafsi, ambao ni “kuondolewa  madhambi” yangu yote niliyokuwa nimewahi kuyafanya huko nyuma; ndugu, jamaa na marafiki zangu wote, walishuhudia “badiliko la kitabia” ambalo ni matokeo ya kuokoka kwa nguvu za Bwana Yesu. Kana kwamba hii haikutosha, hata tukio la “ujazo wa Roho Mtakatifu” liliponitukia halikuishia kuwa siri yangu binafsi, bali lilikuwa na kishindo kama kile kile cha siku ya Pentekoste ambapo maelfu ya watu walikusanyika ili kushuhudia kilichowatokea mitume wa Yesu Kristo.



Tumtafute Mungu ili sisi kujua
tumfanyie nini na si yeye atufanyie nini

Kumbuka kwamba kiini cha mada ni “mambo yanayostahili kupewa kipaumbe katika maombi yetu kwa Mungu”. Yaliyotangulia mawili ambayo ni “kupata kibali cha Mungu” na “kupokea hekima ya Mungu” yote yalitupa picha ya umuhimu wake. Hili la kuuona utukufu wa Mungu ndilo linapiga muhuri wa yale yaliyotangulia, au kuyathibisha yale yaliyotangulia.

Japokuwa ninalosema hapa si jambo geni kwangu, na wala si ufunuo mpya kabisa kwangu, lakini najisikia kusema kwamba, nimefunuliwa kwa upya kuhusu hoja hii. Hoya ya kumwomba Mungu atuonyeshe anataka tumfanyie nini, badala ya sisi kung’ang’ania kumtaka Mungu atutendee nini.
Kuna siri gani katika hoja hii? Kuna siri kubwa kupita kawaida. Laiti wacha Mungu wote tungeliupata ufunuo huu.! Latini kila binandamu aliye hai angeliupata ufunuo huu.  Dunia ingebadilika na kuvunja rekodi ya mabadiliko. Lakini tumefungwa akili zetu hatuoni yatupasayo kuomba mbele za Mungu. Naweza kusema kwamba, ni Ibilisi tu ndiye amepofusha fikira zetu, kwa sababu ya ubinafsi wetu, tunazidi “Kuzunguka kwenye jangwa la maombi yasiyojibiwa” kwa sababu tu “hatujui kuomba jinsi itupasavyo”!

Ninasikitika sana kwamba, hata sisi watumishi tumechangia kwa kiasi kikubwa kuwapotosha wafuasi kwa kuwafanya waendelee kujenga mtazamo wa kumwomba Mungu mambo yao binafsi tu badala ya kuwaelekeza kumwomba Mungu awafunulie anawataka wamfanyie nini Mungu.

Mara nyingi tumeweka mkazo zaidi kuwafundisha watu wamtolee Mungu fedha na mali zao kwa ajili ya kazi yake. Ingawa hili nalo ni mapenzi ya Mungu wafuasi kulijua, lakini tulipaswa kuwaekeza wajifunze kumtafuta Mungu ili awaambie anawataka wamfanyie nini, na sio tu kumtolea fedha na mali. Sisi wote ni mashahidi kwamba, wako watu wanamtolea Mungu lakini hawaoni matokeo ya kutoa kwao kwa sababu hata katika kutoa kwenyewe hawatoi kwa njia iliyo sahihi mbele za Mungu. Tunashindwa kuwaambia kwamba Mungu hana shida na fedha na mali zao, bali anataka kujenga mahusiano ya kibinafsi kati yake na wao, na kwamba matoleo ni matokeo.

Ninatamani Mungu anipe fursa nyingine tena, upako mwingine tena, nguvu nyingine tena, ili nipate kibali mbele zake tena, nipokee hekima yake tena kwa ajili ya kuwahamasisha, kuwaelemisha, kuwarejesha kiimani watu katika kujitoa wao wenyewe WAMTAFUTE MUNGU ILI KUJUA KUTOKA ANAWATAKA WAMFANYIE NINI NA SIO YEYE AWAFANYIE NINI!
Mwisho


TAMASHA LA WAJUMBE WA KRISTO KATIKA PICHA

$
0
0

Siku ya Jumapili kwenye kanisa la TAG Bethel Christian Center jijini Arusha, kumefanyika tamasha lilioandaliwa na CAS Band kwa lengo la kutambulisha jina jipya la band hiyo ambayo sasa linaitwa Bethel Alive Band.

Majira ya saa 10 jioni mpaka saa 12 na nusu jioni ndipo tukio hilo lilifanyika, GK ilikuwepo na hapa inakupa matukio katika picha kama yalivyojiri.

CAS Band ambao kwa sasa ni Bethel Alive Band

                                                                           Paul Clement





 
 Angel Benarnd




















 Picha 15 za Tamasha La Wajumbe wa Kristo
 











MAHAFALI YA 11 YA KOZI YA LIFE TRANSFORMATION LIVING WATER CENTRE

$
0
0
Baadhi ya wanafunzi walihitimu  Life Transformation koziwakitoa shuhuda mbele ya waumini kanisani hapo wakati wa ibada
Siku ya Jumapili Katika Kanisa la Living Water Centre Kawe kulikuwa na mahafali ya 11 ya kozi inayoitwa Life Transforming, kozi ambayo inakuwa ni darasa la kukulia maisha ya wokovu ama darasa la utumishi katika Ufalme wa Mungu.

Apostle Onesmo Ndegi, kiongozi wa huduma ya Living Water Centre Ministry Kawe  ambaye ndio kiongozi wa kozi hiyo alikuwepo kuhudhuria mahafali hayo, ambapo kozi hiyo ilianza mwaka 2004 ikiwa na wanafunzi wachache huku iidadi ikizidi kuongezeka, na tangu chuo kianze mwaka huu ni mahafali ya 11.

Mahafari hayo yalipambwa na Uimbaji, maigizo, dance na shuhuda za kile ambacho Mungu amewatendea wanafunzi hao katika kipindi chote walichosoma. Wengi wao katika shuhuda wamesema darasa hilo limewafundisha kumtumikia Mungu zaidi

Wakitoa shukrani zao kwa Mungu na mtumishi wamesema kuwa wamefundishika vyema kwa sababu wapo tofauti sana na walivyokuwa awali kabla ya kuanza darasa na wamefanyika utu upya na kwao hadi jana wanahitimu darasa wamepata mabadiliko makubwa.

Katika risala yao walisema kuwa elimu hii ya kozi ya Life Transformation imewapa msingi na kuwajenga kiroho na kimwili, pia imewapa uwezo wa kujitambua na kufikiri, kufanya mambo kwa usahihi na kufanya maamuzi thabiti juu ya maisha yao, kwa msaada wa Roho Mtakatifu, aliye msaidizi wetu. 

"Imetuwezesha kufahamu kiundani maana ya wokovu na umuhimu wa wokovu katika maisha yetu. Tumepata elimu sahihi juu ya jinsi ya kuukulia wokovu, kuwa waadilifu, kuwa na moyo wa msamaha, kujua nafasi ya kiongozi wa kiroho, nini hasa maana ya imani na utakatifu kwa ujumla wake. Vilevile tumeelewa umuhimu wa kulisoma neno na kujua msaada mkubwa uliopo katika neno kwenye maisha yetu na jinsi itupasavyo kuliishi Neno." Alisema msoma risala.

Katika kozi hiyo wamekuwa wakisoma na kufanya majaribio ya mitihani mara kwa mara jambo lililowasaidia kuwainua katika kukua kiroho na pia wakaahidi kuyaishi yale mema yote waliyo yapata katika darasa hilo ili kuzidi kufikia lile kusudi la Mungu aliloliweka juu yao.

Kozi hiyo huwa inafanyika katika kanisa la Living Water Centre Ministry Makuti Kawe Dar es Salaam kila mwanzoni mwa mwaka mwezi January kwa miezi 3-4. Tangu miaka kadhaa imepita hadi mahafali hii ya mwaka 2015 kozi hiyo imesaidia watu wengi kuwa watumishi wazuri wa Mungu kutokana na masomo wanayojifunza.



Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa huduma ya Living Water Centre Ministry   na Mke wake Lilian Ndegi wakifuatilia shuhuda kwa umakini sana
Mhitimu akitoa shuhuda mbele ya waumini kanisani hapo wakati wa ibada

Baadhi ya wahitimu wa darasa hilo wakitoa shukrani zao kwa waalimu na watumishi waliohusika kuwafundisha.
Wahitimu wa darasa hilo wakiimba katika kwaya yao ya pamoja 
Furaha kiongozi wa kwaya hiyo akiongoza nyimbo.
Umati wa waumini na ndugu wa wahitimu walipohudhulia ibada hiyo kuja kuwatazama ndugu zao






Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa huduma ya Living Water Centre Ministry,Mke wake Lilian Ndegi,na wachungaji wengine waliokaa viti vya mbele wakiimba na kucheza mbele za Mungu

Katika uwepo wa Bwana



Mchungaji  Naomi Mhamba mmoja wa waalimu wa darasa hilo



Lilian Ndegi akiongoza maombi
Ilikuwa furaha sana mbele za Bwana
Kwaya ya The Living Waters wakihudumu katika mahafali hayo










Wahitimu wakicheza na kufurahi mbele za Bwana
Risala ya wahitimu ikisomwa mbele ya Kiongozi wa Kanisa hilo Apostle Onesmo Ndegi na waumini kwa ujumla.

Risala ya wahitimu ikikabidhiwa kwa Kiongozi wa Kanisa hilo Apostle Onesmo Ndegi na wachungaji wengine
 Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Apostle Onesmo Ndegi akijibu risala ya wahitimu

Pia mahafali hayo yalikwenda sambamba na ugawaji wa vyeti kwa wahitimu hao

 ugawaji wa vyeti kwa wahitimu hao
Mmoja wa wahitimu hao alipokuwa akizungumza juu ya wao kama darasa la Life Transformation kozi juu ya zawadi walizo nazo kwa watumishi walio husika katika kuwatumikia na kuwaundisha
zawadi zikigawiwa kwa watumishi na waalimu wa darasa hilo.

Baadhi ya zawadi za vifaa vya usafi  zilizo wasilishwa na wahitimu wa darasa hilo katika mahali hayo
Lilian Ndegi mmoja mwa waalimu wa darasa hilo alipokuwa akiongea na kuwahisi wahitimu hao juu ya maisha yao ya Mungu baada ya kumaliza darasa
Picha ya pamoja kati ya wanafunzi na watumishi wa Mungu walihusika katika kipindi chote cha darasa Life Transformation kozi
Picha ya pamoja kati ya wanafunzi na watumishi wa Mungu walihusika katika kipindi chote cha darasa Life Transformation kozi

SOMO: MAMBO MAWILI MATATU YA KUFANYA ILI KUVUKA NYAKATI NGUMU

$
0
0


MAMBO MAWILI MATATU YA KUFANYA ILI KUVUKA NYAKATI NGUMU;

1. Iongeleshe hiyo hali/ jambo/ jaribu/ tatizo/ changamoto/ uhitaji.
"Usikae kimya tu. Kile usichokisemesha hakitabadilika kuwa vile unataka kiwe"
*Daudi alimsemesha Goliati (1Samweli 17:44-45).
*Yesu aliusemesha mtini ukanyauka (Marko 11:14-20).
*Yesu aliisemesha homa iliyokuwa inamtesa mama mkwe wa Petro (Luka 4:38).
*Yesu aliisemesha maiti iliyokuwa kaburini siku nne (Yohana 11:40-44).
*Yesu alisema tunaweza kuiambia milima ing'oke na ikatii (Marko 11:24).
*Ni muhimu ujue kuwa ULIMI NI MOTO na wewe mwenye nao ndiye unaamua unateketeza kipi, unasafisha kipi kwa moto ulionao kwenye ulimi (Yakobo 3:6a).

2. Izungumzishe nafsi yako na moyo wako.
-Wewe ni roho una nafsi na unakaa katika mwili. Kama usipopata "sapoti" ya nafsi yako kwenye hali yoyote unayopitia, na ukaacha nafsi yako iwaze na kufikiri na kutafakari kila wazo na fikira inayokuja ndani yako, hakika utapoteza vita.
Watu waliofanikiwa ni wale wanaoweza kuzitawala na kuzitiisha nafsi zao.
Kwanini kutiisha na kutawala nafsi yako?
Nafsi yako ni kiwanda kinachobeba mambo matatu makubwa uliyonayo: Hisia, akili na utashi.
Ebu fikiri upo katikati ya upinzani halafu "akili yako haiko sawa" au "hisia zako umeshindwa kuzithibiti" ama "umekosa utashi" wa kuendelea kupambana!

Kwenye Biblia, Daudi ni mfano hai wa watu waliokuwa wakijua siri hii ya kuiongelesha nafsi yake. Ifuatayo ni mistari michache aliyokuwa akiisemesha nafsi yake;

"Nafsi yangu, umngoje Mungu peke yake kwa kimya.
Tumaini langu hutoka kwake"
(Zaburi 62:5).

"Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Naam vyote vilivyomo ndani yangu vilihimidi jina lake takatifu"
(Zaburi 103:1).

"Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, Wala usizisahau fadhili zake zote.
Akusamehe (wewe nafsi yangu) maovu yako yote, akuponya magonjwa yako yote.
Aukomboa uhai wako na kaburi, akutia taji ya fadhili na rehema..."
(Zaburi 103:2-4).

*Mzee Yakobo naye aliwahi kuiongelesha nafsi yake;

" Simeoni na Lawi ni ndugu; panga zao ni silaha za jeuri.
Nafsi yangu, usiingie katika siri yao,
Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao..."
(Mwanzo 49:5-6).

Na wewe unaweza kuisemesha nafsi yako kwa maneno ya kujenga, ahadi za Mungu nakadhalika.
"Wewe ni nabii wa maisha yako. Usipofanya chochote Mungu hafanyi chochote"
-Inuka sogea kwenye kioo, jiangalie kwa dakika mbili tatu, jitamkie kupenya na kuvuka, jitamkie uhuru, jitamkie ushindi, jitamkie kibali, jitamkie upendeleo, jitamkie neema iliyozidi.
Usiruhusu kinywa chako kusema kinyume na maisha yako.
"Yale unayojiongelea na kujisemea yanaweza kukufingua au kukufunga"
(Mithali 6:2).

3. Muongeleshe Mungu kuhusu hilo jambo.

*Jizoeze kukata rufaa mbele za Mungu haraka sana unapogundua huna nguvu na akili za kibinadamu za kutatua jambo fulani (Isaya 38:1-8).

*Ni vema ujue Mungu huwatendea watu sawa na "walivyosema masikioni mwake" na si zaidi au pungufu ya walichosema (Hesabu 14:28).

*Ni vema ujue kuwa Mungu huwapa watu haki au hukumu kutegemea na walichosema kwake.
"Kwa maneno yako utahesabiwa haki (ukitumia vizuri ulimi wako kwenye uwepo wa Mungu), na kwa maneno yaki utahukumiwa (ukitumia vibaya maneno yako kwenye uwepo wa Mungu)" (Mathayo 12:34-37).

* Mungu anasubiri ukusudie Neno ili alithibitishe na Mwanga uziangazie njia zako (nguvu za Ufalme wake, Ufalme wa nuru zikusaidie kupenya)" (Ayubu 22:28).

* Mungu anasubiri umwambie ili ayaumbe matunda ya midomo yako (Isaya 57:19).

Hitimisho:
-Lisemeshe linalokusumbua
-Isemeshe nafsi yako
-Msemeshe Mungu

Mwl Dickson Cornel Kabigumila


SOMO: SADAKA IGUSAYO MOYO WA MUNGU (2)

$
0
0
Na Kelvin Kitaso
GK Contributor.
"Utoaji ulio mwema ni mlago wa mafanikio na uponyaji wa kimwhili, kiuchumi, na kiroho"

Wiki iliyopita tulitazama sehemu ya kwanza ya namna ambavyo wengi wanapapasa tu, lakini wachache wanamgusa Mungu kwa utoaji wao. Unaeweza kuiona tofauti hiyo (bofya hapa kusoma) kwenye hilo toleo. Wiki hii tunaenedelea na namna ya kuugusa moyo wa Mungu.

Nakumbuka siku moja nikiwa nimesafiri kuelekea mahali pa faragha kwa ajili ya maombi binafsi, nikiwa huko nilipata mguso wa tofauti sana wa kutoa mavazi yote ya thamani niliyokuwa nayo nimpatie mtu wa Mungu ambaye nilimkuta katika eneo hilo, suala hili lilikuwa gumu sana, haswa ukizingatia nami sikuwa na mavazi mazuri na ya kupendeza zaidi ya yale, nilishindana na ile sauti ya kufanya jambo hili, ila mwisho nikaona ni vyema niitii ile sauti na kutoa, haikuchukua muda mrefu kuna mama mmoja alikuja nyumbani na kuleta nguo nyingi zaidi ya zile nilizotoa na kupata viatu vizuri, kwangu hii ni uaminifu wa Mungu asemaye, “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa kifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakacho pimiwa”

Dhabihu inayougusa moyo wa Mungu ni dhabihu inayouma katika moyo wa mwanadamu, yaani kutoa kitu ukipendacho na ukionacho kuwa bora kuliko vyote na wapenda kukitumia ila kwa ajili ya BWANA unaamua kutoa si jambo rahisi na kufanya hivyo ni ishara ya upendo sana kwa Mungu na huonyesha kuwa unamjua unayemtumikia. Yaani dhabihu ambayo yaweza kuugusa moyo wa Mungu hata wewe mwenyewe ukitoa unaona umetoa kitu mbele za BWANA na wakati mwingine hata nafsi yako yagoma kabisa kwa kuwa nafsi ina tabia ya kujipenda yenyewe.

Mwanzo 22:2 “Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.” Mungu anamtaka Ibrahimu atoe mtoto pekee aliye naye na ampendaye, si jambo rahisi kwa watu walio wengi kufanya hivi. Kwa mfano huu ni sawa na umehangaika kupanga miaka mingi sana halafu unapata tu nyumba yako mwenyewe ukasikia Mungu anakuambia nataka utoe hiyo nyumba uliyonayo umpatie mtu Fulani, au umetembea muda mrefu sana kwa miguu halafu umepata gari zuri la pekee na ulipendalo sana halafu ukasikia Mungu anakuambia toa hilo gari umpatie mtu fulani si jambo rahisi.

Kumtii Mungu ni jambo la msingi sana katika maisha yetu, akisema hata kama jambo ni gumu sana wewe tii tu kwa kuwa kamwe hafanyi jambo hili kumkomoa mwanadamu, ila yeye hufanya yote kwa utukufu wake na ili kumfanya mwanadamu afurahie wema wake. Kwa Ibrahimu ukiendelea kusoma utaona kuwa Mungu anamuambia kwa kuwa hakumzuilia mwanae pekee ni lazima ambariki.

Sauti ya Mungu wakati mwingine inakuja kinyume na wewe ulivyo na waweza jiuliza mbona mimi nina vichache sana kwa nini amechagua mimi nitoe na si wale wenye navyo, ila jawabu ni kuwa Mungu amekuheshimu na amechagua kukubariki ndiyo maana amekuchagua wewe kati ya wengi.

Kijana mmoja katika Mathayo 19:21-22 “Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, Nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate. 22 Yule kijana aliposikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.” Kutoa na kuacha unavyomiliki kwa ajili ya Mungu ni suala la kujikana, kwa yule kijana alipoambiwa atoe alivyonavyo awape maskini aliondoka kwa kuhuzunika na akaona kuwa Mungu hamtakii mema kwa kumuagiza kutoa vitu vyake, ila laiti angejua siri iliyomkuta Ibrahimu na mjane wa Sarepta basi angetoa naye kwa kuwa angepata maradufu ya vile alivyokuwa navyo.

Mfano mwingine ni kitabu cha 1 Wafalme 17:13-16 “Eliya akamwambia, Usiogope; enenda ukafanye kama ulivyosema; lakini unifanyie kwanza mkate mdogo ukaniletee; kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao. 14 Kwa kuwa BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Lile pipa la unga halitapunguka, wala ile chupa ya mafuta haitaisha, hata siku ile BWANA atakapoleta mvua juu ya nchi. 15 Basi akaenda, akafanya kama alivyosema Eliya; na yeye mwenyewe, na Eliya, na nyumba yake, wakala siku nyingi. 16 Lile pipa la unga halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa na neno la BWANA alilonena kwa kinywa cha Eliya.”

Kutoa si kuwa navyo vitu vingi sana ila hata vile vidogo ulivyonavyo Mungu anataka umtumikie navyo, mjane wa Sarepta alidhani kuwa kutoa kwa ajili ya mtumishi wa Mungu ni mpaka awe na vitu vingi sana ila sivyo Mungu anavyotaka kwa watu wake. Kutoa ni moyo na wala si wingi wa vitu ulivyo navyo.

Kutoa ni muhimu sana kwa kuwa ni kujiwekea hazina mbinguni ambapo nondo na kutu hawali, kama isemavyo katika Mathayo 6:19-21 “Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; 20 bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; 21 kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.”

Kutoa mbele za Mungu unajiwekea hazina mbinguni mahali ambapo utakuwa ukiishi milele, mfano mmoja aliutoa Mzee Moses Kulola kwa kusema “unakuta mtu anajisifu kuwa ana milioni kumi (10) benki ana mali nyingi sana ila hana hazina yoyote mbinguni na ni bahiri katika kutoa, ukimuuliza mtu huyu anaenda mbinguni, akifika bila shaka hata mahali pake kama atapata bahati hiyo hakutakuwa na hazina halizojiwekea.” Ukifahamu kuwa wewe duniani unapita kuelekea mbinguni weka juhudi katika siri hii pia. Kutoa katika hali ya kawaida ni kama kupoteza ila ni njia ya kujazwa vingi zaidi, ndiyo maana biblia usema kuwa “amfadhiliye/amsaidiaye maskini amkopesha BWANA”  

Mungu anataka watu wake kujitoa kwa ajili ya kuifanya kazi ya injili na ana thamini sana wote wanaojitoa kwa ajili ya injili. Hagai 1, Na BWANA uumizwa sana na watu wanaothamini mambo ya nyumba zao na kusahau kazi ya nyumba ya BWANA.

Alisema nami mama yangu kuwa imenipasa kujisikia vibaya na kuona aibu sana pale napopendeza na kuonekana nipo vizuri sana huku wakitazama familia yangu na wazazi wangu hata kwa sehemu ndogo sana hatufananii, yaani nimewaacha mbali sana na hata aibu kutambulisha kuwa ni wazazi wangu. Lengo la nasaha hii kwangu ni kunihimiza kuwa nina wajibu wa kuwafanya wazazi wangu wang’ae na kupendeza hata watu wakitazama waone namna ninavyo jali.


Sehemu  tatu za sadaka igusayo moyo wa Mungu

       Kutoa miili yetu kama sadaka na dhabihu takatifu iliyo hai.
       Kutoa muda wako kama dhabihu takatifu iliyo hai ili ikamfanyie yeye manukato.
       Kutoa mali na fedha zako kwa ajili ya kumtumikia BWANA.

Katika maeneo yote haya Mungu alifanya ili mwanadamu afurahie uzuri na uaminifu wa Muumba wake, na anafurahi sana kuona mwanadamu anashiriki pamoja naye na kumshirikisha katika kila jambo ampalo.

Itaendelea wiki ijayo...

Mwalimu Kelvin Kitaso anapatikana kupitia 0767190019 / 0713804078 na pia kupitia barua pepe; kitasokelvin@gmail.com

SOMO: FAIDA ZA KUTEMBEA KATIKA BARAKA ZA AGANO NA MUNGU - MWALIMU MWAKASEGE (1 & 2)

$
0
0


SEMINA YA MWALIMU CHRISTOPHER  MWAKASEGE - DODOMA
SOMO: FAIDA ZA KUTEMBEA KATIKA BARAKA ZA AGANO NA MUNGU
Neno kuu: Eph 1:3

DAY ONE.


LENGO: Kukusaidia uzidi kufaidika na baraka zinazopatikana ndani ya imani uliyonayo katika Kristo Yesu.
•Kutokuwa na msukumo wa kuwashuhudia wengine habari za Yesu ni dalili ya kutokuridhika na wokovu.
•Usipoona faida ya kuwa ndani ya Yesu huwezi kupata msukumo ndani yako wa kushuhudia wengine.

MSISITIZO: BARAKA ZA AGANO. Msisitizo zaidi kwenye agano lenyewe.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA (MSINGI)

1. Mungu anaweza kumbariki mtu nje/ ndani ya agano naye. Mwanzo 17:15-21
•Ishmael alibarikiwa na Mungu nje ya agano.
•Isaka alibarikiwa na Mungu ndani ya agano.

2. Unaweza ukawa ndani ya agano na Mungu na usifaidike na baraka zilizomo ndani yake. Mwanzo 39:1-6
Mfano: Yakobo
•Yakobo alitakiwa afaidi baraka za agano, lakini kwa kuuzwa kwa Yusufu baraka zote zilikwenda misri.

3. Kufaidika na baraka zilizopo ndani ya agano ni uamuzi wako hata kama wewe ni mhusika wa agano hilo. Kumb 30:19-20
•Mungu ameweka uchaguzi ndani ya agano kuna baraka na laana, uzima na mauti. Ndani ya agano kuna mabadilishano.

4. Hali yako ya maisha inategemea kama unatembea na kuishi katika agano la Mungu. Mwanzo 49:1-2,28
•Kitu kilichobadilisha watoto kuwa kabila ni baraka walizoachiliwa na baba yao Yakobo.
•Kuna baraka zinazotengeneza na kubadilisha maisha ya watu. Mwanzo 28:1,6-7.




DAY TWO.


NJIA ZINAZOWEZA KUKUSAIDIA KUTOFAUTISHA KATI YA BARAKA ZA MUNGU ZILIZOMO NDANI YA AGANO NA BARAKA ZISIZO NDANI YA AGANO.

Maana ya baraka: kustawi, kuwezeshwa, kuinuliwa, kufanikuiwa, kujulikana, kuwa na furaha, amani, kutoshelezwa, kutengenezwa unavyotakiwa kuwa, kulindwa, kuongozwa.
•Kufanikiwa kupo ila si kila kufanikiwa kumetokea ndani ya agano.

1. Baraka zinazokuja kwa kuwa umeomba ingawa zipo nje ya baraka zako za kurithi kutoka kwa Mungu. Mwanzo 17:15-23
•Baraka ya Ishmael ni matokeo ya Ibrahim kumwombea kwa Mungu.
•Baraka ya Isaka ni matokeo ya Mungu kumwekea.
•Baraka za agano ni baraka za kurithi. Mwanzo 15:18-20, 17:1-4, 7-8.
Baraka alizopewa Ibrahim zilikuwa ndani ya agano.
Swali: Baraka unazoomba kwa Mungu zipo ndani/ nje ya agano? Gal 3:13-14,29,9
Eph 1:3, Gal 4:6-7, Rom 8:16-17
Sisi tu warithi wa Ibrahim sawasawa na ahadi na tu warithi wa Kristo.
•Usisome biblia kama biblia bali soma biblia kama agano maana kuna baraka zinazokuhusu wewe.
•Omba sawasawa na urithi.

2. Kuangalia baraka za kujitafutia tofauti na alizokuahidi Mungu. Mwanzo 17:15-17
•Baraka za agano hutafuti bali unapewa maelekezo jinsi ya kuzipata.
•Baraka inakuja na baraka. Mwanzo 28:1-9

3. Kutaka kubarikiwa kwa kufuata mkumbo badala ya kufuata maelekezo upewayo na Mungu. Mwanzo 49:28, 26:1-5-25
Mfano: kutaka kuoa/ kuolewa kwa kufuata mkumbo au kwavile wengi wameoa/ kuolewa bila kuangalia agano la Mungu maana ndoa ipo kwenye agano Mungu atakupa maelekezo jinsi ya kukutana na huyo mtu.
Kuanzisha biashara kwa kuwa umeona jirani yako mwenye hiyo biashara amefanikiwa.

Litaendelea jumatano ijayo… shukrani kwa 'Neno lililo Hai kwa kuandaa somo hili.


MAMA WA MIAKA 76 AKUTANISHWA NA BINTIYE MIAKA 49 TOKA ALIPOJIFUNGUA AKIAMBIWA ALIFARIKI

$
0
0
Mama na mwana wakiwa wenye furaha baada ya miaka 49 toka watenganishwe
Hebu fikiria unapoambiwa kitu katika moja ya siku yako kubwa maishani, siku ambayo mtoto wako alizaliwa lakini alifariki mara baada ya kuzaliwa ….lakini unakuja kugundua mtoto wako yupo mahali fulani duniani. Hiki ndicho kilichotokea kwa mwanamke huyu wa huko Missouri nchini Marekani.

Mwanamke mwenye umri wa miaka 76 anayefahamika kwajina la Zella Jackson Price kutoka eneo la Olivette Missouri ameishi nusu ya maisha yake akiamini binti yake alifariki siku alipomzaa. Lakini mwanamke huyo alipatwa na mshtuko alipogundua kuwa amekuwa akiishi akimini uongo alioambiwa kwa miaka 49 alipojifungua binti yake na kudanganywa kuwa amefariki. Binti yake anayefahamika kwa jina la Melanie ambaye ni mzima wa afya hatimaye aliweza kukutanishwa na mama yake mzazi, binti huyo aliyekuwa ameasiliwa na familia nyingine alitaka kumjua mama yake mzazi toka siku nyingi na alipatwa na mshituko ndoto yake ilipotimia kwakukutana na mama yake mzazi pamoja na kaka yake

Melanie amemshukuru Mungu kwa nafasi ya pili kuweza kukutana na mtu aliyekuwa anamuhitaji kwa muda mrefu sana, ingawa binti huyo ni kiziwi lakini anaweza kujieleza kwakutumia lugha ya vitendo. Mungu ni mkubwa. Hata hivyo haijaelezwa ilikuwaje mwanamama huyo kuambiwa mtoto wake amekufa kumbe alichukuliwa na familia nyingine. Ambapo kwa mujibu wa taarifa, familia hiyo inapanga kuanza uchunguzi wake kujua nini kilitokea hospitalini kwa mtoto huyo kuchukuliwa.

Angalia video mama na bintiye walipokutanishwa kwa mara ya kwanza baada ya miaka 49


MAMBO MATANO AMBAYO KILA MTU HUPENDA KUFANYIWA

$
0
0
Na Faraja Mndeme,
GK Contributor.

1.KUSIKILIZWA.
Moja ya hitaji muhimu la mwanadamu yoyote ni kupenda kusikilizwa na watu wanaomzunguka.Hakuna mwanadamu yoyote ambaye hapendi kusikilizwa.Unapompa  mwingine thamani ya kumsikiliza unapata nafasi ya kuweza kupata nafasi kwenye moyo wake.Hata iwapo muda mwingine huenda kinachoongelewa hakikupendi sana,msikilize bila kumuhukumu wala kumwingilie pindi anapozungumza.Msikilize kwa umakini na utaratibu.Mara nyingi huenda tunasikiliza ili kuweza kutoa majibu ya kile kinachozungumzwa lakini muda mwingine imetupasa kusiliza tu bila kutoa jibu lolote.Baadhi wengine hawajawahi kupata nafasi kusikilizwa bila kuhukumiwa na wengine hawajawahi kusikilizwa kabisa.Hii ni Moja ya namna mojawapo ya kuweza kupata kibali kutoka kwa wengine.

2. KUPENDWA.
K wa miaka kadha wa kadha sijawahi  kutana na mwanadamu ambaye anasema hapendi kupendwa.Kila mmoja wetu wanatamani kuona hisia zao zinathaminiwa.Kupenda mwingine kuna ambata na mambo kadha wa kadha.Unapoaamua kuwapenda wengene hauangali namna walivyo na n wanaweza kuwa na mchango gani kwenye maisha yako bali unapojenga utamaduni wa kuwapenda wengine unapata wigo mpana wa kuweza kupata kibali kwenye maisha yao binafsi,biashara,kazi na kwenye shughuli mbali mbali.Ni muhimu kuhakikisha unawapenda wengine bila ukomo.Upendo hauchagui,umri,rangi,kabila au dini.Upendo ni lugha inayoweza kuongelewa na mioyo yote ya wanadamu ulimwenginu.Wapende wengine bila kuhukumu namna ya makosa yao yalivyo na madhaifu yao.


3.  KUTHAMINIWA.
Kila mmoja wetu anatamani kuonekana ni bora kwa wengine licha ya madhaifu walio nayo.Mahangaiko mrngi tunayoyaona leo kwenye ulimwengu huu ni ya kutafuta kuonekana una aina fulani ya thamani.Mavazi tunayovaa,vyakula tunavyokula,makazi yetu na mambo mengi haya yote yanaonyesha namna kila mtu anavyopenda kuonekana ni bora hata iwapo kuna mapungufu kadha wa kadha.Thamani ya mwanadamu haishuki bali tabia ya mtu ndio inaweza kushuka au kupanda thamani.Thamani ya mwanadamu haina kilinganisho cha gharama hapa ulimwenguni.Hakikisha unajenga utaratibu wa kuwathamini wengine,thamini mawazo yao,maisha yao na kile wanachokifanya bila kujenga hali ya kutanguliza kuhukumu bila kuonyesha uthamani wao.


4. KUKUBALIWA.
Wanadamu wengi wa dunia ya tatu tumekuwa na chgamoto ya kuwaku bali wengine kama walivyo,Mahangaiko mengi tunayoyaona leo ni kwa sababu wengi wetu hatujajengewa mfumo wa kujikubali na kuwakubali wengine kama walivyo.Madhaifu yao ndio nguvu zetu,Ni muhimi unajenga kuwakubali wengine bila kujenga hoja zisizo na msingi ambazo zitaonyesha wa kuwadhalilisha na kuwafedhehesha.Muda mwingine iwapo unaona huwezi kumkubali mtu kama alivyo usionyesha kitendo chochote ambacho kitaonyesha hisi hasi ambazo zitakuwa hazina msingi wowote.Unapotaka kibali kwa moyo wa mwingine anza kumkubali na kupokea kama alivyo.Taratibu taratibu ndipo unaweza kumsaidia kutokana na hali aliyokuwa nayo.


5. KUPONGEZWA.
Miezi michahche iliyopita nilikuwa nafanya kozi fupi ya namna ya kuwafundisha Mbwa ili kuweza kufanya kile unachotaka.Katikati ya kozi niligundu moja ya hatua muhimu ya pale Mbwa anapofanya vizuri kile ulichomwagiza basi Unampongeza.Mara unapojenga utamaduni wa kumpongeza ndipo alipojenga jitihada za kufanya vyema zaidi kili ulichomwagiza afanye.Je iwapo Mbwa napenda kupongezwa vipi kuhusu mwanadamu ambaye ana hisia kamili? Ni muhimu unajenga tabia ya kuwapongeza wengine pale wanapofanya vyema bila kinyongo na kijicho.Wapongeze na wafurahie kwa mafanikio yao.Pongeze zinaweza zisiwe vitu vya thamani  bali hata namna unavyowazungumzia kwa wengine.Kuna njia kadha wa kadha ya kuonyesha pongezi zako kwa wengine.Pongezi ni moja ya njia nyingine ya kupata kibali kwa Wakuu na Wanadamu pia.


E-mail:naki1419@gmail.com
+255788454585
God Bless Y’All

GLORIOUS WORSHIP TEAM NA SUNDAY CELEBRATION MSIMU WA 6

$
0
0

Kama ilivyo ada kwa siku za Jumapili, Glorious Worship Team inakuletea Sunday Celebration ambayo inakujia mahsusi kukuinua viwango vyako kiroho na kimwili, kupitia sifa na kuabudu, pamoja na mafundisho ya namna mbalimbali - bure bila kiingilio kwenye ukumbi wa Victoria Service Station.

Wakati unakaribishwa kwa ajili ya tarehe 26, yaani Jumapili hii, GK tunakuletea picha kadhaa za namna mambo yalivyokuwa Jumapili iliyopita, ambapo Eric Shigongo sanjari na Masanja Mkandamizaji walinena na watu waliojitokeza siku hiyo.












UBATIZO NI HAKI YAKO (1) - MCHUNGAJI MADUMLA

$
0
0
Mchungaji Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe…

Haki ya msingi kwako ni ubatizo. Haki hii ni kwa kila aaminie jina la Yesu Kristo,anapaswa abatizwe kama vile Yesu Kristo alivyobatizwa akionesha kielelezo cha imani yetu.Biblia inasema;

” Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali.
Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake;” Mathayo 3:15-16

Hivyo basi ubatizo ni haki yako ya msingi. Na kwa sababu ubatizo ni haki yako ya msingi basi ujue shetani na mapepo yake hayatakupa mpenyo kuipata haki hii ya ubatizo kiuharisia wake,maana shetana na nguvu za giza zipo tayari kuregeza uzi ukayafanya mambo mengine ya kiimani lakini sio ubatizo!


Wabatizwa wakiwa katika mto Yordani-Israeli katika moja ya ziara yangu ( Katikati ni askofu wa jimbo la Tarime EAGT,Askofu Fransis Mbwilo )

Tafsiri nyepesi na iliyo sahihi ya ubatizo ni;

Ubatizo ni tendo la imani la kuuzika utu wa kale pamoja na mambo yake na kufufuka katika nguvu za Kristo Yesu./Au kufa na kufufuka pamoja na Kristo Yesu.

Neno linasema; ” Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?
Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.” Warumi 3:4

Biblia inaposema ”… Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake… ” maana yake tuliuzika utu wa kale wenye kuharibika.Kumbuka hili;huwezi kuzika mwili nusu,bali kinachozikwa ni lazima kiwe kitu kizima yaani ni chote, mfano mtu azikwapo-ni lazima azikwe mwili wote maana haiwezekani kuzikwa kichwa tu na kubakia kiwili wili,hivyo hata katika ubatizo mtu hawezi akabatizwa kwa kunyunyuziwa maji,bali apaswa azamishwe mwili mzima kuwakilisha tendo la kiimani la kuzikwa na kufufuka na Yesu Kristo.


~ Mkristo asiyebatizwa amekosa haki yake.

~ Mkristo aliyebatizwa kwa ubatizo mwingine uwaye yote isipokuwa ubatizo aliobatizwa Yesu Kristo amekosa haki yake pia.

~ Hakuna ujanja ujanja wa ubatizo wa kunyunyuziwa maji kichwani au njia nyingine yoyote ile,ubatizo halisi ni mmoja tu wa maji mengi uliovuviwa na Roho mtakatifu.

Ni afadhari sana upoteze haki nyingine kuliko kupoteza haki yako ya ubatizo. Kwa sababu ubatizo ni sehemu kubwa ya wokovu,yaani asemaye ameokoka sharti abatizwe.Maana imeandikwa;

“ Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.” Marko 16:16

Ooh,kumbe!

~ Ubatizo huja baada ya kuamini. Kwa lugha nyepesi ni kwamba hakuna ubatizo pasipo kuamini. Na ndio maana nalikueleza kuwa ubatizo ni tendo la imani. Kama kuna suala la kuamini kwanza ndipo ubatizwe hii inahusishwa na uwepo wa mafundisho ya msingi juu ya ubatizo.

Biblia imeweka mkazo juu ya kuamini kabla kubatizwa, ” Aaminiye na kubatizwa ataokoka;…”

Mtu hawezi kubatizwa pasipo kuamini.

Imeandikwa;

“ Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe? [ Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.]Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza.” Matendo 3:36-38

Towashi alipoamini tu,akabatizwa saa ile ile. Na ndivyo inavyopaswa katika ubatizo,pale mtu anapoamini fundisho la Kristo Yesu juu ya ubatizo inafaa abatizwe saa ile ile. Towashi alikuwa darasani akifundishwa neno la Bwana kupitia kinywa cha Filipo,

Kama Towashi atuoneshavyo kwamba ili mtu abatizwe ni lazima apitie darasa la fundisho la ubatizo ili apate haki yake,kisha akiamini ubatizwa mara.

Sasa,unisikilize mpendwa; 

Kama kuna hali ya kupitia darasa kusudi uamini,ili hatimae ubatizwe basi mtoto mchanga hawezi kupitia darasa lolote lile,wala mtoto mchanga hawezi kuamini. Na kama hawezi hivyo vyote,basi ni dhahili hastahili ubatizo kabisa maana hawezi kuamini.

Bali kwa habari ya mtoto mchanga,anaweza kuwekwa wafku kwa Bwana kupitia mtumishi wa Mungu iwe katika ibada au hata nyumbani anaweza kupelekwa kwa Bwana kwa kuwekwa wafku,ikiwa na maana mtoto huyo anakabiziwa kwa Mungu mwenyewe.

Haki hii ya ubatizo ikifanywa kama mapokeo tu,haina maana na wala udhihilisho wa nguvu za Roho mtakatifu hautaonekana.

Sikia,hata kama watu watabatizwa kwa maji mengi,lakini kama ubatizo huo haukuambatana na mafundisho ya kina yenye kuuleta uwepo wa Roho mtakatifu na ikatokea kwamba Roho wa Bwana hakuhusika basi ubatizo huo utakuwa ni wa kimapokeo na wala utu wa kale kwa wale watakao batizwa hautavuliwa. Ngoja nikupe mfano kidogo;

Sauli kabla ya kuchaguliwa na Bwana awe mfungwa wa Kristo Yesu,yaana mtume wa Bwana-alibatizwa kwa ubatizo wa maji mengi na akaendelea kuwaudhi waamini wa Kristo Yesu. Mtu huyu alibatizwa kama mapokeo ya dini yao ya kiyahudi,lakini katika ubatizo huo hakukuwa na kuuzika utu wa kale maana bado aliendelea kuua. Imeandikwa;

” Enyi wanaume, ndugu zangu na baba zangu, nisikilizeni, nikijitetea mbele yenu sasa. Waliposikia kwamba anasema nao kwa lugha ya Kiebrania wakazidi kunyamaza; akasema,

Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi;nikawaudhi watu wa Njia hii hata kuwaua, nikawafunga, nikiwatia gerezani, wanaume na wanawake. ” Matendo 22:1-4

Paulo anawaeleza kwamba alipitia taratibu zote za sheria ya baba zake,ambapo sheria moja wapo ya dini ya Kiyahudi ni ubatizo wa Yohana. Ubatizo wa Yohana ni ubatizo wa maji mengi,sasa ingawa Paulo alibatizwa huko kwa maji mengi kama mapokeo ya kidini lakini bado aliendelea kuwa muuaji yaani utu wake wa kale haukufa!

Mpaka pale alipobatizwa tena kwa Roho mtakatifu ndipo akauzika utu wake wa kale na kuupata utu wa utukufu kwa ajili ya kazi ya Bwana. Ndio maana ninakuambia kila ubatizo ni lazima usimamiwe na kuongozwa na Roho mtakatifu mwenyewe ili nguvu za kuzika utu kale zionekane.

Makanisa ya leo,ipo shida hii;

* Wengi ubatiza kwa kufuata mapokeo pasipo kuongozwa na Roho mtakatifu,maana hata fundisho lenye nguvu hukosekana na hatimae ubatizo unakuwa hauna nguvu yoyote. Na ubatizo usio kuwa na nguvu yoyote ni sawa kama kuogelea tu katika maji kisha na kurudi nyumbani ukiwa vile vile.

* Makanisa mengi huwanyima waanio haki hii ya msingi . Maana huwazuia kwa kuwaambia ubatizo waliobatizwa awali wakiwa wachanga unatosha! Wengine bado huendelea kuwanyunyizia maji badala ya kuwazamisha kama ipasavyo.

Ifike wakati sasa waamini wajue kabisa kwamba katika ubatizo ndipo mahali sahihi pa kuzika magonjwa na kila aina ya udhaifu uliopo katika miili yetu…



* Kwa huduma ya maombi na maombezi,nipigie sasa kwa namba hii;0655-11 11 49.

Mch.Gasper Madumla

Beroya bible fellowship church.

ITAENDELEA

UBARIKIWE.

KWA TAARIFA YAKO: SAFARI YA GOSPEL KITAA HADI HIVI SASA

$
0
0
Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu

Januari 2012, wafuasi wakiwa 600
Gospel Kitaa, ambayo imeanza mwaka 2011, imekuwa na lengo hasa la kuwavuta vijana na kuwafanya wawe watumishi wa Mungu, kwa namna ambavyo anapenda wamtumikie. KWA TAARIFA YAKO jina la Gospel Kitaa lililenga hasa jamii ya watu mbalimbali, kwanza Gospel ikilenga kuwavuta wale wote wanaopenda na wasio na mashaka na injili, na pia neno Kitaa likiwalenga vijana moja kwa moja, ambao hufika kutazama kinachojiri "kitaani".

Kwa mwendo wa kusuasua na kama mzaa ndivyo ambavyo blogu hii ilianza, ikiendeshwa na Ambwene M. Mwamwaja, kabla ya kuungana naye Elie J. Chansa, na kisha Silas E. Mbise, na hivi karibuni Boniface Kazi. KWA TAARIFA YAKO Team GK wanaoonekana ni hao 4, ila pia kuna wale ambao hawaonekani, mmojawapo ni wewe unayetembelea tovuti kila siku :-) .

Mwenendo


Mwaka 2011 mwezi Aprili ndio ambapo habari ya kwanza iliandikwa kwenye blog hii, ambayo ilikuwa inamhusu mwimbaji Joyce Mlabwa, ambaye alikuwa ametoa toleo lake la pili la album ya picha za sauti. (bofya hapa kusoma) Kipindi hicho blog ikifahamika kama gospelkitaa.blogspot.com

Mwezi Aprili ulishuhudia habari moja tu ikiandikwa, kisha ikifuatiwa na habari mbili kuandikwa mwezi Mei, kisha kufuatiwa na miezi 4 ya ukimya kutokana na majukumu mengine ya kujenga taifa. Hata hivyo nguvu iliongezwa mara baada ya timu kuongezeka, baada Elie kujunga na GK, ambapo mwaka 2012 ukashuhudia jumla ya habari 750 zikiandikwa, kulinganisha na habari 18 kwa mwaka 2011.

KWA TAARIFA YAKO, GK ambayo ilizaliwa jijini Manchester Uingereza ambako wazo la Ambwene kuwa na blog ya kuandika habari za Kristo lilikamilika kwa vitendo akisaidiwa na rafiki yake Dkt Mbonea Mrango. Ila KWA TAARIFA YAKO makao makuu ya Gospel kitaa yalikuwa Kurasini kwenye majengo ya WAPO Radio FM ambako timu nzima ilikutana hapo, iliendelea kufanya vema, na kuanza kupata wadau mbalimbali ambao pia walikuwa wakiisikiliza WAPO Radio FM kwa njia ya mtandao, mara tu ilipoanza. Na hicho ndio chanzo cha mitandao mingine mingi kunakili ratiba ya vipindi kama ilivyoandikwa, ikiwemo mitandao ambayo haiandiki kuhusu habari za injili.

Julai 2014, wafuasi 9000
Uanzishwaji wa ukurasa wa facebook ulifanikisha kueneza injili kwa watu wengi zaidi, ambapo wafuasi walianza kufuatilia mtandao huu kutoka kila kona ya dunia. Ufuatiliaji wa habari za makanisa mbalimbali bila ya kubagua imekuwa sababu nyingine ya GK kupata mashiko, ambapo pamoja na kukua kwake, changamoto nazo zilizidi kukua, ikiwemo ile ya kufuatilia habari kwa muda mrefu na kisha mara baada ya kuandika, watu wengine kuinakili kama ilivyo na kuifanya yao (bila kueleza chanzo chao). KWA TAARIFA YAKO hilo ndilo lililopelekea kuanza mfumo wa kuweka alama kwenye picha na video ambazo GK imezipiga. Tazama baadhi ya video hizo kwa kubofya hapa.

Kwa kadri siku zilivyokuwa zinaenda na changamoto kuzidi, ndivyo ambavyo kumekuwa na mabadiliko kadha wa kadha ili kuendana na teknolojia, kuwezesha kufikisha injili katika viwango vya juu. Mwaka 2013 ulishuhudia mabadiliko ambayo kwa KWA TAARIFA YAKO hata mitandao mingine ililazimika kuiga mfano, ambapo Gospel Kitaa ilihama kutoka www.gospelkitaa.blogspot.com kwenda www.gospelkitaa.co.tz/ ukiuliza waendeshaji, safari kwao bado kufika mwisho.

Ni mengi yangewezwa kuzungumzwa kuhusu safari ya GK hadi kufikia hivi sasa, ila kiufupi. Tunaamini kwamba kuna mahala mtu huguswa na kile ambacho huwa tunakichapisha hapa, aidha kwa utafiti wetu, ama kupitia walimu mbalimbali na wahubiri ambao hutuma mafundisho yao kwa ajili ya kukufikia. Kama ambavyo hatutozi kwa ajili ya kuweka mafundisho kutoka kwa mtu yeyote, ndivyo tunaamini kwamba mafundisho yanafanyika baraka kwako. Maoni yako ni muhimu kama kuna mafundisho uliyoguswa nayo, jambo ambalo pia linamtia moyo mwalimu kuendelea kufundisha. Kama ungependa kuwa sehemu ya Team GK kwenye mkoa wowote uliopo, milango yetu iko wazi kwa ajili ya kumtwalia BWANA Yesu utukufu.

Ila kama ulikuwa hujui, KWA TAARIFA YAKO Team GK na majukumu yao ni kama ifuatavyo. Ambwene Mwamwaja; Mkurugenzi/Mwandishi mwandamizi, Elie Chansa; Mhariri/Mpiga picha mkuu, Silas Mbise; Mratibu/Mwandishi Mpiga picha, Boniface Kazi; Mpiga picha/Graphics

Katika yote tunayofanya na kupitia, tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha kueneza Injili kwa mfumo wa dijitali. Pamoja na yote, KWA TAARIFA YAKO mtandao huu usingefaa kitu kama haukupata watembeleaji wa kila siku kama wewe. Ahsante sana, endelea kueneza ujumbe kwa wengine injili na izidi kusonga mbele.

Hiyo ndio KWA TAARIFA YAKO, vinginevyo tukutane wiki ijayo...

SOMO: NENO LA MUNGU HALITAPITA BILA KUTENDA

$
0
0


NENO LA MUNGU HALITAPITA BILA KUTENDA

Na King Sam

SHALOM MWANA WA MUNGU,MUNGU AMEAHIDI KUKUBARIKI KUKUINUA KUKUTAJIRISHA KUKUPA USHINDI NDIVYO LILIVYO NENO LAKE HALIBADILIKI

Mathayo 24:35. Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

KAMWE NENO LAKE HALITAPITA KILE ALICHOSEMA NDIYO KITATIMIA KATIKA MAISHA YAKO,TATIZO HALIKO KWAKE LIKO KWAKO,KAMA MUNGU AMESEMA NITAKUPONYA HAWEZI KUSEMA UONGO NENO LAKE HALIJIPINGI NI AMINA NA KWELI,

UNATAKIWA KUJUWA TU HIVI KUNA MUDA WA KUPOKEA ALICHOSEMA MUNGU, MUNGU SI MUONGO,YAWEZEKANA WEWE UMEGEUKIA MIUNGU MINGINE UKIFIKIRI MUNGU AMECHELEWA KUKUPA ALICHOSEMA MAANA KUNA WATU WENGINE WAMEACHA KUMSUBIRI MUNGU MPAKA WAMEJIPATIA MALI KWA NJIA YA UDANGANYIFU WENGINE HATA KAZI WAMEJIPATIA KWA NJIA ISIYOPENDEZA WENGINE HATA KUOLEWA KWA NINI KWA SABABU WAMESHINDWA KUMSUBIRI MUNGU WAMEONA KAMA AMECHELEWA KAMA WANA WA ISRAEL WALIPOONA MUSA AMECHELEWA

Kutoka 32:1 Hata watu walipoona ya kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana wakamwendea Haruni, wakamwambia, Haya! Katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata.

KUNA MAANGAMIZI KWA KILE AMBACHO MTU AMEJIPATIA KWA KUTOKUMSUBIRI MUNGU AKAJIPATIA KWA NJIA NYINGINE NDIYO MAANA UNAONA KUNA MATATIZO YA NDOA KWA SABABU MTU ALIKATA TAMAA NA KUAMUA KUJITAFUTIA MCHUMBA NJE YA MUNGU,HATA KAMA NI BIASHARA NDIVYO HIVYO KILA KITU UTAKACHO JIPATIA UNAPOONA KAMA MUNGU AMEKAWIA UJUWE KITAKUWA NA MATATIZO KATIKA MAISHA YAKO KWA MTU WA HIVYO,

MUNGU HACHELEWI KILA KITU KINAWAKATI WAKE MAANA AMESEMA KWA NENO LAKE LITATIMIA TU KATIKA JINA LA YESU WEWE SUBIRI

ANGALIA HUYU MTU KWENYE BIBLIA NDIPO UTAJUWA KWAMBA MUDA WAKO UKIFIKA NENO LITATIMIA TU

Yohana 5:5 Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane.6 Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima? ALIKUWA NA MIAKA MINGAPI LAKINI MIDA WAKE ULIPOFIKA HAKUTOKA KWA DESTURI KAMA WENGINE WALIVYO PONA,WEWE MUDA WAKO UKIFIKA KAMA NI UPONYAJI AU BIASHARA AU KUINGILIWA NK ITAKUWA NI KWA NJIA AMBAYO SI YA MAZOEA KAMA WENGINE WALIVYOZOEA KATIKA JINA LA YESU,

MUNGU ANAJUWA MUDA WAKO WA KUTOKA HAPO ULIPO WEWE UNATAKIWA KUMWAMINI MUNGU TU UNAONA HUYU MWANAMKE ALIKUWA NATOKA DAMU MIAKA KUMI NA KIWILI LAKINI ALIAMINI TATIZO LAKE LITAISHA AKISHIKA UPINDO WA VYAZI LA YESU,

TATIZO WATU HAWANA IMANI KAMA UKIWA NA IMANI UNAWEZA SUBIRI UKIJUWA MUNGU HASEMI UONGO

BIBLIA INASEMA PASIPO IMANI..

Waebrania 11:6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

NDUGU YANGU HAKUNA HALI UNAYOPITIA AMBAYO UWEZI UKASEMA HAKUNA MAJIBU WEWE ANGALIA. NENO LA MUNGU TU MUNGU AMETOA MAJIBU YA HICHO UNACHOKIPITIA KILA TATIZO LA MTU LINAJIBU KWA NENO LA MUNGU AMESEMA UTASHINDA AMESEMA YEYE NI BWANA AKUPONYAYE NK

JUWA TU JE UNAMSUBIRI BWANA HUKU UKIMWAMINI AU UMEGEUKIA MIUNGU MINGINE?

YESU AKUTIE NGUVU UWEZEKUWA NA IMANI NA KUMSUBIRI MUNGU AKUTENDEE ALICHOSEMA MAANA YEYE SIYO MUONGO KATIKA JINA LA YESU POKEA HIYO NEEMA KATIKA JINA LA YESU AMEN.

KUMBUKA WANA WA ASAFU DAY NI LEO SAA 7 MCHANA, PATA MAELEZO


OMBEA TAIFA NA WAIMBAJI HAWA KATIKA CHAGUO LA GK

$
0
0

Leo katika chaguo la GK tupo Kinondoni kanisa la Kilutheri ambako tumekuchagulia kwaya ya Uinjilisti Sayuni kupitia album yao ya tatu ya video tumekuchagulia wimbo uliobeba album hiyo uitwao 'Dua na Maombezi' wimbo maalumu ambao unahimiza watu kuliombea taifa ili Mungu aliponye na rushwa, ajali, majanga mbalimbali pia kuwaombea watanzania ambao wanapitia mapito mbalimbali yakiwemo kufungwa magerezani, ugonjwa na madhaifu mengine mbalimbali ili Mungu akawe kimbilio lao na taifa letu limgeukie Mungu wimbo kutoka kitabu cha 1Timotheo 2:1.

Tunakutakia utazamaji mwema na kutendea kazi ujumbe uliomo kwenye wimbo huu kutoka kwa Uinjilisti Sayuni . Jumapili njema

PICHA ZA MATUKIO DUNIANI KWA WIKI ILIYOISHA JANA

$
0
0
©Jorist Wise
Ndani ya siku moja kuna mengi yanaweza kutokea, lakini katika wiki moja, matukio ya kutisha yameikumba dunia, ambapo vifo na majeruhi wengi yametokea. Kuanzia huko Chile ambapo kumekuwa na mlipuko wa Volcano Calbuco uliohamisha maelfu ya wakazi nchini humo, hadi Nepal ambapo zaidi ya wananchi 3500 wanahisiwa kufariki dunia, huku zaidi ya wengine 6000 wakijeruhiwa. Kuachana na hilo, Kaskazini mwa bara la Afrika, majanga ya melei kuzama yanazidi kutokea ambapo wahamiaji wamekuwa wakijaribu kuvuka bahari ili kusaka maisha bora barani Ulaya, Italia ikiwa ni nchi ya kupitia.

Zifuatazo ni picha za matukio hayo kama ambavyo GK imekukusanyia.

Chile

Takriban wakazi 1500 wamehamishwa makazi yao kutokana na mlipuko wa volcano Calbuco ambayo, ambayo imelipuka baada ya miaka 42. madhara makubwa yamejitokeza kusini mwa nchi hiyo, ikiwemo miji ya Puerto Varras na Puerto Montt ambapo maeneo kadhaa yamefunikwa na majivu, jambo ambalo lieleta taharuki kwa binadamu na mifugo.
Mlipuko wa volcano ulioambatana na majivu na radi. ©David Cortes Serey/AFP
Taswira kabla ya mlipuko © Andeshandbook.org
Taswira kutoka upande mwingine. ©Martin Bernetti/AFP/Getty images
Majivu yaliyotokana na mlipuko huo, ambayo pia huathiri usafiri wa anga kwa kiasi kikubwa. ©AP Photo/Diego Main/Aton Chile
Vijana wakiondoa majivu kwenye paa la nyumba yao, ambayo yametokana na mlipuko wa volcano. ©Martin Bernetti/AFP/Getty images
 
Mji ukiwa umebadilishwa rangi kwa uwepo wa majivu ya volcano Calbuco. ©EPA/Felipe Trueba
Armenia
Takriban miaka 100 iliyopita kwenye vita kuu ya kwanza ya dunia (1914-1918), kulitokea mauaji ya takribani Waarmenia milioni moja na laki mbili, ambao walishambuliwa na majeshi ya utawala wa Ottoman (Uturuki). Hata hivyo taifa la Uturuki limekataa kkubali kwamba mauaji hayo yalikuwa ya halaiki. Wakati Armenia wanaadhimisha kwa masikitiko, Uturuki kwa upande wao watakuwa wanaadhimishwa kwa shangwe.

Hivi karibuni Papa Francis alinukuliwa akiyaelezea mauaji hayo kuwa ya halaiki, jambo ambalo lilizua tafrani baina ya taifa la Uturuki na Vatican. Mataifa kadhaa ikiwemo Ufaransa na Urusi yameainisha mauaji hayo kama ya kimbari. Ujerumani imekuwa taifa jingine ambalo hivi karibuni limetoa rai kwa mauaji hayo kutambulika kama ya kimbari. Marekani haiyatambui mauaji hayo kama ya kimbari.

Sehemu ya waombolezaji kwenye kumbukumbu ya miaka 100 ya mauaji ya kimbari nchini Armenia
Mtazamaji akitazama picha kwenye makumbusho ya mauaji ya halaiki nchini Armenia. © Karen Minasyan AFP/Getty Images.
Sehemu ya waandamanaji nchini Armenia, tarehe 24 Aprili 2015.

Burundi
Nchini Burundi kwake Rais Pièrre Nkurunziza machafuko yamezuka na kupekelea vifo vya watu watatu, mara baada ya chama tawala nchini humo, CNDD FDD kutangaza kuwa  Rais Nkurunziza atagombea kwa awamu ya tatu kiti hicho, taarifa ambayo iliibua mtafaruku baina ya vyama vya upinzani vya siasa sanjari na wananchi.

Kufuatia hali ya hofu iliyotawala nchini humo, tayari wakimbizi wanaokadiriwa kuwa zaidi ya laki moja wameshavuka mpaka na kukimbilia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na Uganda - ambapo Tanzania nayo  inatarajiwa kupokea.

Polisi wakitawanya wananchi kwa virungu na gesi "mabomu" ya machozi. Kwa nyakati nbyingize, silaha za moto zimeripotiwa kutumika. ©Reuters

Polisi wakikabiliana na wananchi. ©AFP
Nepal
Tetemeko la ardhi ambalo limeikumba Nepal limepelekea zaidi ya wananchi 3,700 kufariki dunia na wengine zaidi ya 6,000 kujeruhiwa, huku Umoja wa Mataifa ukikadiria kwamba watoto zaidi ya milioni 1 wanahitaji makazi, kutokana na madhara yaliyojitokeza.

Taifa hilo ambalo limebarikiwa kuwa na milima mirefu duninani imeshuhudiwa na mataifa mengine ikipeleka wanajeshi 9 kati ya 10 katika zoezi la uokoaji, ambapo pia mataifa kama Marekani, Ujerumani, Israel, na India wamepeleka misaada na vikosi vya uokoaji, ili kunusuru madhara zaidi ya yale ambayo yamekwisharipotiwa tayari.

Licha ya majengo kuporomoka, majeruhi kadhaa pia wameripotiwa kutoka Mlima mrefu zaidi duniani, Everest, ambapo tetemeko lilipelekea barafu kufunika watalii na waongozaji wao. Tetemeko hilo limeripotiwa kuwa na kipimo cha richa 7.9

Sehemu ya kivutio cha utalii ikiwa imebomolewa na tetemeko hilo
Zoezi la uokoaji likiendelea.
Wanajeshi kazini
Wakazi wakijaribu kumuokoa mtu aliyefunikwa na kifusi ©Narendra Shrestha/EPA
Manusura wa tetemeko hilo akitolewa na waokoaji. ©Omar Havana/Getty Images

Mabaki ya makazi yaliyoharibiwa na tetemeko, Kashamandu, Nepal ©Navesh Chitrakar/Reuters
Athari upande wa barabara. ©Xinhua/Zuma Press
Manusura wa tetemeko akiwa amejawa na hisia ©Narendra Shrestha/EPA
Mwili wa mkazi wa Kashmandu ukiwa umefunikwa na kifusi. ©Navesh Chitrakar/Reuters
Kama unaishi kwa amani, basi hauna budi kumshukuru Mungu licha ya makwazo mengi unayokutana nayo. Sanjari na hilo, usiache kuombea majanga yaliyotokea kwa wananchi wa mataifa haya (wenzetu). Tukutane wiki ijayo.

SOMO : KANISA LA FILEDELFIA - ASKOFU KAKOBE

$
0
0


(UFUNUO 3:7-13)

“Na kwa malaika wa kanisa lililoko filedelfia andika:

Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu na wa kweli, aliye na ufunguo wa daudi,yeye mwenye kufunga wala hapana afunguaye, naye afungaye wala hapana afunguaye, nayajua matendo yako.Tazama nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza jina langu,wala hukulikana jina langu.Tazama, nakupa walo wa sinagogi la shetani, wasemao kuwa ni wayahudi nao sio bali wasema uongo.Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele yako na kujua ya kuwa nimekupenda.Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi name nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.Naja upesi.Shika sana ulichonacho asije mtu akaitwaa taji yako.Yeye ashindaye nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu,wala hatatoka tena humo kabisa, name nitaandika juu yake jina la Mungu wangu na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe lile jipya.Yeyealiye na sikio na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

Vipengele:

( 1 ). Mlengwa.

( 2 ). Wasifu wa Yesu Kristo.

( 3 ). Sifa njema za kanisa.

( 4 ). Karipio.

( 5 ). Maelekezo ya jinsi ya kufanya.

( 6 ). Ahadi.

( 7 ). Unabii kuhusiana na majira ya kanisa.




( 1 ) Mlengwa.

Mlengwa wa waraka huu ni kanisa la filadelfia.

Kanisa hili lilikuwa Asia ndogo maeneo ya Uturuki kwa sasa. Kanisa hili lilikuwa maili 30 kusini mashariki kutoka kanisa la Sardi.Mji huu wa filadelfia zabibu zilistawi sana hivyo mvinyo wa kila namna utokanao na zabibu ulipatikana hivyo kulikuwa na walevi wa kila namna.

( 2 ). Wasifu wa Yesu Kristo.

(Ufunuo 3:7) Yesu kristo hapa anajitokeza kama aliye mtakatifu na wa kweli, akimaanisha katika majira ya unabii wa kanisa ni katika kipindi hiki kanisa lingerejezwa katika utakatifu kama nyakati za kanisa la kwanza vilevile kanisa likarudia kweli, masomo ya utakaso, ubatizo wa maji mengi, ubatizo wa Roho mtaktifu n.k vikaanza kufundishwa tena. Vilevile anajitokeza Kama aliye na ufunguo wa daudi mwenye kufunga wala hapana awezaye kufungua tena mwenye kufungua wala hapana awezaye kufunga. Kinachozungumziwa katika ufunguo huu ni
§ Miujiza: kama Daudu alivyompiga goliath, ni katika majira ya filadelfia miujiza kwa jina la Bwana ikaanza kuonakana tena baada ya kukosekana kwa kipindi chote hicho ambavyo hata kipindi cha martin luther haikuwepo.Katika kipindi hichi Roho Mtakatifu alianza kufanya kazi tena na ule mvinyo uliokuwa mwingi katika mji wa filedelfia ulikuwa unaashiria Roho mtakatifu (Efeso 5: 18), (matendo 2:13) Ujazo wa Roho mtakatifu unafananishwa na kulewa pombe kwa sababu pombe huondoa aibu,huleta ujasiri na Roho mtakatifu hivyohivyo. Akifungua hapana awezaye kufunga, ni katika majira haya Injili ilifunguliwa sana na kweli ilidhihirishwa kipekee.

( 3 ). Sifa njema za kanisa.

(ufunuo 3:7) – wamelitunza neno la Bwana pamoja na kuzungukwa na makanisa

mengi yaliyozungukwa na makanisa yenye mafundisho ya wanikolai na yezebeli kama Sardi na Thiatra.

( 4 ). Karipio.

Hakuna karipio, kanisa hili lilikaa katika kweli, hata sisi tukikaa katika kweli, neno la Mungu kama lilivyo hatuwezi kuwa na karipio lolote, hawezi kuwa na neno juu yetu Yesu atakaa kwetu na Roho mtakatifu atatenda kazi pamoja na sisi hata ukamilifu wa dahari.

( 5 ). Maelekezo ya jinsi ya kufanya.

(Ufunuo 3:11) kanisa hili walitakiwa kushika sana ulichonacho, kushika sana neno(ufunuo3:10-11)

( 6 ). Ahadi.

(Ufunuo 3:8) – Tazama nimekupa mlango uliofunguliwa mbele zako, maana ni kwamba kanisa hili lilikaa katika hili hivyo lilifunguliwa mlango wa kuhubiri injili hata leo sisi tukikaa katika kweli Bwana atafungua mlago.

(Ufunuo 3:9)- tazama nakupa walio wa sinagogi la shetani, wasemao kwamba ni wayahudi, nao sio, bali wasema uongo maana yake ni kwamba pale ambapo kanisa lina juhudi ya kukaa katika usafi na utakatifu wa kristo nitakupa watu wanaojifanya wameokoka(wayahudi) kumbe sio, hao watasujudu mbele ya watu waliokoka maana yake watakiri na kushushwa chini ya watakatifu.

(Ufunuo 3:10)- Kwa kuwa umelishika neno la subira, mimi name nitakulinda.

(ufunuo 3:10)- atalitoa kanisa halitakuwapo katika dhiki kuu.

(ufunuo 3:12)- watakatifu watakuwa ni nguzo mbinguni watang’aa kipekee watatengwa, watafahamu jina jipya la Mungu, Yesu, mbingu mpya hayo yote tutapata kujulishwa tukishinda.

( 7 ). Unabii kuhusiana na majira ya kanisa.

Majira ya kanisa katika unabii yaliashiria jinsi kanisa litakavyokuwa miaka ya 1750 mpaka 1905. Baada ya Martin Luther kuwa amemaliza kazi nzuri katika majira ya kanisa la Sardi(wale wananotoroka) na kuanza kukaa katika kweli wanayofunuliwa, alipotoka Martin luther katika kanisa lake la Evenjilical Church likaja kanisa la Anglican, ambayo ilitokana katika mambo ya kitawala baadaye ikagawanyika vipande viwili High church(ilikuwa kama katholic na sanamu, low church(ilifanana na lutheran) likiwa na tofauti ndogo baadaye likaja Moravian. Katika kipindi hiki kweli nyingi zilianza kufunuliwa na kukawa na mafundisho mengi sana na wahubiri wa kila namna ambao walifundisha mafundisho hayo, na kuyasimamia eg:

v JONATHAN EDWARDS: Huyu alifariki 1758, alijifunza masomo ya akina Martin Luther akawa ameokoka, katika mafundisho yake alifundisha kuwa watu wenye sehemu katika kanisa lazima wawe ni wale waliookoka tu, na watu ambao hawajaokoka hawana sehemu katika kanisa hawawezi kuhesabika kama mshirika sawasawa na (matendo 2:17).

ii) GEORGE WHITEFIELD: Huyu alifariki 1770, kabla ya kufariki huyu ndiye aliyekuwa wa kwanza kufanya mikutano ya hadhara ya injili ambayo leo inafahamika kama crusade, mpaka kipindi chake watu waliamini mahubiri na mafundisho sio hadharani ni kanisani, ilikuwa kama kichekesho, vilevile huyu alikuwa wa kwanza kuhubiri bila majoho kamaYesu na mitume waliohubiri kwenye maboti,gerezani n.k jambo hili halikuwepo katoliki wala kipindi cha martin luther. George Whitefield alihubiri sana kiasi kwamba ilifikia mahali katika mikutano yake ya injili ilifikia kuwa na watu 8000 kila siku mwezi mzima, baadaye alifikia kuhubiri kusanyiko lenye watu 20,000 na linakumbukwa sana kusanyiko moja lililokuwa na watu 20,000 ambalo aliwapelekea kushiriki meza ya Bwana hadharani. Pamoja na kazi ya injili kubwa aliyokuwa na ifanya bado injili yake ilikuwa na mgogoro alifundisha habari za Election and pre-destination kwamba Mungu katika mpango wake tangu mwanzo amewachagua watu wa kwenda mbinguni.

v JOHN WESLEY: Huyu ndiye chimbuko la masomo ya utakatifu ni mtu ambaye anaheshimika sana alileta masomo ya utakaso katika kanisa ambayo yalikuwa yamesahaulika. Mwanzo wake kihistoria, alizaliwa 1703 alifariki 1791, akiwa na miaka 6 aligundua Mungu ana makusudi yake baada yakusahaulika kwenye ghorofa lililowaka moto ambalo hatimaye alipona aliopopewa ngazi na wazazi wakeashuke kupitia dirisha tangu wakati huo aliona Mungu alimuita awahubirie watu watoke katika Moto. Hatimaye 1738 aliokoka, Mungu alimuandaa sana alikulia Anglicana , alijifunza sana kwenye mafundisho ya George Whitefield lakini alipingana na mafundisho ya Pre-destination, and election hadharani, hatimaye George Whitefield akakubali kujinyenyekeza na kumpisha Wesley awe mwalimu, afundishe naye akaacha kuhubiri katika kipindi hichi unyenyekevu ulikuwepo kutokana na unyenyekevu. John Wesley alihubiri sana walimwita kichaa, alifanya kazi kwa saa nyingi sana aliweka record ya kutembea maili 250,000 kutumia farasi, alitoa sermons (hotuba) 40,000. Aliweka mkazo mkubwa sana katika utakatifu na utakaso, alipata vita vikali sana, shetani alishindana sana na Wesley, alikutana na mateso mengi sana maudhi, alitupiwa mayai viza(yaliooza) sehemu nyengine alikuwa anrushiwa mawe: ilikuwa haipiti hata siku moja hajafanyiwa moja kati ya hayo, hakujali! Siku moja alihubiri bila kupata hayo yote hajarushiwa mawe wala kutukanwa akaogopa sana, akaingia kichakani kutubu, akijua ameshusha viwango alikuwa akitubu kwa sauti kwamba ‘Bwana bila shaka nimeanza kukosea ndio maana leo mpaka jioni sijapigwa mawe’ kwa sababu aliomba kwa kelele wakapita wahuni wakasikia sala ile wakamrushia mawe Wesley, Wesley baada ya kuona hivyo alimshukuru Bwana hapohapo akasema ‘Bwana asante kwa kuwa leo haijapita nimerushuwa mawe tayari’.Kanisa lake liliitwa Methodist.

v WILLIAM CARY: Huyu ni mmishenari anayekumbukwa sana India baada ya kipindi cha Mtume Tomatho kufia huko mda mrefu, huyu aliweka msisitizo mkubwa kuhubiri injili ulimwenguni mwote akawakumbusha watu maneno ya Yesu kristo ya kuhubiri injili ulimwenguni kote, wakati huo injili inahubiriwa sana Uingereza, Marekani na nchi za kandokando alianzisha mashirika mbalimbali kufanya shughuli hiyo mashirika kama ‘London missionary society la mwaka 1795, Church missionary society (1799), British and foreign bible society lililosambaza sana Biblia (1804) matokeo yake wakatokea watu wengi ambao walisafiri kutoka nchi za mbali watu kama DAVID LIVINGSTONE kuja mpaka Afrika, CARY mwenyewe alienda mpaka India.

v WILLIAM BOOTH: Huyu alianzisha jeshi la wokovu(Salvation army) akaweka msisitizo mkubwa sana katika mafundisho ya utii, na wakristo kama askari wa Yesu.Walikuwa wanitana askari mwanzo lilikuwa linaitwa Haleluya Army, watu wakawa wanapeana vyeo baadaye likaitwa volunteer army ndio likaja salvation army, wakiwa wanavaa uniform kama za askari.

v CHARLES SPERGION: Huyu aliishi1784-1872 huyu anakumbukwa sana juu ya mkazo aliouweka katika mafundisho ya ubatizo wa maji tele, akapinga ubatizo wa watoto wadogo, mwaka 1863 ndio kulikuwa na mkazo mkubwa sana wa mafundisho hayo ya ubatizo.

v DWITT LEAMAN MUDDY: Huyu alishi 1837-1899 anakumbukwa sana kama baba wa injili kule marekani huyu naye alihubiri kwa uzito mkubwa na kuwaleta watu wengi katka wokovu 1894.

Baadaye yakaibuka kwa ghafla juu ya Mafundisho ya ubatizo wa Roho Mtakatifu mji wa Sunderland, watu wakwa wananena kwa Lugha: kukatokea uamsho wa ajabu sana watu wakaanza kuombea bila kufundishwa na mtu wakaanza kutoa mapepobaada ya hapo akotokea mhubiri mwingine aliyeitwa:

v SMITH WIGGLESWORTH: Huyu ni mmarekani aliishi1859-1946, baada ya kujifunza uamsho huo wa sunderland ambaye aliombewa akapona vidonda vya tumbo. Huyu ndiye mhubiri wa kwanza aliyehubiri mikutano ya injili kutumia ishara,miujiza katika injili yake vilema walitembea, wafu walifufuliwa, vipofu waliona.

Mpaka majira hayo vikawa vimerudi vitu vingi sana vilivyokuwa vimepotea tangu nyakati za kanisa la kwanza Eg: wokovu,ubatizo wa maji tele, ubatizo wa Roho mtakatifu,maombezi, mikutano ya injili ,utakatifu na utakaso na utii wa kijeshi wimbi hili liliitwa PENTECOSTALISMkwa sababu lilihusishwa na matendo ya mitume sura ya pili ya wakati wa mitume sku ya Pentecoste.



SOMO: SADAKA IGUSAYO MOYO WA MUNGU (Sehemu ya mwisho)

$
0
0
Na Kelvin Kitaso,
GK Contributor.

Wiki iliyopita tulimaliza kwa kugusia sehemu tatu za sadaka igusayo moyo wa Mungu. (soma hapa). Basi kwa wiki hii tutazichambua hizo sehemu tatu kwa sehemu hii ya mwisho kama ifuatavyo;


1.    Kutoa miili kama dhabihu iliyo hai ya kumpendeza Mungu

Maandiko matakatifu katika kitabu cha Warumi 12:1 yanasema “Basi ndugu zangu nawasihi kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.” Sehemu ya maandiko haya ni sehemu inayoonyesha msisitizo juu ya nini ambacho Mungu anafurahishwa kuona tunakifanya katika kuishi kwetu. 

Anasema itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, hii umaanisha kuna sadaka zilizo hai na sadaka nyingine ni sadaka zisizo hai mbele za Mungu. Mtume Paulo anazungumza kuwa ili Mungu akukubali ni lazima kutoa mwili wako kuwa dhabihu iliyo hai. Dhabihu iliyo hai katika miili yetu ni kujitoa kwa kila namna na kuruhusu miili yetu itumike mbele za Mungu kwa ajili ya utukufu wake.

Kuitoa miili kuwa dhabihu ni kuruhusu miili yetu kutii na kufuata makusudi ya Mungu, na pia ni kukubali kuishi kwa ajili ya injili. Kama umedhabihu mwili wako mbele za BWANA ni lazima utakuwa radhi kupatwa na jambo lolote kwa ajili ya BWANA na kwenda popote atakapokupeleka na kuacha lolote analokataza na kusema chochote anachokuamuru useme na kutenda lolote atakalo kuambia utende. Wakati mwingine ni kukubali mateso na aibu kwa ajili ya BWANA.

Unapojitoa katika kuifanya kazi ya Mungu kwa moyo na kupenda pasipo kuhimizwa na mtu awaye yeyote hiyo kwa Mungu ni dhabihu iliyo hai, unapofanya kazi ya Mungu kama kuomba, kuhudhuria ibada, kuhubiri/kufundisha, kufanya usafi katika nyumba ya Mungu, kutembelea wagonjwa na wenye shida mbalimbali, kuimba, na kufanya vitu vingi ila kama hautaki kupata sifa za wanadamu bali unafanya kwa ajili ya BWANA hiyo kwa Mungu ni dhabihu iliyo hai.

 Lakini pia anaongezea kusema takatifu ya kumpendeza Mungu. Huku ni kujitoa huku ukiwa na moyo safi mbele za Mungu. Ukitoa dhabihu iliyo hai na katika hali ya usafi wa moyo ni lazima utampendeza Mungu na kujitoa kwako kutakuwa ni ibada yenye maana; watu wengi wamekuwa wakidharau huduma kama kufanya usafi kanisani, kutembelea wenye shida mbalimbali na huduma nyingine ambazo uonekana ndogo ila huku ni kukosa maarifa katika mambo ya Mungu, kwa sababu Mungu anaangalia kama umejitoa kwa kumaanisha huku ukifurahia toka ndani ya moyo wako au unafanya kwa sababu umepangiwa zamu au umelazimishwa na viongozi wako, kama unafanya kwa moyo ni lazima Mungu aihesabu kazi yako kuwa ni kazi iliyo njema na itakuwa ni ibada iliyo njema kwake.

Fanya kila kitu kwa kujitoa kwa moyo na kupenda huku ukifanya ukiwa katika hali ya usafi wa moyo na ukitambua kuwa kila ukifanyacho kwa moyo na kupenda kwa ajili ya BWANA hiyo ni ibada, hata kwa viongozi wa kiserikali wanapofanya mambo katika hali ya usafi wa moyo na kupenda na kufanya kwa ajili ya BWANA, huwa ni ibada yenye maana mbele za Mungu.

Nikukumbushe kuwa kama ni mtakatifu lakini hujatoa mwili wako kuwa dhabihu mbele za BWANA, kwa Mungu hakuna thawabu uipatayo na pia kama unajitoa sana na kufanya mengi sana lakini kama si msafi wa moyo bado unapoteza muda wako na si ibada mbele za Mungu.

Pia ni vyema kufahamu kuwa miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu na ni vyema kulitunza kwa ajili ya utukufu wa Mungu na kutoruhusu jambo lolote lile litakalo fanya kujinajisi na kuwa mchafu, kwa kuwa Mungu uketi pamoja na walio safi wa mioyo. Ni lazima mwili usiambatanishwe na kitu chochote ambacho ni najisi. Kuwa dhabihu hai mbele za Mungu ni kuuhua mwili katika mambo ya ulimwengu huu na kuuweka wakfu kwa ajili ya BWANA.

Yesu aliwaeleza wanafunzi wake kuwa wakati wa hukumu wapo wengi watakao simama mbele za Mungu na kusema kuwa Bwana sisi tulijitoa sana kwa ajili ya kazi yako lakini Yesu atawajibu na kuwaambia siwajui, ila wapo watakatifu ambao hawakujitoa ambao uzungumzwa kuwa hawataipokea taji ya kazi yao.

2.    Kutoa muda kwa ajili ya BWANA

Ni ukweli kuwa muda wako ndiyo mafanikio yako, unavyoutumia ndivyo unaonyesha kama utafanikiwa au utashindwa kufanikiwa. Kwenye sura zilizo tangulia tulitazama kuwa matumizi ya muda vibaya ni kikwazo kikubwa cha mafanikio yako. Ila katika sura hii tutatazama kuwa uchoyo wa kumnyima Mungu muda ni kikwazo cha mafanikio ya mtu pia.

ukitazama umuhimu wa mawasiliano kwa wapenzi walio ndani ya ndoa na hata wanaokaribia kuoana, utagundua kuwa mazungumzo imara ya mara kwa mara ndio ubora wa mahusiano na hata ndoa kwao. Na ukimpatia mpenzi wako muda mdogo au ukimnyima kabisa muda wa kuzungumza nawe ni lazima utakuwa unaelekea kwenye hatari ya kuvuruga mahusiano yako au ndoa.

Jambo hili linauhusiano sana na Mungu wetu kuwa anapenda tuwe na muda naye na kuzungumza naye na hata kufurahi naye, ila tunapomnyima muda wa kukaa nasi ni kujitengenezea maangamizo yetu wenyewe na wakati mwingine ni kuvunja ukaribu kabisa naye. Kama uwezavyo kumtengea mpenzi wako au rafiki zako muda wa kuzungumza nao ndivyo unapaswa kumtolea Mungu sadaka ya muda wako. Fahamu ya kuwa muda unaoutoa mbele za Mungu ni sawa na sadaka na kama ukitoa vyema na kwa moyo wa kupenda ni lazima Mungu akubariki.

Waefeso 5:15-16 “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.” Tuna wakati mdogo sana ila ni lazima tuwe makini tunavyoutumia, epuka kutumia muda wako kama wasiomjua Mungu wanavyoutumia, kwa kuwa wao hawana hata muda wa kukaa na Mungu hata kidogo, ila kama watu wenye hekima za Mungu ni vyema kuukomboa wakati(kufanya mambo ya maana tu ambayo ni mema hata mbele za Mungu)

Visingizio ni ishara ya kupotea, epuka kila wakati kutoa visingizio kwa kuwa hivyo vilikuwepo, vipo na vitaendelea kuwepo ila waweza kuvishinda kwa kujikana wewe mwenyewe. Kuna watu ushindwa kumfanyia Mungu ibada kwa kuwa na visingizio kuwa hawana muda, muda huwa haukamatiki mkononi, na kama ukisubiri kuupata muda kamwe hautoweza kuupata, ila ukiamua kuutumia uliopo ni lazima utafaulu kufanya hata yasiyowezekana.

Acha visingizio kuwa una mambo mengi kwa kuwa hayatakuja kutokea yakawa machache ili upate muda wa kukaa na Mungu wako, pia ukisema una ratiba ngumu inayokunyima muda na Mungu ujue kuwa haitakuja tokea hiyo ratiba ikawa rahisi mpaka umeirahisisha kwa kuchukua maamuzi magumu ya kuwa na muda na Mungu.

Jiulize kuwa mbona mambo mengine unafanya lakini kwenye suala la Mungu tu ndipo unakosa muda, hii ni ishara ya kuwa Mungu kwako si muhimu kama vilivyo vitu vingine. Ni vyema kuweka msimamo wako wa kuwa na muda wako na Mungu na epuka kutokea kitu kingine kukuvurugia. Kama ilivyo kwa mtu wa karibu yako hauoni raha akiwa mbali au usipo wasiliana naye, ndivyo wapaswa kujisikia kwa Mungu kama haujawasiliana naye au kumtafuta na uhuzunike na kuugua sana.

Kama mtu mwenye shauku ya kumjua Mungu na kufanikiwa katika mambo yote ni lazima utumie vyema muda wako, kwa kuwa na ratiba ya kuhudhuria ibada zilizopo, na kuwa na ibada yako binafsi ambapo utamsifu, kumuabudu, kujifunza neno na kuomba Mungu.

Mathayo 26:40-41 “Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja. 41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho I radhi lakini mwili ni dhaifu”
Yesu anawaambia wanafunzi wake wangekesha hata saa moja, ni vyema kufanya jambo hili kudumu na BWANA hata saa moja kama mambo ni mengi kwa kuhudhuria ibada na wakati mwingine saa laweza likawa jingi ila Mungu anajali sana muda ulioweka kuwasiliana naye.

Muda ni sadaka ambayo unapaswa umtolee Mungu na epuka kutumia muda wote ndani ya siku pasipo kumpa BWANA muda wake.

3.    Kumtolea Mungu fedha na mali.

Eneo jingine lililo la muhimu sana katika maisha ya mwamini ni eneo la utoaji wa fedha na mali kwa ajili ya Bwana. Eneo hili ni muhimu sana kwa kuwa ni sababu kubwa sana ya Mungu kubariki watu wake na kwa mtu ambaye amekosa uaminifu katika hili eneo ukaaa chini ya laana ila kwa aliye mwaminifu uwa ndani ya Baraka.
Kuna aina mbali mbali za utoaji wa fedha na mali, aina hizo ni kama:

A.     Sadaka ya kuwasaidia watu walio katika uhitaji.
Hii ni sadaka ya mtu kumsaidia mtu haswa Yule ambaye hana matumaini na hana msaada kwa kutoa vile alivyonavyo na kumpatia. Hii ni sadaka ya upendo kwa kuonyesha kumpenda Mungu na kumpenda Yule unayemsaidia.

Hii ni sadaka ambayo mtu anaifanya mbele za mtu kwa ajili ya Mungu, na ikifanyika kwa mtu kujitakia utukufu wake huwa haina thawabu mbele za Mungu ila ikifanyika kwa moyo wa kupenda na kumtukuza Mungu ni njema na ubeba thawabu kubwa mbele za Mungu.

Luka 6:38 “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa kifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakacho pimiwa.”  Yesu anapotoa neno hili anazungumza na watu walioamini kuwa imewapasa kutoa vitu vyao kwa watu(wenye uhitaji) ila kutoa kwao si bure kwa kuwa ni lazima Mungu atawarudishia tena  kupitia watu,  si kama walivyotoa bali ni zaidi kwa kipimo cha kujaa  na kushindiliwa na kusukwa-sukwa hata kumwagika.

Mfano wa sadaka hii katika biblia ni:
       Sadaka ya Rahabu kujitoa na kujihatarisha ili wapelelezi kutoka Israeli wapone.
Kitabu cha Yoshua 2:1-6
       Sadaka ya BWANA Yesu kwetu wanadamu.
Kitabu cha Isaya 53
       Sadaka ya mjane wa Sarepta kwa Eliya.
Kitabu cha 1 Wafalme 17:13-16 “
       Sadaka ya Kornelio kwa watu wenye shida mbali.
Kornelio alikuwa mtoaji sana na aliwapa watu sadaka nyingi sana, kama inenavyo katika Matendo ya mitume 10:2 “mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima.
Sadaka ya mtu kujitoa na kutoa vitu vyake vya thamani ni sadaka yenye thamani sana mbele za Mungu na ni ishara ya kuwa mtu anampenda Mungu na yule anayemsaidia.

B.     Sadaka kwa ajili ya kuendeleza kazi ya Mungu.
Sadaka hii huitwa kwa majina mengi, na wengine huiita sadaka ya lazima. Wengine matoleo, wengine upenda kuiita sadaka ya ibada. Hii sadaka utolewa kila watu wa Mungu wakutanikapo pamoja kufanya ibada, na mlengo mkuu wa sadaka hii ni kuiendeleza kazi ya injili ipate kusonga mbele.

Ni sadaka ambayo utumika kuimalisha miundombinu ya kanisa, na pia kuwa saidia watumishi wa Mungu, na shughuli nyingine nyingi kama ilivyopangwa na kanisa husika la mahali pamoja. Hii ni sadaka muhimu sana na ni ya lazima kwa kila muumini kuangalia kuitoa kila anapokuwepo ibadani.
Hii ndiyo sadaka inenewayo kuwa usiingie nyumbani kwa BWANA mikono mitupu.

C.     Sadaka ya malimbuko.
Hii ni sadaka ambayo ni ya mwanzo wa kila pato ulipatalo katika yale uyafanyayo. Kama ni biashara basi yale mapato ya kwanza ni malimbuko yako kwa BWANA, kama ni kazi huwa mshahara wa kwanza, kama ni mazao uwa yale ya kwanza na vivyo hivyo kwa wanyama. Sadaka hii pia kwa nyakati za leo uwasilishwa kanisani.

D.    Sadaka ya shukrani
Kitabu cha Zaburi 50:14
Hii ufanywa kwa lengo la kumshukuru Mungu kwa lile lililotokea katika maisha liwe zuri au baya.
Mwalimu Mwakasege anaielezea kuwa ni sadaka ya muhimu kuifanya kila wakati unapofanyiwa jambo au unapokumbwa na jambo, na uelezea kuwa hii ni sadaka ya msingi sana kumshawishi Mungu azidishe utendaji wake katika maisha ya mwamini.

E.     Nadhiri.
 Zaburi 50:5
Matendo ya Mitume 5:1-11

F.     Fungu la kumi.
Malaki 3:8-12
Hii ni sehemu ya kumi ya mapato yako yote uyapatayo, ni  sadaka muhimu sana ambayo pia ipo kwa ajili ya kuiendeleza kazi yake.

-Mwisho-
___
Mwalimu Kelvin Kitaso anapatikana kupitia 0767190019 / 0713804078 na pia kupitia barua pepe; kitasokelvin@gmail.com





WANAUME KAZINI (MEN AT WORK) KATIKA PICHA JIJINI ARUSHA

$
0
0
Tangu zamani kumekuwa na mikutano ya wanawake, na hata polisi ukienda utakutana na dawati la jinsia. Lakini pamoja nayo wanaume wanakumbwa na maswahibu mengi. Ukienda kanisani, mashauri mengi kwa wanawake huwa ni kuhusu wanaume. Watoto wa mtaani utakutana na wengi wa kiume, ukienda polisi utakutana na kesi nyingi za wanaume. Pamoja nayo, ukitazama kasi ya vifo, wanaume ndio wanaongoza zaidi.

Pamoja na mambo mengi kuwakumba wanaume, bado huwa wanakaa kimya. Men at work ipo kwa ajili ya kushughulika nalo.


Transform Men, Transform Nations lilikuwa ni jukwaa la kujuzana na kukumbushana mambo muhimu katika maisha yetu ambapo mambo makuu sita yanazingatiwa na Men at Work, nayo ni; Uongozi, Upendo, Ulinzi, Uwajibikaji (Ugavi), Ubaba pamoja na Afya.
Tukio hili muhimu kwa familia, hasa kinababa lilifanyika The Arusha Hotel tarehe 26 Aprili 2015, ambapo mamia ya wakinababa walihudhuria katika kusanyiko hili la kwanza tokea kuanza kwa jukwaa hili. Zifuatazo ni baadhi ya picha za tukio hilo kama ambavyo GK ilipita kwa ufupi kuchukua ya kukufahamisha.

Malezi, Uwajibikaji, Ulinzi na usalama ni sehemu ya mada ambazo Bwana Maxwell alizichochea japo kwa uchache kabla ya ushirikishi wa hadhira kwa pamoja.
Dk.Richard Sungura ambaye alifundisha somo la Afya
 


                                                                     Efra Musica


 Picha 27 Za Wanaume Kazini







 


 




 

 



 

Mwezi Julai men at work wanajipanga kwa ajili ya Dar es Salaam, kisha muelekeo uwe Mwanza, kabla ya kuiteka Tanzania kwa ujumla, na kisha kusambaa hadi Afrika Mashariki.

Ifahamike kwamba Men at Work haijaja kuondoa kazi za Beijing, wala kupambana na malengo ya wanawake, wala kuwepo kwa ajili ya kutetea haki za wanaume, bali masuala ya uwajibikaji kwa mujibu wa Biblia.

Viewing all 1245 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>