Quantcast
Channel: Gospel Kitaa™
Viewing all 1245 articles
Browse latest View live

TAZAMA BINTI ALIYEFARIKI AOMBEWA NA MCHUNGAJI GWAJIMA NA KUWA HAI TENA

$
0
0

Angalia video chini ikionyesha binti aliyefahamika kwa jina la Joyce anayedaiwa kufariki dunia akiwa shuleni huko Vetenari jijini Dar es salaam alikokuwa akisoma masomo ya ziada ama tuition kwa kimombo siku ya jumatatu, mama pamoja na mwalimu wake anayesimamia kituo hicho ambacho ni shule ya chekechea walimchukua binti huyo hadi kanisani ufufuo na uzima akiwa katika hali ya mfu na kuombewa mbele ya maelfu ya waumini wa kanisa hilo na hatimaye kuwa hai tena. Tizama video hii ujionee mwenyewe kama GK ilivyojionea.




CHAGUO LA GK WIMBO WA INJILI USIOCHUJA NCHINI LICHA YA MIAKA KUPITA

$
0
0


Chaguo la GK siku ya leo ni kutoka kwa mwanamama Upendo Nkone ambaye ni mke wa askofu Mbeyela, wimbo tuliokuchagulia kutoka kwake ni ule uliotamba na kuendelea kuwepo masikioni mwa watu mpaka leo hii 'Usifurahi Juu Yangu'. Wimbo huu umerekodiwa jumapili iliyopita wakati mwanamama huyu akiimba katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam kwenye ibada ya shukurani kwa Mungu iliyoandaliwa na kanisa la Ufufuo na Uzima.

Nimatumaini yetu kwamba utabarikiwa kupitia wimbo huu kwamba licha ya kuimbwa kwa cd lakini utaona mwimbaji na waumini walivyouimba kwa kumaanisha na kuonyesha uwepo wa Mungu ulivyofunika eneo hilo. Barikiwa

Upendo na mumewe Askofu Mbeyela.




PICHA KAMILI UZINDUZI WA ALBUM YA KAMATA PINDO LA YESU YA ROSE MUHANDO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Angalia picha mablimbali za uzinduzi wa album ya malkia wa muziki wa injili nchini Rose Muhando iitwayo 'Kamata pindo la Yesu' iliyofanyika jumapili iliyopita katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam, chini ya Msama Promotions mgeni mwalikwa akiwa waziri mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tatu mheshimiwa Fredrick Sumaye. Ukitaka kuangalia video za namna uimbaji ulivyokuwa siku hiyo bonyeza hapa.

Jessica BM na kundi lake wakimsifu Mungu.
Haya sasa mambo yalinoga zaidi kama uonavyo.
Jessica BM akipunga mkono kwa furaha.
Meza kuu ikiwa imesheheni.
Mgeni rasmi mheshimiwa Fredrick Sumaye wakati anaingia ukumbini.
Glorious worship Team wakiwa jukwaani.
Baadhi ya umati wa watu waliohduhuria uzinduzi huo.
Mwanamama Upendo Kilahiro hakuwa nyuma kuziangusha ngome za shetani katika uzinduzi huo.
Watu wakifurahia kilichokuwa kikiendelea.
Timu ya wanamuziki wa John Lisu wakiwajibika.
Waimbaji wa kundi la John Lisu wakiimba

John Lisu akimsifu Mungu.
Safu ya wapigaji ya John Lisu wakiwa wamejipanga vyema katika kumsifu Mungu.
Gitaa linaponoga basi mwili nao lazima uwe na pozi zake, John Lisu akiwa kazini.
Ephraim Sekeleti kutoka Zambia hakuwa nyuma katika uzinduzi huo.
Ephraim Sekeleti.
Hudson Kamoga wa Msama Promotions akisoma risala kwa mgeni rasmi.
Mheshimiwa Sumaye akisalimiana na Rose Muhando.
Hatua ya kuzindua ikianza.
Hatimaye ikazinduliwa rasmi.
Kamata Pindo ikiwa hewani.
Askofu Bruno Mwakibolwa wa E.A.G.T Mito ya Baraka, ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza a makanisa ya Kipentekoste jijini Dar es Salaam hakuwa nyuma kusapoti kazi ya injili.

Mtume Dunstan Maboya





Jessica wa Boniphace Magupa. (mtu na mkewe)


Ni ngumu kuketi wakati Rose anaiimba, lakini pia ilikuwa ngumu zaidi kwa Emanuel Mbasha kutofika jukwaani.




Mgeni rasmi akimkabidhi Msama ahadi yake ya kununulia CD











Wengine wanapongeza kwa hela/mshiko/ankara, jamaa akaamua kumbeba huyu.

Mtume John Komanya





Mama Sumaye, Rose na Baba Sumaye

Jamani kwaherini

Mgeni rasmi akisindikiza kutoka ukumbini

Team WAPO FM, I Laizer, Beatrice Kamanga na David Gille



Wanahabari kutoka WAPO wakijaribu kufatisha style, bila mafanikio.

Umati ukianza kutawanyika


Gadlod akifurhia kuwa pembeni ya boksi la Rose... Yaelekea kuna mambo mazuri humo.

Mama na binti yake

Boniphace Magupa, Silas Mbise na Ezekiel (aliyetupa mgongo)

Team Msama wakijadiiana jambo baada ya uzinduzi kukamilika.
Team GK baada ya kumaliza majukumu kwenye tukio.



DAR ES SALAAM ILIVYOHITIMISHA MAOMBI YA SIKU 40 KWA WAPENTEKOSTE NCHINI

$
0
0
Wapentekoste nchini Tanzania hapo jana August 10 wamehitimisha maombi ya kuliombea taifa kwa toba na kumsihi Mungu kuliepusha na machafuko mbalimbali ya uvunjifu wa amani, pia kuombea mchakato wa katiba pamoja na chaguzi mbalimbali zinazokuja. 

Kwa mkoa wa Dar es Salaam maombi hayo yamefanyika katika kanisa la City Christian Center (CCC) Upanga, na GK ilikuwa sehemu ya tukio hilo.

Mwenyekiti wa baraza la makanisa ya kipentekoste mkoa wa Dar es salaam (CPCT) Askofu Dkt Bruno Mwakibolwa aliwaoongoza waumini mbalimbali katika kilele cha maombi hayo ambapo pia imeelezwa kuwa maombi hayo sio mwisho, bali kila mmoja anatakiwa kuendelea kuliombea taifa la Tanzania.
Askofu Dkt Bruno Mwakibolwa

Zifuatazo ni baadhi ya picha zikionyesha jinsi hali ilivyokuwa

 KWANZA NENO LA MUNGU LIKATOLEWA
Askofu Mboya akihubiri





Mchungaji msaidizi wa ccc upanga Deus Cheyo  (kushoto) akiwa na Askofu Mwakibolwa wakisikiliza neno kwa makini





MAOMBI YAKAANZA
Askofu Kameta







Nabii Mwasumbi akiongoza maombi


Maombi ni silaha ya kutulinda katika maisha yetu, sisi na ndugu zetu. Ni mstari mmojawapo uliopo kwenye wimbo ambao kundi la The Warriors kutoka Naioth Gospel Assembly wameimba. Nasi tunasisitiza kwamba maombi ndio ufunguo wa mambo yetu, tusisite na wala tusichoke kumuomba Mungu.


HABARI PICHA: KWAYA YA TUMAINI 'SHANGILIENI' YAWEKA WAKFU DVD YA NISAMEHE

$
0
0

Watu wanaonenenda bila maono, hakika hawana wanalotazamia kutimiza maishani, na hili limekuwa tofauti - kwani Jumapili tarehe 10 kwenye parishi ya Mtakatifu James inayoongozwa na Canon Andrew Kajembe, iliyopo Kaloleni jijini Arusha, dayosisi ya Mlima Kilimanjaro, ambapo kwaya kongwe nchini, Tumaini 'Shangilieni' ilikuwa ikiweka wakfu DVD yake ya Nisamehe.

DVD hiyo yenye nyimbo 11 ambayo iliwekwa wakfu na Askofu wa Dayosisi ya Mlima Kilimanjaro, Stanley Mount Kilimanjaro, iliambatana na changizo lenye nia ya kukusanya shilingi milioni 65 za Kitanzania, kwa lengo la kujenga kituo cha kutoa mafunzo ya muziki, ili kundi la vijana, ambalo ni kundi lenye vipaji mbalimbali vilivyokosa fursa ya kuendelezwa lipate kujinusuru na changamoto kadha wa kadha za maisha.

Kwa mujibu wa risala ilyosomwa kwa mgeni rasmi, Bi Janeth Jackson Simon ambaye alichangia kiasi cha shilingi milioni 5, kwaya ya Tumaini ambayo ina waimbaji 80 na matoleo 11 hadi sasa imeeleza kuwa milioni 65 zitatumika kununua eneo la ujenzi wa kituo hicho ambacho kinatarajiwa si tu kukuza vipaji kwa vijana, bali pia kupunguza ukosefu wa ajira nchini.

Zifuatazo ni picha za tukio hilo kama ambavyo GK ilikuwepo na kushuhudia.


Barabara ya Kaloleni, lilipo kanisa la St James




Kwaya ya Upendo ikisindikiza kwaya kuu 


kwaya ya Mtakatifu Cecilia





Efatha Choir


Askofu wa dayosisi, Stanley Mount Kilimanjaro akihubiri kwenye ibada ya pili


Mama Askofu Stanley, akiwa na mwana, Caleb









Askofu akisindikizwa mara baada ya kumaliza kuhudumu kwenye ibada ya pili






Gari iliyombeba Askofu Stanley Mount Kilimanjaro ikiondoka



Mgeni rasmi, Janeth Jackson Simon akikabidhiwa keki maalumu








Meneja wa mfuko wa jamii wa PPF kanda ya kaskazini akitamka mchango wake



Kwa mzee huyu, maneno yalikuwa machache na vitendo kwa sana. Kwani alishukuru kupata madhabahu ya kuteketezea sadaka yake






















Mnada ukaanza


Mchungaji msaidizi akipewa nakala ya DVD mara baada ya kuchangia kwaya

Zawadi kwa mama




Tumalize kwa kutazåma wimbo mmojawapo uliopo kwenye DVD hiyo, Niongoze Bwana, kama ulivyoimbwa kanisani hapo.



SOMO: UFAHAMU WA MIUJIZA YA MUNGU NA MIUJIZA YA MANABII WA UONGO

$
0
0
Askofu mkuu Zachary Kakobe.

UFAHAMU KUHUSU MIUJIZA YA MUNGU NA JINSI YA KUZIFAHAMU ISHARA NA AJABU ZA UONGO ZA SHETANI NA MANABII WAKE WA UONGO

NENO LA MSINGI:

2 WATHESALONIKE 2:9:

“Yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa KUTENDA KWAKE SHETANI, KWA UWEZO WOTE, NA ISHARA NA AJABU ZA UONGO.”

<><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><>

Katika somo la leo la Kanisa la Nyumbani, tunajifunza somo muhimu linaloambatana na majira tuliyo nayo ya nyakati za mwisho. Siku hizi, mahali pengi duniani ikiwamo Tanzania, kumezuka watu wa kila namna wakisema ni watumishi wa Mungu na kwamba wamepewa karama ya kutenda miujiza kwa ajili ya kuwasaidia watu. Kwa sababu hii, watu kila mahali wanamiminika kuwafuata, wakihitaji watoto au uponyaji mbalimbali wa mwili. Sehemu nyingine watu hao wanaodaiwa kuwa ni watumishi wa Mungu, wanatumia maji ya baraka kuponya; wengine wanatumia sanamu ya Bikira Maria; wengine wanawapeleka watu makaburini; wengine wanakwenda kupewa maji mahali inaposemekana alitokea Bikira Maria; wengine wanapewa madaftari ambamo humo wameandikiwa kwamba “Mungu” amesema watazaa mtoto wa kiume na wameandikiwa jina la kumwita, au mtoto wa kike na jina ambalo “Mungu” amemchagulia, na kupeleka madaftari hayo kila mara kuombewa na kukatazwa kwenda kliniki n.k. Wengine wamebeba “mimba” zilizotokana na maombezi ya watu hawa kwa miaka miwili bila kujifungua na kupata mateso makali mno. Wengine wameshuhudia kwamba wamepona kabisa baada ya kuhudumiwa na watu wa jinsi hiyo. Hapa ndipo penye mtego. Ili tusinaswe na mitego ya namna hii, Kanisa la Mungu linapaswa kufahamu Biblia inasema nini kuhusu Miujiza, Ishara na Ajabu za Mungu na zile za Shetani.



SHETANI ANA UWEZO WA KUFANYA MIUJIZA, ISHARA NA AJABU ZA UONGO

Miujiza kadhaa kwa kipimo kidogo cha uwezo ulio na mpaka. Wakati wana wa Israeli walipokuwa hawajatoka Misri, waganga na wachawi wa Farao, walifanya miujiza kwa uwezo wa shetani:

(a) Wachawi hawa walipozibwaga fimbo zao chini, ziligeuka kuwa nyoka kwa mfano wa muujiza alioufanya Mungu kwa kuwatumia Musa na Haruni [SOMA KUTOKA 7:8-12]



(b) Wachawi hawa walifanya muujiza wa kubadilisha maji kuwa damu kwa mfano wa muujiza alioufanya Mungu kwa kuwatumia Musa na Haruni [SOMA KUTOKA 7:19-22].



Unaona! Shetani ana uwezo wa kufanya miujiza na ishara. Biblia inasema katika:

UFUNUO WA YOHANA 16:14:

“Hizo ndizo roho za MASHETANI, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote, kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.”

Wakati wa dhiki Kuu, roho za Mashetani zitafanya ishara kubwa, hata kufanya moto kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu. [SOMA UFUNUO 13:11-13].

Lakini pamoja na ufahamu huu ulio nao sasa kwamba Shetani ana uwezo wa kufanya ishara na miujiza, bado inakupasa kufahamu jambo moja. Shetani ana mpaka katika uwezo wake wa kufanya miujiza. Hana uwezo wa Mungu wa KUTENDA MAMBO YOTE. Shetani hawezi kutenda mambo yote. Wachawi na waganga wa Farao ingawa walifanya miujiza tuliyoiona, hata hivyo walishindwa kufanya muujiza alioufanya Mungu kwa kuwatumia Musa na Haruni; pale walipoyabadilisha mavumbi ya nchi kuwa chawa. Wachawi hao waliposhindwa walikiri mbele ya Farao kwamba uwezo wa Mungu uko juu mno kuliko uwezo wao. [SOMA KUTOKA 8:16-19]. Wachawi na waganga wa Farao pia walishindwa kuzuia majipu yenye kufura yaliyotumbuka juu ya wanadamu wote wa Misri kutokana na mavumbi aliyoyarusha Musa hewani. Wachawi hao nao walipigwa majipu hayo [SOMA KUTOKA 9:8-11]. Fimbo ya Haruni ilizimeza fimbo za wachawi kudhihirisha uwezo wa Mungu ulivyo mkubwa mno kuliko wa majeshi yote ya shetani [SOMA KUTOKA 7:11-12].

ISHARA, AJABU NA MIUJIZA YA SHETANI WAKATI WOTE INA LENGO LA KUWAPOTEZA WANADAMU ILI WAANGAMIZWE

MATHAYO 24:24:

“Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu WAPATE KUWAPOTEZA, kama yamkini, hata walio wateule.”

Ishara, ajabu na Miujiza ya Shetani ndiyo maana inaitwa pia “NGUVU YA UPOTEVU” kwa jinsi ambavyo miujiza hiyo ilivyo madanganyo ya udhalimu kwa hao wanaopotea ambao hawataki kuiamini kweli ya Mungu na kuokolewa na hatimaye kuzidi kuipenda kweli katika wokovu. Nguvu hiyo ya upotevu juu ya wanadamu, hatimaye inawafanya wanadamu hao kuhukumiwa na kwenda Jehanum ya moto. [SOMA 2 WATHESALONIKE 2:7-12]. Kwa sababu hii, Kanisa la Mungu lazima liwe macho na kufahamu waziwazi jinsi ya kuzifahamu ishara, ajabu na miujiza ya Shetani na kutofautisha na ile itokanayo na Mungu. Kwa maarifa haya, ni rahisi kuziepuka kazi zote za Shetani na manabii wake; na pia kuwasaidia wengine waliokwisha kunaswa.

ALAMA TISA ZINAZOAMBATANA NA ISHARA, AJABU NA MIUJIZA

INAYOTOKANA NA MUNGU

Kwa kuangalia alama hizi tisa zifuatazo, na kuhakikisha kwamba ZOTE ZINAKUWEPO; ndipo tunapoweza kuzitambua ishara, ajabu na miujiza inayotokana na Mungu na kuifahamu na kukwepa miujiza ya Shetani na manabii wake:

(1) Mtu anayetumiwa kufanya ishara, ajabu au miujiza na Mungu, inabidi awe ameamini au kuokolewa; akikiri mwenyewe wokovu ulio katika Kristo Yesu na kuushuhudia.

MARKO 16:17; “Na ishara hizi zitafuatana na hao WAAMINIO …..”.

Mtu yeyote asiyeokolewa na kukiri wokovu na kuushuhudia, hawezi kufanya miujiza itokanayo na Mungu. Miujiza hiyo hutokana na Shetani.

(2) Huduma ya Uponyaji au Ishara yoyote inayotokana na Mungu lazima iambatane na Biblia au Neno la Mungu kwa kuwa Neno la Mungu ndiyo dawa ya Ugonjwa na tena ndilo linalofanya

miujiza. Huduma yoyote ya uponyaji wa miujiza isiyoambatana na Biblia au Neno la Mungu, inatokana na Shetani.

ZABURI 107:20: “HULITUMIA NENO LAKE, HUWAPONYA, huwatoa katika maangamizo yao.”

MITHALI 4:20-22: “Mwanangu, SIKILIZA MANENO YANGU; ….UZISIKIE KAULI ZANGU …..MAANA NI UHAI kwa wale wazipatao, na AFYA YA MWILI WAO WOTE.”

YOHANA 6:63: “…..MANENO HAYO NILIYOWAAMBIA niroho tena NI UZIMA.”

(3) Huduma yoyote ya Uponyaji wa Miujiza inayotokana na Mungu, LAZIMA iambatane na kuhubiri Injili na kufundisha Neno la Mungu, Angalia maandiko:

(a) HUDUMA YA YESU:

(i) Kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao na vipofu kupata kuona tena, KULIAMBATANA na kuwahubiri maskini habari njema [SOMA LUKA 4:18].

(ii) Yesu alipokuwa akifundisha Neno la Mungu ndipo uweza wa Bwana ulipokuwapo kuponya:

LUKA 4:17:



“Ikawa siku zile mojawapo ALIKUWA AKIFUNDISHA …. NA UWEZA WA BWANA ULIKUWAPO APATE KUPONYA.”

(4) YESU ALIPOWATUMA WANAFUNZI KUFANYA HUDUMA YA UPONYAJI

Wakati wote Yesu Kristo alipowatuma wanafunzi wake na kuwapa uwezo wa kuponya maradhi, au kuwaambia wapoze wagonjwa kwa miujiza; jambo hilo LILIAMBATANA na kutumwa kuhubiri au kuutangaza ufalme wa Mungu. Mambo haya mawili lazima yaende pamoja.

LUKA 9:1-2: “Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi. Akawatuma WAUTANGAZE UFALME WA MUNGU NA KUPOZAWAGONJWA.”

LUKA 10:1-2, 9: “Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine,sabini, akawatuma wawili wawili …. Akawaambia … WAPOZENI WAGONJWA waliomo, WAAMBIENI, UFALME WA MUNGU UMEKARIBIA.”

MATHAYO 10:7-8: “Na katika kuenenda kwenu, HUBIRINI,mkisema, Ufalme wa Mbinguni umekaribia. POZENI WAGONJWA, FUFUENI WAFU, TAKASENI WENYE UKOMA, TOENI PEPO; mmepata bure, toeni bure.”

Katika kujifunza juu ya Huduma ya Yesu ya miujiza na uponyaji, na ile ambayo aliwapa wanafunzi wake; umeona kwamba kuponya wagonjwa kwa miujiza na kufanya ishara na ajabu zinazotokana na Mungu, LAZIMA kuambatane na kuhubiri Injili, na kuwaambia watu watubu dhambi zao na kuokolewa maana ufalme wa Mungu umekaribia. Ukimwona mtu anasema ni mtumishi wa Mungu na kwamba eti amepewa karama na Mungu kuponya wagonjwa, halafu akawa nyumbani kwake tu au ofisini kwake na watu wanamwijia kuponywa bila kuelezwa habari za kutubu na kuokolewa, ufahamu huyo ni nabii wa uongo, na anatumia NGUVU YA UPOTEVU ya Shetani kufanya ishara za uongo. Uponyaji wa Miujiza wa Mungu hauwi kama hospitali ambapo watu wanaenda kupewa vidonge tu bila kuhubiriwa Injili. Miujiza lazima iambatane na kuhubiri Injili. Mtu ukimsikia anasema yeye amepewa karama na Mungu kuponya wagonjwa tu, lakini hakupewa karama ya kuhubiri; hivyo kuhubiri amewaachia wengine, ujue huyo ni nabii wa uongo. Yeyote aliyepewa kufanya miujiza na Mungu, pia huyohuyo atahubiri Injili. Yesu, Petro, Paulo, Filipo na yeyote katika Biblia walifanya miujiza PAMOJA NA kuhubiri Injili.

Uponyaji wowote, muujiza wowote, au ishara yoyote inayofanywa kutokana na Mungu LAZIMA IFANYWE KWA JINA LA YESU SOMA: LUKA 10:17; MATENDO 4:30; MARKO 16:17; MATENDO 3:6; MATENDO 4:10; MATENDO 3:13, 16; MATENDO 16:18. Jina la Yesu, ndilo linalomtia mtu dhaifu, nguvu. Imani katika Yesu ndiyo inayoleta uzima [MATENDO 3:16]. Ukimwona mtu anayejiita mtumishi wa Mungu na kwamba anaombea wagonjwa, lakini halitumii Jina la Yesu ila anamtaja “Mungu” tu; ujue mtu huyo ni nabii wa uongo. Hakuna muujiza wowote wa Mungu pasipo kulitaja jina la Yesu! “PEPO WANATUTII KWA JINA LAKO”, “KWA JINA LANGU WATATOA PEPO.” Siyo kwa jina la Mungu au kwa kumtaja Mungu ila kwa jina la Yesu. LAZIMA Yesu atajwe katika kuufanya muujiza unaotokana na Mungu.

(5) Mtu anayetumiwa kufanya miujiza, ishara au ajabu na Mungu, hukusanya pamoja na Yesu, na kutumia miujiza kuliongeza Kanisa la Mungu kwa wale waaminio au wanaookolewa. Lengo la Mungu kutoa uwezo wa kufanya miujiza kwa watumishi wake, ni kuwafanya wasioamini waweze kuamini kwa kuziona nguvu za Mungu. Huduma yoyote ya miujiza isiyokuwa na lengo la kuwaongeza walioamini kwa Bwana Yesu au katika Kanisa la Mungu siyo huduma ya Mungu.

MATENDO 5:12,14:

“Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu; ….walioamini wakazidi kwa Bwana, wengi, wanaume na wanawake”.

Miujiza hutumika kukusanya watu na kuwaleta katika Kanisa ambalo kiongozi wake ni Yesu[SOMA PIA LUKA 11:23; MATHAYO 23:37; ZABURI 50:5].

(6) Mtu anayetumiwa kufanya ishara na Mungu, inabidi awe na Kanisa ambako anaongozwa na kutoa ripoti ya huduma yake inavyokwenda; au ni lazima afanye huduma yake kwa kushirikiana na Makanisa ya Mungu [SOMA MATENDO 14:27; MATENDO 21:17-19].

Tukimwona mtu ambaye inasemekana anafanya miujiza na hashirikiani na makanisa ya Mungu katika huduma yake, au hana Kanisa lolote ambalo anaongozwa na kutoa ripoti ya huduma yake inavyokwenda; basi, ufahamu huyo anatumia “Nguvu ya Upotevu” ya Shetani na ni nabii wa uongo.

(7) Ishara, ajabu, au miujiza inayotokana na Mungu; hutusogeza katika kumjua, kumwabudu, kumtumikia Yesu Kristo na kushika maagizo yake pamoja na kweli yote ya Neno la Mungu. Tukiona huduma ya miujiza ambayo inaambatana na maagizo yaliyo kinyume na Neno la Mungu katika nyakati tulizo nazo, kwa mfano kutumia sanamu ya Bikira Maria au sanamu ya Yesu, kufukiza uvumba, kutumia Rozari, kuzuru makaburi, kutumia maji ya baraka, kuwaomba wafu watuombee n.k.; basi tufahamu kwamba huduma hiyo siyo ya Mungu bali ni ya nabii wa uongo. [SOMA KUMBUKUMBU 13:1-4].

(8) Mtu anayetumiwa na Mungu kufanya ishara, miujiza au uponyaji wowote; hatapokea fedha au zawadi yoyote KABLA ya ishara, muujiza au uponyaji huo au BAADA ya ishara hiyo au uponyaji huo. Sadaka yoyote itaelekezwa katika kazi ya Mungu iwe Kanisani au namna nyingine na siyo kumpa mtu huyo binafsi kama “asante” ya huduma. Uponyaji au Muujiza wa Mungu wakati wote ni BURE! [SOMA:2 WAFALME 5:14-16; DANIELI 5:16-17; 1 WAFALME 13:6-7; MATENDO 8:18-20; MATHAYO 10:8]

(9) Uponyaji wowote wa Muujiza, au ishara yoyote inayotokana na Mungu; itakuwa ni kwa utukufu wa Mungu, na muujiza huo utampa utukufu au heshima Mwana wa Mungu Yesu Kristo. Yesu Kristo ni LAZIMA atajwe na kupewa utukufu au heshima yote. Hatatajwa Mungu tu, ila lazima atajwe Yesu Kristo pia. Ikiwa mtu anatukuzwa au kupewa heshima kwa miujiza au ishara azifanyazo na kukubali utukufu huo kama Mganga bingwa, na akaendelea kuzifanya ishara hizo, basi ufahamu kwamba huyo ni nabii wa uongo anayetumia “nguvu ya upotevu.” Mungu KAMWE hampi utukufu wake mwanadamu.

YOHANA 11:4

“Naye Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ILI MWANA WA MUNGU ATUKUZWE KWA HUO”. [SOMA PIA ISAYA 42:8; ISAYA 48:11].

Barnaba na Paulo walipotumiwa na Mungu kufanya miujiza na watu wakawapa utukufu kana kwamba ni Miungu, MARA ILE ILE waliukataa utukufu wowote na wakamwinua Mungu aliye hai wakati huohuo. [SOMA MATENDO 14:8-18]. Wasingefanya hivyo, ingekuwa ni hatari kwao. Herode alipopokea utukufu kana kwamba ni Mungu, pale pale alipigwa na malaika wa Bwana kwa sababu hakumpa Mungu utukufu na akaliwa na chango na kutokwa na roho [SOMA MATENDO YA MITUME 12:21-23].



H U K U M U


Watu wafanyao ishara na ajabu za uongo za Shetani na kuwapoteza watu, wasipotubu, hukumu yao itakuwa pamoja na manabii wote wa uongo. Mahali pao ni katika ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti. KUMBUKUMBU 13:1-5. Watu wanaowaendea kutafuta ishara, miujiza au uponyaji na kuuamini uongo huo na kuwatetea kwamba ni watumishi wa Mungu kwa sababu walifanya muujiza fulani n.k.; wasipotubu, hao nao WATAHUKUMIWA na kutupwa katika ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti. [SOMA 2 WATHESALONIKE 2:9-12]. Inakupasa ujilinde, usiwe miongoni mwao.

U O N G O W A S H E T A N I

Shetani siyo Muumbaji. Kamwe hana uwezo wa kuumba! Kwa sababu hii, pamoja na nguvu yake ya upotevu, shetani hawezi kumpa mtu mtoto. Ampate wapi? Ilivyo ni kwamba, Shetani ni mjanja, anapowaona watu wakienda kutafuta watoto kwa manabii kama hawa wa uongo, huwasoma watu hao walivyo. Wengine huwa siyo kwamba wana tatizo lolote. Ujauzito unaweza ukawa umechelewa tu kutokana na sababu za kawaida tu na hofu ya watu hao ikawafanya waende kwa nabii huyo wa uongo. Shetani ndiye mleta hofu na tena huweza kumuunganisha mtu na nabii wake wa uongo. Anapompata mtu mmoja wa namna hii, na baadaye akapata ujauzito katika hali ambayo ingekuwa ni ya kawaida tu, huutumia “muujiza” huo wa uongo kuwapoteza maelfu ya watu. Ndiyo maana kwa manabii hawa wa uongo, utaona ni wachache sana wanaosemekana wameombewa na kupata mtoto. Wengi huenda hapo na kusikia hadithi ya mmoja au wawili kwa muda mrefu uliopita. Ukiwauliza wanasema “Nasikia yuko mmoja alipata mtoto, tena yeye alikuwa mwislamu.” Zote hizi ni kazi za uongo za Shetani ili kuwapoteza wengi. Walio wengi wanakwenda huko kwa miaka mingi wakisumbuka na kuteseka na kupata “mimba bandia”. Utamwona mtu tumbo lake kubwa lakini hajifungui. Akipimwa kliniki, haonekani mtoto. Wengine wamekuwa na mimba miaka karibu miwili na mtoto haonekani. Wengine wanasema ninasikia kitoto kinacheza kwa miaka! Yote haya ni mapepo. Baada ya mapepo haya kukemewa kwa Jina la Yesu, yanahama na mtu huyo kuwa huru. Inatupasa kumwamini Mungu aliye hai. Yeye aliyempa Zakaria na Elisabeti mtoto wa ajabu, Yohana Mbatizaji katika uzee wao; anaweza kumpa mtoto kila amwaminiye. Yeye aliyempa Ibrahimu na Sara mtoto wa ahadi Isaka na kumpa Hana mtoto wa ajabu Samweli aliyekuwa nabii mkubwa, ana uwezo wa kumpa mtoto yeyote aaminiye. Mwamini tu Yesu, utaona mambo ya ajabu!

TOFAUTI YA “Mungu” NA “mungu”

Neno “Mungu” na “mungu” katika kutamka, yanatamkwa vilevile. Ni katika maandishi tu; ndipo unapoweza kuyatofautisha kutokana na herufi kubwa “M” na herufi ndogo “m”. Ukiamua kuandika herufi zote za majina hayo kuwa kubwa, utaona majina hayo tena yanafanana! Hapa ndipo penye mtego mkubwa wa Shetani. Waganga wa Kienyeji na manabii hawa wa uongo, hutumia “mungu” yenye herufi ndogo “m” wanapokuwa wanamtaja “mungu” wao Shetani. Wao ni watumishi wa “mungu” na kamwe wao siyo Watumishi wa Mungu! Huyo “mungu” wao shetani naye anatoa karama za uponyaji za udanganyifu, anapompa nabii wake ruhusa ya kutumia pepo wa uaguzi [MATENDO 16:16] na pepo wake wa utambuzi

[1 SAMWELI 28:7] Siyo kusudi la somo letu leo kujifunza jinsi pepo wa uaguzi na pepo wa utambuzi wa shetani wanavyofanya kazi ya udanganyifu, hata hivyo jambo moja tu ni kwamba kuwaendea waganga hawa wanaotumia pepo hawa, ni kumwendea shetani yaani “mungu” wa dunia hii na kutafuta kifo [SOMA 1 NYAKATI 10:13-14].

Manabii hawa wa uongo wanaotumia nguvu ya upotevu, wanapoombea wagonjwa, humwita “mungu” wao shetani.

Angalia tofauti ya “mungu” ikimaanisha shetani na “Mungu” ikimaanisha Mungu aliye hai

[SOMA YONA 1:5-6; 2 WAKORINTHO 4:3-4].

Manabii hawa wa uongo, au waganga wa kienyeji, WANAJUA KABISA kwamba “mungu” wao ni shetani maana huwasiliana naye kama “BOSS” wao na kuwadanganya watu kuwa ni Mungu! Mara nyingi wanapoandika hupenda kutumia herufi kubwa “MUNGU” ili kuzidi kuwadanganya na kuwapoteza wengi wakidhani ni Mungu aliye hai kumbi ni “mungu”.

UFAHAMU ZAIDI KUHUSU MIUJIZA YA MUNGU

Nyakati hizi za mwisho, pamoja na kujifunza yote tuliyojifunza, bado tunahitaji kufahamu zaidi ya haya, kuhusu miujiza; ili tusipeperushwe na “elimu kwa uongo” ya Shetani kuhusu miujiza. Yafuatayo ni muhimu kuyafahamu kuhusu miujiza ya Mungu.

(1) MIUJIZA YA MUNGU HAIFANYIKI ILI KUMTHIBITISHA MTU KUWA NI

MTAKATIFU

Watu wengi waliookoka nyakati hizi, wamevamiwa na elimu potofu kudhani kwamba miujiza inathibitisha kwamba mtu yule aliyehudumu madhabahuni au mkutanoni au katika huduma ya aina yoyote ni mtakatifu sana. Kutokana na mawazo haya potofu utasikia kundi la watu lililoandaa mkutano likisema “Mungu ameonyesha kwamba hakuna tatizo katika namna yetu ya kuenenda katika wokovu. Umeona miujiza iliyofanyika? Ingekuwa tunayoyafanya siyo sawa mbele za Mungu, miujiza yote hii ingefanyika kwetu?” Utasikia wengine wakisema “Unaona! Ingekuwa Mchungaji huyu ana hatia mbele za Mungu, je miujiza ingefanyika namna hii katika huduma yake?” Watu wametumia uwepo wa miujiza kuhalalisha dhambi. Huku ni kukosa maarifa:

(a) MIUJIZA YA MUNGU HULITHIBITISHA NENO LA MUNGU

Ishara na miujiza hufanyika kulithibitisha NENO na siyo kumthibitisha Mchungaji au kulithibitisha kundi au kulithibitisha Kanisa kwamba linakwenda sawasawa na mapenzi ya Mungu.

MARKO 16:20:

“Wao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, NA KULITHIBITISHA LILE NENO KWA ISHARA zilizofuatana nalo.”

(b) MIUJIZA YA MUNGU HAIFANYIKI KUTOKANA NA UTAKATIFU AU NGUVU ZA MHUDUMU AU NGUVU ZA KUNDI LILILOANDAA MKUTANO

MATENDO 3:12:

“Hata Petro alipoyaona haya akawajibu wale watu, Enyi Waisraeli mbona mnastaajabu haya, au mbona mnatukazia macho sisi, kana kwamba tumemfanya huyu aende KWA NGUVU ZETU SISI, AU KWA UTAUWA (UTAKATIFU) WETU SISI?”

(c) MIUJIZA YA MUNGU HUFANYWA NA MUNGU KWA AJILI YA NAFSI YAKE MWENYEWE NA SIYO KUTOKANA NA NAFASI YA MTU YEYOTE

Mungu anapofanya miujiza, huifanya kwa ajili ya nafsi yake na kwa ajili ya kujitukuza yeye mwenyewe, na siyo kumtukuza Mchungaji aliyehudumu, au kulitukuza kundi au Kanisa lililoandaa mkutano.

ISAYA 48:11

“Kwa ajili ya nafsi yangu, kwa ajili ya nafsi yangu, nitatenda haya; je! litiwe unajisi jina langu? WALA SITAMPA MWINGINE UTUKUFU WANGU.”



(2) KUHANI AU MCHUNGAJI ANAYEHUDUMU MKUTANO, ANAWEZA AKAWA KATIKA DHAMBI, NA MIUJIZA BADO IKAWA INATENDEKA

Watu wengine wanafikiri kwamba Kuhani aliyetiwa mafuta, hawezi kufanya dhambi. Wanafikiri Askofu, Mchungaji, au Mwinjilisti maarufu hawezi kuwa katika dhambi na akawa ameanguka. Huku ni kukosa ufahamu. Makuhani waliotiwa mafuta wanaweza kukosa mno na kuwa katika machukizo kama ya mataifa wakimpa nafasi Ibilisi:

MAMBO YA WALAWI 4:3:

“Kama Kuhani aliyetiwa mafuta akifanya dhambi, hata analeta hatia juu ya watu……”.



2 MAMBO YA NYAKATI 36:14:

” Na zaidi ya hayo wakuu wote wa makuhani, na watu WAKAKOSA MNO sawasawa na machukizo yote ya mataifa; wakainajisi nyumba ya BWANA aliyoitakasa katika Yerusalemu.”



Ndiyo maana Biblia inatupa ushauri wa kufuata kuhusu viongozi wetu wa kiroho. Inatupasa kuiga imani yao BAADA ya KUUCHUNGUZA SANA MWISHO WA MWENENDO WAO na kuulinganisha na maandiko [SOMA WAEBRANIA 13:7]. Tukiona mwenendo wa Kiongozi fulani wa kiroho hata kama ni wa ngazi ya juu kiasi gani, hauendani na maandiko, kamwe tusiifuate imani yake na kuhalalisha dhambi anayoifanya.

Sasa basi, ukiyajua haya; bado kunakuwa na mtego mkubwa zaidi. Kuhani aliyetiwa mafuta, akiwa katika hali ya dhambi; anaweza kuhudumia mikutano na miujiza mikubwa ikatendeka. Katika miaka ya 1940, alikuwepo Mhubiri maarufu sana huko Marekani akijulikana kwa jina la A.A. ALLEN. Huduma ya mhubiri huyu iliambatana na miujiza mikubwa na ilivuta watu wengi sana. Jambo la kuhuzunisha ni kwamba alipokufa, madaktari walithibitisha kwamba alikufa kutokana na ulevi wa kiwango cha juu sana; baada ya kufanya uchunguzi wa damu yake na mengineyo katika kuipima maiti yake.

Mhubiri mmoja mwingine huko Nigeria, akiwa ametoka tu kuzini na mwanamke saa za mchana, aligongewa hodi na mgonjwa mmoja aliyetaka maombezi. Mhubiri huyu alikuwa na sifa kubwa ya miujiza mikubwa kutendeka katika huduma yake. Mgonjwa huyu akiwa katika hali ya kukaribia kufa alikuja pale akijua kwamba akiombewa anaweza kupona. Mhubiri yule alipomwona mgonjwa yule na kuiona hali yake, na kuwaza kwamba anataka yeye amwombee wakati ametoka kwenye uzinzi; alipiga magoti na kuanza kuomba kwa machozi kwamba Mungu amsamehe kwa upumbavu alioufanya. Lugha aliyokuwa akiitumia Mhubiri huyu kuomba msamaha kwa Mungu, ilikuwa ni lugha ambayo yule mgonjwa alikuwa haijui. Kutokana na sababu hii ya kutokuijua lugha, yule mgonjwa alidhani yule Mhubiri anamwombea awe mzima. Muda mfupi tu, yule mgonjwa akarukaruka na kusema “Bwana asifiwe nimepona.” Akaondoka kwa furaha sana akirudi nyumbani kwa shangwe baada ya kupokea muujiza huo mkubwa. Yule mhubiri akabaki amechanganyikiwa. Kwa maneno yake alipokuwa akizungumza na Mchungaji mmoja wa Kanisa moja kubwa huko Lagos anasema “Nimechanganyikiwa. Njia za Mungu ziko juu sana sizielewi. Mimi nilikuwa ninatubu dhambi ya uzinzi kwa machozi. Mgonjwa akafikiri ninamuombea. Kwa yeye kuamini hivyo akawa mzima mara moja. Sikuomba lolote juu yake. Nisingeweza kuomba lolote juu yake katika hali ya kuhukumiwa niliyokuwa nayo. Ninashangaa hii ni nini!”

Iko mifano mingi ya miujiza iliyotendeka katika huduma iliyo dhahiri katika dhambi. Mhubiri mmoja maarufu Marekani mwenye wake wawili lakini pamoja na hali hiyo, vilema wanatembea, vipofu wanaona na miujiza mikubwa inatendeka katika huduma yake. Nafasi haitoshi kueleza mifano mingi ya jinsi hii. Ukisoma Kitabu kinachoitwa “All things are possible” kilichoandikwa na J. Buckingham, utaona mifano tele! Sasa swali ni kwamba, kwa jinsi gani miujiza inaweza kufanyika katika hali hii ya dhambi? Yafuatayo ni majibu:-



(a) IMANI YA MTU BINAFSI ANAYELISIKIA NENO

Yesu Kristo mara nyingi aliwaambia watu “Imani yako imekuponya”

[ANGALIA MATHAYO 9:22; MARKO 10:52] Yesu pia aliwaambia wengine “Kadri ya Imani yenu mpate” na mara wakafumbuka macho yao [SOMA MATHAYO 9:29-30]. Unaweza kuona hapa kwamba imani ya mgonjwa mwenyewe inaweza ikamfungua mtu yule na muujiza ule usiwe na uhusiano wowote na Mhubiri. Biblia inasema pia kwamba Imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Kristo. [SOMA WARUMI 10:17]. Mgonjwa anapokuja mkutanoni akiwa hajui lolote kuhusu maisha ya mhubiri, na kusikia Neno la Kristo kwamba Yesu huponya hata leo kwa kuwa yeye habadiliki; mara hupata imani na imani hiyo kumfanya mara moja awe mzima pamoja na Mhubiri yule kuwa katika dhambi.



(b) NENO LA MUNGU KUTHIBITISHWA [MARKO 16:20]

Mahali popote ambapo watu wengi watakusanyika katika mkutano wa Neno la Mungu, lazima neno la Mungu lithibitishwe. Wahubiri wengi wameifahamu siri hii. Ukitaka kuona miujiza mikubwa, jambo la kufanya ni kukusanya maelfu au malaki ya watu kuhudhuria kwenye mkutano. Palipo maelfu ya watu, kuna mengi. Wengine wanaweza wakawa wametoka mbali sana huenda mamia ya maili kufuata mkutano, huku wakitaka kuona kama kweli Yesu Kristo yuko hai leo. Wengine wanaweza kuwa waislamu wakiwa wamekuja huku wakibishana na kusema kwamba “Watu hawa ni waongo, haiwezekani kabisa mtu akaponywa eti kwa kuomba kwa jina la Yesu tu. Huu ni ujanja wao ili kuwafanya watu wengi wawe Wakristo. Wanachukuana wao kwa wao na kushuhudia uongo. Ingekuwa ni kweli, basi kwa jina la Mtume Mohammed, tungeona miujiza mikubwa zaidi maana yeye ndiye nabii wa mwisho.”

Mahali pa namna hii, hata kama mhubiri anayehubiri ametoka katika uzinzi au kundi lililoandaa mkutano liko mbali na kweli, ili mradi tu Mhubiri ahubiri Injili ya wokovu na kumtaja Yesu anayeokoa na kuponya, basi miujiza mikubwa itatendeka bila kujali maisha ya mhubiri au hali ya kundi lililoandaa mkutano. Mungu hayuko tayari kuona malaki ya watu wakiondoka na kulitukana Neno kwamba siyo la kweli kwa sababu ya mhubiri mmoja tu madhabahuni au kundi la watu mia walioandaa mkutano. Ni lazima alithibitishe Neno lake kwamba ni kweli. Kwa kufanya hivyo, hamthibitishi mhubiri huyo au kundi hilo kama tulivyotangulia kuona.



(c) MUNGU ATAFANYA LOLOTE ILI KUZIOKOA ROHO ZINAZOANGAMIA



Biblia inasema roho zote za wanadamu ni mali ya Mungu [SOMA EZEKIELI 18:4] Roho moja ya mwanadamu, ni ya thamani mno mbele za Mungu. Ni zaidi sana roho za maelfu ya watu. Mungu hapendi hata MMOJA apotee bali wote wafikilie toba kwa jinsi roho za watu aliowaumba zilivyo za thamani kubwa. Ni kwa sababu hii ndiyo maana kuja kwa Yesu bado kunakawia [SOMA 2 PETRO 3:9] Kutokana na ishara ambazo wagonjwa hufanyiwa, watu wengi sana huamua kumfuata Yesu [SOMA YOHANA 6:2]. Kwa sababu hii, wanapokusanyika maelfu ya watu, Mungu anajua kwamba kutokana na ishara kadhaa kwa wagonjwa anaweza kuziokoa roho zake nyingi. Hataacha kazi yake muhimu ya kuziokoa roho zilizokusanyika kwa ajili ya upumbavu wa roho moja iliyo madhabahuni au roho chache zilizoandaa mkutano. Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa. Ataendelea kufanya ishara ili kuzivuta roho za watu na kuziokoa kutokana na huruma yake.



(d) MUNGU NI LAZIMA AJIPATIE UTUKUFU KATIKA UMATI WA WATU

Miujiza juu ya wagonjwa ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu [YOHANA 11:4] Mungu anapofanya miujiza, hujipatia utukufu kwa wanadamu kwa jinsi ambavyo kazi zake zinavyodhihirishwa waziwazi [YOHANA 9:3]. Watu wanapomtukuza Yesu kutokana na kazi zake, ndiyo mwanzo wa kuvutwa katika ufalme wa Mungu [SOMA LUKA 7:14-16]. Kwa ajili ya nafsi yake, Mungu atafanya ishara ili ajipatie utukufu na kujionyesha kwamba hakuna mwingine ila yeye. Hatakubali kulitia unajisi jina lake mbele ya maelfu ya watu kwa ajili ya mtu mmoja aliyesimama madhabahuni. [ISAYA 48:11].



KARAMA ZA MUNGU HAZINA MAJUTO [WARUMI 11:29]

Mungu anapompa karama fulani mtu yeyote kwa Roho Mtakatifu, hajuti wakati wowote na kuziondoa. Mhubiri fulani anaweza akawa alianza vizuri na mwisho wake ukawa mbaya. Kwa kuwa karama za Mungu hazina majuto, bado utaona katika huduma ya mtu miujiza pamoja na udhaifu alio nao.



MAMBO MATATU YA KUJIFUNZA KUTOKANA NA UFAHAMU HUU

JUU YA MIUJIZA YA MUNGU

(1) Ni kwa sababu hii Yesu alisema siku ya mwisho watakuwepo watu wengi watakaosema walitenda miujiza kwa jina lake na yeye atawaambia ” Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu” [SOMA MATHAYO 7:22-23]. Tumeona jinsi ambavyo mtu atendaye maovu anavyoweza kutenda miujiza kwa jina la Yesu. Kufanya miujiza siyo kibali cha kuingia mbinguni bali utakatifu pekee ndiyo tiketi ya kumuona Mungu [WAEBRANIA 12:14].

(2) Hata kama kwa Mhubiri fulani au katika mkutano fulani ulioandaliwa na kundi fulani au makanisa kadhaa kunatendeka miujiza mikubwa, KAMWE tusizithibitishe dhambi wanazozifanya kutokana na miujiza inayofanyika. Hatuwezi kusema kuoa wake wawili ni halali kutokana na Mhubiri huyu wa Marekani aliyeoa wake wawili na anatenda miujiza kwa jina la Yesu. Hatuwezi kusema Ubatizo wa maji tele siyo lazima kutokana na Mhubiri, kundi, au Kanisa linalopinga ubatizo wa Maji tele kuendelea kutenda miujiza. MIUJIZA SIYO KIPIMO. Neno la Mungu ndiyo kipimo Yuda alikuwa miongoni mwa wanafunzi ambao walitumwa na Yesu kuhubiri na pepo wakatoka katika huduma yake alipolitumia jina la Yesu. Hata hivyo, Yuda yuko Jehanum leo. Miujiza haikumfanya Yuda aingie mbinguni.

Kutokana na kukosa ufahamu huu, wengi wamepotoshwa na Shetani na kuwafuata wengi katika udhalimu wao wakipinga kweli ya Neno la Mungu. hawa wanaolipinga Neno la Mungu huku wakisema “Hata kwetu mbona miujiza inatendeka” na ukazithibitisha dhambi zao na kuzifanya, utaangamia kama Yuda pamoja nao msipotubu.

(3) Ikiwa katika huduma yako miujiza inafanyika lakini huendani sawa na Neno la Mungu, inakupasa kuliangalia Neno mara moja na kulifuata baada ya kutubu, au siyo utaangamia kama Yuda.



MIUJIZA KATIKA UTAKATIFU


Pamoja na miujiza kuweza kufanywa na watu waliookoka ambao wanatenda dhambi, hata hivyo; kiwango cha miujiza kinachofanyika mahali ulipo Utakatifu, kinakuwa cha juu mno. Pasipo Utakatifu haiwezekani kufanya miujiza mikubwa kuliko ile aliyoifanya Yesu [SOMA YOHANA 14:12]. Wakati wa Kanisa la Kwanza, miujiza ya ajabu ilifanyika kutokana na kanisa kwenda sawasawa na Neno la Mungu. Angalia mfano wa miujiza hiyo katika [MATENDO 5:15-16].



M A S W A L I

(1) Je Shetani anaweza kufanya miujiza? Kama jibu lako ni Ndiyo, toa maandiko ya kuthibitisha jibu hilo.

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

(2) Lengo la miujiza ya Shetani ni nini? Thibitisha jibu kwa andiko.

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————

(3) Taja kwa kifupi alama tisa zinazoambatana na miujiza ya Mungu.

(a)————————————————————————————————————-

(b)————————————————————————————————————-

(c)————————————————————————————————————-

(d)————————————————————————————————————-

(e)————————————————————————————————————-

(f)————————————————————————————————————–

(g)————————————————————————————————————-

(h)————————————————————————————————————-

(i)————————————————————————————————————–



(4) Je miujiza ya Mungu inafanyika ili kumthibitisha Mhubiri, Kundi lililoandaa mkutano au Kanisa? Kama jibu lako ni siyo, thibitisha jibu lako kwa maandiko.

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

(5) Je miujiza ya Mungu inafanywa kutokana na Utakatifu au nguvu za Mhubiri au kundi lililoandaa mkutano? Kama jibu lako ni siyo, Toa maandiko ya kulithibitisha jibu lako.

—————————————————————————————————————-

(6) Je Kuhani aliyetiwa mafuta anaweza akafanya dhambi? Tumia maandiko kujibu.

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

(7) Ni kwa sababu zipi tunaweza kuona miujiza mahali ambapo wahudumu wako dhambini? Taja sababu tano.

(a)————————————————————————————————————-

(b)————————————————————————————————————-

(c)————————————————————————————————————-

(d)————————————————————————————————————-

(e)————————————————————————————————————-

(8) Je kufanya miujiza ni kipimo cha kuingia mbinguni? Taja mtu aliyefanya miujiza na kwenda motoni.

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

<><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><

Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni? Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14). Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27). Kinyonge ni kipi? Ni yule anayetenda dhambi. Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge! Je, wewe ni mtakatifu? Jibu ni la! Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13; YOHANA 14:6). Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii? Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni; “Mungu Baba asante kwa ujumbe huu. Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi. Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha. Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo. Bwana Yesu niwezeshe. Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu. Amen”. Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni. Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu. MUNGU AKUBARIKI !!!

VITU VICHACHE VITAVYOKUONGEZEA THAMANI NA MAHUSIANO MAZURI NA WATU

$
0
0
Faraja Naftal Mndeme
Wiki iliyopita tulitazama namna unavyoweza kutumia mitandao ya kijamii ipate kukuongezea thamani, bila kukuathiri. Leo tutazame vitu vichache ambavyo vinaweza kukusaidia na kuongeza thamani  kuishi na kuwa na Mahusiano Mazuri na Watu Wengine.

1. Epuka kumkosoa/Kumuonya mtu katika ya Hadhara ya Watu pindi Anapokosea.

Muda mwingine tumependa kuonekana kwamba tuwajuvi wa vitu vingi kuliko wengine hii inapelekea watu wengi kuwa na migongano isiyokuwa na ulazima kwenye maisha ya kila siku.Ni muhimu unapomuona mwenzako/ndugu/jamaa amekosea tafuta muda muafaka kaa naye pembene mwelekeze na mshauri juu ya lile alilolkosoa.Epuka kutumia sehemu za kijamii kama sehemu ya kujionyesha ya kwamba wewe ni bora kuliko wengine hii itakusaidia kujenga uhusiano mzuri na wengine.Muda mwingine mtu anaweza kukufanyia kosa ambalo halivumiliki lakini hakikisha unadhibiti mihemko yako ambayo inaweza kukuletea madhara siku za usoni kwenye mahusiano yako na na wengine.Jitahidi kuvumilia na kutafuta faragha ili muongee na kuyamaliza ili kuweza kuboresha uhusiano wenu.

2. Epuka kulazimisha mawazo au ushauri wako kuwa lazima ufanyiwe kazi.Mara nyingi tumekuwa na mtazamo kwamba kile unachofikiria wewe ni bora zaidi ya wengine na imewapasa wengine kufwata kile unachofikiri wewe ni sahihi lakini kiukweli hakikisha ushauri na mtazamo na mawazo yako kwenye juu ya jambo Fulani iwe ni maoni tu na sio lazima wafanye vile unavyotaka wewe kwenye jambo lolote.Unapotoa ushauri/Mtazamo wako mwache mwingine atumie muda wake kufikiri na kuchuja juu ya swala husika ndipo atoke na maamuzi yake binafsi yasiokuwa na shuruti pia mawazo yako yasipofanyiwa kazi ni sawa maana kila mtu anakitu anachofikiri kwake ni sahihi na kitamsaidia.

3. Ongea na zungumza tumaini kwenye maisha ya watu wengine.Hakikisha hatumii muda mwingi kuzungumza mambo ambayo ni hasi kwenye maisha yaw engine juu ya yale wanayopitia au kukumbana nayo,jenga tabia ya kuwa mjenzi badala ya mbomoaji wa maisha ya wengine.Maneno na mazungumzo yetu ya kila siku kwenye maisha ya wengine husaidia kujenga uhusuano mzuri wenye kudumu na furaha na usiokuwa na maswali ya hapa na pale kwenye maisha yetu ya kila siku na watu wengine.Ongea tumaini na Baraka,ongea upendo na furaha kwenye maisha yaw engine kuwa mjenzi bora wa jamii yetu ya kila siku.Tumia kinywa chako na maneno yako kuweka tumaini la kudumu lisilo tetereka kwenye maisha yaw engine.

4. Shiriki kwenye Shughuli mbali mbali za Kijamii.Hakikisha pamoja na mambo mengi uliokuwa nayo kwenye maisha ya kila siku lakini tenga muda kidogo kwa ajili ya kushiriki kwenye shughuli mbali mbali za watu wengine ikiwemo misiba,harusi na harambee mbali mbali n.k.Hakikisha jamii inakuwa sehemu ya maisha yako na namna hii itakusaidia hata siku ukiwa na uhitaji watu watashiriki vya kwako.Epuka kujifungia nyumba kwa kigezo kwamba hauna fedha/muda wala kitu chochote kushiriki kwenye maisha ya wengine. Maisha yetu yamejengwa kwenye maswala mazima ya utegemezi,hakuna mtu aliyekamilika katika kila jambo ,kila mmoja ana muhitaji mwingine kwa namna moja au nyingine pia.
5. Wapongeze wengine wanapofanya vizuri zaidi yako.Mara nyingi tumekuwa na tabia ya kupenda kuangalia madhaifu ya watu wengine bila kuangalia mafanikio walio nayo kwenye maisha katika Nyanja mbali mbali.Unapomuona mtu mwingine amefanikiwa kufanya vyema kwenye jambo Fulani mpongeze pila kinyongo wala kusitasita maana hata siku nyingine wewe utafanikiwa kufanikiwa jambo Fulani ndipo nao watakapofanikiwa kuona mchango wako.Epuka kuwa na tabia ya kukosoa kosoa kila jambo unaloliona,pale panapostahiki pongeza fanya pila kinyongo lakini pia pale panapohitajika maonyo tumia busara na utaratibu ufaao kufanya vivyo.

God Bless Y’All
Kwa sasa mwandishi anapatikana kupitia namba 0719742559, hadi pale namba ya awali ya airtel itakapokaa sawa kwa ajili ya kufanya kazi upya.

MWALIMU MWAKASEGE ANAWAPIGA MSASA WACHUNGAJI WA MORAVIAN NCHINI

$
0
0
Mwalimu Christopher Mwakasege katikati akiwa amekaa na maaskofu wa Moravian.
Baada ya mgogoro wa muda mrefu ndani ya kanisa la Moravian nchini (KMT) wachungaji wa kanisa hilo nchini wapo mkoani Dodoma kwa semina ya kuwekana sawa katika huduma ikifundishwa na mwalimu Christopher Mwakasege ambaye amealikwa kama mfundishaji katika semina hiyo.

Semina hiyo ambayo imeanza siku ya leo licha ya kuhudhuriwa na maaskofu na wachungaji wa kanisa hilo nchini pia mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi alikuwepo katika ufunguzi wa semina hiyo asubuhi ya leo kwakupata nafasi ya kuzungumza machache na kuwakaribisha viongozi wa kanisa hilo mkoani humo. Ni takribani miaka mitatu sasa tangu mgogoro ufukute ndani ya kanisa hilo huku siku za karibuni ikishuhudiwa baadhi ya wachungaji wakivuliwa madaraka ya kuongoza sharika zao kutokana na mgogoro huo.

Mwaka 1997 ulitokea mgogoro mkubwa ndani ya kanisa hilo pale watu wa kutoka Kyela waliponyimwa haki ya kuwa na jimbo lao huku pia ikidaiwa kitendo cha mchungaji kutotambua cheti cha safari cha mmoja wa waumini wa kanisa hilo kutoka Kyela katika ibada ya jumapili iliyofanyika usharika wa Mabibo jijini Dar es salaam ndipo mgawanyo ulipotokea na kuzaa kanisa jipya la Kiinjili la Moravian Tanzania ambalo kwasasa linazidi kupanua wigo wake katika jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake kadhalika na mikoani. Endapo mgogoro huu uliopo usipoisha kwa amani kuna uwezekano kanisa la tatu la Moravian huenda likaanzishwa nchini. Mungu aingilie kati AMEN

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt Rehema Nchimbi akitoa neno la ukaribisho.
Askofu Nicodem akizungumza mara baada ya salamu za ufunguzi kutoka kwa mkuu wa mkoa
Katibu mkuu wa kanisa la Moravian akizungumza jambo.
Mwalimu Christopher Mwakasege akipiga gombo kwa wachungaji.


Maaskofu na wachungaji wakiwa katika semina hiyo.


Hii ndio hali katika semina hiyo ©Mapasa Ipyana


KWA TAARIFA YAKO: KWAYA MAARUFU DUNIANI KUTOKA AFRIKA INAVYOGUSA WENGI

$
0
0
Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka maoni yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu.
Sehemu ya waimbaji wa Soweto Gospel Choir kwenye huduma. ©fb/Soweto Gospel Choir
Iwapo utazungumzia kwaya za nchini Afrika Kusini, basi Soweto Gospel Choir ni kati ya hizo chache ambazo unaweza kuwa umezitaja. Kwaya hii yenye miaka 11 tangu kuanzishwa kwake mnamo Novemba 2012. Kwaya hiyo ambayo imejizolea umaarufu duniani kote ikipata mialiko ya kumtumikia Mungu, yaweza ukawa hujui - KWA TAARIFA YAKO inaundwa na wambaji wenye uwezo kutoka makanisa mbalimbali nchini humo.

Soweto Gospel Choir, ama SGC kwa ufupi kama ambavyo wanafahamika, si kwamba tu wanafahamika duniani kote kutokana na uimbaj wao stadi, KWA TAARIFA YAKO wameshajikusanyia tuzo zaidi ya kumi, ikiwemo tuzo inayoheshimika zaidi duniani ya Grammy, mara nne, ikiwemo kupendekezwa kwenye tuzo ya Oscar.

Ubora wa uimbaji wa kwaya hiyo pamoja na kuimba nyimbo za kijamii, umeifikisha mbali kwaya hii, ikiwemo kuimba sanjari na mwanamama Celine Dion, na pia John Legend, huku kwa upande wa injili wakiimba pamoja na Kirk Franklin na hata kwenye mialiko ya viongozi kama Bill Clinton, ukiachilia mbali kwa mlezi wao, Askofu Mkuu Desmond Tutu.
Mandela akiwa na baadhi ya wanakikundi enzi za uhai wake. ©SGC
Nyimbo zao zimeenda mbali zaidi kwani pamoja na kushiriki kwenye nyimbo za kijamii, KWA TAARIFA YAKO Soweto Gospel Choir wanaweza pia kusikika kwenye filamu za kimataifa na hata michezo ya 'computer', (computer games). Filam mojawapo ambayo wameshiriki kurekodi wimbo ninafahamika kama Wall-E unaofahamika kama Down to Earth - ambao ulishinda tuzo, huku kwa watumiaji wa michezo ya computer, Civilization IV ndio ukiwa mchezo ambao KWA TAARIFA YAKO wimbo wa Kiswahili, Baba Yetu umeimbwa.


Kwaya hii si tu kwamba inaimba vema na kugusa wadau wa muziki duniani kote, ila pia wanafahamika kwa kudumisha utamaduni, kwani mavazi yao tu huonyesha kwamba ni wazalendo wanaojivunia Uafrika wao, huku pia wakiimba nyimbo kwa lugha yao pamoja na Kiswahili, na KWA TAARIFA YAKO, wimbo mmojawapo maarufu waliouimba kwa upya ni wa Malaika.

Kama vile haitoshi kumtumikia Mungu na kuigusa jamii kwa njia ya uimbaji, KWA TAARIFA YAKO kwaya hii imeanzisha mfuko kwa ajili ya kuhudumia jamii za walioathirika na ugonjwa wa UKIMWI, huku wakitazamia zaidi wale wenye nia ya kusaidia jamii hizo lakini pasi kuwa na kitu mkononi.

Baadhi ya wanakwaya kwenye huduma. ©SGC
Kwa kumalizia, albamu ya kwanza ya kwaya hii ilirekodiwa ikiwa ni mwezi mmoja tu tokea kuanzishwa kwake Novemba, na si tu kwamba ilifanya vema kwenye maeneo mbalimbali, bali pia ilipelekea kutunikiwa tuzo za kimataifa nchini Marekani.

Hiyo ndiyo KWA TAARIFA YAKO, vinginevyo tukutane wiki ijayo.

UJUMBE WA LEO NI KWA WAAJIRIWA TU

$
0
0


“Ukitumika Kwa Uaminifu Kwenye Ndoto ya Mwenzako, Mungu Atakuinua Na Kukupa Neema Uwe Mtu Mkuu”

Yusufu alitafsiri ndoto ya Farao lakini pia aliwekwa kutumikia ndoto ya Farao kwa miaka 14 [Miaka Saba ya Shibe Na Miaka 7 ya Njaa] Lakini alipomaliza kutumikia miaka 14 ndoto ya mtu mwingine kwa uaminifu, Mungu alimheshimisha na kumfanya mkuu hadi wakati anaingia kaburini.

Waajiriwa Wengi wanafanyia kazi “MISHAHARA TU” na haawako tayari “KUTUMIKIA NDOTO YA MWAJIRI” Na Kwakuwa wanakosa uaminifu kwenye ndoto ya mtu mwingine; MUNGU ANAWANYIMA UWEZO WA KUTUMIKIA NDOTO ZAO BINAFSI, HIVYO WANAFUKUZWA AU KUSTAAFU WAKIWA HAWANA MWELEKEO WA MAISHA NA WANAISHIA KUWA NA MAISHA MABAYA SANA NA MWISHO WA TAABU!
Mwajiriwa, “USIUTUMIKIE MSHAHARA WA MWAJIRI BALI KUSUDI LA MUNGU KWENYE OFISI ALIKOKUWEKA KWA MUDA HUO UTAKAOKUWEPO”

KAMA NINGEAMBIWA NIKUAMBIE NENO MOJA LEO:

Ningekuambia hili: "Uko duniani kwa Neno maalum la Mungu lisiloweza kugeuzwa au kuzuiwa, mbegu isiyoharibika, lenye kutimiza kila kusudi lililotumwa, Hivyo maisha yako yako salama na hakika utafanikiwa na kustawi endapo utapuuza hali na changamoto unazopitia leo/sasa na kuweka jicho lako kwa YESU mwenye kuanzisha na kuitimiza kazi njema ndani yako"
Maandiko ya kutafakari:
1Petro 1:23, Filipi 1:6, Isaya 55:10
Mwl D.C.K
www.yesunibwana.org

WAPIGIE KURA ROSE MUHANDO, CHRISTINA SHUSHO NA GAZUKO TUZO ZA AFRIKA

$
0
0

Waimbaji watatu wa muziki wa injili nchini Rose Muhando, Christina Shusho pamoja na mwimbaji wa muziki wa kufokafoka ama rap za injili Gazuko Junior wanapigiwa kura kwasasa pamoja na waimbaji wengine wa bara la Afrika ili kumpata mmoja wao atakayeshinda tuzo za Africa gospel music awards 2014 katika vipengele tofauti, tuzo zinazotarajiwa kutolewa mapema wiki ijayo jijini London nchini Uingereza.

Rose Muhando anawania tuzo ya mwimbaji wa kike wa mwaka Female artiste of the year ikiwa ni mara yake ya kwanza kuwemo katika tuzo hizo. Yeye anawania tuzo na waimbaji wengine maarufu Afrika akiwemo Ntokozo Mbambo, Vicky Vilakazi, Diana Hamilton, Winnie Mashaba, Gloria Muliro pamoja na Sarah K wote wa Kenya pamoja na waimbaji wengine ikiwa jumla ya waimbaji 15. Kikubwa ni kumpigia kura ROSE MUHANDO katika kipengele hiki.

Kwa upande wa Christina Shusho ambaye alichukua tuzo ya mwimbaji bora wa mwaka 2013 kwa Afrika Mashariki ameingia katika vipengele viwili mwaka huu. Kipengele cha kwanza kikiwa ni mwimbaji bora wa mwaka kwa Afrika mashariki Artiste of the year East Africa, mwaka huu akipambana na waimbaji kama Eunice Njeri, Sarah K, Gloria Muliro, Solomon Mukubwa ambaye katika tuzo hizo ametambulishwa kama Mtanzania, waimbaji wengine wa Kenya, Uganda pamoja na Ethiopia ikiwa jumla ya waimbaji 12. Kikubwa unapopiga kura tafuta jina la CHRISTINA SHUSHO na umpigie kura yako.

Aidha tuzo ya pili anayowania mwanamama Christina Shusho ni tuzo ya video bora ya mwaka Video of the year kupitia wimbo wake wa 'Nataka Nimjue' tuzo ambayo anawania na wanamuziki wengine kama Tehila Crew la Nigeria ambao pia mwaka jana waliondoka na tuzo, Daddy Owen wa Kenya, Sammie Okposo wa Nigeria na waimbaji wengine wanaofanya jumla ya waimbaji 15 wanaowania tuzo hizo. Kikubwa sie ni CHRISTINA SHUSHO wa kumpigia kura ingawa katika kipengele hiki kutakuwa na ushindani mkubwa hasa ikizingatiwa kwamba Afrika magharibi wanawapigia kura za kutosha waimbaji wao hata sisi tukijituma tunaweza.

Kwa mara ya kwanza katika historia mwanakaka Gazuko Junior kupitia uimbaji wake wa kufokafoka Afro Rap Artiste of the Year na waimbaji kutoka Uholanzi, Uingereza, Nigeria, Ghana, Malawi, Kenya, Botswana pamoja na Zambia. Kikubwa ni kumpigia kura GAZUKO JUNIOR ili tuzo ije Tanzania.
ama rap anawania tuzo ya mwimbaji bora wa rap wa mwaka

Ili kupiga kura BONYEZA HAPA

KUMBUKA ZIMEBAKI SIKU 3 TU KABLA ZOEZI LA UPIGAJI KURA KUFUNGWA. UNARUHUSIWA KUPIGA MARA NYINGI UWEZAVYO.

CHAGUO LA GK: UKO JUU YA KWAKE JOHN LISU

$
0
0

Chaguo la GK kwa wiki hii ni kutoka kwa nguli wa nyimbo za kuabudu nchini, si mwingine bali ni John Lisu. Uko Juu ni wimbo ambao kwa hakika unamrudishia sifa na utukufu BWANA wetu Yesu Kritso, na hapa tunakuchagulia kama ambavyo aliuimba kwenye nyumba ya ufufuo ya uzima, kwa Askofu Gwajima - ambapo hadi kwa mpangilio wa vyombo na sauti, John Lisu alitunukiwa gari na kanisa hilo.


Ambatana na John katika kumtukuza Mungu Jumapili hii, ukimkubusha mambo aliyokutendea na kumshukuru kwayo. Jumapili njema

USIKUBALI KUFA KIMYA KIMYA,PAZA SAUTI YAKO KWA BWANA,UOKOLEWE.

$
0
0
Mtumishi Gasper Madumla.
" Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji.
Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu.
Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe.
Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?" Mathayo 14:28-31

Bwana Yesu asifiwe...
Nakusalimu mpendwa katika Kristo Yesu,na karibu katika fundisho hili zuri usomalo mahali hapa ambapo pamefanyika baraka kwa watu wengi,watu walio ndani ya Tanzania hata wale walio nje ya nchi ya Tanzania maana kupitia mahali hapa nimepata simu za watu wengi,na wengine wameokoka kwa kufuatilia mafundisho haya nikupayo,nami najua ya kwamba siku ya leo ni siku yako ya kumgeukia Mungu kwa moyo mmoja,kwa kuziacha dhambi zako,kisha Bwana awe mwokozi wa maisha yako,ukaokoke.

Katika maandiko hayo hapo juu tuliyoyasoma,tunaona kwanza
Ingawa Petro aliona shaka hata kuzama ,lakini alikuwa na kiwango kikubwa cha imani kwa sababu aliweza kupiga hatua kadhaa kwenye maji. Biblia haikutuambia ni hatua ngapi ambazo Petro alizopiga juu ya maji. Zipo baadhi ya hatua alizozipiga juu ya maji ndipo baadae alipoona shaka akaanza kuzama. Hivyo Petro alikuwa na imani kubwa sana ingawa aliona shaka.

Kutembea juu ya maji si mchezo!
Ukitaka kuamini kwamba kutembea juu ya maji ni kiwango kikubwa cha imani,basi nenda kajaribu wewe.
Ngoja nikupe zoezi la kufanya siku ya leo,ili kuhakikisha hiki ninachokuambia kwamba kutembea juu ya maji ni kiwango kikubwa.

Zoezi lenyewe ndio hili:

MAHITAJI YA ZOEZI.
01. Mtumbwi.
02.Bahari

Hakikisha unakuwa ndani ya mtumbwi na pia uhakikishe huo mtumbwi upo baharini,mfano bahari ya hindi hivi. Alafu kwa kiwango chako cha imani utoke katika mtumbwi na ujitupe baharini uanze kutembea juu ya maji ya bahari. Ukishajitupa juu ya maji kwa lengo la kutembea,hapo ndipo utajipima imani yako,kwamba utatembea juu ya maji au la!

Bwana Yesu asifiwe...

Biblia inasema Petro alipoanza kuzama alipaza sauti yake,akapiga yowe, akisema, " Bwana, niokoe. " ndiposa Bwana Yesu akamuokoa,ndio maana neno la Mungu kupitia kitabu cha Warumi linasema;

" kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. " Warumi 10:13.

Bwana Yesu pia alikuwa akimfundisha Petro pamoja nasi neno lilo hilo,kwamba yatupasa kuliitia jina la Bwana ili tuokolewe. Tazama kwa habari ya Petro,Bwana Yesu si kana kwamba alikuwa hamuoni Petro akizama,bali Bwana alimuhitaji Petro ampazie sauti ili amuokoe,maana yake kama uombi basi hakuna msaada.

Katika mazingira hayo,Patro aliokoka baada ya kuliitia jina la Bwana, " Bwana uniokoe " laiti kama asingeliitia jina la Bwana,angelikufa kimya kimya lakini Petro hakukubali afe kimya kimya. Uzima wa Petro ulikuwa ni kuliitia jina la Bwana.

Alikadhalika uzima wako leo ni kuliitia jina la Bwana. Nje ya macho ya Bwana hakuna kitakachofanyika kikafanikiwa.
Hivi,..
Ngoja nikuulize swali;
Tuwe wawazi kabisa siku ya leo,yaani tusifichane.
Unafikiri;
Petro asingelipaza sauti yake,je angepona na yale maji?

Kama jibu ni hapana asingepona,basi ndivyo hali ilivyo katika maisha yetu. Kama hatutapaza sauti kwa Bwana basi ni dhahili tutakufa kimya kimya huku tukiwa tunazama.

Leo hii,Petro anatufundisha fundisho kubwa sana mahali hapa kwamba;
Pasipo kuliitia jina la Bwana,twataka kufa kimya kimya. Mtunga Zaburi naye hutuambia hivi;

"Katika shida yangu nalimwita Bwana; Bwana akanijibu akaniweka panapo nafasi. " Zaburi 118:15

Yawezekana ipo shida kwako,
Yawezakana unaangamia kwa mateso ya magonjwa,
Yawezekana unazama katika dimbwi la shida kimya kimya.
Yawezekana unazama taratibu taratibu katika dimbwi la dhambi,
LAKINI LEO USIKUBALI UFE KIMYA KIMYA,LIITIE JINA LA BWANA,UOKOKE.

Sasa unisikilize sana;
Petro hakuweza kujiokoa yeye mwenyewe katika yale maji hata kama angefanyaje! Ilimbidi Bwana Yesu amuokoe.
Nami ninakuambia kwamba:
Hakuna mtu awezae kujisaidia mwenyewe pasipo kusaidiwa. Narudia tena;

•Hakuna awezae kujisaidia pasipo kusaidiwa.

• Hata kama U mjanja kiasi gani,Lakini bado unamuhitaji Bwana Yesu akuokoe.

Sasa;
Watu wengi hujidanganya kwa msemo huu; " jisadie ili Mungu akusaidie " msemo huu ni msemo wa kuzuka,usio na mantiki ya kimaandiko mahali popote pale . Mungu yupo wa kutusaidia,sisi wenyewe hatuna uwezo wa kujisaidia. Tunapokuwa na shida kimbilio letu ni Bwana.

Haleluya...

Watu wengi leo wamekubali kufa kimya kimya kwa magonjwa yao. Wakidhani kuwa Mungu anawaona hivyo magonjwa na mabalaa yataondolewa pasipo kupaza sauti kwa Bwana. Mimi nakutangazia kuwa ukinyamaza kimya pasipo kumpazia sauti Bwana;utakufa huku unajion mwenyewe. Sasa umefika wakati wa kupaza sauti kwake yeye Bwana illi atuokoe.

Bwana Yesu asifiwe...

Lakini pia kupitia maandiko hayo ( Mathayo 14:28-31) tunajifunza kwamba;

• Tunapomfuata Bwana Yesu hatutakiwi kuona shaka mioyoni mwetu,tukiona shaka kamwe hatuwezi kufikia lengo.
Tena ikiwa unamfuata Bwana Yesu huku una shaka moyoni mwako,basi ni afadhali sana usimame kwanza,kisha ukishaondoa shaka ndiposa umfuate.

Siku ya leo,kataa kufa kimya kimya shout to the Lord,omba msaada wa Bwana. Misingi ya dini yako isikufanye ufe kimya kimya,wala dhehebu lako lisikufanye ufe kimya kimya.
Wala hata wazazi wako wasikufanye ufe kimya kimya. Ikiwa umenielewa basi unipigie simu yangu hapo chini tuombe kwa pamoja katika tatizo au shida unayoipitia wewe au hata wazazi wako,au ndugu zako.
Piga;
0655-111149.

UBARIKIWE.

HOJA: UKIHESHIMIWA, HESHIMIKA (3)

$
0
0
Juma lililopita tuliangalia sehemu muhimu ya sababu kubwa ya kibibilia ambayo husababisha wengi wanaofanikiwa na kuheshimiwa hupoteza heshima zao katika jamii: Endelea na sehemu hii ya mwisho.

Kutokujiheshimu huzaa kutokuheshimika
Kutokujiheshimu ni kupunguza au kuacha kabisa kufanya mambo yale yaliyokufanya uheshimike.
Askofu Sylvester Gamanywa.
Kufanya mambo kinyume na matarajio ya wale waliokuwa wanakuheshimu. 
Mara nyingi watu wakutanapo kwa mara ya kwanza, kwa kuwa hawafahamiani kabisa, kila mmoja hujaribu kujiheshimu kwa muda, na kweli kwa muda huo huheshimika mbele ya wasiomjua. 
Lakini kwa kadiri wahusika wanapokaa pamoja kwa mudaa mrefu zaidi, kila mmoja huanza kujivua “heshima bandia” aliyokuwa amejivika kwa muda na kuonesha baadhi ya tabia zake. 
Hali hii hutokea katika mijumuiko mbali mbali inayokutanisha watu wageni kwa ajili ya matukio au shughuli za kijumuiya. Maeneo kama mashuleni, kambini, makazini, makazi mapya na katika majengo ya mikutano na ibada na kadhalika.
Kuanzia hapo viwango vya heshima ambavyo muhusika alikuwa amejipatia mioyoni mwa wasiomjua, tayari huanza kupoteza mvuto, tena huendelea kufifia zaidi kwa kadri muhusika anavyozidi kuonesha madhaifu yake ya kitabia.
Iko mifano mingi katika jamii ya baadhi ya watu walioupata umaarufu wa kuheshimiwa, na baada ya wahusika kuanza au kuweka hadharani vitendo visivyokubaliana na heshima stahiki, ghafla wamepoteza heshima zao!
Viashiria vya kupoteza heshima
Hivi mtu atajuaye kwamba amepoteza heshima mbele ya waliokuwa wakimheshimu? Kitu
cha kwanza ni kupoteza sifa zile alizokuwa akizipata muhusika. Kama alikuwa anapongezwa kwa mambo yale ambao yamepatia heshima, sasa anaanza kupata lawama badala ya pongezi. 
Kama alikuwa ana wafuasi wengi wanaomsikiliza, mara anapoteza wafuasi kwa sababu kile walichokuwa wanakifuata hakipo tena, au kimechuja kwa sababu watu wamepoteza imani naye. 
Kama muhusika alikuwa akitoa huduma bora kwa watu wengi ambao walikuwa wanapenda huduma zake; baada ya muhusika kuchakachua viwango vya ubora wa huduma zake, hupoteza wateja wake kwa kuwa huduma hizo hazikubaliki wal kuaminika kama hapo awali.
Naomba nitoe angalizo hapa mapema. Si kila mwenye wafuasi wengi, au wateja wengi anafuatwa kwa kuwa anafanya mambo ya heshima. Ziko huduma zisizo na heshima, na hivyo hata wafuasi au wateja nao pia; hata kama ni wengi sana huenda ama hawajali mambo ya heshima ya mtu au wenyewe binafsi pia hawana heshima. 
Kwa hiyo “wingi” wa wafuasi au wateja sio kigezo pekee cha kuthibitisha heshima ya mtu. Heshima ya mtu hutambulika kwa tabia na mwenendo wa aina ya huduma anazozitoa sambamba na aina ya wafuasi au wateja wake. 
Madhara ya kupoteza heshima
1.Kuvunja imani za wengine
Kama tulivyokwisha kudokeza huko nyuma ni kwamba, mtu maarufu anaposhindwa kutunza heshima yake, sio kwamba anaacha kuheshimika kama hapo awali; bali hii huleta madhara mengine kwa wale waliokuwa wakimheshimu. Madhara yenyewe ni wafuasi au wateja kupoteza imani na mtu mwenyewe. 
Kupoteza imani na mtu hakuishii kumpuuza muhusika peke yake, bali waathirika hupoteza imani na wengine wenye kutoa huduma zinazofanana na yule aliyechakachua maadili ya huduma husika. Wengi hujenga mtazamo hasi dhidi ya wengine ambao hata kama wao bado wanajiheshimu; nao pia huanza kushukiwa vibaya kwamba huenda hata wao wanafanana na huyo; kwa tafsiri ya mithali isemayo kwamba “Samaki mmoja akioza, wote wameoza”!
Kimsingi, kipengele hiki ndicho kinachobeba uzito wa makala na mada hii. Nasema hivi kwa sababu nimeshuhudia na wengine ni mashahidi katika hili. Hivi sasa sio siri kwamba huduma nyingi za kikanisa ziko kwenye mazingira tata na hatarishi. 
Kashfa nyingi zinazowaandama wale wanaoitwa “watumishi wa Mungu” au “wakuu wa dini” au “viongozi wa taasisi binafsi za kiroho” zimechafua imani za wafuasi wengi kiasi kwamba “imani za wengi zimeathirika”! Watu wengi sio kwamba waanazidi kupoteza imani na watumishi wa huduma za kikanisa, bali wanapoteza imani na Mungu huyo anayehubiriwa na hao “watumishi bandia”!
2.Kufilisika
Madhara mengine yatokanayo na kupoteza heshima, ni pamoja na muhusika kuishiwa na kufikia ukomo wa ubora wa huduma alizokuwa anazitoa hapo awali. Kinachosalia ni “bora huduma” badala ya “huduma bora”! Kukoma kwa ubora wa huduma pia husababisha kukoma kwa mapato yaliyokuwa yakiambata na huduma bora. Hii ndio maana ya kufilisika. 
Madhara ya kufilisika ni pamoja na kushindwa kumudu gharama za uendeshaji huduma pamoja na matumizi binafsi nayo kuathirika. Katika mazingira ya jinsi hii, muhusika hulazimika ama kuuza vitu vya thamani ili kulipa bili na madeni huzidi huongezeka. 
3.Maradhi
Kupoteza heshima sio kitu kidogo na rahisi. Japokuwa hapo mwanzo muhusika anaweza kujifanya hajali sana na kujitetea kwa maneno mengi; lakini kwa ndani ya nafsi tayari anayo maumivu makali ambayo hatimaye humletea maradhi yatokanayo na maumivu ya hisia hasi. Maradhi hayo ni pamoja na “msongo wa mawazo” (Stress) au “mfadhaiko wa mawazo” (Depression)! 
Magonjwa kama shinikizo la damu, kisukari, hata saratani ni baadhi ya chanzo kikuu ni mfadhaiko na msongo wa mawazo ambapo muhusika katika kujituliza hujikuta akila na kunywa vyakula ambavyo huathiri afya yake pasipo yeye kujua.
4.Kufupisha maisha
Hapa sasa mambo yakifikia kilele cha kero ndipo muhusika huamua kufanya maamuzi magumu. Wengi hujiua kwa ama kujinyonga, kunywa sumu, au kujipiga risasi. Kwa bahati mbaya watu wengi wana tafsiri potofu kuhusu kifo. Wanadhani kufa ni kuepukana na shida na matatizo ya duniani na kupumzika milele. Kwa dhana hii wenye kujiua wanadhani wakifa watapumzika. Kumbe ndiyo wameanza awamu ya pili yenye mateso yasiyokoma milele!
Kilele cha mambo yote
ni hukumu ya milele

Katika kifungu kidogo cha 4 hapa nimedokeza kuhusu dhana potofu kuhusu kifo. Kufikiri kufa ni kupumzika. Nilidokeza kwamba kwa wengine kufa ni kuanza awamu ya pili yenye mateso yasiyokoma. Pengine hapa niweke bayana suala hili ili kuweka waziwazi ukweli wa mambo.
Yesu Kristo alitoa mfano wa watu wawili walioishi duniani na kila mmoja wakati wa uhai wake aliishi aina fulani ya maisha ambayo yalikuwa na mwonekano tofauti katika jamii. Watu hao mmoja alikuwa tajiri na wa pili alikuwa maskini na mwenye maradhi ya ngozi. Tajiri aliishi maisha ya anasa na udhalimu wakati maskini aliishi maisha ya uchaji Mungu. Yesu alisimulia kwamba wote walikufa. Kisha Yesu akasema kila mmoja alikwenda mahali maalum kulingana na aina ya maisha aliyoishi duniani. Tajiri alikwenda kuzimu mahali penye mateso makali kupindukia. Yule maskini kwa kuwa alikuwa mchaji alikwenda mahali paitwapo “kifuani pa Ibrahimu”. 
Kisa kinasimulia kwamba Yule Tajiri kule kuzimu aliweza kuwaona Ibrahimu na yule maskini Razaro na kuomba Razaro amletee angalau tone la maji kwani alikuwa akiunguua vibaya sana. Ibrahimu alimjibu kama ifuatavyo: “Mwanangu kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo hivyo alipata mabaya; na sasa yeye upo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa…..” Unaweza kusoma kisa kizima katika Luka 16:19-31)
Nilichotaka kusisitiza hapa ni kwamba, si kila mfu afaye huenda kupumzika. Inategemea mfu husika aliishi aina gani ya maisha machoni pa Mungu. Pili, mahali aendako mtu baada ya kufa hutegemeana na uchaguzi wa maisha aliyoishi duniani. 
Mfano wa tajiri alioutoa Yesu hakuma akilaani utajiri wa Yule tajiri, bali alikuwa akionesha “matumizi mabaya ya utajiri” ambayo ndiyo yalisababisha aende kuzimu kwenye maumivu makali. Matumizi ya tajiri yalikuwa ni kuvaa na kula kwa anasa duniani. 
Alikataa kutumiia mali zake kuwasaidia maskini, hata wale walioletwa mbele zake aliwapuuza kwa kuwatupia makombo akiwemo Lazaro. Ndiyo maana alipokufa ilibidi apokee laana nyingi kuzima badala ya Baraka:“Mwenye kuwagawia masikini hatahitaji kitu, bali afichaye macho yake atakuwa na laana nyingi.” (Mith.28:27);
Hitimisho
Nataka kumaliza kwa kauli ya mada hii ya kwamba, “ukiheshimiwa heshimika”! Tumesoma kwamba juhudi katika kutafuta mali na umaarufu si dhambi. Lakini baada ya kuvipata unavitumiaje, na wewe mwenyewe tabia yako inasomekaje mbele za wengine katika jamii. Tumepitia uchambuzi wa baadhi ya wengi wenye kufanikiwa duniani wakaheshimiwa kwa mafaniko, na kisha hushindwa kutunza heshima zile walizozipata; hatimaye kujikuta wanapoteza heshima hizo. Tulijifunza kuhusu tatizo la kujikinai baada ya kufanikiwa. Naweza kusema kwamba kwa walio wengi changamoto sio kufanikiwa, bali ni jinsi ya kuyatunza mafanikio yenyewe. 
Binadamu hujisahau upesi hata kusahau kule alikotoka. Haya basi hilo linaweza kuzungumzika. La kushangaza zaidi ni binadamu kutokujali kule aondako! Na miye napenda kukumbusha tena, na kwa wengine, hii yaweza kuwa ni onyo la mwisho kwa wahusika. Mungu amesema waziwazi katika neno lake kwamba:
“Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wa kila mahali watubu. Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu Yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.” (Mdo.17:30-31)
“Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri ya alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.” (2 Kor.5:10)
“hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.” (Mhu.12:13-14)
“Ukeheshimiwa heshimika”

mwisho

SOMO: UFUFUO NA UZIMA - ASKOFU KAKOBE

$
0
0
SOMO: UFUFUO NA UZIMA

Leo, katika Siku yetu ya Kuichambua Biblia, tunaendelea kujifunza Kitabu cha YOHANA katika Biblia zetu na kutafakari YOHANA 11:17-46. Kichwa cha Somo letu la leo, ni “UFUFUO NA UZIMA“, hata hivyo, kuna mengi zaidi ya kujifunza katika mistari hii. Tutayagawa mafundisho tunayoyapata katika mistari hii katika vipengele tisa:-


(1) KUTOKUCHELEWA KWA MUNGU (MST. 17-18);

(2) MAHUDHURIO YA WATU WENGI KATIKA MSIBA (MST. 19);


(3) UFUFUO NA UZIMA (MST. 20-25);

(4) AISHIYE NA KUNIAMINI, HATAKUFA KABISA HATA MILELE (MST. 26- 27)

(5) YESU AKALIA MACHOZI (MST. 28-37);

(6) LIONDOENI JIWE (MST. 38-40);

(7) NGUVU YA SHUKRANI (MST. 41);

(8) LAZARO, NJOO HUKU NJE (MST. 42-44);

(9) KUMWAMINI YESU BAADA YA KUONA ALIYOYAFANYA (MST. 45-46).



(1) KUTOKUCHELEWA KWA MUNGU (MST. 17-18)

Yesu Kristo, alifika Bethania kwa Lazaro, na kumkuta amekwisha kuwamo kaburini yapata siku nne. Ilionekana kana kwamba amekwisha kuchelewa na haiwezekani tena kwa Lazaro kuwa mzima. Hata Martha na Mariamu, wakasema “Kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa“ (MST. 21, 32), kwa kumaanisha kwamba kwa sasa amekwisha chelewa. Ni muhimu kufahamu kwamba kuchelewa, ni kwetu wandamu tu. Tukichelewa usafiri wa basi au ndege, tayari tunakuwa katika tatizo kubwa n.k. Kwake Yesu, sivyo, Yesu hachelewi kamwe. Yesu alimponya mtu kiwete aliyekuwa katika hali hiyo kwa miaka 38 (YOHANA 5:2-9). Alimponya pia mwanamke aliyetokwa damu kwa miaka 12 (MARKO 5:25-34). Alimponya mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka 18 akiwa amepindana (LUKA 13:11-13). Alimponya mtu kipofu aliyekuwa katika hali hiyo, TANGU KUZALIWA (YOHANA 9:1-11). Hata kama tatizo letu limechukua muda mrefu kiasi gani, na kuonekana kana kwamba mambo yamekwisha kuharibika, ni muhimu kukumbuka kwamba Mungu wetu hachelewi. Anaweza kuingilia kati popote pale na kutujibu kwa utukufu wake. Wakati wake wa kufanya miujiza, huwa mzuri zaidi kuliko wakati wetu. Inatupasa kuwa na subira kama Ayubu, na kuungojea wakati wa Mungu wetu asiyechelewa (YAKOBO 5:11).


(2) MAHUDHURIO YA WATU WENGI KATIKA MSIBA (MST. 19)

Watu wengi katika Wayahudi, walikuwa wamekuja kwa Martha na Mariamu, ili kuwafariji katika msiba huo. Huu pia, ndiyo wajibu wa kila ajiitaye Mkristo. Inatupasa kuhudhuria kwa wingi wetu katika misiba ya ndugu zetu katika Kristo na kutoa faraja zote. Mungu mwenyewe, alimzika Musa (KUMBUKUMBU 34:5-6). Ikiwa Mungu alichukua kwa uzito mkubwa mazishi ya Musa, sisi nasi tunajifunza kama Wakristo kuchukulia kwa uzito mkubwa mazishi ya ndugu zetu katika Bwana. Vivyo hivyo Yohana Mbatizaji alizikwa kwa uzito mkubwa na ndugu katika Bwana (MATHAYO 14:6-12). Mahudhurio yetu katika msiba wa ndugu yetu katika Bwana, hayana budi kuwa ya watu wengi ili tuonyeshe upendo wetu wa Kikristo. Siyo hilo tu, tunajifunza hapa kwamba Yesu naye, alihudhuria katika msiba huu. Ndivyo ilivyo hata leo, Yesu huhudhuria katika msiba wa kila mtu aliyeokoka. Ndiyo maana hutupa faraja ya kipekee.

(3) UFUFUO NA UZIMA (MST. 20-25)

Yesu anajitaja hapa kwamba, “Mimi ndimi huo ufufuo na uzima (MST. 25). Yesu ni UZIMA(YOHANA 14:6), hata hivyo, Yeye ni zaidi ya Uzima, Yeye ni Ufufuo na Uzima. Kwa kuwa Yeye ni Uzima, hutuponya katika magonjwa yetu. Kwa kuwa Yeye ni Ufufuo, ana uwezo pia wa kufufua viungo vyetu vilivyokufa kabisa. Yesu kama Uzima, anaweza kuziponya Ndoa, kazi au biashara zetu zinazolegalega. Hata hivyo, Yesu kama Ufufuo, ana uwezo wa kuzifufua ndoa, kazi au biashara zetu zilizokufa kabisa. Anaweza pia kufufua maisha yetu ya maombi, na kumtumikia Mungu, yaliyokufa.

(4) AISHIYE NA KUNIAMINI HATAKUFA KABISA HATA MILELE (MST. 26-27)

Kufa hapa, kunazungumzia mauti ya milele au ghadhabu ya Mungu, moto wa milele (YOHANA 3:36). Yeye aliyeokoka, hukumu hiyo ya adhabu huwa mbali naye (WARUMI 8:1-2).

(5) YESU AKALIA MACHOZI (MST. 26-37)

Yesu hulia na waliao, na kufurahi pamoja na wafurahio, kama anavyotuagiza kufanya (WARUMI 12:15). Anatupenda upeo. Huzuni yetu, ni huzuni yake na furaha yetu, ni furaha yake. Hivyo hatupaswi kuwa na mashaka juu ya kuhusika kwake na matatizo yetu.

(6) LIONDOENI JIWE (MST. 38-40)

Kuna sehemu yetu ya kufanya katika ukamilishaji wa kila muujiza tunaouhitaji. Ikiwa hatuliondoi jiwe, ni vigumu kumwona Lazaro akifufuka. Hatuna budi kuangalia kwamba kuna jiwe gani la kuondoa, katika kupata miujiza yetu. Ikiwa tunaomba mfanikio ya kifedha, jiwe la kuondoa, ni kuhakikisha tunatoa fungu la kumi la mapato yetu YOTE hata kama ni madogo. Ikiwa tunataka kazi, jiwe la kuondoa, ni kuhakikisha tunahusika kikamilifu kutafuta kazi na kuondoa uvivu. Ikiwa tunahitaji mtoto, tuhakikishe tunakutana waume na wake zetu katika siku za mwezi zilizo na rutuba ya uzazi na tuondoe kila namna ya chuki na ugomvi siku hizo, maana hayo yatatufanya tusikutane siku za rutuba na kukutana siku zisizo na rutuba.

(7) NGUVU YA SHUKRANI (MST. 41)

“Baba NAKUSHUKURU“, ni maneno ya Yesu yanayotufundisha kushukuru. Tukiondoa shukrani katika maisha yetu ya maombi, tunabakiwa na sifuri. Shukrani zina nguvu ya ufufuo. Tunapaswa kuunga maombi na shukrani wakati wote, ikiwa tunataka kuona nguvu ya Ufufuo ya Yesu ikitenda kazi (1 WATHESALONIKE 5:17-18; WAKOLOSAI 3:15). Je, ni kweli kwamba Mungu hajatutendea lolote lililo jema? Mbona tunaomba tu bila kushukuru? Tuanze na shukrani kwanza kabla ya maombi yetu kila inapowezekana. Tumshukuru hata kwa hewa tunayoivuta bila malipo.

(8) LAZARO, NJOO HUKU NJE (MST. 42-44)

Watu WOTE waliomo makaburini, wataisikia sauti ya Yesu wakati wa Ufufuo (YOHANA 5:28-29). Hapa Yesu alisema “LAZARO NJOO HUKU NJE“. Kama angesema “NJONI HUKU NJE“, wote waliokufa tangu wakati wa Adamu, wangekuja! Ni kwa sababu hii alitaja jina la huyu Lazaro anayehusiana na Martha na Mariamu.

(9) KUMWAMINI YESU BAADA YA KUONA ALIYOYAFANYA (MST. 45-46)

Wengine huwa tayari kuokoka, KABLA ya kuona miujiza; lakini wengine huwa tayari kuokoka,BAADA ya kuona miujiza kama hapa. Katika kushuhudia kwetu, hatupaswi kumwekea Mungu mipaka na kusisitiza kumwombea mtu matatizo yake pale tu anapokuwa tayari kuokoka kwanza. Asipokuwa tayari kuokolewa, tumwombee tu. Mapepo yake yakitoka au akipata muujiza wowote, ni rahisi kuvutwa kwa Yesu na kuokolewa pia kama watu hawa. Akiokoka kabla ya maombezi, ni vema zaidi, hata hivyo tusiweke hiyo kuwa KANUNI.

…………………………………………………………………………………………………………………………………..

Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni? Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14). Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27). Kinyonge ni kipi? Ni yule anayetenda dhambi. Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge! Je, wewe ni mtakatifu? Jibu ni la! Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13; YOHANA 14:6). Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii? Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni; “Mungu Baba asante kwa ujumbe huu. Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi. Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha. Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo. Bwana Yesu niwezeshe. Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu. Amen”. Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni. Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu. MUNGU AKUBARIKI !!!

Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        


Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

TB JOSHUA ATUMA MSAADA WA CHUPA 4000 ZA MAJI YA UPAKO KUPONYA EBOLA

$
0
0


Nabii maarufu ndani na nje ya bara la Afrika TB Joshua wa kanisa la All nations (Scoan) la nchini Nigeria ametuma chupa 4000 za maji ya upako pamoja na dola za kimarekani 50,000 nchini Sierra Leon ili kusaidia kutibu ugonjwa wa ebola ambao umeikamata nchi hiyo.

Nabii Joshua amesema kupitia tovuti ya kanisa lake kwamba maji hayo yamesafirishwa kwa ndege maalumu ya kukodi ambayo gharama yake pia ni dola 50,000 na kufanya gharama kamili dola 100,000 (laki moja) kwa msaada alioutoa akishirikiana na wadau wa Emanuel TV ya kanisa lake.

Katika taarifa yake kupitia tovuti hiyo nabii TB Joshua amesema Mungu mwenye nguvu atajidhihirisha uweza wake kupitia maji hayo ya upako ambayo yametolewa kwa watu waliokumbwa na ebola. "Sio maji ndiyo ya ponyayo wagonjwa ila ni Yesu mwenyewe, lazima mtu anayemuombea mwingine na yule anayeombewa wawe na imani. lazima imani iwe hai ili kupata uponyaji kwasababu ndiyo husababisha uponyaji na sio maji ya upako" amekaririwa nabii Joshua.

Watu waliotumia maji hayo ya upako wamekiri kuwa na imani nayo kutokana na wengi kufunguliwa na miujiza mingi kutendeka kutoka hali ya kutokuwa na uwezo wa kuzaa na hatimaye kupata mtoto lakini pia maji hayo yamekuwa kinga ya risasi kupenya kwenye gari kama mtu mmoja kutoka nchini Ghana alivyopona mikononi mwa majambazi waliokuwa wakishambulia kwa risasi gari lake yeye akiwemo ndani bila mafanikio.

MALIZA MWEZI NA SEMINA YA WANANDOA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mwisho wa mwezi huu wa nane jijini Dar es Salaam, kutakuwa na semina ya wanandoa, ambayo ni sehemu ya mfululizo wa semina hizo zenye mafanikio zinazoandaliwa na Branea Spiritual Family.

Pamoja na kwamba kuna mambo unaweza kufanya kuepuka vishawishi, hasahasa mume wa mtu (bofya hapa kusoma) Semina hiyo ambayo kwa mwaka jana imefanyika Jumamosi ya mwisho ya mwezi wa nane kama ilivyo kwa mwaka huu - itakuwa na wazungumzaji waliobarikiwa na kufanyika baraka pia kwa jamii, mathalani Apostle Ndegi sanjari na Mama Hiza

Kuna mengi ambayo hata hayawezi kuzungumzika ama kuandikika hapa, ila kwa mawasiliano zaidi kuhusiana na semina hiyo ambayo itafanyika kwenye ukumbi wa kanisa la Sinza Christian Centre bila kiingilio chochote, unaweza kupiga namba 0767-555792 ama 0718-193901.

Tazama kipeperushi kwa taarifa zaidi.

AINA 4 ZA MUDA ZILIZO MUHIMU KWA MAENDELEO BINAFSI NA YA JAMII

$
0
0
Na Faraja Mndeme.

Wiki iliyopita tulitazama vitu vichache vitakavyokuongezea thamani na mahusiano mazuri na watu, bofya hapa kusoma. Wiki hii basi na tutazame aina nne za muda ambazo ni muhimu kwenye maendeleo binafsi na kwenye jamii.


Muda wako ukoje? ©Ever Moore Milestone
1. Muda Binafsi
Mara nyingi kulingana na mfumo wa ulimwengu wa maisha tulio nao, ni watu wachache sana ambao wanaweza kutenga muda binafsi, yaani wao na nafsi zao bila muingiliano wa kitu chochote - wakaketi chini wakajitathmini, wakajirekebisha na kuazimia wao binafsi juu ya mabadiliko wanayoyataka kulingana na changamoto zinazowakabili kwenye maisha ya kila siku. Jamii yetu na watu wengi kila wakati wako busy kiasi kwamba mpaka wanajisahau kwamba muda mwingine wanajihitaji wao kama wao binafsi kuweza kufikia mambo mbalimbali ya maisha yao. Muda mwingi tumejishughulisha na mambo mengi amabayo mara nyingine hayana ulazima na mengine baada ya muda fulani kupita hatutayahitaji tena. Ni muhimu kuhakikisha unakuwa na muda binafsi mara kwa mara ili kuhakikisha kwamba unakuwa na uwekezaji wa kutosha kwako binafsi kuanzia kwenye maarifa, kiuchumi, kisiasa na kijamii pia. Mara nyingine hata changamoto tunazokutana nazo, hatuhitaji msaada wa watu wengine, bali tunapaswa kuwa tu na muda binafsi (wewe kama wewe) bila mwingiliano wa vitu vingine ili kuweza kujitafakari, kujikosoa, kujirekebisha na kufikiria suluhisho lenye ubora zaidi kwenye maisha yetu.

2. Muda wa Familia
Ni rahisi sana kujikita kwenye mambo kadha wa kadha ambayo huenda yakawa yanakuweka busy kuliko kawaida huku ukipitiwa/ukisahau kwamba kuna watu ambao wanakuhitaji kwa ukaribu zaidi kuliko shughuli unazofanya kila siku. Shughuli za kila siku zinaweza zikawa zinafikia ukomo mara kwa mara lakini familia yako haiwezi kufikia ukomo mara kwa mara. Hakikisha unatenga muda wa mara kwa mara wa kukaa ya familia yako kwa ukaribu zaidi na kuweza kushirikishana juu ya maswala mbali mbali na changamoto zinazokubabili ili kuweza kupata tumaini jipya na kutiwa moyo. Rafiki wa kwanza kwenye maisha yako ni watu wa nyumbani mwako. Hakikisha unawapenda, unatenga muda mara kwa mara kwa ajili yao. Hakikisha unakuwa nao karibu kwenye kila jambo ili kuweza kutengeneza 'bond' inayodumu na isiyokuwa na ukomo. Familia yako haiwezi kukutupa kabisa kwenye kile unachopitia, hivyo ni muhimu kuhakikisha unawekeza muda wa kutosha juu ya familia yako - jitoe, ithamini, ipende na ujivunie maana wewe ni sehemu ya familia hiyo. Unapokuwa na upendo usiokuwa na manung’uniko juu ya familia yako, inakusaidia pia kuwa vizuri hata kisaikolojia. Hakikisha unawapenda Baba, Mama, Mke, Mume, Watoto, Ndugu wengine kwa ukaribu zaidi kwa kutoa muda wako kwao.

3. Muda wa Marafiki
Mara nyini kwenye maisha tumekuwa na urafiki kwa sababu mimi nakuhitaji, ili hali nikiwa sina uhitaji urafiki huo unakuwa unakufa kwa muda fulani. Yaani siku nikihitaji msaada wako juu ya swala fulani ndipo napoibuka kukutafuta. Urafiki ni zaidi ya undugu wa kawaida. Urafiki usiokuwa na mipaka ni ule ambao pindi nakuhitaji au sikuhitaji bado u sehemu ya maisha yangu. Marafiki wa kweli hutenga muda wa kukaa na kuongea, kushauriana, kuonyana na hata kusaidiana kufikia malengo kadha wa kadha ya kimaisha. Rafiki ni mtu muhimu sana kwenye maisha maana hakuna anayeweza kuishi pekee yake bila utegemezi wa kumhitaji mtu mwinginie. Kila mtu anamuhitaji mtu mwingine kwenye kila nyanja ya maisha, na hakuna aliye bora kuliko mwingine - ni tofauti ya vipawa tu kwamba cha huyu kinaonekana na cha yule hakionekani, cha huyu kinafanya vizuri kulingana na utashi na maarifa aliyo nayo, na cha yule hakifanyi vizuri. Tunapokutana kwa pamoja ndipo tunaposaidiana kuweza kusonga mbele na kujengana katika nyanja mbalimbali za kimaisha.

4. Muda wa Ibada
Kila jambo kwenye maisha linapita, na kila kitu kina ukomo wake ingawa inaweza isiwe leo au kesho - lakini Mungu hana ukomo, wala hana mwanzo, kwa sababu sote tulitokana na yeye na sote tutarudi kwake. Tofauti ni aina na wakati wa kurudi, lakini mwisho wa siku maisha yetu wanadamu yana mwanzo na mwisho. Ni muhimu kujijengea tabia ya kuwa na ibada za mara kwa mara kulingana na dini yako ili kuweza kupata muongozo wa Ki-Mungu kwenye maswala mbalimbali na changamoto mbalimbali za kimaisha zinazotukabili huku tukitambua kwamba yupo ambaye alituumba na mwenye mamlaka juu ya maisha yetu ya kila siku. Ni muhimu kuhakikisha kwamba unakuwa na ukaribu na muumba wako ili unapopatwa na misukosuko ya maisha na mambo kadha wa kadha anakuwa yupo karibu nawe kukutia moyo, kukujenga na kukusaidia kuvuka dhidi ya yanayokukabili. Marafiki wa kweli hutumia muda mwingi kwa pamoja na kusaidia kwenye mambo kadha wa kadha. Hakikisha siku nzima haipiti bila kuwa na mawasiliano na ibada kati yako na Muumba wako.

God Bless Y’all
+255719742559

WAIMBAJI WAAMUA KUPAMBANA NA UNENE, MWINGINE ATANGAZA NIA

$
0
0

Baada ya juhudi za mwimbaji nyota wa muziki wa injili Afrika ya kusini mwanadada Ntokozo Mbambo wa Mbatha kufanikiwa kupunguza unene kwa asilimia kubwa mwimbaji mwingine wa kundi la Soweto gospel Choir mwanadada Sipokazi Nxumalo wa Linda nayeye pia ametangaza hapo jana kuamua kupunguza unene ili awe sawa na Ntokozo.

Sipokazi ambaye anafahamika vyema na wapenzi wa Soweto kutokana na uimbaji wake mahiri ndani ya kundi hilo, ametangaza uamuzi huo kupitia ukurasa wake wa facebook akieleza wazi kuvutiwa na waimbaji wenzake ambao anavutiwa na sauti zao kwa jinsi walivyoweka juhudi na sasa matunda yameonekana.

Nikiwa na Sipokazi mara baada ya onyesho lao jijini London november mwaka jana.
  1. Jill Scott Kierra Sheard Ntokozo Mbambo Mbatha Kelly Price All of these are my favourite female vocalists and they've all done it#losttheweight....,,I'm inspired by their end results they look amazing ok im doing this now!!!!!! Clearly it's doable##teamattackthatfat##teamlookandfeelyoungagain##doingitforME — feeling inspired.
    LikeLike ·  · 

































Ntokozo amewashangaza wengi nchini kwao Afrika ya kusini baada ya kufanya mazoezi na kujinyima kula vitu vyenye mafuta na hatimaye sasa unene aliokuwa nao awali umepungua ambapo hata sasa mwanadada huyo anayetarajia kuachia wimbo mpya hivi karibuni ikiwa maandalizi ya album yake mpya bado anakwenda katika vituo vya mazoezi (gym) na kula chakula bora ili kulinda mabadiliko yake ya mwili ambayo wengi hususani wanawake wamempongeza.

Muonekano wasasa wa Ntokozo Mbambo baada ya kupungua, hapa akiwa na mumewe Nqubeko.

Mtazame Sipokazi akiimbisha wimbo Noyana walipotembelea Australia miaka ya nyuma




SABABU 6 ZA WAPALESTINA WASIO NA HATIA KUFARIKI

$
0
0
Na Ron Cantor.
Baadhi ya makombora yaliorushwa kutoka Gaza kuelekea ardhi ya Israel. ©Amir Cohen/Reuters
Katika kipindi cha wiki kadha zilizopita, kumekuwa na mapigano baina ya Hamas na Israel, ambapo Hamas wamerusha zaidi ya makombora 2000 kwenye taifa la Israel, na si kusini mwa taifa hilo tu, bali asilimia 80 ya nchi hiyo. Tukio hili liko kinyume na mikataba yote ya kivita. Kushambulia wasio wapiganaji ni ugaidi, mkataba wa Geneva unakataza.

Kufuatia mashambulizi hayo, Israel haikuwa na budi kurejesha mashambulizi, na katika kufanya hivyo, Wapalestina zaidi ya 600 wameuawa, taarifa zinaeleza kwamba karibia asilimia 80 hawakuwa wapiganaji. Lakini takwimu hizi zinatoka kwa Hamas, kundi ambalo linatia shaka kwenye usahihi wa taarifa zao - kwa sifa yao ya ugaidi, pamoja na propaganda zao kuliko ukweli. Lakini pamoja na hayo, yatupasa kujiuliza, nani wa kulaumiwa kutokana na vifo hivi vya raia?

Mahmoud Abbas, Rais wa mamlaka ya Palestina, ameituhumu Israel kwa mauaji ya halaiki. Rais wa Uturuki naye akasema kuwa ukatili wa Israel umekithiri kuliko ule wa Adolf Hitler. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amelaumu mashambulizi ye Israel na kuyaita mabaya kuliko. Na pia John Kerry ameripotiwa kukebehi mashambulizi haya, pale ambapo alidhani kipaza sauti chake kimezimwa, kabla ya mahojiano kwenye kituo cha TV cha Fox.

Pamoja na yote hayo, binadamu yeyote mwenye kuzungumza ukweli atatambua ya kwamba lawama zote zinastahili kuelekezwa kwa aliyeanzisha mgogoro huu, Hamas.

Watoto hawa wanastahili kumlaumu nani? ©Finbarr O'Reilly/Reuters
1. Hamas wanatumia wanawake na watoto kama ngao
Kuna ushahidi wa kutosha kwamba Hamas wanazungushia silaha zao maeneo ya watoto. Huu si utu kabisa. Nia zao hapa ni mbili, kwanza kuzuia mashambulizi ya Israeli dhidi yao, na pili; iwapo Israeli watashambulia, basi Hamas waweze kutembeza miili ya watoto mitaani.

Kuna kipindi nilimsikia mshauri wa Abbas akisema kwenye kituo cha runinga cha CNN kwamba hakuna mama yeyote anayeweza kumruhusu mtoto wake kutumiwa namna hii. Lakini ni kina mama hao hao ambao huenda kwenye vituo vya runinga wakimsifu Allah kuwa watoto wao wamejitoa mhanga. Ni kina mama hao hao ambao hugawa pipi mtaani wakati Waisraeli wanapouawa na kufurahia habari ya mauaji ya vijana watatu wa Kiisraeli

Tofauti kati yetu nao ni moja, sisi tunatumia silaha zetu kulinda wananchi wetu, wao wanatumia famlia zao kulinda silaha zao. Anaeleza Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa Israel.

2. Hamas wanaficha silaha zao kwenye makazi ya watu
Wiki hii pekee, makombora zaidi ya 20 yalipatikana kwenye shule ambayo inafadhiliwa na Umoja wa Mataifa. Israel inaojua haya, inaacha kama yailvyo pamoja na kujua maeneo yalipo ili yaje kutumika dhidi yake?

Na, UN hivi karibuni baada ya kutambua kuhusu uwepo wa makombora hayo, ikayakabidhi kwa polisi wa Gaza chini ya Hamas, yaani wameyakabidhi ili yaweze kutumika dhidi ya taifa la Israel, Bwana Ban Ki Moon, hiyo ni mbaya kuliko.

Vifaru vya jeshi la wananchi wa Israeli vilipopiga hospitali na kupelekea kuwa na vifo na majeruhi kwa wananchi, ilitokana na Hamas kuficha silaha zao za kushambulia vifaru kando tu ya hospitali hiyo. Silaha hizo tayari zimeshaua askari kadhaa wa Kiisraeli. Na Hamas wameamua kufanya hivyo kwa makusudi kana kwamba wameiwekea Israeli chambo ipate kunasa kwenye mtego wa kulipua hospitali.

"Licha ya kwamba Jeshi la Israeli linachukua hatua stakihi kupunguza vifo vya wananchi wasio na hatia, Hamas kwa makusudi wamehamishia shughulizi zao za ugaidi kwenye makazi ya watu, wanahusika moja kwa moja." Anaeleza msemaji wa Jeshi la Israeli"

lakini tuwe wakweli tu, kuna tofauti kubwa kati ya mashambulizi ya pande hizi mbili, ambapo Israel wanalenga kupunguza nguvu ya mashambulizi kutoka Hamas. Ila kwa upande wa Hamaa, wanachofanya ni kushambulia raia wa Israeli - japo hawako vizuri, maana kati ya zaidi ya makombora 2000 yaliyolengwa kwenye ardhi ya Israeli ndani ya wiki mbili, kumeripotiwa kifo cha mtu mmoja tu.

3. Wapalalestina wasio na hatia walichagua kuongozwa na Hamas
Mnamo mwaka 2006 wakati Israeli iliondoka Gaza na kutarajia amani, wakaziw a Gaza waliamua kuiweka Hamas madarakani. Sasa hapa naelewa kwamba hii ilitokana na sababu kwamba Mamlaka ya Wapalestina ilikuwa (na hata sasa) imekithiri rushwa, na wanasiasa wake walikuwa wakijinufaisha kwa misaada kutoka Marekani, Umoja wa Mataifa, na hata Ulaya. Lakini licha ya hivyo wakaamua kuezeka utawala wa kigaidi ambao utaongoza kiislamu na kutoa kafara vijana na mabinti wake kwa mawazo machache tu kama vile mtu ameamua kwenda kununua sabuni ya mche.

4. Wapalestina wasio na hatia hawathubutu kusimama dhidi ya Hamas ili wasirushe makombora kwenye mikusanyiko ya Israeli
Mfumo huu wa ugaidi ulianza takriban miaka 10 iliyopita, na Hamas badi wanandelea kutaala Gaza. Hakuna aliyesimama dhidi yao. Hii ni mara ya tatu ndani ya miaka 5 wamealika mashambulizi kutoka Israeli, kutokana na makombora yao yasiyo na hatamu. Na hivi majuzi baada ya wakazi wa Gaza takriban 600 kufariki, huenda wangesema inatosha. Lakini Hamas wakatangaza kwamba wamemkamata mateka askari mmoja wa Israeli. Mithili ya mbwa aliyekosa mwelekeo baada ya kitenesi kuchezeshwa machoni pake - ndivyo ambavyo Wahamas wakaingia mtaani kusheherekea utekaji huo (licha ya kutothibitishwa kipindi hicho).

5. Hamas wana mahandaki yanayotokezea kwenye nyumba za wananchi na misikiti
kama ambavyo imeripotia hivi karibuni na gazeti 'The Times of Israel', kumepatikana njia za chini ya ardhi kwenye makazi ya watu na misikiti, kwa mujibu wa Jeshi la Israel.

Mengi yamefanyika kutokana na kile kinachoitwa kuwa ni mauaji ya halaiki kwa wanawake na watoto. Lakini jambo moja ambao halielezwi kwa umma, ni kwamba kumekuwa na maeneo lengwa zaidi ya 100, ikiwemo misikiti miwili ambayo imetumika kama kambi za Hamas ikiwemo kuhifahi silaha, (timesofisrael) imeeleza.

Pamoja na hayo, Jeshi la Israeli lilitoa tahadhari kwa wananchi wa Gaza kuondoka maeneo ambayo wapo kabla jeshi hilo halijaingia. hivi Marekani na Uingereza ziliarifu wakazi wa Berlin, Ujerumani (miaka ya 40) kabla ya kuangusha tani 70,000 za mabomu? La hasha! wakazi wa Berlin hawakuonywa kuhusu ujio wa mashambulizi, na wala hawakusubria kupigiwa simu ama kupewa vipeperushi kuhusu kiama kilichokuwa mbele yao. Takriban watu milioni moja na laki saba waliukimbia mji. Huku Gaza ni kinyume chake, kwani Hamas wanahamasisha wakazi waendelee kuwepo - ili wafe.

Na kwenye shambulizi la mabomu hayo ya tani elfu 70 dhidi ya Berlin, hakuna aliyeilaumu Marekani na Uingereza, kwa maelezo kwamba walikuwa wanajitetea. Ndivyo pia basi ilivyo kwa Israeli, kwani wapo Gaza kwa ajili ya kuharibu mahandaki na njia za chini ya ardhi ambazo Hamas wanazitumia kuishambulia Israel.

6. Hamas wanafurahia vifo vya wananchi wa kawaida
Hili ni jambo ambalo haswa wao ndo walikuwa wanalitaka. Amewahi kusema Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu. "Hii ni vita yenye ukatili zaidi na iliyo mbaya ambayo nimewahi kuona, sio tu kwamba Hamas wanawalenga wananchi wa Israeli na kujificha nyuma ya wananchi wao, lengo lao ni kuona vifo vingi vya wananchi vikitokea" ili vyombo vya habari vionyeshe kwa lengo la kuonewa huruma kutoka na dunia nzima.

Wakati Israel inataka kuepusha vifo vya Wapalestina, Hamas wanataka wafe, na kadri ya wingi wa mauti, ndiyo furaha yao inazidi. Huu ndio mkakati wao. Wakati makamanda wa Hamas wamejificha kwenye mahandaki, wanashangilia kwa kadri wanavyosikia kuwa kuna wananchi wao wameuwawa kutokna na mkakati wao. Na hilo linaonekana kuwa kama mashine ya uendeshaji mtambo wa propaganda zao.

Hivyo basi jiulize, NANI KWELI WA KULAUMIWA?


Makala hii imenukuliwa kutoka Charisma News, na kuchapwa upya kwa lugha ya Kiswahili hapa GK.

Kuhusu Mwandishi;
Ron Cantor ni mhariri wa Messiah's Mandate International, nchini Israel. Huduma inayolenfa kueneza ujumbe wa Yesu kutoka Israeli kwenda mwisho wa nchi (Matendo ya Mitume 1:8) Bwana Canto pia husafiri nchi mbalimbali akifundisha kuhusu asili ya Wayahudi kutoka agano jipya. Pamoja na hayo, pia huhudumu kwenye kundi la wachungaji la Tiferet Yeshua, kusanyiko la wazungumzaji wa Kiebrania Tel Aviv. Kitbau chake cha hivi karibuni kuchapishwa kinafahamika kama Identity Theft. Unaweza kumfuatilia kwenye mtandao wa Twitter kupitia @RonSCantor 

Viewing all 1245 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>