Sacrifice Of Praise Africa Concert ni matamasha endelevu ya kumtolea Mungu dhabihu za sifa yanayoandaliwa na watu wa mungu bila ya kujali jinsia,umri,rangi,kabila, wala Imani.
Kusudi la Sacrifice Of Praise Africa Concert ni kumtolea BWANA dhabihu za sifa na kuhudumia watu kutoka pande zote kwa nyimbo za kusifu na kuabudu, sala, pamoja na maombi, na shuhuda mbalimbali kupita kwaya na uimbaji wa mtu mmoja mmoja.
Pia kupitia matamasha haya wamekusudia kuibuwa vipaji vya wasanii wa nyimbo za injili ambao bado hajatoka wa kufamika katika muziki wa injili kwa kupatiwa mafunzo ya kitaalamu ya muziki na uimbaji.
Kwa lengo la kuwasimamia katika kazi wasanii wa nyimbo za injili, kuandaa matamasha ya nyimbo za injili, mafunzo ya ufundi mitambo, mafunzo ya muziki na sauti, na pia kutoa mafunzo ya muziki wa live na kurekodi.
Malengo ya Sacrifice Of Praise Africa Concert kwa mwaka huu wa 2015 kabla ya uchaguzi ni kufanya ibada hizi (matamasha haya) na maombi ya amani kwa taifa la Tanzania.
Kwa mwaka huu Sacrifice Of Praise Africa Concert inataraji kufika katika mikoa mitano hapa Tanzania; Arusha, Morogoro, Dodoma, Mbeya, na Dar es Salaam
Kwa dhumuni la kuifikia Africa nzima kwa uinjilisti wa nyimbo na kuunganisha mtandao wa wasanii wa nyimbo za injili Afrika nzima.
Ungana nasi katika tukio zima la Sacrifice Of Praise Africa Concert Season 2 Tanga ambayo ilifanyika katika kanisa la E.A.G.T mikanjuni kuanza saa nane mchana ambapo dhabihu za sifa zilianza kushuka.
Hatimaye Dezzydery akimkaribisha MC King Chavala
Shela Mnyinyi katika uimbaji wake akamsifu Mungu kwa nyimbo ya kiasili

Mchungaji wa kanisa la E.A.G.T Mikanjuni - Josephine
Katika kuwekwa wakfu Sacrifice Of Praise Africa msimu wa pili Tanga
Wimbaji Christina Msengu katika uimbaji wake
Na huyu ni Hellen Kijazi
katika upigaji wa saxophone Mise Anaeli kutoka Dar es salaam
Daniel Manimba, Mratibu - Sacrifice Of Praise Africa Concert
Dezzyderry, Mratibu - Sacrifice Of Praise Africa Concert
Mwalimu Emmanuel Mkawaya
Mzee Ambaye aliguswa na kuitaji kutoa mchango wake wa kifedha katika kufanikisha matamasha endelevu ya Sacrifice Of Praise Africa Concert
na sasa ni Sacrifice Of Praise Africa Concert Mass Choir
uwepo wa Bwana Yesu ukishuka katika Dhabihu za sifa
Katika uwepo wake
Ni katika ugawaji wa zawadi/vyeti ambayo vilionyesha juu ya kushiriki katika Sacrifice Of Praise Africa Concert msimu wa pili.
Upigaji wa picha za pamoja watu wakiwa na furaha kubwa mmno kukamilisha kumpa Mungu dhabihu za sifa